Pages

Subscribe:
Showing posts with label Injili Ya Amani. Show all posts
Showing posts with label Injili Ya Amani. Show all posts

Thursday, 25 August 2022

NGUVU YA AGANO


Alhamisi 25 August 2022

NGUVU YA AGANO 

Na Mwalimu ELIMELECK NDASHIKIWE

        Hakika ni jambo la kushangaza kwani siku chache zilizopita nilikuaidi kukuandikia kitabu hiki cha Nguvu ya Agano kama Mungu atanipa kibali na siku ile alinipa, leo amenitaka kuanza kukumegea baadhi ya vitu vilivyomo kwenye hicho kitabu na nilikuaidia kuwa katika kitabu hiki nitazungumzia kiundani aina yote ya maagano ikiwemo yale ya Mungu na yakipepo.

          Atukuzuzwe Mungu juu mbinguni na duniani ilipo sehemu ya kuweka miguu yake, leo nitakujuza kiundani kuhusu maagano ama Nguvu iliyopo kwenye maagano ambayo tunaingia na Mungu. Pia jambo hili likupe kiu yakuingi agano ama maagano binafsi na Mungu ili kuwa katika uwakika mkubwa wakutembea na Mungu, kwani kama kuna kitu Mungu hukiheshimu ni Agano.


        Agano ni mapatano baina ya pande kuu mbili au zaidi dhidi ya jambo fulani. 

       Katika maagano ama Agano kuna mambo kadha wa kadha kama nilivyokujuza huku nyuma, ikiwemo, Ishara, Mapatano, ama makubaliano, Kiapo cha uamainifu na kadhalika. Huko mbeleni katika kitabu hiki nitakujuza kwa undani zaidi kuhusu mambo hayo.

      Nataka tuione hiyo Nguvu iliyopo katika maagano ya kimungu ikiwa ni baada ya kuiona iliyopo kwenye maagano ya kipepo siku kadhaa zilizopita kwenye makala ya Msaada kwa wanaoota ndoto wakiwa wanakula vyakula.Pamoja na zile za Namna ya kujinasua kwenye vifungo vya pepo mahaba.

         Kumbuka pia Bibilia ni Agano au ni mkusanyiko wa maagano makuu mawili, yaani lile la Kale na Jipya, ndio maana hutaacha kumuona Mungu kama utasoma Bbilia kwa Sura ya Kiagano, na ufahamu ni kati ya Mwanadamu na Mungu. Na Agano ni mapatano. Ukisoma kwa mtazamo huo wa kuona kilichopo ndani yake kuwa ni mapatano baina yako na Mungu hutatoka kama ulivyo mara baada ya kusoma maandiko na hutakubali kusoma kwa sura ya kawaida ama mazoea.



1. AGANO LA IBRAHIMU:
         Kuna Agano Mungu alifunga na Ibrahimu aliye baba yetu wa imani na Agano hili limekuwa na Nguvu kubwa sana  na Nguvu moja wapo ni hii. Tulione hilo Agano, Agano hili limetiwa nguvu katika sura kadha wa kadha za kitabu hiki cha Mwanzo kwa hiyo tutatazama kila kipengele kilichopo miongoni mwa Agano hili kulingana na uhitaji wa hoja nitakayo ijenga katika mada ama pwenti husika,ila nataka kukudokezea kipengele kimoja kabla ya kusonga mbele zaidi.

           Ni Mwanzo 15: 18 
Siku ile Bwana akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
19 Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni,
20 na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai,
21 na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, na Myebusi.

    Umeliona hilo jambo hapo? Tutalichambua huko mbeleni.
(a) Lili husika katika kumbariki Kiuzao Ibrahimu, Kikawaida Ibrahimu umri wake wa kupata mtoto ulikuwa umepita, ila kwa sababu ya Agano hili la Mungu kumpa uzao na ambao utakuwa kama Mchanga wa Bahari na kuwa tajiri Mungu alilazimika kutimiza jambo hilo bila kuangalia kikwazo cha Umri wake ama ule wa mkewe.

       Tuone hiyo ahadi ya uzao kiagano, 
Mwanzo 17: 
      Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.

     8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.

     9 Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako.

     10 Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa.

Katika hilo hakuna namna Mungu angeweza kuacha kumpa Isaka, maana tayari ameshajifunga na kiapo, na makubaliano yaliyopo kwenye Agano hilo.

      Kumbuka Lengo kuu la kitabu ama mafundisho haya ni kukupa mwanga wa kuyatumia maagano haya yaliyopo kweye bibilia ili kujinasua mahali ulipo ama kunufaika na Baraka zilizomo ndani ya Bibilia maana bibilia ni mkusanyiko wa maagano makuu mawili yaani lile la Kale na Jipya ambalo maandiko huliita kuwa ni bora zaidi.

       Wakati tunasonga mbele  nataka kukupa uwakika wa kwamba Baraka hizi ni matokeo ya Agano hilo, ndiposa Ibrahimu akampata huyo mwana bila kuangalia umri wake ama kigezo chochote kile cha kibaolojia ili na wewe kama mwana wa Agano hili uwe na ujasiri wakumuomba Mungu bila kuangalia kizuizi chochote kile kilichopo mbele yako.


     Tudhibitishe jambo hili kutoka kwenye kinywa cha Mungu mwenyewe, 
Ni Mwanzo 17: 21 
        Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao.
22 Mungu akaacha kusema naye, akapanda kutoka kwa Ibrahimu.

Hapo Ni Mungu anayanena hayo wala Sio Jirani yake na Mungu.

(b) Lilimpa Baraka za Mali, Kumbuka Agano hufanywa Imara kwa sadaka, maombi na kadhalika, ndio maana wale wanaofanya maagano na mapepo hupaswa kutoa kafara za damu za wanyama, ndege, hata watu. Na kanuni hiyo Shetani ameiiga kwa Mungu.
Mara baada ya Ibrahimu kukubali kumtoa Mwanaye Mungu alinena naye kuhusu kumbariki kiuchumi ikiwa ni sehemu ya kiagano.

      Mwanzo 22: 15 
Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni

16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,

17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;

18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.

Hapo panatajwa kumiliki malango ya Adui, maana yake ni kuwa na uwezo wa ulimwengu wa roho wakuteka na kutaifisha mali ama utajiri wa adui zako kisha kuugeuza kuwa wako, kwa kifupi ni kuwafanya mateka wa uchumi. Tulihakiki jambo hilo kwenye kitabu hiki hapa:
Isaya 60: 11 Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.

Pia sentesi inayofunga mazungumzo hayo ipo katika mstari wa 18, hapo kwenye kitabu cha Mwanzo, ambayo inadhiirisha dhairi kuwa Agano hili ndilo lililopenyeza Baraka kwa kila taifa duniani, ndio maana mataifa yakitaka kubarikiwa ni vyema kujiunganisha ama kujiambatanisha kiroho na Taifa la Iziraeli. Nataka kukuonyesha sentensi hiyo; “na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia
Najua unatamani kuendelea nami ila kwa kweli muda sio rafiki yangu, ila kabla sijakutaka tuonane kesho, ambapo nitaendelea na Agano hili kabla ya kuchambua lile la Nuhu, na mengineyo, ninataka kukupa uwakika kwamba wewe ni sehemu ya Agano hili la Ibrahimu ili kukujengea Imani dhabiti itakayokusaidia kupata uwalali wa kuingia kwenye maombi leo ili kudai Baraka zako za kiagano kama mwana wa Mungu.

Kabla ya andiko hilo kumbuka Yesu alikuwa akiwaponya watu wengi ila alitia mkaza sana kwa watu wa Uzao wa Ibrahimu, ndio maana alipomuona yule mama mgonjwa alimuhurumia na kusema kuwa imekuaje hivi kwa mtu wa uzao wa Ibrahmu, alikadhalika kwa mama mkaninayo yule aliyebembeleza na kusema kuwa hata mbwa hula makombo ya bwana zao na kisha kutendewa mujuza. Pale unamuona Yesu akisema kuwa alitumwa kwa ajili ya watu wa Uzao wa Ibrahimu, ukiona Uzao wa Ibrahmu kama wewe uliyepita darasa hili langu picha unayoipata pale ni kwamba hii ilikuwa ni kauli ya KIAGANO.

Maana yake ni kwamba Yesu alipaswa kutilia mkazo kwa watu hawa kwa sababu ya Nguvu ya kiagano. Kwa mantiki hiyo Mungu hapendezwi na mateso ama taabu kwa mtu wa Uzao wa Ibrahimu. Yaani wewe uliyeokoka na mimi pia. Maana wapo wa uzao huo kibaolojia ambao ni Wayahudi na wapo wa Uzao huo ambao ni wale wa Imani yaani waliokoka. Na jambo hili limetiwa muhuri na Mungu mwenyewe kimaandiko.

Kwa ujasiri fungua nami maandiko haya hapa: Ni WAGALATIA 3.29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Neno ahadi hapo linawakilisha AGANO, Maana kama umekuwa mwanafunzi wangu Mwaminifu na Makini utakumbuka vipengele vyote tulivyo visoma vimesheheni ahadi za Ibrahimu kubarikiwa.
Tukutane kesho, ila kama huja Okoka fahamu kuwa hutaweza kuridhi Baraka hizi na maombi utakayoomba hayatakuwa na Nguvu ya kiagano. Na kwa aliyeokoka hivi sasa ninamtaka kuingia kwenye hayo maombi ya kiagano ili kufungua milango iliyofungwa nakudai baraka zako za Watoto, Utajiri na kadhalika.

                                         

Hakuna maoni:

Sunday, 22 November 2020

NGUVU ILIYOKUWAMO NDANI YA UPENDO KUTUOKOA

MUNGU KWETU SISI NI KIMBILIO NA NGUVU
MSAADA UTAKAOONEKANA TELE NYAKATI ZOTE


Bwana Yesu Kristo asifiwe sana mtumishi wa Mungu,

Hakika ninapokaa na kuutafakari upendo mkuu ambao Mungu ameudhihirisha kwetu, macho yangu ya rohoni yanaona vitu vingi ndani ya huo upendo.

        Ndipo nilipogundua ya kwamba kumbe UPENDO ni kama kifurushi kilochotumika kubebea mahitaji ya wanadamu, au zawadi za watoto wa Mungu zitokazo kwa Mungu mwenyewe!


Ev. Elimeleck S Ndashikiwe



      Ndipo nikagundua ya kuwa ndani ya huo upendo kuna vitu vingi sana, nikaona moyo wa Mungu kwa kanisa, wokovu kwa kanisa, mavazi yatupasayo watoto wake vikiwa ndani ya huo upendo!


YOHANA 3:16

Kwa maana jindi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanae wa pekee ili tumuamini yaani tumpokee,

Tupate uzima wa milele uliokuwa umefichwa ndani ya Upendo!


        Msukumo wa kiMungu kutuhitaji wanadamu ili turudi kwenye njia yake, shabaha yake ilikuwa kwanza atuandalie vijizawadi ambavyo vitatushawishi na kuwa chambo kitupeleka kwenye wokovu!

       Pasipo upendo yawezekana angetumia njia nyingine, lkn aliona kuutumia upendo kama package au kifurushi inafaa! Akatununua kwa damu yake ya thamani ili tumuamini.


   KWA NINI TUMUAMINI?

Ni kwa sababu ulimwengu mzima ulikuwa umeigeukia miungu mingine na kuiamini,

        Mungu akaona kabisa haipendezi, ili atuondoe kwenye mikono ya imani nyingine ni lazima atuletee vizawadi vitakavyotushawishi kuvikimbilia kwake, tukishavikimbilia kwake tupate kumsikiliza,

Na tukishamsikiliza tu Imani yake mpya inaingia ndani yetu kwa upya tena, ndiposa tumuamini kwa kuwa chanzo cha imani ni kusikia, tena kulisikia Neno la Kristo.




