![]() |
Ndugu nakukaribisha katika somo hili muhimu
kwa maisha ya waenda mbinguni.Na kumbuka
kuwa HUWEZI KUWA MKRISTO KAMA HUNA
KRISTO MOYONI MWAKO. Hivyo hakikisha
kwanza unakuwa na KRISTO maishani mwako
ndipo utakuwa MKRISTO sahihi na sio mkristo
jina.
Je mtu anaweza kuwa baharia bila kwenda
baharini?
Mkristo maana yake ni mfuasi wa
YESU KRISTO. Tunasoma katika Biblia kuwa
YESU alikuwa na desturi ya kwenda hekaluni na
angali anapatikana mahali pa ibada hata leo.
Wakristo ni watu wanaompenda MUNGU, na kwa
hivyo wanawapenda watu wa MUNGU na nyumba
ya MUNGU. Biblia haiwapendekezi Wakristo
pekee, Hata ile hali ya kuwa Mkristo
asiyekwenda kanisani haimfai mtu yeyote. Ni
kama mtu anayeishi kwa kula tu mkate na maji
hali anaweza kupata chakula kizuri kwa afya
yake. Kama alivyosema mwana mpotevu.
''Nyumbani mwa Baba yangu kuna chakula kingi,
wanakula mpaka wanakiacha''(Luka 15:17).
Katika kanisa utapokea mkate wa uzima ambao
ni neno la MUNGU. Kumbuka ya kuwa vitabu
fulani katika Biblia viliandikwa kama barua kwa
makanisa na faida yake kamili inaweza tu
kupatikana unaposhirikiana na wengine..
Ni
afadhali kupata kilicho bora zaidi.
Kumbuka
mwanajeshi hufanya kazi kwenye jeshi .
kaa
la moto likitengwa na mengine litazima.
Hakuna ndoa ya mtu mmoja tu peke yake, Ndoa
ni uhusiano na upendo. Ndoa inakuhusisha na
jamaa wa pande zote mbili.
Hakuna mtu
anayeweza kuwa mkristo wa peke yake tu.
mtu
hawezi kuzaliwa tu peke yake bila ya kuwa na
wazazi na jamaa wa karibu..
Unapozaliwa mara
ya pili yaani unapobatizwa ubatizo wa maji
mengi na pia unapobatizwa ubatizo wa ROHO
MTAKATIFU unafanyika sehemu ya jamii ya
waaminio, Biblia katika Marko 16:16 inasema
''Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini
atahukumiwa'' hivyo kubatizwa pia ni muhimu ili
kuitimiza haki yote ya MUNGU. Jambo hili la
kuamini na kubatizwa lina manufaa makubwa
kwako, huu ni urithi wako na kama mtume Paulo
anavyosema , MKRISTO NI WA AINA MOJA TU-
MSHRIKA WA MWILI WA KRISTO.
Sisi ni washirika wa mwili wake katika
ulimwengu huu. Kanisa liko duniani kwa sababu
sisi sio roho tu bali pia ni watu wenye mwili na
damu. BWANA aliliunda Kanisa hapa duniani
kwa manufaa yetu na ametukirimia vipawa
kutoka mbinguni ili tuweze kupata nguvu kutoka
kwa wenzetu na kufurahia ushirika wa KIKRISTO
na upendo. Maandiko yamejaa habari za ushirika
na kutushauri kwamba tusiache kutumia nafasi
nzuri za ushirikiano na kushauriana na kwamba
tusiache kukusanyikana pamoja kumwabudu
MUNGU wetu.
JINSI YA KUWA KRISTO MWENYE AFYA .
1: Kula chakula kizuri yaani NENO LA MUNGU.
2: Kunywa maji mengi yaani ROHO MTAKATIFU.
3: Fanya mazoezi yaani MTUMIKIE MUNGU NA
KUTENDA KAZI KWA AJILI YAKE.
4: Pata hewa safi yaani HUSIKA KATIKA IBADA
NA SIFA.
J5: iburudishe yaani KWENYE USHIRIKIANO NA
WAKRISTO WENGINE.
MUNGU awabariki sana na kama hujamba
BWANA YESU maisha yako wakati wa kufanya
hivyo ni sasa maana hakuna uzima wa milele
bila YESU KRISTO (Yohana 14:6) hivyo kwa
sababu ndugu unataka uzima wa milele mpe
YESU maisha yako na utakuwa huru mbali na
uonevu wa shetani.
MUNGU akubariki tena
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.
0 comments:
Post a Comment