Pages

Subscribe:

Friday, 7 April 2017

JE, NI KWELI UMEOKOKA?

UHAKIKA WA WOKOVU

Yoh 3:16-18;
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanae wa pekee ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa
milele.

Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali
ulimwengu uokolewe katika yeye.

Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyehamini amekwisha kuhukumiwa; kwa
sababu hakuliamini jina la mwanawe wa pekee.

Luk 9:59;
Kwa maana mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, balikuziokoa,
Yoh 12:47;
Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi si mhukumu, maana sikuja niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.

1Tim 1:15;
Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa ya kwamba, Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.
1Tim 2:14;
Mungu … hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yalio kweli.

Efe 2:5,8
Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja
na Kristo, yaani, mmeokolewa kwa Neema, Kwa maana mmeokolewakwa Neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;

1Kor 1:18; Kwa sababu neno la Msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi, bali kwetutunaookolewa ni nguvu ya Mungu.

Mdo 4:10-12
Jueni nyote na watu wote wa Israel ya kuwa, kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,
ambaye ninyi mlimsulubisha, na Mungu akamfufua katika wafu … kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu.
Yeye ndiye jiwe lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limekuwa jiwe kuu la pembeni.

Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu
litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

Mdo 2:22-24, 36-40, 43-44, 47;

Enyi waume wa Israel, sikilizeni maneno haya:
Yesu wanazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara,
ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;

Mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani,
ninyi mkamsulubisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua; ambaye Mungu alimfufua,

akifunga uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao… Basi nyumba yote ya Israel nawajue yakini ya
kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulubisha kuwa Bwana na Kristo. Walipoyasikia hayo wakachomwa mioyo yao,
wakamwambia Petro na mitume wengine,

Tutendeje, ndugu zetu? Petro akamwambia,
Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu,
na kwa watu wote walio mbali, na kwa watu wote watakao itwa na Bwana Mungu wetu wamjie.

Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, jiokoeni na
kizazi hiki chenye ukaidi … Kila mtu akaingiwa na hofu
ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume.

Na wote walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika …

Wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku
kwa wale waliokuwawakiokolewa.

(Mdo 2:22-24, 36-40, 43-44, 47) Rum 10:9-10;

Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, nakuamini mioyoni
mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

Mdo 16:30-31;
Kisha akawaleta nje akasema. Bwana zangu, Yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?

Wakamwambia, mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.

2Kor 6:2
Kwa maana asema, wakati uliokubalika nalikusukia, siku ya wokovunalikusaidia;
Tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; Tazama, siku ya wokovu ndio sasa.

Ebr 2:1-3
Kwa hiyo, imetupasa kuangalia zaidi hayo yaliyosikiwa, tusije tukayakosa, kwa maana,
ikiwa lile neno lililonenwa na malaika, lilikuwa imara,
na kila kosa na uasi, ulipata ujira wa haki.

Sisi je!
Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii?
Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukadhibitika kwetu na wale wanaosikia.

TUMEOKOLEWA KUTOKA KWENYE NINI?

1. TUMEOKOLEWA KUTOKA KATIKA NGUVU YA DHAMBI / UASI

Maana sijui nifanyalo; kwasababu lile nilipendalo silitemdi;
Bali lile nilichukialo ndilo nilitendalo … naikiri kuwa ile sheria ni njema.
Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo,
bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.

Kwa maana najua kuwa, ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema,
kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati …
lakini katika viungo vyangu, naona sheria iliyo mbali,
inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.

Ole wangu, masikini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

NAMSHUKURU MUNGU, KWA YESU KRISTO BWANA WETU.

(Rum 7:15-15
“Nanyi mlikuwa wafu kwasababu ya makosa na dhambi zenu. Ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya
ulimwengu huu, na kwa kumfuaata Mfalme wa uwezo wa anga,

roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;
ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao,
katika tama za miili yetu, tulipo yatimiza matendo ya mwili na nia, kukawa kwa tabia yetu watoto wahasira kama na hao wengine.

Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda;
hata wakati ule tulipokuwa wafu kwasababu ya makosa yetu;

alituhuisha pamoja na Kristo;
yaani, mmeokolewa kwa neema akatufufua pamoja naye akatuketisha pamoja
naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu.”

Efe 2:1-1-2-6
“Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria
ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti”.

Rum 8:1-2
… “tukijua neno hili, ya kuwa, utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike.

Tusitumikie dhambi tena … Basi dhambi isitawale ndani ya miili yenu …
kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi.

Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mli-itii
kwa mioyo yenu, ile namna ya elimu (Injili ya wokovu),
ambayo mliwekwa chini yake.

Na mlipokwisha kuwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki … kwa maana
mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki.

Ni faida gani mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayo yatahayarikia sasa?

Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti.
Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu,
mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima. … Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa.

Ezek 28:20-23
… kwa maana mshahara wa dhambi nimauti wa milele,
bali karama (zawadi) ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Rum 6:23

Pia soma;
Tito 2:11-12;
Tito3:3-4; 2Kor 4:3-4;
Efe 4:18-19;
1Tim 1:13-1

5 TUMEOLOKEWA KUTOKA KATIKA NGUVU ZA GIZA.
“Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake”.
(Kol 1:13)

“Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa
kwa mwili wenu, mliwafanya hai pamoja naye, akisha kutusamehe makosa yote; akisha
kuifuata ile hati iliyoandikwa kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu;

akaiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani;
akiisha kuzivua enzi za mamlaka, na kuzifanya kwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia
katika msalaba huo”.
Kol 2:13-15.

Tazama,
nimwewapa amri ya kukanyaga nge na nyoka na nguvu zote za yule adui, wala hakuna
kitu kitakachowadhuru.
Luk 10:19.

Pia soma;
Math 27:45,50-54;
Ebr 2:14-15;
Luk 11:21-22; Yoh 19:28-30

3.TUMEOKOLEWA KUTOKA KATIKA LAANA YA TORATI.

“Fahamuni basi, yakuwa wale walio na imani,
hao ndio wana wa Ibrahim.
Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani
kwamba Mungu atawahesabia haki mataifa kwa imani,
lilimhubiri Ibrahim habari njema zamani, kusema, katika wewe mataifa watabarikiwa.

Basi hao walio na imani hubarikiwa pamoja na Ibrahim aliyekuwa mwenye imani.
Kwa maana wale wale wote walio wa matendo ya sheria,
wako chini ya laana maana imeandikwa amelaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati, ayafanye.

Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria;
kwa sababu mwenye haki ataishi kwa imani. Na torati haikuja kwa imani, bali ,ayatendaye hayo, ataishi katika hayo.

Kristo alitukomboa katika laana ya Torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu;
maana imeandikwa , amelaaniwa kila mtu aangikwae juu ya msalaba; ili kwamba baraka ya Ibrahim iwafikirie mataifa
katika Yesu Kristo,
tupate kupokea ahadi ya roho kwa njia ya imani”.

Gal 3:7-14, 23-29
“Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.

Rum 10:4) Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu.
Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka”.

(Ebr 8:13
Basi twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria
… Basi,
mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au
mwandamo wa mwezi, au Sabato;
Rum 3:28; Kol 2:16.

Pia soma
Mdo 15:1-10-29;
Gal 2:16;
Rum 8:3;
Rum 7:12,14-16;
Rum 8:1-4;
Yer 31:31-34

4. TUMEOKOLEWA KUTOKA KATIKA DUNIA (UOVU WA DUNIA).

“Neema na iwe kwenu, naamani, zitokazo kwa Mungu Baba,
na Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu,
ili atuokoe na dunia hii mbovu, iliyopo sasa.

Gal 1:3-4
“Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako.
Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa,
ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.

Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda
kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza;
wala hapana mmoja wapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.

Na sasa naja kwako;
ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.

Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umechukia;
kwa kuwa wao si waulimwengu, kama mimi
nisivyo na ulimwengu.

Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu;
basi uwalinde na yule muovu.