      Mwamini leo Yesu Kristo kupotia Neno lake, nawe utapokea wokovu mkuu tuliodhihirishiwa bure kabisa!

Tusonge hapa;

              Zaburi 91

1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

2 Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.

3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.

4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.

5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,

6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,

7 Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.

8 Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki.

9 Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.

10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.

11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.

12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.


     Nawapenda sana tena sana, Mungu wa mbinguni akubariki sana wewe uliyejaaliwa kuusoma ujumbe huu!


    Na kama una maoni au swali lolote niulize kwa namba

+255 689 240 840


Inapatikana pia kwa njia ya WhatsApp.

Friday, 6 September 2019

KANUNI ZA KIROHO By Ev. Elimeleck Ndashikiwe

    Kila jambo maishani lina kanuni zake.
Kadhalika maisha ya kiroho yana kanuni zake za jinsi ya kushirikiana na Mungu.

     1. MWENYEZI MUNGU ANAKUPENDA, NAYE ANATAKA KUKUPANGIA MPANGO WA AJABU KWA MAISHA YAKO.

       UPENDO WA MUNGU
  Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
       Yohana 3:16

MPANGO WA MUNGU KWAKO
      Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
Yohana 10:10

      Je, kwa nini watu wengi hawana uzima huo? Ni kwa sababu . . .

      2. MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI.
       Dhambi zake zimemtenga na Mungu.Kwa hiyo hajui upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yake.

      MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI
Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
        Warumi 3:23

    Mungu alimwumba mwanadamu kwa kusudi la kushirikiana naye, lakini mwanadamu alikwenda kinyume cha mpango wa Mungu.
     Alichagua kumwasi Mungu badala ya kumtii.
  Kumwasi Mungu ni kufanya dhambi.

       Mtu anapoishi kinyume cha mapenzi ya Mungu anaendelea kuishi maisha ya dhambi.

      MWANADAMU AMETENGANA NA MUNGU
    Lakini maovu yenu yamewatenga ninyi na Mungu wenu.
        Isaya 59:2

       Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi.
       Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi.
    Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa nija nyingi:
   dini, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi.

     Mwanadamu bado ni mwenye dhambi. Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu . .

      3. YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI.
     Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu.
        ALIKUFA ILI ATULETE KWA MUNGU
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu.
        1 Petro 3:18

      YESU YU HAI
Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alitufuka siku ya tatu,
     kama yanenavyojil maandiko.
      1 Wakorintho 15:3,4

YESU NDIYE NJIA YA PEKEE
       Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
           Yohana 14:6

      Mwanadamu peke yake hawezi kushirikiana na Mungu. Mungu alimtuma Yesu afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na tena awe daraja kati yetu na Mungu ili atulete kwa Mungu.

      Sasa kanuni ya nne itakuambia jinsi uwezavyo kumjua maishani mwako . . .

    4. INAKUPASA KUMPOKEA YESU AWE MWOKOZI NA MTAWALA WAKO.
         Ndipo utajua upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yako.

   UNAMPOKEA KRISTO KWA IMANI
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.
        Yohana 1:12

   Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
Waefeso 2:8,9

     INAKUPASA KUMKARIBISHA YESU, MAISHANI MWAKO
     Ndashikiwe
nasimama milangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake . . .

    Kumpokea Yesu Kristo ni:
Kujua wewe ni mwenye dhambi na kugeuka nafsi yako kwa Mungu na kutubu.
      Kumtegemea Mungu kwa kukusamehe kabisa.

   MUNGU WANGU WA MBINGUNI AWABARIKI SANA TENA SANA

   By Ev. Elimeleck Ndashikiwe

    Tel: +255762 680 380

USHINDI

HUWEZI KUWA SHUJAA IKIWA AU USIPOSHINDANA NA UKASHINDA

          Mungu wetu ni mwaminifu wakati wote, anatupatia nguvu ya kushinda na kuweza.

ISAYA 7:14 Yeye ni shujaa anayo mamlaka, uweza na nguvu kutufanikisha ktk hatua zetu zote

MWAMINI YEYE NAWE UTADHIBITIKA, WAHESHIMU NA WATUMISHI WAKE UTAINULIWA.

Sunday, 1 October 2017

UFALME WA HAKI By Ev. Elimeleck Ndashikiwe

         Math. 13:10-17
10. Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano?

11. Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni,
bali wao hawakujaliwa.

12. Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.

13. Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.

14. Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.

15. Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema,
Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.

16. Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia.

17. Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie.

       Sura ya 13 ya Mathayo ni mwanzo mpya wa mafundisho ya Bwana Yesu

hasa akielezea yatakayotokea baada ya Yeye kurudi mbinguni kama
“Mfalme atakayetawala”.

       Wasomaji wa Biblia wanajua kuwa Mathayo anaanza Injili yake kwa kuonyesha Kuwa Yesu NDIYE Mtoto wa kiume aliyetabiriwa atakayemiliki katika Kiti cha Enzi cha Daudi

      Sura 1
     Kuwa ushahidi wa ufalme wake ni Mamajusi toka Mashariki waliokuja kumwona pamoja na tunu; na ubatizo aliobatizwa na Yohana pale Yordani.

       Sura 2 &3
   Kuwa baada ya Ubatizo na Majaribu, Bwana Yesu alitoa Kanuni sa Ufalme wake ujao

katika Hotuba ya Mlimani

        Sura 5-7
  Misingi ya kanuni hizi ni misingi ya kiroho na Kimaadili
      kanuni zinazosimamia Ufalme wa Mungu Kanuni hizi ndizo zile zilizotabiriwa juu ya ufalme wake hapa duniani ambazo Masihi-Mfalme
            angelizileta akitokea Kanuni hizi zina kweli ambazo hata leo zinatumika na zitatumika katika Utawala wake wa Miaka 1000 Miujiza inayomdhihirisha kuwa ndiye Mfalme.

