WATU WA MATAIFA HUCHUKIA NINI HASA KATIKA INJILI YA KRISTO?
-
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.Karibuni sana tujifunze Neno
la MUNGU.Kama umewahi kushuhudia Injili mitaani utanielewa vizuri Zaidi
juu y...
Wednesday, 23 September 2015
NGUVU YA IMANI
FUNZO LA IMANI
Imani ina uhusiano wa karibu na maombi. imani ni tamko inayodhihirishwa katika maombi. imani humtukuza Mungu.jibu kwa maombi ina masharti katika imani.
1.IMANI NA NENO LA MUNGU
Imani yetu yote ndani ya maombi yatakiwa iwe na msingi ya ahadi zinazopatikana ndani ya neno la Mungu (mtu alisema kuna ahadi kupita 3,000 zinazopatikana katika Biblia) ahadi zote zitarudisha kila utu wa maisha ya mwanadamu.
Warumi. 10:17
Imani huja kwa kusikia neno la Mungu.
Mathayo. 17:20
Mbegu ya haradali, imani inayokuwa.
Isaya. 55:10-11
Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;
Hosea6.6
Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketeza.
2.IMANI NA UTIIFU
Warumu. 16:26
....ikajulikana na mataifa yotekama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii imani.
Warumi. 1:5
ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote wapate kujiitisha kwa imani kwa ajili ya jina lake;
Mathayo. 17:24-27
samaki na shekeli. petro hapa alikuwa mtiifu licha ya ujuzi wake wa kufua samaki na neti.
Yohana. 21:6,11...
akawambia , litupeni jarife upande wa kume wa chombo, nanyi mtapata. v11 basi simoni petro,akapanda chomboni, akalivuta jarife pwani, limejaa samaki wakubwa, mia hamsini na watatu; na ijapokuwa ni wengi namna hiyo, jarife halikupasuka.
Petro tena alikuwa mtiifu kwa neno lake Bwana na kulitupa jarife upande wa kushoto wa chombo na ilipokucha- hii ni uvuvi usio wa kawaida katika ziwa ya galilaya. Petero alipokea tuzo lake.
3.IMANI NA KUTUBU
2 Mambo ya nyakati 7:14
ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kuomba na kunitafuta uso na kusiacha njia zao mbaya basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi.
4.IMANI NA KUMKUMBUSHA MUNGU AHADI ZAKE KATIKA NENO LAKE.
1Wafalme 8:25
Na sasa, Ee Bwana, Mungu wa israeli umfikilizie mtumishi wako, daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidia, ukisema, hutakosa kuwa na mtu wa kuketi katika kiti cha enzi cha israeli machoni pangu; kama watoto wako wakiangalia njia zao,ili kuenenda mbele zangu kama vile ulivyoenenda.
Warumi. 4:20
lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;
2.Wakorintho 1:20
maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuza kwa sisi.
5.IMANI NA MATUNDA YA ROHO MTAKATIFU.
Wagalatia 5:22-23
lakini tunda la roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili,uaminifu. upole, kiasi: juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
utaratibu wa kujazwa na Roho Mtakatifu wa Bwana Mungu pia ni utaratibu ya kuzaa matunda ya roho mtakatifu. Hivyo basi imani huongezeka tunapojazwa na Roho Mtakatifu na matunda yake.
siri moja ya maisha ya kufunga na kuomba ni, kufunga huogeza imani kwa sababu ya `kutisha mwili~ kufunga husabisha ujazwe na ujazwe now mtakatifu na imani huongezeka sana wakati wa kufunga na kuomba.
6.IMANI KINYUME NA MAMBO YANAYOONEKANA.
waebrania.11:1
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Mungu aliumba mbingu na nchi kutumia maneno ya imani. kwa maneno ya imani ikawepo. wakati mwingine tunafundishwa ya kwamba Mungu aliumba vitu vyote bila kutumia chochote ila kwa kusema neno lake tu. huo sio ukweli. Imani ni kitu usichokiona inayobadilisha, kwa imani kuwa kitu kinachoweza kutazamwa.
7.IMANI NA USHINDI
Waebrania 11:33-34.
ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, v.34 walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. walizima nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.
8.IMANI NA UTAKASO WA MOYO.
Matendo ya mitume. 15:9.
Wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani.
9.IMANI NA VIPAWA VYA ROHO MTAKATIFU.
Wakorinto12:8-10.
Maana mtu mmoja kwa roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo roho yeye yule; v.9 mwingine imani katika roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika roho yule mmoja; v10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha:
kuna aina tofauti za imani; imani yakuokoa, imani ikiwa tunda la roho mtakatifu. Aina hii ya imani imetajwa hapa ni imani ikiwa kipawa cha roho mtakatifu, sehemu ya imani inayopeanwa kumwandaa muumini kwa kazi ya huduma.
ni imani(kama tunda la roho) inayoweza karama tisa za roho mtakatifu kufanya kazi. kisha kuna imani ya kawaida ambayo sio ya Roho wa Mungu. Hii ni aina ya imani tunayo wakati tunapoamini kwa mfano rekodi za historia au mkulima ambaye amepanda mbegu kwenye udongo na kutarajia mavuno badaye.
10.IMANI HUTENDA KAZI KATIKA UPENDO
Wagalatia5:6
Maana katika kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
wakorintho13:2
Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo hainifaidi kitu.
11. IMANI NA SHERIA ZA MUNGU ZA ROHONI.
Inabidi tutimize amri za Mungu ambayo ameunganisha na kazi ya imani
Marko 11:25 (msamaha ya kwanza nani muhimu) nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na baba yenu aliye mbinguni awasemehe na ninyi makosa yenu.
Tena ukiwa na dhambi moyoni, imani haitatenda kazi. Hata mfarisayo alijua hivyo.
Yohana 9:31 Sasa twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.
12.IMANI NA KUTAMKA NA KUKIRI MBELE YA WATU.
Marko 11:23. ...
Amin, nawambia, ye yote atakayeuambia mlima huu, ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yemetukia, yatakuwa yake.
Warumi 10:9-10.
kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. v10. kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
13.IMANI UKUWA
Wathesalonika 1:3
Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lilio katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu.
Imani kama ile ya mbegu ya haradali humea na kuwa mti mkubwa. mti ya haradali huweza kufikia urefu wa mita 4-5.
14. IMANI NA WOKOVU
Waefeso2:8
kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
15 IMANI HUPEANWA KWA KILA MKRISTO ,KILA MKISTO ANA IMANI.
Warumi 12:3
kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu aivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.
16. IMANI NA MAOMBI NA KULIA KWA MAJONZI INAWEZA KUBADILISHA MPANGOWA MUNGU NA MAPENZI YAKE.
2.Wafalme20:1-11
Hezekiah alikuwa mgonjwa hadi kiasi cha kufa, aligeuka kwa upande wa ukuta na kumllilia na kuomba. Mungu Akabadilisha unabii wake na mwelekeo wa mfalme, kwa sababu ya maombi ya hezekiah. miaka 15 yaliongezwa kwa maisha yake.
17. IMANI NA MAJARIBIO.
1.Petro 1:7
Ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekana kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.
18. IMANI NA MATENDO.
James 2:17 Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa.
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Hivyo imani hufanya kazi.
19. IMANI NA KUMPENDEZA MUNGU.
waibrania. 11:6
lakini bila imani ni vigumu kumpendeza Mungu.
20. IMANI NA KUHESABIWA HAKI.
Habakuki. 2:4
Tazama roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.
21. IMANI NA MAOMBI.
Mathayo 21:22
Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.
Imani ni jambo la muhimu katika kutekeleza maombi.
22. IMANI NA KUFUNGA
Imani huengezeka kwa haraka wakati wa kufunga na hata baada ya kufunga.
Imani ya kufunga ni kutoa nguvu nyingi dhidi ya roho chafu hasa baada ya kunga kabisa.
Mathayo 17:15-21 kijana mwenye wazimu. v.20 kwasabu ya kuamini.......v.21 lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.)
23. IMANI NA KUKUBALI KATIKA ROHO
Mathayo 18:19 Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na baba yangu aliye mbinguni.
Tunaweza tukaongezea imani yetu kwa imani ya mtu mwingine na kupata matokeo mazuri zaidi katika maombi. Imani itaongezeka.
Kuelewana kiroho si kuelewana kiakili au kwa kiwango cha masomo, lakini njia hii ya kuelewana ni kuelewana ya kiroho.
