JINSI YA KUSIFU AU KUONGOZA SIFA NA KUABUDU VIZURI. A. SEHEMU YA KWANZA • Anza na nyimbo za kukutana na watu au akili yako pale ilipo au kukutana na mahitaji yako au ya watu pale walipo. • Mara nyingi watu huanzia katika hali ya kusongwa na shughuli za kila siku za maisha (masumbufu) • Hivyo anza na nyimbo au pambio zinazohusiana na kuwatia watu moyo pale walipo. • Imba nyimbo zenye kuamsha kiu na hamu ya watu juu ya kukutana na Mungu kwa msaada wa yale yanayowatatiza. • Ni kukutana na watu Misri (nje ya kambi au hekalu) walipo na kuwatia moyo kama Musa ili waanze safari ya kwenda kuelekea Kaanani (ndani ya hekalu) ambako ni nchi yenye asali na maziwa (wema na uzuri wa Mungu kwa msaada) kwenye faraja na amani ya kweli. • Imba nyimbo za kujipa au za kuwapa watu tumaini, furaha, na utayari wa kumwendea Mungu – kuiamsha kiu na hamu ya msaada wa Mungu. • Imba nyimbo za kujialika au kuwaalika watu ili kuanza safari ya kuuendea kiimani wema na uzuri wa Mungu. • Imba nyimbo za kuelezea Jinsi Mungu anavyoweza kukutendea au kuwatendea mema kama ukimwamini au wakimwamini na kumwendeayeye anayewapenda sana! • Nyimbo zinazoelezea au zinazokumbusha matendo makuu ya Mungu alivyokutendea, alivyowatendea, anavyoweza kukutendea au kuwatendea. • Katika nyimbo za injili; ni nyimbo za maisha ya Kikristo, Uinjilisti, na Kualikwa. • Zaweza kuwa ni nyimbo za haraka au taratibu. B. SEHEMU YA PILI • Nyimbo za kumfurahia, kumshangilia, na kumualika Mungu. • Ni kufanya watu waliokwishaingia Kanani /hemani / hekaluni – washangilie na kufurahia, na tena wakimshukuru Mungu kwa kuwafikisha salama (katika mji wa BWANA au nyumbani mwa BWANA. • Ni nyimbo zinazoufanya mioyo watu kujiachilia kwa Mungu waliyemwendea ili aonekane. • Ni kuyafanya mawazo yasiwe ya kujiangalia mwenyewe tena ila Mungu tu. • Ni kuyaelekeza mawazo kwa Mungu na kumshukuru kwa yale aliyoyatenda, anayoyatenda, na atakayoyatenda kwa ajili yetu. • Ni nyimbo zinazoelekeza zaidi kwa Mungu na vipawa vyake atoavyo kwa wanadamu. • Ni nyimbo kuelezea jinsi unavyomjua na jinsi anavyotenda, jinsi ulivyo ndani yake, raha na faida toka kwa Mungu, ili kwueafikisha na kuwaweka watu katika hali ya kuwa tayari kuingia rahani na kumuona Mungu. • Sehemu hii inabidi ichukue muda mrefu na wa kutosha sana, pamoja na uhamasishaji mwingi: ili watu waingie kikwelikweli katika raha na imani kwa Mungu; yaani, wautambue kikweli kweli ukuu, wema, ukarimu, na uzuri wa utukufu wa Mungu katika Kristo Yesu! C. SEHEMU YA TATU • Ni sehemu ya kumuinua Mungu, kumuabudu Mungu, na kujiachilia mbele zake. • Inahusu kuingia na kuwaongoza watu kuingia katika kumuinua Mungu na kisha kufikia katika kumuabudu Mungu Mkuu! • Ni hatua ambayo kusifu kwetu sasa husogea jirani na upendo wa Mungu, heshima, na hali ya kujiweka wakfu kitakatifu kwa Mungu. • Kasi ya mwendo wa nyimbo na vitendo hupungua hatua kwa hatua na kuwa wa taratibu na sauti ya kutulia sana. • Ni hatua ambayo umakini wako unatakiwa uwe kwa jinsi Mungu alivyokuwa, alivyo sasa, na atakavyokuwa kwa uzuri wake, ikuu wa Mungu, na upendo mkuu; na wa tabia zake za uungu ambazo ametushirikisha nasi pia. • Mara