MAMBO KUMI YANAYOWEZA KUWACHELEWESHA WACHUMBA KUFUNGA NDOA. Bwana YESU
KRISTO
-
Na Peter & Jemimah Mabula Watendakazi katika Shamba la MUNGU wa
Mbinguni Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.Karibu upate maarifa
ya kukusaidia kat...
Wednesday, 23 September 2015
WAZAZI MTULEE VEMA
ATHARI ZINAZOMKUMBA MTOTO ANAYELELEWA KWA MALEZI YA MABAVU.
Watoto wanaokuwa katika malezi ya kimabavu hujikuta wanafuata sheria kila wakati, hali hii inaweza kuwaletea matatizo mbalimbali kama vile:
1. Tatizo la kutokujiamini.
2. Tatizo la kutowaamini wengine pia.
3. Wakati mwingine watoto huwa na tabia za ukali.
4. Huwa na hofu na wasi wasi mara kwa mara.
5. Watoto kuwa na hali ya ukorofi hasa anapo kuwa nje na wazazi.
6. Kuwa na nidhamu ya uwoga akiwa mtoto na hata akiwa mfanyakazi.
MOJA WAPO YA DALILI YA MZAZI ANAYETUMIA MABAVU KULEA WATOTO WAKE
UNAJITAHIDI KUDHIBITI TABIA YA MTOTO
Badala ya kuwafundisha watoto waweze kujidhibiti wenyewe, wazazi wanaokuwa wanalea kwa kutumia nguvu huwa wanataka kuwadhibiti watoto wao. Watoto wankuwa na nafasi ndogo na uchaguzi mdogo kujaribu kujifunza heshima zao wenyewe. Wanakuwa wanatilia mkazo katika kufuata kanuni bila hata ya kuwepo kwa aina yoyote ya ubunifu wa heshima na utii.
Watoto kama hawa wanapoendelea kukua wanakuwa na tabia kama zifuatazo:
1. Ukali kupita kiasi
2. Kuwa na misimamo mikali isiyo na tija wala msingi wowote.
3. Kama ni mke, anakuwa ni mke anayependa kumtawala mumewe kwa kutumia nguvu zaidi ya makubaliano.
4. Kama ni mume pia anakuwa ni mume anayependa kumtawala mkewe kwa kutumia nguvu zaidi ya makubaliano.
5. Mtoto huyu atakapokuwa mzazi atawalea watoto wake vile vile au hata zaidi ya jinsi wazazi wake walivyokuwa wakiwalea kimabavu.
6. Hatakuwa na maamuzi yake binafsi atategemea maamuzi ya wengine zaidi.
7. Mara nyingi maamuzi yake hayatakuwa sahihi atafanya maamuzi yasiyo sahihi mara kwa mara.
UTAJIJUAJE KAMA WEWE NI MZAZI UNAYELEA WATOTO WAKO KWA MABAVU?
Unajaribu Kuwatia Aibu Watoto Wako Kwa Tabia Zao Mbaya.
1. Wazazi wanaolea kwa mabavu ni wakali, waweza kusema maneno kama “wewe sio msikivu” au “nirudie kukuambia mara ngapi jambo moja ?”
2. .
3. Wazazi hawa wanaweza kuwaita watoto wao majina ya wanyama tena wanyama wenye tabia mbaya.
Mfano: Nguruwe wewe, Ngombe mkubwa, Paka au Nyau wewe, nyani au wewe chizi nk.
4. Wazazi hawa hawajali kujenga au kutengeneza uwezo wa mtoto kujitambua wenyewe. Mtoto anakuwa hajajengewa uwezo wa kujitambua na kujikubali mwenyewe.
5. .
6. Kwa ujumla wanadhani kumdhalilisha mtoto ni njia nzuri ya kumfanya awe na ari ya kuwa na tabia njema hapo baadae kumbe ndio uua ule utu wa ndani wa mtoto "low self-esteem"
7. .
8. Wazazi wengine huwazalilisha kwa kuwasema vibaya mbale za watu au mbele za watoto wenzao au hata kuwaadhibu mbele ya watoto wenzao au kundi la watu.
Watoto Wanao Kojoa Kitandani na Kudharirishwa na Wazazi. (Kindumbwendumbwe)
Kwamfano kuna baadhi ya wazazi mtoto anapokuwa anatabia ya kukojoa kitandani huwapaka masizi na kuwavua nguo na kuwatembeza barabarani na watoto wenzao kuwaimbia "kindumbwendumbwe" huku kundi la watoto wa mtaani wakicheka na kumzungusha mtoto huku na kumwita kikojozi.
Huu ni uharibifu mkubwa sana katika moyo wa mtoto. Kama sio neema ya Mungu mtoto huyu anaweza kukua na kidonda hiki kwa miaka mingi sana kwa wengine ni kinyongo mpaka anaingia kaburini ingawa wengine wanakuwa hawasemi wala kuonyesha kinyongo hiki ila wanabakinacho moyoni. Ndio maana watoto waliolelewa katika malezi haya hata wakiwa watu wazima huwa hawana furaha wala mapenzi mema na wazazi wake maana walijeruhiwa jeraha kubwa sana.
Mfano:
• Mtoto alimuuza baba yake mzazi kwa 20,000Tsh kwa watu waliokuwa wakitafuta kununua viungo vya sehemu za siri za mwanaume.
• .
• Baba alikuwa anamchukia sana mtoto kiasi kwamba hataki apewe chakula. Mama yake alikuwa anamuibia chakula na kumuwekea kwenye banda la mbwa ili alie huko baba yake asije akamuona anakula chakula.
WAZAZI WANAOJUA KUADHIBU TU WATOTO WANAPOKOSEA, LAKINI HAWAJUI KUMPONGEZA MTOTO ANAPOFANYA VIZURI!
Unapendelea Kutumia Adhabu Kuliko Kuwapongeza Watoto
Wengi wa wazazi wanaolea kwa kutumia nguvu, hawa amini katika kuwapongeza watoto wao kwa kufanya tabia njema. Wanawaza kuwa watoto wanatakiwa wawe na tabia njema na hawana haja ya kupongezwa kwa kufuata kanuni. Vile vile pale ambapo kanuni inapokuwa imevunjwa, athari yake huwa inaonekana mara moja.
Wazazi katika hundi hili:
1. Macho yao huona makosa tu.
2. Macho yao hayawezi kuona wala kumulika jema lolote linalofanywa na mtoto.
3. Ni wazazi ambao siku zote hutoa lawama tu kwa mtoto.
4. Ni wazazi ambao hakuna siku wanaweza kumpongeza mtoto kwa chochote hata pale ambapo mtoto anapokuwa amefanya vizuri.
5. Watoto wenye wazazi kama hawa huvunjika moyo na kujidharau sana.
6. Mtoto akifanya mambo mengi mazuri haambiwi chochote.
7. Mtoto akifanya jambo moja dogo baya linainuliwa kama bendera na mara kwa mara litakuwa linarudiwa rudiwa kusemwa semwa kama wimbo wa taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment