Pages

Subscribe:

Tuesday, 8 May 2018

UCHAMBUZI WA BIBLIA kitabu cha MWANZO.

👉 Maelezo ya Kitabu cha Mwanzo Cha Biblia👇✔

Utangulizi
Neno  Mwanzo”  linatokana na neno la Kiyunani “genesis”
       ambalo maana yake ni “asili,” “chimbuko” au “chanzo,”
         ambalo ndilo jina lililopewa kitabu hiki na watafsiri wa Agano la Kale la Kiyunani lijulikanalo kama Septuagint.

       Katika karne ya tatu kabla ya Kristo.

Ingawa kitabu hiki cha Mwanzo kinaanza kuelezea uumbaji wa vitu vyote,
mtazamo mkubwa ni uumbaji wa mwanadamu.

           Kitabu hiki kinaeleza mwanzo wa ulimwengu,
mwanzo wa mwanadamu yaani, mwanamke na mwanamume,
       mwanzo wa dhambi ya mwanadamu,
mwanzo wa ahadi na mipango ya Mungu ya wokovu na
      uhusiano wa kipekee kati ya Abrahamu na Mungu.

Kitabu kinaelezea juu ya watu mahsusi wa Mungu na mipango Yake katika maisha yao.
  Baadhi ya watu hawa ni Adamu na Eva, wanadamu wa kwanza kabisa kuumbwa,
Nuhu, Abrahamu, Isaka, Yakobo, Yusufu na ndugu zake na wengine wengi.

             Mwanzo ni kitabu cha kwanza miongoni mwa vile vitabu vinavyoitwa,
‘‘Vitabu Vitano vya Musa,’’ 
      vilivyoko mwanzoni mwa Biblia.

Vitabu hivi vinaitwa pia vitabu vya sheria kwa sababu ndipo palipoandikwa maagizo na sheria za Mungu kwa watu wa Israeli.
                   Kitabu hiki cha Mwanzo kama kitabu cha utangulizi katika habari za Mungu kuendelea kujifunua mwenyewe katika jamaaa ya wanadamu,

     jambo hili ni la muhimu sana.

Katika kitabu hiki ndiko tunapopata ahadi ya kwanza kabisa ya ukombozi wa mwanadamu aliyeanguka, “….uzao wa mwanamke utakaoponda kichwa…”(3:15).

Mwanzo kinaelezea jinsi ilivyotokea hadi Israeli wakafanyika watu maalum wa Mungu.

      Wazo Kuu Kueleza uumbaji, anguko, Ukombozi wa uzao wa mwanadamu kwa njia ya Yesu Kristo.

        Katika maeneo haya ndipo ulipo ufunuo wote wa ki-Mungu na kweli yote katika Maandiko.

           Kitabu hiki ni kama kitalu cha mbegu cha Biblia nzima,
         hivyo ni muhimu sana kuwa na uelewa sahihi wa kila sehemu.

         Mwanzo ndio msingi ambako ufunuo wote wa ki-Mungu ulipo na ambako umejengwa.

         Kila msingi mkuu wa imani katika Maandiko, mizizi yake iko katika Mwanzo kama asili, kitu kamili au mfano,au ufunuo wa halisi.

Mwandishi Musa

Kuna uwezekano mkubwa kwamba Mwanzo ambacho ni mojawapo ya vile vitabu vitano vilivyoandikwa na Musa, isipokuwa sura ya mwisho ya kitabu cha Kumbukumbu la Torati  inayoelezeajuu ya kifo cha Musa.

Mahali Sehemu ambayo kwa sasa inaitwa Mashariki ya Kati.
Wahusika Wakuu ni Adamu, Eva, Kaini, Abeli, Enoki, Nuhu, Abrahamu, Sara, Loti, Isaka, Rebeka, Yakobo, Yusufu na ndugu zake.

Tarehe Kitabu hiki kiliandikwa 1688 K.K.

Mgawanyo
• Kuumbwa kwa ulimwengu, dunia, mwanadamu. (1:1-2:25)

• Anguko la mwanadamu na matokeo ya dhambi. (3:1-5:32)

• Habari za Noa. (6:1-9:29)

• Kutawanywa kwa mataifa. (10:1-11:32)

• Maisha ya Abrahamu. (12:1-25:18)

• Isaki na familia yake. (25:19-26:35)

• Yakobo na wanawe. (27:1-37:1)

• Maisha ya Yosefu. (37:2-50:26)

Barikiwa sana mtumishi wa MUNGU,

Ni Mimi ndugu yako
Ev. Elimeleck Ndashikiwe.

9 comments:

  1. Mungu akuinue lakini Nina maoni ya kwamba use unatuachia sehem ya kuuliza maswali maana itatujenga kiroho ,, ndimi Dani Kasembe wa Burundi, danikasembe@gmail.com

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ameeeen Mtumishi ubarikiwe pia, Mungu atuwezeshe daima

      Delete
    2. Amina mtumishi Mungu akutie nguvu na akuzidishie ufahamu. Ila tungepata maswali kwa kila mlango yangetujenga zaidi. Asante

      Delete
    3. 0756 240 846 napatikana muda WOTE na WhatsApp number ni hiyo hiyo

      Delete
  2. Ameeeen Mtumishi, maswali naomba niwe naulizwa ktk namba zangu za WhatsApp,

    Hapa ni vigumu kuingia Mara na Mara

    +255715 445846, +255762 680 380

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ubarikiwe sana mtu wa Mungu kwa ufafanuzi wako mzuri hasa kwa mimi ambaye ndio naanza kuisoma biblia kwa mara ya kwanza kabisa hivyo bado nitakubitaji sana ili unisaidie kufika vile viwango vya kiroho ambavyo Mungu ametaka nifike.

      Delete
    2. Ameeeen Uwe huru kuuliza swali lolote

      Delete
    3. Follow me in WhatsApp number 0756 240 846

      Delete
  3. Namba zangu mpya ni hizi

    +255 689 240 840 &
    +255 756 240 846

    ReplyDelete