Pages

Subscribe:

Thursday, 31 March 2016

DHAMBI YA UONGO

Kuongopa Twa jiumiza tunapo sema uongo Imeandikwa, Waefeso 4:25 "Basi uvueni uongo mkasemakweli kila mtu na jirani yake kwa maana tuviungo kila mmoja kiungo cha wenzake." Amri ya tisa ya onya kusema uongo. Ieandikwa, Kutoka 20:16 "Usimchudie jirani yako uongo." Kusema uongo si kuw akama Kristo. Imeandikwa, Wakolosai 3:9-10 "Msiambiane uongo kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale pamoja na matendo yake mkiva utu mpya unao fanywa upya upate ufahamu sawa sawa na mfano wake yeye aliyeuumba." Mungu anachukia uongo. Imeandikwa, Mithali 12:22 "Midomo ya uongo ni chukizo kwa Bwana Bali watendao uamini ndio furaha yake." Wenye uongo hawatauona ufalme wa Mungu. Imeandikwa, Zaburi 101:7 "Hatakaa ndani ya nyumba yangu yeye atendaye hila asemaye uongo hata dhibitika mbele ya macho yangu." Wasio waminifu hawatauona ufalme wa Mungu. Imeandikwa Ufunuo 22:15 "Huko nje wako mbwa na hao wabuduo sanamu na kila, mtu apedaye uongo na kuufanya." Twakua waongo tunaposema kuwa sisi ni wakristo ikiwa hatutendi kulingana na Kristo. Imeandikwa 1Yohana 2:4 "Yeye asemaye nimemjua wala hazishiki amri zake ni mwongo wala kweli haiku ndani yake." Wanafiki ni waongo. Imeandikwa, Yakobo 3:14 "Lakini mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu msijisifu wala msiseme uongo juu ya kweli." Mungu atawasamehe. Imeandikwa, 1Yohana 1:9 "Tukiziungama dhambi zetu yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wetu."