Wao sio wa ulimwengu, kama mimi nisivyo waulimwengu.
Uwatakase kwa ile kweli;
neno lako ndio kweli kama vile ulivyonituma
mimi ulimwenguni, nami hivyohivyo naliwatuma hao ulimwenguni.

Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe,
ili na hao watakaswe katika kweli”.
Yoh 17:11-19 (14-16)

Pia Yoh 8:21-24 (23);
1Kor 5:9-11; Rum 12:1-2

5. TUMEOKOLEWA KUTOKA KATIKA JEHANUM YA MOTO.

“Kwahiyo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji ikaangamia, lakini mbingu
za sasa na nchi, zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu,
na kuangamia kwao wanadamu wasio mcha Mungu. Lakini wapenzi, msilisahau neno hili

… Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee,
bali wote wafikie toba.

Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi; katika siku hiyo, mbingu zitatoweka
kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa,
na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea..

Basi kwakuwa vitu hivi vyota vitafumuliwa,
hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani?

Katika mwenendo mtakatifu na utauwa! Mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza;
ambayo katika hiyo, mbingu zitafumuliwa na zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka.

Lakini kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo
haki yakaa ndani yake”.
2 Pet 3:6-13

“Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, nayeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake,
na mahali pao hapakuonekana.

Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi;
na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima;
na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu,
sawasawa na matendo yao.

Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake;
Na mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadri ya matendo
yake mauti za kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto.

Hii ndio mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
Naiwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa
katika lile ziwa la moto.”

Ufu 20:11-15
“Amini, amini nawaambia, yeye asikiaye neno
langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna na uzima wa milele; wala haingii hukumuni,
bali amepita kutoka mauti kuingia uzimani”.
Yoh 5:24.

Pia
Luk 10:20;
Fil 4:3; 1Yoh 3:14;
Rum 5:6-9;

6. TUMEOKOLEWA KUTOKA KATIKA MAGONJWA.
Nanyi mtamtumikia Bwana Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako na maji yako.

Nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.

Kut 23:25
… Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote, wala hatatia juu yako maradhi yeyote,
mabaya uyajuayo …”

Kumb 7:15
Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo,
akawatoa pepo kwa jina lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi (wagonjwa).

Ili litimie lile neno lililonenwa na Nabii Isaya akisema;
“Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu na kuyachukuwa magonjwa yetu.”

Math 8:16-17
“Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji,
akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote, na udhaifu wa kila aina”.

Math 9:35
“ … Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili,
akawapa amri juu ya pepo wachafu; wawatoe na kupoza, magonjwa yote na udhaifu wa kila aina

Math 10:1
Yeye mwenyewe alizichukuwa dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa
wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki;
Na kwa kupigwa kwake mliponywa.

1Pet 2:24
“Hakika ameyachukuwa masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu ….

Bali alijeruliwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu.

Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake; Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Isa 53:4 -5
Damu ya Msalaba iliyoondoa dhambi, ndiyo iliyoondoa magonywa pia.

Yatupasa kuyaona magonjwa kama tunavyoiona dhambi.
Hatupaswi kuyaona kuwa ni sehemu ya maisha yetu.

Magonjwa ni matokeo ya anguko la mwanadamu katika dhambi. Tukiisha okolewa
toka dhambini, yatupasa kuokolewa kutoka katika magonjwa pia.

Afya njema ni matunda ya msalaba kama ilivyo wokovu.

Tunatakiwa kuchukia magonjwa kama tunavyochukia dhambi, kwasababu yote haya,
ni kazi za shetani.
Yatupasa kuzikataa na kuzivunja katika maisha yetu.

Kifo cha Yesu, kitakuwa hakina maana kamili,
kama tutaokolewa katika dhambi, halafu tubaki katika magonjwa pia, wakati Yesu aliyefia dhambi,
ndiye aliyefia magonjwa pia.

Msalaba ulifanya vyote,

uliondoa dhambi na magonjwa pia.

“Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu na kuyachukuwa magonjwa yetu.”
Math 8:16-17.

      Mungu akubariki mtumishi wa Mungu.
Wewe ni mshindi.

Your beloved
         Ev. Elimeleck S Ndashikiwe.

0 comments:

Post a Comment