         Sura 8-10
    Hadi hapo ilikuwa dhahiri kuwa Wayahudi walikuwa wamekataa kabisa ushahidi wowote kuwa Yesu ndiye Masihi na Mfalme aliyetabiriwa Kukataliwa na kuahirishwa kwa Ufalme wake vikitabiriwa.

         Bwana anaonyesha hili kwa kuikemea miji ile ambayo miujiza yake mingi ilifanyika,
na miji ile haikutubu yaani Korazini, Bethsaida nan Kapernaumu.

        Sura 11 (Hasa 21-25).
Kuwa Mafarisayo wanafikia kiwango cha juu sana kukana katakata Umasihi na Ufalme wa Yesu na kuanza kudai kuwa Bwana Yesu anatoa pepo kwa Belzebul
        mkuu wa pepo –

        Sura 12 (Mistari ya 14, 22-29)
Sura ya 13 inakabili 
         swali la nini kitakachotokea wakati Mfalme aliyekataliwa atakaporudi mbinguni,
yaani wakati ufalme aliouahidi utakapoahirishwa hadi ajapo mara ya pili.

       Wazo la kuahirishwa kunaeleweka tu kibinaadamu
kama ilivyotokea kule Kadeshi-Banea

lakini sio katika mpango wa milele wa Mungu,
kwani mpango wa Mungu haubadiliki. Labda sasa tuone kwa kifupi sana kilichotokea pale Kadeshi-Banea:

    1. Hesabu 12 (Huko Hazeroth – Mst 16)
Haruni na Miriam wanampinga Musa kwa sababu ya kuoa mwanamke Mkushi – Mungu anampiga Miriam kwa ukoma

2. Hesabu 13 (Nyika ya Parani – Mst 3,26)
Musa anatuma wapelelezi kuipeleleza Kanaani – Wapelelezi wanarudi wka Musa (Mst 26) – Wapelelezi wanatoa taarifa mbaya ya kukatisha tamaa (Mst 28-33)

3. Hesabu 14 (Kadeshi-Banea) – Uasi mkuu (Mst 1-10).
         Mungu anaamua kuwaangamiza wote (Mst 11-12) – Musa anawaombea neema kwa Mungu (Mst 13-19) – Mungu anawasamehe (Mst 20-21)
           Mungu anaahirisha kwa wana wa Israeli kuingia Kaanani kwa kizazi kile hadi kifie jangwani.

    Mungu anaamua kuwa kila siku waliyopeleleza Kanaani italipiwa kwa mwaka (Mst 26-35).

     Yaani Miaka 40 baadae ndio wataingia Kaanani
       Wale walioleta taarifa mbaya wanapigwa kwa tauni na kufa palepale (Mst 36-37)
     Watu wanatubu na kuasi hapohapo (Msh 39-45)

Sunday, 9 July 2017

JUMAPILI YA BARAKA

Mungu ni mwema kwangu hakika,

Uzima huu nitautumia KUMFIRISI SHETANI.

Saturday, 10 June 2017

SOMO LA UONGOZI

Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu.....

Ev. Elimeleck Ndashikiwe

Nawapenda sana sana.

Fundisho hili linawahusu watu wote hususani wale wanaohudumu kanisani kwenye nafasi mbali mbali,

mfano waimbaji,
wakuu na viongozi wa idara mbali mbali,

pamoja na wale waliopo katika zile huduma tano
           Waefeso 4:11.

Mpango wa Mungu sio kutoa adhabu kwa watu wake,
bali mpango wake ni kuwafanya watu kumtumikia Yeye tu kwa moyo,roho akili na nguvu zote.

Lakini panapo stahili kupata adhabu basi Mungu hasiti kuachilia adhabu sawa sawa na dhambi au kosa lillilopo.
Tukumbuke ya kwamba Mungu wetu sio dhalimu,
bali ni mwaminifu na mpole si mwepesi wa hasira naye ni mwingi wa huruma
         Yoeli 2:13.


Hata hivyo tunakubaliana kwamba adhabu haiji bila kosa. Ikiwa mtu amekosa anapewa nafasi ya toba/kugeuka na kusamehewa mara moja.
Lakini anapoendelea kukosea kwa nia ya kupenda kukosea basi anastahili anyooshwe kwa adhabu,

ukizingatia kazi ya Mungu sio kazi ya kuchezea chezea wala sio kazi ya kuleta masihara.

Ikiwa umeitwa tu “mkristo” na umeokoka basi ujihesabu wewe ni mtumishi wa Mungu mahali ulipo,na uwe makini sana na njia
zako~

chunga unaongea nini!,

chunga marafiki zako ni akina nani ! Chunga unafanya nini!! N.K


“Adhabu ya kuliwa na chango madhabahuni”
Huu ni msamiati mgumu kwa sababu hata neno “chango” ni msamiati bado.

Hivyo neno “chango” ni aina fulani ya minyoo au wadudu wanaotafuna tumbo.

Sasa
kivipi minyoo ikawa ni adhabu kwa mkristo/mtumishi?

          ~ Kumbuka;
Bwana Mungu ana namna yake ya kuwanyoosha watu wake kwa adhabu pale inapostahili,
Yeye Mungu anaweza kufanya chochote kile kwa mtu yoyote yule.

Adhabu ya namna hii inakuja kwa mtu yule anayetwaa utukufu wa Mungu na kujilingalinisha
na Mungu mfano mzuri ni Herode yule aliyemuua Yakobo ndugu wa Yohana kwa upanga

(Matendo 12:1-4)

Biblia inatuambia;

“ Basi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifalme, akaketi katika kiti cha enzi,
akatoa hotuba mbele yao.
Watu wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu,
si sauti ya mwanadamu.

Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho.”
             Matendo 12:21-23


Simulizi hii ya kifo cha Herode ni onyo kwa watu wote
wanaotwaa utukufu wa Mungu.
Herode hali akijua hotuba anayoitoa sio ya Mungu ni ya kwake lakini hakutaka kuonesha
hivyo bali alipendezwa na sauti za watu kuona yeye ni Mungu atoae hotuba.

Watu waliokuwa wakimsikiliza hawakuwa na ufahamu sahihi wa kuitambua sauti ya Mungu
bali yeye hali akijua sio sauti ya Mungu na hakutaka kumpa utukufu Mungu,Mungu akampiga kwa chango nao wakamla.


Hivyo Herode hakuuwawa na wanadamu bali Mungu mwenyewe kwa sababu hakutaka kumpa Mungu utukufu. Ikiwa kama hakutaka kumpa Mungu utukufu,basi ni
dhahiri mtu huyu alijiinua na kujifanya yeye ndio mungu mtu.

Kitu ambacho ni machukizo makubwa sana kwa Bwana ni kutwaa utukufu wake na kumpa mwingine,
kwa maana Bwana mwenyewe asema ;


              “Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.”
              Isaya 42:8



Leo hii nini kinaendelea madhabahuni?

                  Watu wengi wanapenda sifa na kujiinua ili watazamwe kuwa wao ni miungu watu.
Tena baadhi ya watu wanadiriki hata kusema
“Mungu kaniambia…”

na kumbe ndani yao wanashuhudiwa hawajaambiwa chochote kile,bali ni maneno yao wao wenyewe.

Hata kama ni kweli Bwana amekuambia,
swali la kujiuliza Je umeambiwa useme kwa wakati huo?

Haya na mengineyo mengi yanaendelea leo kwenye madhabahu ya Bwana. Hakika mimi
ninakuambia watu wa namna hii wanaojiiunua na kuchukua utukufu wa Mungu watapigwa na chango mpaka kufa kama
ilivyokuwa kwa Herode.!

                     Kuna adhabu ya kupigwa na chango kwa wale watakao iacha kweli wakajitwalia utukufu ambao utukufu huo ulitakiwa
uwe ni kwa Bwana tu.

              Mimi nachelea kusema kila wakati neno hili “Bwana kaniambia…au Bwana kanisemesha...”

ikiwa sijaongea na Bwana kwa nini niseme uongo kwa nia ya kujiinua?

Sitaki kupigwa na adhabu ya chango!!!

          ~ Herode alikufa kimwili kwa kuliwa na minyoo ya gafula kama adhabu bali leo unaweza ukaliwa na magonjwa au ukaliwa kiroho
kiasi kwamba mbele za Mungu hakika ni umekufa hali kimwili upo hai. Ni hali mbaya sana hii!!!

Sio kila adhabu au majanga yote yanaletwa na shetani bali mengine ni adhabu ya Kiungu yenyewe

~ kuna wakati Mungu anaweza akaruhusu adhabu fulani mbaya kwenye maisha yako kwa sababu ya tabia ya kupenda kujiinua kwamba
unatwaa utukufu wa Mungu.
Wito wangu kwako wewe mkristo uliyeokoka ni kwamba,
epuka tabia ya kujitwalia utukufu wa Mungu.

Ikiwa Mungu amekutumia kwenye eneo lolote lile,
basi usiseme umefanya wewe kwa mikono yako bali sema Mungu ndie amefanya yote hayo,
na papo hapo kumbuka kuzikataa sauti za watu wanaokusifia bali kaza kusema ni Bwana tu ndie kayafanya yote.

Usijiinue kwa namna yoyote ile kwa maana usije ukafanana na Herode aliyepigwa na chango.
Ikiwa unaona unasumbuliwa na roho ya kujisifu fulani hivi,
au ikiwa una mtu anayekuumiza kwa tabia yake ya namna hii,

nawe hupendi awe nayo,
kwa maana hiyo roho ni ya rusifa/shetani basi

               naomba usisite kunipigia simu kwa namba zangu hizi tuombe pamoja



+255715445846
+255684485460


Monday, 8 May 2017

WAKATI WA DHIKI KUU, KUIFIA IMANI

IMANI YA MTU NDIPO ITAKAPOINEKANA

Wakristo Wanaokufa kwa ajili ya Imani Mpinga Kristo atawatesa
wakati huu wa dhiki kuu.

Wakristo ambao watakuwa hawafuati mambo yake.
Hawatatii amri zake ila watendelea kuomba Mungu wa kweli wa taifa la Israeli
kupitia Masihi Yesu kristo.

Kwa ajili hii, wakristo watakuwa na uhusiano wa karibu na mwanamke Israeli
Ufu. 12:17.

Katika
Warumi 11:15-20.
Paulo anasema wakristo kutoka mataifa yasiyo ya kiyahudi wamefanywa kuwa sehemu ya mti wa mzeituni kwa hivyo,
wana uhusiano wa karibu sana nao.

Uhusiano huu ndio msingi wa mapenzi tuliyonayo
kwa watu wa taifa la Israeli.

Ombi letu ni kwamba wayahudi kutoka taifa la Israeli nao pia watamtambua Kristo kuwa mwokozi na kuingia katika mapatano naye
Heb. 8: 8-13.

Wakristo wa kweli watatambua mara moja
kwamba mpinga Kristo ni kiongozi wa uwongo.

Wao watamkataa,
pia watakataa kanisa lile la dunia atakaloanzisha.
Kwao, katika milki hii ya mnyama (the beast),

kuna njia moja tuu, nayo ni ile ya mateso na kufa kwa ajili ya Imani.

Kuhusu hawa watakaokufa kwa ajili ya imani yao,
Yohana anasema hivi:

"Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu,
na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.
Wakalia kwa sauti kuu,
wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutohukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?"
Ufu. 6:9-10.

Kati ya hawa watakaokufa kwa ajili ya imani,
watakuwa wale ambao wamekubali wokovu baada ya huduma kanisani kupitia kazi ya wayahudi 144,000, kutakuwa na wakristo kama hawa wengi.

Wao watajitoa kumpinga Kristo, na kuichua uongo wake.
Ikiwa wakati huu utakupata, jua kwamba wokovu wako hautahusika na kumpinga muovu,
na kukataa chapa yake, lakii haya yote yatategemea sana kumkubali Kristo.

Lazima utubu dhambi zako, mkubali Kristo awe Bwana wa maisha yako, na usafishwe na damu yake.
Ni kupitia haya utakuwa umejiandaa vyema
kumpinga huyu muovu, hata kama msimamo wako huu wa upinzani waweza kukufanya upoteze maisha yako.

Lazima uwe tayari kufa kwa ajili ya imani yako. Sababu ni kwamba waKristo hawatapona dhiki kuu:

"Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe,
wakaambiwa wastarehe bado mda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao"
(Ufu. 6:11).

Watakapofika mbinguni, hawa waliokufa kwa ajili ya imani yao watapewa mwili wa kufufuka,
nao watakuwa na furaha kuu pamoja na Mungu.

Hawatakumbuka shida na machozi ya mateso, njaa, na vifo kwa ajili ya imani. Kuhusu watakaofufuka,

          Yohana anasema:
"Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu,
watu wa kila taifa, na kabila na jamaa, na
lugha wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya mwana kondoo wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende
mikononi mwao…

Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe.
Akaniambia, hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao,
na kuyafanya meupe katika damu ya mwanakondoo…

Kwa maana huyo Mwana kondoo,
aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga,

naye atawaongoza kwenye chemi chemi za maji yenye uhai,
na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao"
Ufu. 7: 9, 14, 17.

Mkutano katika Mlima wa Mizeituni Kristo ataonekana mara ya pili hapa duniani
jinsi vile imeelezwa katika Ufu 19, na hii itakuwa pale katika mlima wa mizeituni.

Twasoma:
"Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa mizeituni,
unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki,
nao mlima wa mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi;

litakuwako huko bonde kubwa sana; nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini,
na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini.

Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima yangu;
kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli;

naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia,
mfalme wa Yuda; na Bwana, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye"
Zek. 14:4-5.

Mwokozi wetu Kristo atakuja tena pamoja na watakatifu ambao walikuwa wameungana naye kwa muda wa miaka saba iliotangulia.
Sasa anakuja kuleta makubaliano (reconciled) na wale waliobaki taifa la Israeli

ambao wakati wa vita vya Har-Magedoni,

walikimbilia usalama katika sehemu zilizo na mawe kwenye mlima wa mizeituni.
Mkutano huu utakuwa kwa ajili ya kuwapa wokovu.

"Katika siku hiyo watu wa nyumba ya Daudi,
na wenyeji wa Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi"
(Zek. 13:1).

Pale wayahudi ambao wamepona wanapotaja alama za misumari mkononi na kuuliza:
"Na mtu atamwambia, J
e! jeraha hizi uizo nazo kati ya mkono yako ni nini?
naye atajibu,
Ni jeraha nilizotiwa katika nyumba ya rafiki zangu"
Zek. 13:6.

Huu utakuwa wakati mgumu kwani wayahudi
watajuta kwa ajli ya kutenda dhambi, na pia kwa ajili mababu zao walimkataa masihi wakati yeye alipokuja mara ya kwanza.

Katika Zekaria:
"Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi,
na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba;

nao watamtazama yeye ambaye walimchoma;
nao watamuombolezea, kama vile mtu amuombolezeaye mwanawe wa pekee;

nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.

Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu,
kama maombolezo ya Haddarimoni katika bonde la Megido"
(Zek. 12:10-11).

Kristo ataunganishwa na wale aliosafishwa,
wanaokimbia na wenye huzuni, naye atawatia moyo na maneno haya:

"Nami nitaleta fungu lile la tatu na kulipitisha
kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwayo,
nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo;
wataliita jina langu,nami nitawasikia; mimi nitasema,
watu hawa ndio wangu; nao watasema, Bwana
ndiye Mungu wangu"
(Zek. 13:9).






MUNGU WANGU WA MBINGUNI AKUBARIKI MSOMAJI WANGU,

Nakupenda sana ndo maana najitahidi kukushirikisha hiki kidogo.

Lakini pia, nikuombe, nitie moyo na unishike kwa mkono wako, ukiwa na chochote
kama sadaka kwa Bwana, ukiguswa nibariki pia.

Ndimi ndugu yako
           Ev. Elimeleck S Ndashikiwe

Tel: +255767445846
        +255715445846

WAKATI WA DHIKI KUU DUNIANI Sehemu ya II

WIKI MOJA YA DHIKI KUU

Katika taifa la kiyahudi Israeli,
wana mtindo wa kuhesabu ambapo nambari saba inatumika sana.

Kwa mfano baada ya siku saba,
hii ni wiki moja,
baada ya miaka sita, mwaka wa saba ni mwaka maalum,
mwaka wa sabato, na baada ya miaka saba mara saba,

mwaka wa hamsini (jubilee) huwa ni mwaka maalum wa sherehe.

         Walawi 25:1-10
Na kwa vile dhiki kuu na kudumu kwa muda wa miaka saba,
jinsi vile tunasoma katika

Dan 9:27
kuna umuhimu wa kutilia maanani sana jinsi vile wayahudi huhesabu siku na miaka yao.

Mwaka wa mwisho kabla ya mwaka maalum wa hamsini unaotangulia kurudi kwa
Masihi utakuwa wakati wa majaribu mengi na msisimko wa kiroho katika taifa la wayahudi.

Taifa hili bado limefunikwa macho, na mengi yatalikumba wakati wa miaka ile saba ya dhiki

(soma Yer. 30:7; Dan. 9:27; Eze. 22:19-21; Zek.13:8-9).

Baada ya muda huu wa taabu na kujibadili,
taifa la Wayahudi litaingia kwenye utaratibu maalum wa taifa kuu la wateule ambao wataokoloewa kutoka kwa maafa ya dhiki kuu.