Saturday, 26 March 2016

YESU MSALABANI 1. MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima Watu wengine wanatumia sentensi hii kupotosha kwa kusema kuwa kama Mungu alimuacha pale msalabani basi sio mwana wa Mungu. Ni kweli aliachwa kwasababu ya dhambi zetu. Alionekana mwenye dhambi si kwa kutenda bali kwa kubeba dhambi zetu na baba yake kwa sababu ya utakatifu wake alimpa mgongo. Alipopigwa magonjwa yako yaliadhibiwa katika mwili wa Yesu ndio maana Isaya 53:5 inasema kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Yesu alikataliwa ili sisi tupate kukubaliwa na Mungu baba. 2. BABA WASAMEHE KWA KUWA HAWAJUI WATENDALO Wakati Yesu anasema maneno haya alikuwa katikati ya mateso na maumivu makali lakini bado aliweza kusamehe. Kawaida mtu anapoumizwa hushindwa kusamehe mara moja; mwingine husema nitasema maumivu yakipoa au mwingine atakuambia nitakusamehe ila sitakusahau. Kuna watu wamekufa leo na wengine wana magonjwa yasiyotibika kwa sababu ya kutokusamehe. Unaposhindwa kusamehe Mungu naye hawezi kukusamehe hivyo sio rahisi kupata uponyaji wako kwa sababu Mungu huponya baada ya kukusamehe. “Akusamehe dhambi zako zote akuponye magonjwa yako yote.” Marko2: 1-5 1 Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani. 2 Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake. 3 Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne. 4 Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. 5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Biblia inasema mkiwasamehe wawakoseao na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe, kumbe basi hata msipowasamehe Baba wa mbinguni hatawasamehe pia. Unapokuwa husamehi kunakuwa na mapepo yanayopata mwanya kuingia ndani yako na kupandikiza roho ya uchungu ambayo huzaa presha, magonjwa ya moyo na kisukari. Waebrania12:1 1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, Ile dhambi ikuzingayo ya kutokusamehe iweke kando. Unapoamua kusamehe wale mashetani wanaokaa ndani yako wanahama ndani yako na unapona magonjwa yako yote. 3. AMINI AMINI NAKWAMBIA LEO HII TUTAKUWA WOTE PEPONI Yesu hakuwa na shaka na alipokuwa anakwenda. Alijua anakwenda wapi. Yesu alimwambia yule mwizi aliyemwamini pale msalabani kuwa hakika leo hii tutakuwa wote mbinguni. Msalaba wa Yesu unatupa hakika ya mafanikio yetu, unatupa uhakika juu ya uwepo wa mbingu na haki yetu ya kuishi huko. Duniani zimejaa taarifa nyingi za kubahatisha ila wewe uliyeokoka msalaba wa Yesu ni uhakika wa kwenda mbinguni. Biblia inasema “amini amini nawaambia yeye aniaminie mimi amepita kuingia mbinguni” Tazama nabisha mlangoni mtu atakayeisikia sauti yangu na kunikaribisha nitaingia ndani yake na atakuwa na uzima wa milele. Mbinguni ni kwetu na msalaba wa Yesu kristo ni uhakika wa kwenda Mbinguni na Yesu ndiye njia, kweli na uzima. Yohana 14:1 1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. 4 Nami niendako mwaijua njia. Msalaba ni uhakika wa kuolewa kwako, hakika ya promosheni, hakika ya kazi yako, hakika ya safari yako, hakika ya maisha yako. Kristo alikuwa na uhakika wa wapi aendako na nini anaenda kufanya, kuandaa makao kwa ajili yetu. 4. MAMA TAZAMA MWANAO NA MTOTO TAZAMA MAMA YAKO YOHANA 19:26-27 26 Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. 