Hivyo ni lazima Mke kama Mke uwe ni mwanamke wa IMANI DHABITI.
2 Timotheo 1:5-6
Kijana anayetajwa katika mlango huu, aliishika imani aliyokuwa nayo mama yake, lakini mama wa kijana huyu naye aliishika imani iliyokuwa kwa mama yake pia.
Hivyo bibi ameweza kumfundisha mwanawe imani, na mwana naye akamfundisha mwanawe imani. Hivyo tunaona umuhimu wa mke kuwa na imani inavyoweza kuambukiza watoto na hata wajukuu.
Na kama mke ukiwa mjuzi wa Mambo ya Mungu na kuweza kuambukiza watoto IMANI ILIYO DHABITI, hakuta kuwa na sababu ya watoto kutanga tanga wawapo wakubwa. Watoto watatanga tanga wakijua Imani ya wazazi haikuwa na matunda yoyote, hivyo ni rahisi kuiupuuza imani hiyo. Lakini watoto wakiona Imani ya wazazi inaheshimiwa, inazaa matunda sio rahisi watoto kuiacha imani hiyo.
NI LAZIMA SASA MAMA KAMA MLEVI WA FAMILIA NA MJENZI WA NDOA IMANI YAKO IWE DHABITI NA IMARA. Ni lazima uwe mtu wa kupenda:
1 . Kuhurudhia Ibada.
2. Kusoma neno la Mungu.
3. Kushika taratibu za Dini yako katika Imani yako.
4. Kuwafundisha watoto Imani hiyo kwa kumaanisha.
5. Kupenda kufunga na Kuomba kila mara.
Lakini pia kutoa sadaka kwa Mungu.
FAIDA ZA KUWA MKE WA IMANI.
Faida ziko nyingi sana, hata kila mmoja ni shahidi, na kila anayejua Faida za kuwa na imani thabiti akiamua kuorodhesha nafasi haitatosha. Pamoja na kuwa na faida nyingi sana hizi hapa ni moja ya faida hizo.
1. Kuwa mwanamke wa Hekima na Adabu. Utajikuta umekuwa mwanamke wa hekima na adabu tele, hii ni kwa sababu umekuwa karibu na Imani yako ambaayo ina Mungu ndani yake. Tena utakuwa mwanamke wa Maarifa,, Kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa. Na ukishakuwa mtu wa maarifa hakuna kitakachokushinda kwani Kwa hekima ambayo Mungu atakujalia basi utajikuta unaweza kukabiliana na changamoto nyingi katika maisha lakini pia katika ndoa. Hutakuwa mtu wa kukosea kosea na kufanya uzembe ama kukurupuka , utakuwa mtu wa Utaratibu na mtu wa staha na kuweza kujiendesha.
2. Mumeo atakuheshimu . Katika maisha ya ndoa mara nyingi wanawake wamekuwa wakilalamika kutoheshimiwa, kutothaminiwa na kupuuzwa ama kuumizwa,
Faida moja wapo ya kuwa mwanamke wa Imani Thabiti ni pamoja na Mume kukuheshimu,, kukuthanini na kukupenda.
Hii haitakua na mjadala, kwani moja kwa moja kwa Imani yako itakufundisha nini wajibu wako kama mke, nini unapaswa kufanya. Wakati mwinigne Mume anakushinda na amekuwa kwazo kwako sana,,
umemshtaki kwa wadhamini, kwa wazazi, kwa marafiki zake , kwa boss wake, kwa kaka zake, Ustawi wa jamii, mahakamani, kote huko lakini bado tu hasikii na wewe unampenda na kuipenda ndoa yako… Sasa ni lazima uwe na Imani Thabiti ili iweze kukusaidia. Imani Thabiti haishindwi na jambo lolote lile. Lakini kwa kuishika Imani yako vyema na Kumheshimu Mungu ipasavyo. Ni lazima Mumeo atakuwa na hofu ndani yake . Na atakupenda na kukuheshimu, Sio kwa vile unamlazimisha afanye hivyo la hasha, Lakini kutakuwa na Nguvu ya namna yake itakayomsukuma kukupenda, kukuheshimu na kukuthamini,
Ni kama ATAMUONA MUNGU katika maisha yako, Na atakuwa na hofu ya kukutenda mabaya. 3. Kufanikiwa katika kila idara. Kwa vile utakuwa mwanamke wa Imani, basi Mungu atakuwa pamoja na wewe. Utafanikiwa sana katika idara zote, kiuchumi,, kiimani kiroho na kimwili. Hutakuwa mtu wa kuwa mkia, bali utakuwa mwanamke wa kuwa Kichwa na mafanikio yataambatana na wewe katika kila Nyanja. Mumeo atakuita Heri, lakini watoto wako pia watakuita Heri, kwani utakuwa mwanamke mwenye Hekima na Adabu.
Mithali 31: 30 “Upendeleo hudanganya, na Uzuri ni Ubatili, Bali mwanamke Amchaye Mungu ndiye atakayesifiwa” MWANAMKE ANAPASWA KUFANYA MAMBO GANI KATIKA KUMTUKUTA MUNGU. Badala ya kupoteza muda katika kukaa bar, kunywa pombe, kuzurura na kusogoa ni bora sasa mwanamke uwe mwanamke wa Busara na Utii wenye Adabu. Yako mambo mengi ambayo mwanamke kama mwanamke anapaswa kufanya. Lakini katika hayo mambo mengi, mambo makuu ni haya:
1. Kuomba. 2. Kufunga. 3. Kukarimu. Mwanamke amejaliwa Roho ya Huruma, na uvumilivu na staha, na ndio maana Mungu akaona ni vyema mwanamke aweze kuitwa mama, Abebe ujauzito, Azae, na kunyonyesha, MWANAMKE HAPA ALIONEKANA ANA HURUMA NA UVUMILIVU.
Hivyo basi ni lazima mwanamke uwe muombaji, Tena muombaji wa kuombea mambo mengi. Kujiombea Mwenyewe, kuiiombea Familia lakini na Taifa lako kwa ujumla. Lakini pia Maombi ya Kufunga ni Yamuhimu na yana nguvu. Kila mwanamke anapaswa kwua muombaji wa kufunga pia. Mwisho kabisa mwanamke anapaswa kuwa mtu wa kukirimu, sio mchoyo, sio mtu wa upendeleo wala ubaguzi. Lakini ni lazima mwanamke awe mkarimu. Kwa familia yake lakini na kwa watu wanaomzunguka. Mifano tunayo mingi ya wanawake wacha Mungu walivyofanya. Walikarimu, waliwavika watu nguo waliwapa watu chakula na kuuguza wenye majeraha. Kwa kufanya hivi kwa Kukarimu Unaweza Kumkarimu Mungu bila kujua. Hivyo ni wajibu wa Mwanamke kutokuwa Mchoyo. MWANAMKE UKIFANYA MAMBO HAYA LAZIMA UTAFANIKIWA SANA NA ROHO WA MUNGU ATAKUWA KARIBU NA WEWE.
Ni mimi rafiki yako
Ev. ELIMELECK S NDASHIKIWE
Tel:- 0767445846
0715445846
elimelck@gmail.com
0 comments:
Post a Comment