nyingine, ukimya na utulivu mtakatifu hulifunika kusanyiko la Mungu. Katika hali hii, inamaanisha kuwa kusifu kunahamia hatua nyingine, yaani, kutoka kumuinua Mungu na kuingia katika kuabudu. • Roho Mtakatifu huwaongoza watu sasa kuingia Patakatifu pa patakatifu. Kusifu sasa kunakuwa ni laini na kuingia katika uzuri wa kuabudu kwa kweli katika utakatifu. • Katika hatua hii unatakiwa (mwongozaji wa sifa) kuwa makini sana kuangalia utembeaji wa Roho Mtakatifu na kusikiliza vile atakavyo au atoavyo maelekezo. • Ni vizuri kuwaongoza watu kwa upole na pia kuwaelimisha kwa maneno ya uangalifu sana ya kuwa sasa wanahamia hatua nyingine. Chagua maneno ya busara na kiasi, usiseme maneno mengi au yale ya kuwahamisha watu mbali na utulivu wa kuabudu, bali yenye kuwasaidia na kuwahamasisha kububujika zaidi. a. Kumbuka: Usimzimishe Roho Mtakatifu; Watu wanapobubujika, nyamaza na uwaache watu wabubujike katika Roho, umakini wako na wa watu unatakiwa uelekezwe kwa Mungu pekee, na si kwa kiongozi wa kuabudu au muziki tena! RUHUSU WINGU LA UTUKUFU WA MUNGU KUSHUKA. • Kadiri tuisogeleavyo sehemu takatifu sana, ndivyo uimbaji wetu unatakiwa kuwa ni wa kuhusu sana Mungu mwenyewe (Wewe ni Mungu … ) • Unakuwa upo mbele za Mungu na uwepo wake. • Kumbuka uimbaji ulianzia nje ya kuta kwa kuimba kuhusu sisi wenyewe na mahitaji yetu na hisia zetu au hau yetu juu ya Mungu; sasa safari ya uimbaji mwishowe tunaimalizia ndani, patakatifu pa patakatifu, kwa kumuabudu Mungu. • Ni sehemu ya uwepo mtakatifu wa Mungu. • Katika hatua hii, Mungu na malaika zake watakatifu huwahudumia watu. JINSI YA KUPANGILIA PAMBIO KATIKA KIPINDI CHA SIFA 1. PAMBIO ZA KUFARIJI a. KUONYA b. KUTIA MOYO c. KUKEMEA d. KUHUBIRI 2. PAMBIO ZA KUSIFU / ZINAZOELEZEA JINSI : a. ALIYOTATENDA / ALIVYOTENDA / ALIVYOKUTENDEA/ ALIVYOWATENDEA b. ANAYOTATENDA / ANAVYOTENDA / ANAVYOKUTENDEA / ANAVYOWATENDEA c. ATAKAYOTENDA / ATAKAVYOTENDA / ATAKAVYOKUTENDEA / ATAKAVYOWATENDEA 3. PAMBIO ZA KUMUINUA MUNGU a. KUMUELEZA MUNGU MWENYEWE UNAVYOMFAHAMU b. KUMUELEZA MUNGU TABIA NA SIFA ZAKE c. SI KUELEZA ALIYOYATENDA, BALI JINSI MUNGU ALIVYO 4. PAMBIO ZA KUMUABUDU MUNGU a. KUMUELEZA MUNGU JINSI UNAVYOJISIKIA KUWA NAYE b. KUMUALIKA MUNGU AHUSIKE NAWE c. ELEZA HISIA ZAKO SI ZA WENGINE d. UTAKAVYOJISIKIA KAMA UKIENDELEA KUWA NAYE MILELE i. UPENDO WAKO KWAKE, Sifa zake na kazi zake. ii. FURAHA YAKO KWAKE Sifa zake na kazi zake. iii. AMANI YAKO KWAKE Sifa zake na kazi zake. iv. UZIMA WAKO KWAKE Sifa zake na kazi zake. v. NGUVU WAKO KWAKE Sifa zake na kazi zake. vi. RAHA YAKO KWAKE Sifa zake na kazi zake. vii. UJASIRI WAKO KWAKE Sifa zake na kazi zake. BADHI YA MFANO WA NYIMBO / PAMBIO NA JINSI YA KUPANGILIA (LABDA ROHO ASEME VINGINEVYO NA WEWE!) (I) NYIMBO / PAMBIO ZA KUFARIJI 1. TWENDE JUU SAYUNI X 3 MJI WAKE BWANA 2. TEMBEA NAYESU 3. WPTE WALIOMPOKEA 4. AMINI YESU ANALEA 5. MCHAKA MCHAKA MKIMBILIE YESU 6. MWAMINI X 3 MWOKOZI X 2 7. KIMBILIA KWAKE YESU UTAPONA. 8. NIPE MAJI NINYWE, MAJI YA UZIMA. 