27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake. Msalaba unaweza kuleta upatanisho, msalaba ni nguzo ya upatanishi. Inawezekana kuna migogoro kati yako na ndugu zako au wafanyakazi wako lakini leo kuna msalaba wa upatanishi. Leo mataifa yanapigana kwasababu hakuna mapatano, Baba na Mama wanagombana, hawapatani. Yesu alipokuwa msalabani mkono wake mmoja alimshika Mungu Baba na mkono mwingine akawashika wanadamu huku akiwa anakata roho akapiga kelele akisema pataneni! Leo Yesu anaitwa daraja la upatanisho kati ya wanadamu na Mungu. 5. EE BABA MIKONONI MWAKO NAIWEKA ROHOO YANGU Kumbe Roho inaweza kuwekwa kwenye mikono, yaweza kuwa ya Mungu Baba au mungu wa dunia hii ambaye ni shetani. Msalaba wa Yesu kristo unaweza kukabidhi Roho zetu mikononi mwa Mungu. Yesu akatuonyesha kwamba Roho yake ameiweka mikononi mwa Mungu Baba. Leo hii Roho za watu ziko kwa wachawi, nyingine ziko kwa waganga wa kienyeji. Msalaba unatupa uhakika wa mahali pa kuwekwa roho zetu. Biblia inasema msimwogope yeye awezaye kuua mwili bali mwogopeni yeye awezaye kuiua Roho na mwili. 6. NAONA KIU Yohana 19:28 28 Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu. Ni jambo la kushangaza mtu aliye katika hatua ya kufa kuhitaji maji. Haya maneno hakuwa akiwaambia wale waliomsulibisha bali baba yake wa mbinguni; kwamba pamoja na taabu niliyonayo bado ninaona kiu ya kutimiza mapenzi yako. Yesu alikuwa msalabani tangu asubuhi na hapa alisema, “naona kiu” Msalaba wa Yesu unatupa kiu ya uponyaji, kufufua, miujiza, utoaji, kufunga, kuomba. Inawezekana kuna wakati ulikuwa una kiu ya kuomba lakini leo umekuwa mkavu lakini upo msalaba wa yesu unatupa kiu ya kuyatimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yetu. 7. IMEKWISHA Yesu hakuuwawa bali aliitoa Roho yake ili aitwae tena. Shetani hakujua kama Yesu alikuja ili afe ndio maana aliingia kwa watu wamhukumu kifo lakini. Yesu alikuwa mtii hata mauti ili atimize mapenzi ya baba yake. Alipokuwa msalabani Yesu aliangalia kama ametimiza yote yaliyompasa kufanya, akaangalia akaona uponyaji upo, ufufuo upo na maandiko yote juu yake yametimia ndipo akapiga kelele kusema imekwisha. Baada ya Yesu kukata roho yakafuatia matukio yafuatayo: Tukio la kwanza, Dunia yote ikawa Giza. Mungu akazima jua lake na Dunia ikawa giza “MSALABA NI MSALABA WA MATUKIO” Tukio la pili, miamba ikapasuka. Msalaba unapasua miamba. Je, kuna mtu ofisini au kwenye familia yako amefanyika mwamba? Mkutanishe leo na msalaba wa Yesu wenye uwezo wa kupasua miamba. Tukio la tatu, makaburi yakafunguka. Hapo ndipo penye nguvu ya Ufufuo na Uzima yaani Yesu mwenyewe. Tukio la nne, dunia ikatikisika. Tukio la tano, wanawake wakajipigapiga vifuani wakimaanisha wanamtafuta Yesu. Tukio la sita, pazia la hekalu likapasuka maana yake kila mmoja wetu anayo ruhusa ya kuomba moja kwa moja kwa baba bila kupitia mtu yoyote. Tukio la saba, kwenye msalaba pakawekwa anuani maana yake anuani ya mahali unakoelekea kwa makusudi ya Mungu ipo msalabani. Tukio la nane, yule aliyekuwa anaongoza usulubishaji akasema “hakika mtu huyu alikuwa ni mwana wa Mungu.” Tukio la tisa, ilipofika jioni walienda kuwavunja miguu waliosulubiwa maana kwa sheria ya kiyahudi hairuhusiwi mtu kuwa hai juu ya msalaba sabato inapoingia. Akiwa hajafa hukatwa miguu ili afe kwa kuishiwa damu. Walikuta Yesu amekwishakufa lakini mmojawapo wa wale wanajeshi alimchomi mkuki ubavuni ndipo ilipotoka damu na maji. Hiki ni kithibitisho hakika kuwa Yesu alifia msalabani. Yesu alipokufa kabla ya kufufuka alikwenda kuzimu ambako kulikuwa na dhima wakishangilia kumshinda Yesu.Yesu alimfuata shetani palepale kwenye kiti chake kuzimu akamkanyaga kichwa chake mbele ya malaika zake. Tena zaidi ya hayo akamnyanganya funguo za kuzimu na mauti.

Friday, 25 March 2016

KAZI YA MSALABANI

Ushindi kwa Nguvu ya Msalaba”.

I KORINTHO 6:18… [Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.]…
Nguvu ni uweza wa kutenda jambo Fulani. Nguvu ya Mungu inahitajika kuifanya kazi ya Mungu. Biblia inasema hatuwezi lolote kama hatuna nguvu ya Mungu. Yesu Kristo aliwaambia wanafunzi wake wakae Jerusalemu waisubiri nguvu…..
MATENDO 1:4…. [Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu;]…..

Katika mstari wa 8 ahadi hii imezungumzwa:

“ Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”

Kwa hiyo ukiongelea Ukristo, unaongelea nguvu ya Mungu. Endapo Ukristo hauna nguvu, basi huo hautatofautiana na dini zingenezo zote duniani.

1 KORINTHO 2:4…[Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,]….

Nguvu hii ikiwepo kwako, utatofautishwa na imani nyingine zote.
2 KORINTHO 4:20…. [ Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu.]….

Mtu anaweza kushawishi wengine sana, lakini endapo maneno yake hayana nguvu ya Mungu,basi hayana maana.

1 THESALONIKE 1:5….[ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.]….

Nguvu ya Bwana Yesu inatutofautisha na watu wengine. Mtu amjuaye Yesu kristo lazima nguvu ya Mungu ikae kwake: Nguvu ya uponyaji, kutoa mapepo, kufufua wafu n.k.
WAEFESO 3:20…[Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;
21 naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.]…

LUKA 4:18…[Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,]….

Huu ni utambulisho wa Yesu Kristo na kazi aliyoijia. Baada ya kuifanya kazi hii kwa miaka 3 na nusu, alikamatwa, akateswa na kusulubishwa msalabani….

YOHANA19:28…[Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.].

MATUKIO YA MSALABA
Jua lilipoteza NURU na dunia ilikuwa giza.
LUKA 23:44-…..[Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda, 45 jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati.]….

Jua lilisalimu amri. Utukufu wa jua ni kuwaka na kuichoma nchi. Jua likinyamaza maana yake kwenye msalaba, vitu ambavyo kihistoria haviondoki kamwe, vinaweza kutiishwa na kuondoka.
Endapo tutautazama msalaba ina maana, magonjwa yatainama, vilivyopotea vitarudi kwa Jina la Yesu. Kila kilichopotea kinapatikana pale msalabani.

Je, unalo jambo umelipoteza katika maisha yako?

Msalaba ni kama mtambo ambao vitu vilivyopotea: mfano, Kazi/mke/mume/watoto/elimu n.k vilivyopotea vinarudi upya katika Jina la Yesu.

Msalaba sio mti kama ambavyo wengine wanawaza na hata kuchonga miti yenye mfano wa msalaba na na kupeleka majumbani kwao. Pazia la hekalu likapasuka toka juu hadi chini….

Leo ndugu yangu unatakiwa ubebe nguvu ya msalaba na kisha utembee nayo, ili utakapofanya mambo yafanikiwe katika Jina la Yesu.

Wakati wa Agano la Kale, Mungu aliwahi kuwaagiza wana wa Israeli kutengeneza Hema la Kukutania, lenye maeneo matatu:- ·

Nyuani mwa Bwana ·
Patakatifu ·
Patakatifu pa Patakatifu

KUTOKA 26:31-33 …. [Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi;
32 kisha litungike katika nguzo nne za mti wa mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika matako ya fedha manne.
33 Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana.]…..

Mahali pale palipowekwa Sanduku la Agano palitengwa kwa pazia, maana hapa ni Patakatifu pa Patatkatifu.

Pazia liliwakilisha kuwatenga wasiostahili kuingia mahali hapa Patakatifu pa Patakatifu.

YESU alivunja vizuizi vyote vya kumuona Mungu, ili kila mmoja aende kwa Mungu endapo ataukimbilia Msalaba.

Nguvu ya msalaba inatupa nguvu ya kumuendea Mungu moja kwa moja. Ukiona umeshindwa na dhambi, siyo wakati tena wa kusemaMtakatifu Petro uniombee/ au Mtakaatifu X uniombee”…

Msalaba wa Yesu ulipasua kizuizi hicho, na sasa tunamwendea Mungu moja kwa moja kwa njia ya Msalaba.
Kumbuka kuwa Patakatifu pa patakatifu pana Utukufu.

MAOMBI:
Pazia lolote lililozuia maisha yako leo nalipasua kwa Jina la Yesu.
Ee pazia la kunizuia nisikutane na Baraka zangu,kwa nguvu ya msalaba pasuka…………
Kwa Jina la Yesu.

Lipo pazia ambalo ndugu yangu haulioni. Ndiyo maana watu wengine mnaota ndoto za kukutana na wazuiao maishani mwenu. Unaweza kuwa umeomba kwa muda mrefu kumpata mume/mewnza wa maisha yako, lakini zuio linatokea kwa mmoja wa wazazi wako akisema
“Huwezi kuolewa na mtu wa kabila hilo”.