Kutakuwa na muamko wa kiroho katika taifa hili baada ya miaka hiyo saba.
Ni
kutokana na jinsi wayahudi wanahesabu miaka na siku ndipo tunapata uhakika kwamba kweli dhiki kuu itachukua miaka saba.

Hata Danieli anataja haya katika
Dan 9:27

Miaka ya mwisho ya dhiki hii itachukua miezi 42 ambayo ni sawa na siku 1260. Kwa hivyo,
tunaweza kusema haya: ·

Kutakuwa na watumishi wa Mungu maalum wawili ambao watafanya kazi ya Bwana kwa muda wa siku 1260 wakati wa dhiki kuu
(soma Ufu.11:3). ·

Hekalu kuu ya Yerusalemu itaharibiwa na kuchafuliwa kwa muda wa miezi 42 (soma Ufu.11:2).

Mwanamke,
yaani Wayahudi waisraeli watakimbilia jangwani ambapo watawindwa,
lakini hapa watakuwa chini ya ulinzi wake Mungu kwa
muda wa siku 1260
(soma Ufu.12:6). ·

Mpinga Kristo
atakuwa na uwezo na mamlaka makubwa kwa muda wa miezi 42
(Ufu.13:5).

Wateule 144,000 Tukio la muhimu sana wakati wa mwanzo wa dhiki kuu ni ufufuo kiroho utakaotokea kati ya wayahudi.

         Ufu. 7:4
yasema wazi kwamba kutakuwa na watenda kazi na
watumishi  144,000 kutoka taifa la Israeli ambao watakuwa na muhuri kwenye vichwa vyao:

"Na nikasikia nambari ya wale waliokuwa na mihuri
144,000 ya makabila yote ya Israeli walikuwa na mihuri"
(Ufu. 7:4).

Hakuna lile ambalo halieleweki kuhusu haya ambayo tumesoma hapa juu.

Ni kosa kusema kwamba ufufuo wa kiroho unaotajwa katika Ufunuo 7:1-8 utaletwa na kanisa au kikundi fulani maalum.

Somo hili lagusia taifa la Israeli.

Wakati huu,
Mungu atakuwa tayari amewaondoa wale walio na imani halisi kutoka hapa duniani.

Atawafufua wayahudi 144,000 kati ya wale ambao wamerudishiwa imani yao, au
wamemrudia Mungu na kupokea wokovu ili wawe mashahidi wake.

Ufunuo 7 yakubaliana na maneno ya unabii katika biblia ambapo kuna hakikisho
kwamba Mungu hatafufua tu taifa la Israeli na kuwarudisha hapa duniani, ila katika siku za baadaye watafufuka kiroho.

"Kwa hiyo waambieni nyumba ya Israeli, Bwana Mungu asema hivi:
sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya Israeli,
bali kwa ajili ya jina langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa,
mlilolitia unajisi kati kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndiye Bwana,

asema Bwana Mungu,
nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao maana nitawatwaa kati ya mataifa,
nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe.

Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi,
nitawatakaseni uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.

Nami nitawapa ninyi roho mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu. Nami nitatoa moyo wa jiwe iliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.

Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu,
na kuzitenda.

Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu,
nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu"
(Ezek. 36:22-28).

Leo hii kuna wayahudi wengi sana ambao wamepokea ujumbe wa
Agano Jipya unaohusu mwokozi wetu Yesu Kristo.

Hata hivyo wengi wao hawataki kuamua mara moja kumtambua kristo kuwa mwokozi na
wanafanya hivyo kwa ajili ya hofu kwamba huenda wakateswa na kupata taabu

au kwa ajili ya kutojua ni nini kitatokea pale wanapopokea wokovu.

Uamuzi utachukuliwa baada ya kunyakuliwa kwa wale walio na imani na wale
wayahudi wateule ambao tayari wamemkubali Kristo wamenyakuliwa pamoja na kanisa lote la Kristo.

Wale watakaoachwa itawabidii wafikirie kwa
makini kuhusu uamuzi wao utakaochelewa.

Kwa ajili ya matukio haya yote, idadi kubwa ya wayahudi kote duniani watanyenyekea na kutubu dhambi zao wakiongozwa na Roho Mtakatifu

na hapo kukubali kwamba Kristo ndiye Masihi.

      Ufunuo 7:3
Mungu atawachukua wateule wake 144,000
ambao ni watumishi wake waliowekewa muhuri pale mwanzo wa dhiki kuu, na yeye.

Wale walioachwa nyuma itawabidi wachunguze
upya msimamo wao.

Ev. Elimeleck nakukumbusha ya kwamba ktk siku hiyo au wakati huo wa dhiki kuu hakuna mzaha mzaha kama tulivyozoea leo na jana,

Tutatafutana lkn hali itakuwa mbaya mno kuliko.

Itaendeleaaa.......

         Fuatana nami
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe

DHIKI KUU DUNIANI

TAIFA LA ISRAELI WAKATI WA DHIKI KUU

Heshima Yarudi Yerusalemu

Watu wengi hufanya makosa pale ambapo hawaangalii na kuchunguza kwa makini yale yanayosemwa kuhusu taifa la Israeli siku za mwisho.

             Kwa vile hawajui au hawaelewi ni yapi yametajwa kuhusu taifa hili,
wao hupata          ugumu kuelewa yale Biblia inasema kuhusu dhiki kuu siku za mwisho.

Pia mengi ya unabii yanayohusu kuenea
(dispensation)  kanisa hayaeleweki na wengi.

Na lile la muhimu sana ambalo halitiliwi maanani ni kurudishwa kwa Yerusalemu katika taifa la Israeli kuwa makao
makuu au mji mkuu wa taifa hili.

Na kuhusu kurudi kwake Kristo mara ya pili, katika

Ufunuo 1:7
"Tazama, yuaja na mawingu; kila jicho litamwona,
na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam.
Amina."

Haya tuliyosoma yanasema wazi kwamba lazima waIsraei warudi katika taifa lao ili waweze kuchukua uamuzi fulani maalum kuhusu Kristo aliyesulubiwa,

na kukataliwa kwa wale waliokuwa wake wakati
yeye alipokuja mara ya kwanza.

