UTANGULIZI
Jina la kitabu hiki
Malaki
maana yake ni “Mjumbe wangu” au “Aliyetumwa na”.
Inawezekana likawa ndilo jina la unabii au kitambulisho maalumu kuwa mwandishi ni mjumbe halisi atokaye kwa Mungu
(2:7; 3:1).
Malaki hataji wakati wa kutoa ujumbe wake.
Inaelekea ujumbe huu ulitolewa wakati fulani wa
matengenezo ya
Ezra na Nehemia,
kwa sababu hali na matendo ambayo yanazungumzwa yafanana na ya nyakati hizo.
Wayahudi waliporudi kutoka utumwani Babeli wakiongozwa na Zerubabeli na Yoshua
walikuwa na hamasa ya kutengeneza upya na kutegemeza taifa lao kidini na kisiasa.
Lakini muda mfupi walilegea (tazama Utangulizi wa Hagai).
Kizazi kilichofuata hakikuwa na uongozi wenye kuenzi kazi nzuri ya viongozi waliowatangulia.
Watu wakarudi nyuma kiroho, hata wakatafsiri vibaya ahadi za Mungu.
Kurudi tena nchini mwao na kujenga hekalu upya walikutafsiri kuwa ni nyenzo ya
kupata enzi za Masihi.
Kwa kuwa waliyojiwekea wenyewe hayakutokea wakawa na mashaka juu ya ahadi za Mungu kwao,
waliacha ibada, ndoa za mseto kidini na talaka zikahalalika
2:10-12).
Walipopata matatizo walilalamika kuwa Mungu hakubali ibada zao (2:13-16), waliona kuwa Mungu hawatendei haki (2:17).
Malaki
anaweka mambo sawa kwamba Mungu ni mwaminifu kwa agano lake na hivyo basi hawana budi kujilaumu wao wenyewe.
Hii ni kwa sababu dhambi zao zimekuwa kizuizi cha upendo na baraka za Mungu. Malaki ametabiri
“Siku ya BWANA” ambapo waovu watahukumiwa; kwa wanyenyekevu haki itatawala na wanaomcha Mungu watabarikiwa.
YALIYOMO:
1. Upendo wa Mungu kwa Israeli, Sura 1:1-5
2. Uovu wa viongozi wa taifa, Sura 1:6–2:17
3. Mjumbe wa Bwana, Sura 3 4. Siku ya Bwana, Sura 4
0 comments:
Post a Comment