Pages

Subscribe:

Tuesday, 6 October 2015

NGAO YA IMANI KWA MWAMINI

Ngao  Ngao hukinga

Mungu wetu ni ngao hutukinga na mashambulizi,

alimwambia Abramu,
“…Usiogope, Abramu mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.” (Mwanzo 15:1).

Imani katika Mungu hutukinga na maadui zetu, tunapomwamini kwa kuutumaini uaminifu na upendo wake, yeye huwa ngao kwetu. Kumwamini kunaendana na yeye kufanyika ngao,

“Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na makimbilio yangu;” (2 Samweli 22:3).

Tukiweka  imani yetu kwa Mungu, tukimkiri na kumtegemea anakuwa kinga yetu pande zote, “Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.” (Zaburi 3:3).

Mtegemee na kumsema hivyo, naye atakuwa KINGA NA NGAO kwako. Tumwaminipo Mungu, nguvu yake huwa ngao kwetu na kutukinga na mashambulizi. Ngao ya imani ni nguvu ya Mungu ambayo hutuzingira dhidi ya mashambulizi ya adui, tunapoziweka imani zetu kwa Mungu. Biblia inaonyesha kwa kusema, “Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.” (1 Petro 1:5).

Maana mojawapo ya nenomnalindwakatika andiko hili nimnakingwakwa mfano wa kukingwa na ngaoImani zetu zikiwa thabiti kwa Mungu humpinga Shetani, huachilia nguvu ya Mungu ambayo huwa ngao ya kumpinga Shetani, “Basi mtiini MunguMpingeni Shetani, naye atawakimbia.” (Yakobo 4:7)

Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani,…” (1 Petro 5:9).

Waefeso 6:16 maandiko yanasema, “zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu,”

Hapa imani imetajwa kama silaha ikifananishwa na ngao. Ngao hii imeonekana kuwa na uwezo wa kuzuia mishale ya moto ya Shetani. Mishale hii bila shaka ni hila zote ambazo Shetani huzitumia katika fikra au mawazo ili kumtoa mtu katika hali ya kuamini kwa kumtumaini Mungu katika kudhihirisha alichosema.

Wakati fulani nilikuwa katika jaribu, wazo likanijia lisemaloMungu hakupendi angekuwa anakupenda yasingekupata hayaWazo hili lilikuwa kama mshale, moto wake ulikuwa hali ya mashaka na wasiwasi kuhusu upendo wa Mungu kwangu. Niliweza kupinga wazo hilo kwa imani katika pendo la Mungu kama maandiko yanavyoonyesha, alinipenda na kumtoa Yesu kwaajili yangu ili nipate uzima (1Yohana 4:9).

Hatutikisiki katika imani zetu kwa Mungu kwa kuwa tunalijua pendo lake kwetu na kuliamini, imani ya namna hii ni ngao kwetu kwa kuwa humfanya Mungu awe ngao yetu pande zote kwa nguvu zake. Wazo lolote lililo na hofu ndani yake ni mfano wa mshale wenye moto, lazima imani katika uaminifu wa Mungu kwa yale aliyosema ilizuie, kwa kuachilia nguvu ya Mungu.

Mshale ni mfano wa wazo la kishetani, moto ni mfano wa woga au hofu inayokuja na wazo hilo. Ngao ya imani hufanya kazi  kwa njia ya kuamini uaminifu na upendo wa Mungu, Biblia inasema, “…uaminifu wake ni ngao na kigao” (Zaburi 91:4).

Pia Biblia inasema, “Nasi tumelifahamu pendo alilonalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini…” (1Yohana 4:16).

Shetani aletapo wazo kama mshale lisemalo, “ugonjwa huu utakuua” , imani zetu hulipinga kama ngao kwa kuwa tunajua Mungu aliyesema kwa kupigwa kwa Yesu tumepona ni mwaminifu na anatupenda kiasi cha  kudhihirisha uponyaji wake kwetu, Wakati huo huo Mungu anakuwa ngao kwetu na kutukinga kwa imani zetu kwake.

MUNGU WANGU AKUBARIKI MPENDWA WANGU

Ni mimi rafiki yako
Ev. Elimileck S Ndashikiwe

elimelck@gmail.com

0 comments:

Post a Comment