Mji wa Yeruslemu ni mji wa muhimu kabisa kwani hii ndio ishara moja kuu mwokozi
wetu yesu Kristo alitupa kuhusu mwisho wa kuenea kanisa wakati huu, na mwanzo wa dhiki kuu.

Baada ya kueleza kuharibika kwa mji wa Yerusalemu katika
Luka 19:41-44 na 21:5-6

yeye alitaja kutawanyika kwa wayahudi kote duniani,
kwamba Yerusalemu itakaliwa kimabavu na kuharibiwa na mataifa yasiyo ya kiyahudi:

"Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi,
na hasira juu ya taifa hili.

Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote;
na Yerusalemu utakanyagwa na mataifa,
hata majira ya mataifa yatakapotimia"
(Lk. 21:23-24).

         Mtume Paulo anasema wakati huu wa waIsraeli kutawanyika ni wakati ambapo
roho zao zitazidi kuwa ngumu,
na kwao wasio na imani kuwa ni wakati wao kupokea kwa wingi ujumbe wa injili.

Ugumu katika roho za wayahudi umefikia kiwango ambapo mpaka wale wasio na imani wamepokea.

Hata hivyo wote katika taifa la Israeli watapokea wokovu kwa vile imeandikwa katika
Warumi 11:25-26:
"Kwa maana, ndugu zangu sipendi msijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili;
ya kwamba kwa sehemu ngumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa mataifa uwasili.

Hivyo Israeli wote wataokoka;
kama ilivyoandikwa, mwokozi atakuja kutoka Sayuni;
atamtenga Yakobo na maasia yake."

Luka 21:24
hahitaji tu wakati ule ambapo Yerusalemu haitakuwa mji ulionyanyaswa,
bali inazungumzia wakati ambapo kazi ya kuenea kwa kanisa itakuwa imekwisha.

Ni jambo la muhimu kuelewa vyema nakujua
ni yapi yanatokea katika mji wa Yerusalemu chini ya wayahudi ili kuweza kufahamu vyema yale yanayotajwa kuhusu nyakati za mwisho
Lk. 12:54-56.

Wakati taifa la Israeli lilipopata mamlaka ya kuwa taifa mwaka wa 1948, taifa hili lilipewa madaraka juu ya sehemu ndogo tu,
ambayo ni sehemu mpya ya Yerusalemu.

Hii ilikuwa ishara kwamba nyakati za mwisho zilikuwa zinakaribia.

Tukio la muhimu sana lilitokea pale mwaka wa 1967 pale sehemu ya Yerusalemu ambayo ni mji wa kale ambako
kuna Zion na Temple Mount,

na hata sehemu ya mashariki ya Yerusalemu
kuchukuliwa kwa nguvu kutoka Jordan wakati wa vita vikali vya siku sita (Six-day War.)

Hadi wakati huo,
tayari Yerusalemu ilikuwa imejengwa upya, na hii ingefuatwa na Yerusalemu kufanywa kuwa makao makuu ya kisiasa
katika taifa hili la Israeli.

Ni bora kukumbuka hapa kwamba mara ya mwisho Yerusalemu palikuwa ni mahali
ambapo ni mji huru ilikuwa ni pale karne ya sita.

Pale wakati Kristo alipokuwa hapa duniani, bendera iliyokuwa ikipepea Yerusalemu ilikuwa ni bendera ya ufalme wa Kirumi.

Mnamo Agosti 1980,
Waziri mkuu wa Israeli
Menachim Begin
alitangaza wazi kwamba Yerusalemu ndio mji mkuu usioweza kugawanywa wa taifa la Israeli,

na hapo akahamisha makao yake makuu kutoka Tel-Aviv hadi hapa Yerusalemu.

Miaka miwili baadaye,
baraza lake lote la mawaziri lilihamia Yerusalemu.

Hapa basi Yerusalemu ukawa mji mpya ambao ni makao makuu ya kisiasa ya taiafa hili la Israeli.

Lile ambalo lazima litokee hapa ni kufufuka kiimani katika Yerusalemu na kujengwa
upya kwa hekalu.

Hivi sasa, mji huo bado unakaliwa na wageni ambao wako hapo. Jambo kuu ambalo litatokea katika taifa la Israei ni lile
linalohusu jinsi kujitokeza kwa wayahudi maalum 144,000 wakati wa dhiki kuu.

Hekalu itajengwa upya.

Danieli 9:27 na 11:31
na Mathayo 24:15
na 2 Thessalonika 2:4
na mwisho Ufunuo 11:1-2

hapa twasoma jinsi vile hekalu itajengwa upya.

Unabii wa mtume Yohana katika Ufunuo 11 uliandikwa baada ya hekalu iliyotangulia kuharibiwa mwaka wa 70 AD.

Kwa hivyo yale mtume Yohana anayoyataja hapa katika Ufunuo lazima yawe ni yale yatakayotokea baadaye.

Waliobaki katika taifa la Israeli baada ya dhiki kuu watafufuka kiroho pale mwokozi wetu Yesu Kristo atakapojitokeza kwenye mlima wa mizeituni atakaporudi mara ya pili:

"Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa mizeituni,
unaolekea Yerusalemu upande wa Mashariki,
nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake,

upande wa mashariki na upande wa magharibi;
litakuwako huko bonde kubwa sana;
na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini"
(Zek.14:4).

Watu wengi wanangoja siku hii kwa hamu.

Wakati mmoja aliyekuwa meya wa Yerusalemu Teddy Kollek alisema kwamba ni yeye aliyekuwa na kazi kubwa
sana ya umeya duniani,

yaani kuandaa mji huo kumpokea Masihi. 

Itaendeleaaa..........

Ni mimi ndugu yako mpenzi

        Ev. Elimeleck S Ndashikiwe.

Tel +255715445846
       +255767445846