Pages

Subscribe:

Saturday, 5 September 2015

WOKOVU NI ZAWADI BORA YA WANADAMU KUTOKA KWA MUNGU.


BWANA YESU atukuzwe.
Karibu nikujuze mipango ya MUNGU juu wa
wanadamu.
Wokovu ni zawadi bora kutoka kwa MUNGU kwa
ajili yetu wanadamu.
''Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia
ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi
zenu, ni kipawa cha MUNGU; wala si kwa
matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. -
Waefeso 2:8-9''
Ukiupata wokovu unaingia kwenye familia ya
MUNGU.
Wokovu ni kumpokea YESU KRISTO.
Walio na wokovu Biblia inasema neno hili juu
yao. " Naye Alituokoa Katika Nguvu Za Giza,
Akatuhamisha Na Kutuingiza Katika Ufalme Wa
Mwana Wa Pendo Lake. Ambaye Katika Yeye
(YESU) Tuna Ukombozi, Yaani, Msamaha Wa
Dhambi- Wakolosai 1:13-14.
-Ni Furaha Kuu Kuwa Ndani Ya YESU KRISTO.
-Sio wote wamempokea BWANA YESU ila
ni faida kuu kumpokea BWANA YESU maana,
- Kumpokea YESU Ni Kuvuka Kutoka Mautini Na
Kuingia Uzimani.
'' Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele;
asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali
ghadhabu ya MUNGU inamkalia.Yohana 3:36''
YESU Akikuokoa ndugu yangu, Hata Ukiondoka
Duniani kama una Wokovu Wa BWANA YESU
Utakua Unaishi Paradiso(pema Peponi) Hata
Kama Walio Duniani Watakuwa Wanakuita
Marehemu.
-YESU KRISTO Ni Muhimu Kuliko Vyote
Unanavyovifahamu.
''Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu
na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na
kutusafisha na udhalimu wote. -1 Yohana 1:9''
Baada Ya Kifo Ni Hukumu. Neno Hilo Watu
Wengi Hawapendi Kulisikia Ila Ukweli Utabaki
Kuwa Ukweli lakini YESU KRISTO Anaokoa, Na
Kama Ukimpokea Unaokoka, Warumi 8:1-2
inasema '' Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu
juu yao walio katika KRISTO YESU. Kwa sababu
sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika KRISTO
YESU imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi
na mauti. ''
Ukiwa umempokea YESU KRISTO kama BWANA
na MWOKOZI wako MUNGU anakuambia
usiogope.
Hii ni ahadi kwa wateule wa MUNGU, Kwamba
tusiogope.
''Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe,
usifadhaike, kwa maana mimi ni MUNGU wako
nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia naam,
mkono wa kuume wa haki yangu.Tazama wote
walioona hasira juu yako watatahayarika na
kufadhaika, watu washindanao nawe watakuwa
si kitu, na kuangamia. {Isaya 41:10-11}
Ndugu yangu, JEHOVAH MUNGU ana ushindi
wako, ana ushindi wako wa kuyashinda ya dunia
na ana ushindi wako wa kuwashinda kila
mawakala wa shetani ambao wanataka kukutoa
kwenye Wokovu wako. omba tu naye atajibu
maana yeye huliangalia neno lake ili alitimiz.
''Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili
kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na
uzima wa milele. -Yohana 3:16''
MUNGU akubariki sana kwa kujifunza ujumbe wa
leo. Na lengo la MUNGU ni kukuokoa mara tu
baada ya wewe kuijua kweli yake.
Kama unataka kuokoka omba kwa sauti yako
maombi haya kisha baada ya hapo jiunge na
kanisa la kiroho wanaoifundisha kweli ya
KRISTO. OMBA HIVI.
Eee BABA Wa Mbinguni, Ninakuja Kwako Katika
Jina La YESU KRISTO. Neno Lako Linasema "
Yeyote Ajaye Kwangu Sitamtupa Nje Kamwe-
Yohana 6:37." Basi Ninajua Kwamba BWANA
Hutanitupa Nje, Bali Utanipokea. Ninashukuru
Kwa Hili. Ulisema Katika Neno Lako Kwamba "
Ukimkiri YESU Kwa Kinywa Chako Ya Kuwa Ni
BWANA, Na Kuamini Moyoni Mwako Ya Kuwa
MUNGU Alimfufua Katika Wafu, UTAOKOKA,
Kwa Kuwa Kila Atakayeliitia Jina La BWANA
ATAOKOKA-Warumi 10:9,13". Ninaamini Kwa
Moyo Wangu Ya Kuwa YESU KRISTO Ni Mwana
Wa MUNGU. Nisamehe BWANA Dhambi Zangu
Zote, futa jina langu kwenye kitabu cha hukumu
na Liandike Jina Langu Kwenye Kitabu Chako
Cha Uzima. Ninaliitia Jina La YESU Na Ninajua
BABA Wa Mbinguni Unaniokoa Sasa. Neno Lako
Linasema " Kwa Moyo Mtu Huamini Hata Kupata
Haki, Na Kwa Kinywa Hukiri Hata Kupata
Wokovu-Warumi 10:10" Nimeamini Kwa Moyo
Wangu Na Ninamkiri BWANA YESU Sasa Na Kwa
Sababu Hii Nimeokolewa. Nafunga Ukurasa Wa
Dhambi Na Nafungua Ukurasa Wa Mema Tu
ROHO MTAKATIFU Nisaidie. Asante BWANA
YESU Kwa Kuniokoa. Kwa Jina La YESU KRISTO
Nimeomba. AMEN.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi
tutajifunza tena siku nyingine.Endelea kuukulia
wokovu kwa mafundisho kanisani.
ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana
makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee
motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO
BWANA.
MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako katika BWANA YESU.
Peter M Mabula
0714252292
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa
uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio
wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

0 comments:

Post a Comment