Dunia ikatetemeka, dunia ikatikisika:.. MATHAYO 27:51… [51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;]…

Ukiibeba nguvu ya msalaba, mtaa/kata/ukoo/nchi/mkoan.k. vinaweza kutikisika.
Uwezo wa msalaba ni zaidi ya matikisiko haya ya kidunia kama vile tsunami, kwani haya yote hutokea eneo mojatu la dunia lakini upande mwingine halitoke.lakini msalaba wa Yesu ulikitisika maeneo yote,ndiyo maan Biblia inasema nchi ikatisika.

MAOMBI:
Natikisa magonjwa, taabu, dhiki, kuharibu mimba, kukosa kazi…..Tikisika, kwa Jina la Yesu. Miamba ikapasuka:

Ule mtikiso ulizaa tukio hili la nne la msalaba. Miamba ni vitu vigumu sana. kuna miamba ya maisha yako ambayo unaona ngumu sana kuondoka maishani mwako. Yesu ni mwamba.imeandikwa Yesu ni jiwe la pembeni.

MAOMBI:
Miamba ya maisha yako, tunaipelekea nguvu ya msalaba ukaisagesage na kupasuka pasuka yote kwa Jinala Yesu.

Makaburi yakafunuka: Msalaba unayo nguvu ya kupasua na kufunua. Kibinadamu, kaburi likeshafunikwa inakuwa ni mwisho wa maisha ya binadamu, na hakuna awezaye kufanya lolote (siyo mbunge, rais au ndugu yeyote yule awezaye).

Makaburi yana tabia ya kuficha ilivyovishikilia.

MAOMBI:
Leo naileta nguvu ya msalaba kwenye kata/wilaya/ukoo/ popote ambapo wachawi wameniweka kwenye makaburi yao, name nayapasua yote kwa Jina la Yesu.

Miili mingi ya waliolala ikainuka….. Hapa inamaanisha ni wale watu wailiokuwa wamekufa siku nyingi.
MATHAYO 27:52…. [52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;]….
Kwenye msalaba ipo nguvu ya kufufua vitu vilivyokufa. Nguvu ya msalaba inao uwezo huo wa kuleta hai tena kwa Jina la Yesu.
Miradi iliyokufa inafufuliwa, ndoa iliyokufa na kuzikwa inafufuliwa n.k kwa Jina la Yesu.

MAOMBI:
Naagiza nguvu ya msalaba kwa damu ya mwanakondoo, kazi iliyokufa ifufuke, mitaji iliyokufa ifufuke, ndoa zilizokufa zifufuke kwa Jina la Yesu. Aliyekuzika ukiwa hai, majeneza yapasuke na kukuachia kwa Jina la Yesu.

Akida wa kikosi cha kumsulubisha Yesu akasema mwenyewe “Hakika huyu ni Mwana wa Mungu”….
MATHAYO 27:54…[ Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.]….

Kwenye msalaba pana nguvu ya kujua /kugundua vitu ambavyo ulikuwa hujui )it is the centre for discovery).
Yamkini yapo mambo ambayo familia, ofisi, au mamlaka Fulani yameshindwa kujua uwezo ulio ulioko ndani yako wewe.

Hii ni kwa sababbu umefichwa. Iponguvu katika malaba wa Yesu ukiuendea, na baada ya hapo watu wataanza kuuona uwezo huo.

MAOMBI:
Bwana Yesu kwa nguvu ya msalaba, vile vitu vyote ndani yangu ambavyo wengine hawajavigundua, kwa nguvu ya msalaba wako wavigundue mapema kwa Jina la Yesu. Isiwepo kuchelewa kama Akida kwa Jina la Yesu.

Akida alichelewa sana kugundua nguvu ya msalaba (late discovery). Unaweza kuwa Mkristo kabisa na matumaini yako yakiendelea. Pindi utakapofikia miaka 80 pengine ndiyo watu wengine wataanza kushtukia uwezo wako.

MAOMBI:
Nakataa kutoonekana, kutotambulika kwa Jina la Yesu. Naagiza kuanzia sasa, watu wote ambao wanapaswa kuniona,wagundue leo mapema kwa Jina la Yesu. Uwezo wangu uonekane kwa nguvu ya msalaba. Nakataa kufunikwa na kutoonekana kwa Jina la Yesu. Nami binafsi weze kugundua mapema vitu vile vinavyonihusu kuvifanya kwa Jina la Yesu.

Ipo nguvu katika msalaba ya kugeuza mioyo ya watu. Wale waliokuwazia vibaya, wanapaswa kugeuza mioyo yao kwa nguvu ya msalaba. Waliokupinga siku zote,watafika wakati wa kubadili mawazo yao juu yako kwa nguvu ya msalaba kama yule Akida.

Waliokuwa wamekukataa kabisa wataanza kukupigia debe. Mkristo mwenye msalaba anayo nguvu hii ya msalaba.

MAOMBI:
Nageuza mioyo ya waliokukataa ikugeukie kwa Jina la Yesu.

Mungu wangu wa Mbinguni akubariki.
No Mimi ndugu yako
EV. Elimeleck S Ndashikiwe

Tel. +255767445846
        +255715445846

Wednesday, 23 March 2016

Nguvu ya Mungu Kwetu

Ngao ya Imani Ngao Ngao hukinga, Mungu wetu ni ngao hutukinga na mashambulizi, alimwambia Abramu, “…Usiogope, Abramu mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.” (Mwanzo 15:1). Imani katika Mungu hutukinga na maadui zetu, tunapomwamini kwa kuutumaini uaminifu na upendo wake, yeye huwa ngao kwetu. Kumwamini kunaendana na yeye kufanyika ngao, “Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na makimbilio yangu;” (2 Samweli 22:3). Tukiweka imani yetu kwa Mungu, tukimkiri na kumtegemea anakuwa kinga yetu pande zote, “Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.” (Zaburi 3:3). Unataka Mungu awe kinga yako pande zote? Mtegemee na kumsema hivyo, naye atakuwa hivyo kwako. Tumwaminipo Mungu, nguvu yake huwa ngao kwetu na kutukinga na mashambulizi. Ngao ya imani ni nguvu ya Mungu ambayo hutuzingira dhidi ya mashambulizi ya adui, tunapoziweka imani zetu kwa Mungu. Biblia inaonyesha kwa kusema, “Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.” (1 Petro 1:5). Maana mojawapo ya neno “mnalindwa” katika andiko hili ni “mnakingwa” kwa mfano wa kukingwa na ngao. Imani zetu zikiwa thabiti kwa Mungu humpinga Shetani, huachilia nguvu ya Mungu ambayo huwa ngao ya kumpinga Shetani, “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.” (Yakobo 4:7), “Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani,…” (1 Petro 5:9). Katika Waefeso 6:16 maandiko yanasema, “zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu,” Hapa imani imetajwa kama silaha ikifananishwa na ngao. Ngao hii imeonekana kuwa na uwezo wa kuzuia mishale ya moto ya Shetani. Mishale hii bila shaka ni hila zote ambazo Shetani huzitumia katika fikra au mawazo ili kumtoa mtu katika hali ya kuamini kwa kumtumaini Mungu katika kudhihirisha alichosema. Wakati fulani nilikuwa katika jaribu, wazo likanijia lisemalo “Mungu hakupendi angekuwa anakupenda yasingekupata haya” Wazo hili lilikuwa kama mshale, moto wake ulikuwa hali ya mashaka na wasiwasi kuhusu upendo wa Mungu kwangu. Niliweza kupinga wazo hilo kwa imani katika pendo la Mungu kama maandiko yanavyoonyesha, alinipenda na kumtoa Yesu kwaajili yangu ili nipate uzima (1Yohana 4:9). Hatutikisiki katika imani zetu kwa Mungu kwa kuwa tunalijua pendo lake kwetu na kuliamini, imani ya namna hii ni ngao kwetu kwa kuwa humfanya Mungu awe ngao yetu pande zote kwa nguvu zake. Wazo lolote lililo na hofu ndani yake ni mfano wa mshale wenye moto, lazima imani katika uaminifu wa Mungu kwa yale aliyosema ilizuie, kwa kuachilia nguvu ya Mungu. Mshale ni mfano wa wazo la kishetani, moto ni mfano wa woga au hofu inayokuja na wazo hilo. Ngao ya imani hufanya kazi kwa njia ya kuamini uaminifu na upendo wa Mungu, Biblia inasema, “…uaminifu wake ni ngao na kigao” (Zaburi 91:4). Pia Biblia inasema, “Nasi tumelifahamu pendo alilonalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini…” (1Yohana 4:16). Shetani aletapo wazo kama mshale lisemalo, “ugonjwa huu utakuua” , imani zetu hulipinga kama ngao kwa kuwa tunajua Mungu aliyesema kwa kupigwa kwa Yesu tumepona ni mwaminifu na anatupenda kiasi cha kudhihirisha uponyaji wake kwetu, Wakati huo huo Mungu anakuwa ngao kwetu na kutukinga kwa imani zetu kwake.

Saturday, 12 March 2016

AMRI NA TORATI

MARA NYINGI WATU WANASHINDWA KUTOFAUTISAHA KATI YA AMRI ZA MUNGU NA SHERIA ZA MUSA ZIFUATAZO NI TOFAUTI 1. ZA MUNGU Ziliandikwa na Mungu mwenyewe Kwa kidole chake [Torati 31:18] ZA MUSA Ziliandikwa na Musa mwenyewe kwa k wa kidole 2.Ziliandikwa kwenye mbao mbili za mawe yaliyochongwa, Torati 10:1-4 ZA MUSA Ziliandikwa kwenye chuo(kitabu cha dini), Torati 31:24 3., ZA MUNGU Ziliwekwa ndani ya Sanduku la Agano Torati 10:1-4 ZA MUSA Baada ya kuandikwa, ziliwekwa nje pembeni ya Sanduku la Agano, Torati 31:24-27 4 . Waliozivunja, walionekana kutenda dhambi 1Yoh. 3:4, na iliwapasa kufa. Torati 17:2-5 ZA MUSA Waliozivunja, hawakuonekana na dhambi wala haikuwapasa kufa kwani zilikuwa ni kivuli cha Kristo Wakolosai 2:14-17 5. Yesu alikuja kuzitimiliza wala si ku zitangua. Watu wote wanapaswa kuzifundisha…Mathayo 5:17-19 - ZA MUSA Yesu aliziondoa pale msalabani maana zilikuwa ni sheria za maa gizo tu yaliyosimama kama kivuli cha mema yajayo. Kolosai 2:15 6. Sheria(torati) ya Bwana ni takatifu njema na ya haki, nayo yadumu mi lele na milele, Warumi 7:12- ZA MUSA Zilikuwa ni kivuli cha kazi ya Yesu aliyoifanya msalabani, nazo zilikomea hapo. Ebran. 10:1-12 7. Sheria za Bwana ni kamilifu, za adili, kweli na za milele Zaburi 111:7-8 ZA MUSA Ziliishia pale Kristo alipokufa Msalabani. Waebran. 9:10-12, Luka 22:37 A. Mfano wa sheria ya Musa 1. Kuchinja kondoo kama mbadala wa mdhambi. Kutoka 29…, Walawi, Torati, Nyakati nk 2. Kifo yeyote aliyevunja mojawapo au Amri zote 10 za Mungu Kutoka 31:14… Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake. B. Sheria za Mungu, Kutoka 20 :1-17 Hivyo basi Yesu alipokufa Msalabani sheria za kuchinja kondoo tena ziliisha maana mwanakondoo wa Mungu (Yesu) aichukuaye dhambi ya ulimwengu alikuwa ameshachinjwa tayari. Yohana 1:29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!