9. ONJENI KUONE, MUNGU YU MWEMA 10. SIMAMA TUKAIMBE PARADISO 11. NIMPELELEZE NANI FURAHA YA MBINGUNI 12. JINA LANGU LIKO KULE X 3 MBINGUNI 13. SAYUNI X 4 NINAIMANI YA KWAMBA NITAFIKA 14. (MIKONONI, MIKONONI) X 2 TUKIWA SAFARINI, YESU NDIYE KIONGOZI 15. NJIA YEMBAMBA X 2 NITAIFUATA, NIWEZE KUFIKA MBINGUNI 16. WAAMBIENI WATEULE WAJIPE MOYO, BWANA AMEKUSUDIA KUWAPA MEMA 17. JINA LAYESU, NI NGOME YANGU. 18. MWAMBIE YESU X 2 ANAWEZA YOTE 19. YUKO MUNGU MMOJA MBINGUNI YEYE NI MWAMBA 20. AINULIWE MUNGU WETU LEO, AINULIWE, BWANA WA MABWANA 21. SIMAMA USICHELEWE 22. SIMAMA IMARA UMTETEE BWANA 23. NATAMANI NIENDE PARADISO KWA BWANA 24. MSALBA MBELE DUNIANYUMA 25. NINAMJUA ALIYE MWAMBA. 26. NYIMBO ZA KITABUNI - NYIMBO ZA INILI UKURASA WA 91-11 (II) NYIMBO / PAMBIO ZA KUMSIFU MUNGU 1. JINA LAKE IMANUELI HOSANA 2. YU MWEMA BWANA WANGU YESU, YU MWEMA! 3. NIMWUONA MWOKOZI, NIMEMWONA AHA! 4. MSHUKURUNI BWANA KWA KUWA NI MWEMA 5. NISEME NINI BWANA X 3 YOTE NINASHUKURU 6. YESU NI WANGU WA UZIMA WA MILELE 7. WATU WOTE WAMTUKUZE BWANA 8. TUIMBE HALELUYA HOSANA NA YAHWE 9. EE BABA X 3 POKEA SIFA 10. LEO NI SIKU NGEMA TUTAMUONA BWANA 11. MUNGU YU MWEMA X3 KWANGU 12. NINAMJUA ALIYE MWAMBA, ALIYENIOKOA 13. MWIMBIENI BWANA WIMBO MPYA, KWA MAANA AMETENDA MAMBO YA AJABU 14. SIJAMPAT RAFIKI WAKUFANANA NA YESU 15. SIJAONA KAMA YESU 16. MWAMBA NI YESU… 17. (AIME, AIME, AIME!) X 2 18. JINA LA YESU, LIBARIKIWE X 3 NI JINA LA NGUVU ZOTE! 19. NI BWANA WA WATU WOTE 20. NI YEYE YULE X 3 ALIYENIOKOA 21. MSALABA WA YESU, NI MSALABA UMENIOKOA DHAMBI, HALELUYA 22. ALIUBEBA MSALABA KUELEKEA GOLIGOTA 23. POPOTE ALIENDA ALITENDA MEMA 24. NAMPENDA YESU WA GALILAYA AMETENDA MAKUU MOYONI MWANGU 25. AMEJAA NEEMA YESU AMEJAA NEEMA 26. NI WA NEEMA X 3 BABA! 27. HAKUNA WA KUFANANA NAYE! 28. MAHALI NIKEFIKA NIMEONA MKONO WAKO, 29. YESU ANAWEZA YOTE 30. HOSANA MWANA WA DAUDI 31. BABA YETU WA MBINGUNI, MAPENZI YAKO YATIMIZWE! 32. PALE KALIVARI YOTE YALIKWISA 33. NIMEUONA MKONO WA BWANA NIMEUONA! 34. KAMA SI WEWE BWANA NINGEKUWAJE LEO 35. NANA MWANAUME KAMA YESU HALELUYA 36. SIFUNI – OH IMBA IMBA SIFUNI 37. SIFU MUNGU HALELUYA, SIFU MUNGU AME! 38. HAKUNA KAMA YEHOVA X 3 HAKUNA KAMA YEHOVA YIRE! 39. ALIPO YESU YOTE YANAWEZEKANA (III) NYIMBO ZA KUMUINUA MUNGU NA KUABUDU. 1. WEWE NI MUNGU MKUU, WAWEZA YOTE, … 2. HAKUNA MUNGU KAMA WEWE … 3. BWANA WA MABWANA, MUNGU WA MIUNGU, ALFA NA OMEGA …. 4. UMEINULIWA X 3 JUU … 5. HAKUNA, MUNGU KAMA WEWE, HAKUNA POPOTE… 6. BWANA UMETAMALAKI, HAKUNA ALIYE KAMA WEWE. 7. UNASTAHILI KUABUDIWA … 8. NASEMA ASANTE X 3 EWE MUNGU WANGU. 9. NISEME NINI BWANA X 3 YOTE NINASHUKURU. 10. BABA WA MBINGUNI HAKUNA KAMA WEWE. 11. NAFSI YANGU YAKUTAMANI, ROHO YANGU YAONA KIU, KAMA AYALA… 12. MUNGU WETU, TUNAKUABUDU. 13. BABA WA MBINGUNI, MUNGU MTAKATIFU, TUNAUNGANA NA MASERAFI MAKERUBI KUKUABUDU. 14. HAKUNA X 3 KAMA WEWE! HAKUNA, HAKUNA, ALIYE KAMA WEWE! 15. BWANA, UMETAMALAKI, HAKUNA ALIYE KAMA WEWE. 16. ZA KITABUNI - NYIMBO ZA INILI UKURASA WA 19-42.
WATU WA MATAIFA HUCHUKIA NINI HASA KATIKA INJILI YA KRISTO?
-
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.Karibuni sana tujifunze Neno
la MUNGU.Kama umewahi kushuhudia Injili mitaani utanielewa vizuri Zaidi
juu y...
Hakika nampenda sana Mungu wangu wa mbinguni
ReplyDelete