Pages

Subscribe:

Monday, 3 April 2017

UTOAJI WA SADAKA

Mungu amezungumuzia aina mbalimbali za sadaka. Zifuaatzoni aina ya hizo sadaka:

1. AINA ZA SADAKA KIBIBLIA

(i). SADAKA YA AMANI

KUTOKA 32:6….
[Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani,
watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze. ]…

Hizi ni aina ya sadaka za kusababisha amani
ndani ya nchi,familia. Ikikosekana amani mema hayawezi kukujia.

(ii). SADAKA YA DHAMBI.
Israeli wakitenda dhambi, sasdaka hii hutolewa.
Mnyama (ng’ombe au kondoo) huchinjwa ili kufanya dhambi za wana Israeli waachliwe kwenye.

HESABU 6:13-14 …
[Na sheria ya Mnadhiri ni hii, zitakapotimia hizo siku za kujitenga kwake; ataletwa mlangoni pa hema ya kukutania;
14 naye atasongeza sadaka yake kwa Bwana, mwanakondoo mmoja mume wa mwaka wa kwanza mkamilifu, kuwa sadaka ya kuteketezwa,

na mwanakondoo mmoja mke wa mwaka wa kwanza mkamilifu, kuwa sadaka ya dhambi,
na kondoo mume mmoja mkamilifu kwa sadaka ya amani,]….

(iii). SADAKA YA HATIA
Mtu anakuwa ametenda mambo yenye kumtia hatia, hata akataka kujiua.
Yuda Iskariote,
kwa mfano, alijisikia ndani mwake hatia kwa kumsaliti Bwana Yesu na mwishowe akajinyonga.

Wana wa Israeli pindi wanapojisika hatia ndani ya mmioyo yaowalikuwa wanatoa
sadaka ya hatia kwa ajili yao.

Cha muhimu ni kuziacha njia zako mbaya ili hatia ndani yako isiwepo. Yapo mapepo kabisa ya kutia hatia ndani yako.

Hayo ndiyo huinon’goneza masikio yako kukuambia kwamba dhambi uliyoifanya ni kubwa na kwamba haiwezi kusamehewa.

WALAWI 5:6-7 …..
[naye atalipa kwa ajili ya hilo alilolikosa katika kitu kile kitakatifu,
kisha ataongeza na sehemu ya tano, na kumpa kuhani;

naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa huyo kondoo mume wa sadaka ya hatia,
naye atasamehewa.]….

Kwa hiyo aina hii ya sadaka huleta upatanisho.

(iv). SADAKA YA HIARI
Ni sadaka itolewayo kwa Bwana kama hiari,ya kumshukuru Bwana kwa mambo aliyokutendea.

Haulazimiki kuitoa, ila ni kuonesha mapenzi mema kwa Bwana, kwamba unamjali,unapenda aendelee kukuhudumia.

Biblia inasema aheri kutoa kuliko kupokea.

HESABU 29:36….
[lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kusongezwa kwa moto,
harufu ya kupendeza kwa Bwana;

ng'ombe mume mmoja, na kondoo mume mmoja,
na wanakondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba;]…...

Itaendeleaaa........ 

Ni mimi rafiki yako
Ev. Elimeleck Ndashikiwe

0 comments:

Post a Comment