Pages

Subscribe:

Monday, 8 May 2017

WAKATI WA DHIKI KUU DUNIANI Sehemu ya II

WIKI MOJA YA DHIKI KUU

Katika taifa la kiyahudi Israeli,
wana mtindo wa kuhesabu ambapo nambari saba inatumika sana.

Kwa mfano baada ya siku saba,
hii ni wiki moja,
baada ya miaka sita, mwaka wa saba ni mwaka maalum,
mwaka wa sabato, na baada ya miaka saba mara saba,

mwaka wa hamsini (jubilee) huwa ni mwaka maalum wa sherehe.

         Walawi 25:1-10
Na kwa vile dhiki kuu na kudumu kwa muda wa miaka saba,
jinsi vile tunasoma katika

Dan 9:27
kuna umuhimu wa kutilia maanani sana jinsi vile wayahudi huhesabu siku na miaka yao.

Mwaka wa mwisho kabla ya mwaka maalum wa hamsini unaotangulia kurudi kwa
Masihi utakuwa wakati wa majaribu mengi na msisimko wa kiroho katika taifa la wayahudi.

Taifa hili bado limefunikwa macho, na mengi yatalikumba wakati wa miaka ile saba ya dhiki

(soma Yer. 30:7; Dan. 9:27; Eze. 22:19-21; Zek.13:8-9).

Baada ya muda huu wa taabu na kujibadili,
taifa la Wayahudi litaingia kwenye utaratibu maalum wa taifa kuu la wateule ambao wataokoloewa kutoka kwa maafa ya dhiki kuu.

Kutakuwa na muamko wa kiroho katika taifa hili baada ya miaka hiyo saba.
Ni
kutokana na jinsi wayahudi wanahesabu miaka na siku ndipo tunapata uhakika kwamba kweli dhiki kuu itachukua miaka saba.

Hata Danieli anataja haya katika
Dan 9:27

Miaka ya mwisho ya dhiki hii itachukua miezi 42 ambayo ni sawa na siku 1260. Kwa hivyo,
tunaweza kusema haya: ·

Kutakuwa na watumishi wa Mungu maalum wawili ambao watafanya kazi ya Bwana kwa muda wa siku 1260 wakati wa dhiki kuu
(soma Ufu.11:3). ·

Hekalu kuu ya Yerusalemu itaharibiwa na kuchafuliwa kwa muda wa miezi 42 (soma Ufu.11:2).

Mwanamke,
yaani Wayahudi waisraeli watakimbilia jangwani ambapo watawindwa,
lakini hapa watakuwa chini ya ulinzi wake Mungu kwa
muda wa siku 1260
(soma Ufu.12:6). ·

Mpinga Kristo
atakuwa na uwezo na mamlaka makubwa kwa muda wa miezi 42
(Ufu.13:5).

Wateule 144,000 Tukio la muhimu sana wakati wa mwanzo wa dhiki kuu ni ufufuo kiroho utakaotokea kati ya wayahudi.

         Ufu. 7:4
yasema wazi kwamba kutakuwa na watenda kazi na
watumishi  144,000 kutoka taifa la Israeli ambao watakuwa na muhuri kwenye vichwa vyao:

"Na nikasikia nambari ya wale waliokuwa na mihuri
144,000 ya makabila yote ya Israeli walikuwa na mihuri"
(Ufu. 7:4).

Hakuna lile ambalo halieleweki kuhusu haya ambayo tumesoma hapa juu.

Ni kosa kusema kwamba ufufuo wa kiroho unaotajwa katika Ufunuo 7:1-8 utaletwa na kanisa au kikundi fulani maalum.

Somo hili lagusia taifa la Israeli.

Wakati huu,
Mungu atakuwa tayari amewaondoa wale walio na imani halisi kutoka hapa duniani.

Atawafufua wayahudi 144,000 kati ya wale ambao wamerudishiwa imani yao, au
wamemrudia Mungu na kupokea wokovu ili wawe mashahidi wake.

Ufunuo 7 yakubaliana na maneno ya unabii katika biblia ambapo kuna hakikisho
kwamba Mungu hatafufua tu taifa la Israeli na kuwarudisha hapa duniani, ila katika siku za baadaye watafufuka kiroho.

"Kwa hiyo waambieni nyumba ya Israeli, Bwana Mungu asema hivi:
sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya Israeli,
bali kwa ajili ya jina langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa,
mlilolitia unajisi kati kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndiye Bwana,

asema Bwana Mungu,
nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao maana nitawatwaa kati ya mataifa,
nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe.

Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi,
nitawatakaseni uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.

Nami nitawapa ninyi roho mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu. Nami nitatoa moyo wa jiwe iliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.

Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu,
na kuzitenda.

Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu,
nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu"
(Ezek. 36:22-28).

Leo hii kuna wayahudi wengi sana ambao wamepokea ujumbe wa
Agano Jipya unaohusu mwokozi wetu Yesu Kristo.

Hata hivyo wengi wao hawataki kuamua mara moja kumtambua kristo kuwa mwokozi na
wanafanya hivyo kwa ajili ya hofu kwamba huenda wakateswa na kupata taabu

au kwa ajili ya kutojua ni nini kitatokea pale wanapopokea wokovu.

Uamuzi utachukuliwa baada ya kunyakuliwa kwa wale walio na imani na wale
wayahudi wateule ambao tayari wamemkubali Kristo wamenyakuliwa pamoja na kanisa lote la Kristo.

Wale watakaoachwa itawabidii wafikirie kwa
makini kuhusu uamuzi wao utakaochelewa.

Kwa ajili ya matukio haya yote, idadi kubwa ya wayahudi kote duniani watanyenyekea na kutubu dhambi zao wakiongozwa na Roho Mtakatifu

na hapo kukubali kwamba Kristo ndiye Masihi.

      Ufunuo 7:3
Mungu atawachukua wateule wake 144,000
ambao ni watumishi wake waliowekewa muhuri pale mwanzo wa dhiki kuu, na yeye.

Wale walioachwa nyuma itawabidi wachunguze
upya msimamo wao.

Ev. Elimeleck nakukumbusha ya kwamba ktk siku hiyo au wakati huo wa dhiki kuu hakuna mzaha mzaha kama tulivyozoea leo na jana,

Tutatafutana lkn hali itakuwa mbaya mno kuliko.

Itaendeleaaa.......

         Fuatana nami
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe

0 comments:

Post a Comment