24. IMANI NI NGAO
Waefeso 6:16
kuchukua ngao ya imani.... zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
Imani ni ya silaha ya kinga.
25. IMANI NI KITU NA PIA DHIHIRISHO
Waibrania 11:1 basi immani nihakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Mungu hakutengeneza ulimwengu kutokana na vitu visivyokuwepo bali alitengeneza vinavyoonekana kutokana na vitu visivyoonekana au aliibadili ikawa kama hivyo.
26. IMANI NA MAOMBI
Imani na maombi ni mambo yanaunganishwa pamoja.
imani ina tamko lake kupitia maomi.
Tunaweza Kuomba Yesu imani zaidi. Hata wanafunzi wake walifanya hivyo.
....Mungu huongeza imani yetu. Luka 17:5
27. IMANI NA MAPENZI YA MUNGU
Ni rahisi kuwa na imani ikiwa unaomba ndani ya mpango wa Mungu!
1.Yohana 5:14-15... tunajua ya kwamba tukiomba chochote sawasawa na mapenzi yake tunayo basi tunazo zile haja tulizomwomba.
KILE IMANI SI:
1. IMANI SI TUMAINI.
Ni tumaini pasipo kujali kuhusu kitu chochote, vitu vilivyo vyo mbeleni,hio si imani hata kidogo. Imani inajua inayo saa hii. imani ni hakikisho moyoni mwako ya kwamba unayo tayari ulichokiomba, marko11:24. kwa hivyo nawaambieni, kitu chochote ukitakacho, ukiomba, amini yakwamba imeshapokea nawe utapokea.
2. IMANI SI HISIA.
lakini ni amani moyoni; ni mapumziko, tegemeo na hakikisho ndani ya ahadi za Bwana. imani ni hakikisho dhabiti ndani ya neno la Mungu kuwa ya milele, kamilifu na haitawanyiki na ni ukweli dhabiti.
Hisia kubwa haiwezi kamwe kuzaa imani kamilifu. Hisia hupotea haraka, lakini imai ni lazima isimame kama vile mwamba na hiyo mwamba ni imani ndani ya ahadi za Bwana ndani ya neno lake.
3. IMANI SI KUJUA, NA KUELEWA, SI YA AKILI, LAKINI NI YA ROHO.
Imani ni mambo ya kiroho, kwa sababu roho huishi ndani ya hekalu la mwanadamu, ambayo ndiyo roho ya mwanadamu. 1.wacorintho 3:16 hamjui yakuwa ninyi, mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
Tunaamini na Roho, tunaamini na moyo, na sio na kuelewa kwetu.
Marko. 11.23....wala asione shaka moyoni mwake.
wakati utakapofika wa kupokea yasiyowezekana kutoka kwa Mungu, kujua kwetu kutakuwa ni nadra, ndio, itakuwa ni kizuizi kikubwa sana kutokana na imani.
4. KINYUME YA IMANI NI UOGA.
Uoga ni kuamini neno ovu la shetani sana kuliko kuamini neno lake Mungu. mwovu shetani atakuja akilini mwako na uoga akijaribu kuchukua imani kutoka kwa moyo wako. Yesu alisema mara kwa mara, usiogope. Uoga haitokani na Mungu. Uoga iko na hukumu yake ndani yake. Upendo unaostahili huoondoa uoga.1.Yohana. 4:18
5. KINYUME NA IMANI NI KUTOAMINI.
kutoamini ni kutoamini Mungu kile ambacho Mungu amesema kwa neno lake, kwa hivyo kufanya Mungu kuwa muongo. Hiyo ndiyo sababu kutoamini ni dhambi kubwa na yenye hatari. 1.yohana 5.10.... yule asiyemuamini Mungu Amemfanya awe muongo.....
6. IMANI SI KUOMBA
Maombi ya imani si maombi ya kuomba bali ni maombi ya nguvu na uhakikisho dhabiti ya kwamba Mungu ameshakubali ombi lako kulingana na ahadi zilizoko katika neno lake.
7. IMANI SI NGUVU ZA KAWAIDA
Ni nguvu za kiroho. Imani ni sehemu Roho Mtakatifu. Ukiwa na imani uko na Roho Mtakatifu. Vile unazidishiwa matunda za Roho katika maisha yako, ndivyo unazidi kuwa na imani..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment