Machukizo ya aina yoyote ndani ya nyumba ya Mungu, yanamnyima Mungu fursa ya kuachilia miujiza kwa watu wake.
Lkn pia kunazuia utekelezaji wa Ahadi za Mungu.
Miujiza ya Mungu ya uponyaji kama wakati wa Yesu na wakati wa mitume haiwezi
kuonekana dhahiri kwa watu wanaoruhusu machukizo kwa watu wa Mungu na ndani maskan i(nyumbani) yake Mungu, U
takuta watu wanashughulika na mapepo tu kila siku lakini miujiza ya vipofu kuona,
viziwi kusikia, viwete kutembea, mabubu kuongea,
wenye kigugumizi kuongea sawasawa, wenye makengeza kuponywa na kila namna ya miujiza mingine kama nyakati za
mitume havionekani.
Mamlaka waliyokuwa nayo mitue ya kumwambia kiwete
‘ Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende
( MATENDO 3;6 )’.
Mamlaka haiko leo kwa watumishi wengi sababu ni kwamba wameruhusu machukizo
nab ado tu wanaendelea kuyatetea kwa bidii nyingi.
YOHANA 2:13-17
Yesu Kristo alipokuta watu wamegeuza hekalu soko alichukizwa mno na kitendo kile
ndipo akaamua kupundua meza zao,
na kuwaondoa wote hekaluni kwa kutumia kikoto.
Aliuliza,
Yesu hakuyavumilia machukizo nyumbani mwa baba yake. Watumishi wa
Mungu leo wanatakiwa kufuata msingi aliouweka BWANA YESU na si kuyaacha machukizo eti kwa visingizio vya kulinda kundilisipungue,
hatuwasaidii washirika wetu.
Tunapaswa kumwondoa mwovu miongoni mwetu ili wengine wajifunze kukaa katika viwango vyote vya neno la Mungu.
( iv ). Wanawake wanapaswa kufunika kichwa wakiwa katika ibada. Wanapaswa kufunika wakiwa kanisani, wanapofanya huduma
yoyote ya kiroho mfano, kuomba, kuhutubu au kuhubiri.
( 1 WAKORITHO 11:4-5,7,10,13
‘ Sheria inayomkataza mwanamume kumwomba Mungu akiwa amevaa kofia pia
inayomkataza kuvaa kofia kanisani hiyo hiyo ndiyo inayomtaka mwanamke afunike
kichwa kwa ajili ya Malaika.
Wanaosema ilikuwa desturi za Wakorintho hawayaelewi maandiko vizuri.
Biblia inasema
‘ Imempasa mwamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani kwa ajili ya Malaika”.
Angalia vizuri neno
‘ imempasa=lazima”.
Hakuna Biblia ya Wakorintho pekee yao,
tukichambua Biblia hivyo sisi Watanzania
hatutabaki na kitabu chichote.
Yote yaliyoandikwa,
yaliandikwa kwa ajili yetu wote
WARUMI 2;16
Mungu atayahukumu mataifa yote kwa injili hiyohiyo
Tukitaka kuziona nguvu za Mungu waziwazi lazima tuwe mbali na machukizo ya aina yoyote.
Mafuta ya Mungu yanakuwa juu ya mtu anayechukia machukizo
WAEBRANIA 1:9 .
Mtu ambaye anatetea machukizo yaliyomo ndani ya maskani ya Mungu lakini
akifanya miujiza au maajabu lazima tujiulize ni nguvu ipi inatenda kazi hapo?
Mungu mwenyewe anasema kuwa mahali penye machukizo,
Mkono wake wa kuponya hauwezi kuwepo
2 NYAKATI 36:14 ,
Pia hawezi kupakwa mafutaNA Mungu
WAEBRANIA 1:9 .
Nyakati hizi tulizonazo watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli, wanapenda kudanganywa.
Paulo mtume alitabiri juu ya nyakati hizi jinsi watu watakavyotafuta waliu wa kuwafundisha
uongo na kuikataa kweli ya neno la Mungu
( 2 timotheo 4:3-4).
Hata wakati wa nabii Isaya walikuwepo watu waliotafuta walimu wengine wa mbali
na Isaya aliyehubiri kweli yote. Walisema kuwa wanataka mafundisho laini yadanganyayo
ISAYA 30;9-10 .
Kama tunataka kuishi na Mungu milele hatuna budi kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha
kuziacha na kuwa tayari kuyafuata maagizo yote ya Neno la Mungu
ZABIRI 119:6 .
Tunasafisha njia zetu kwa kutii neno la Mungu na
siyo walimu wetu wanaotufariji tuendelee kufanya machukizo mbele za Mungu
ZABURI 119;9.
Walimu wanaowatia moyo watu ili waendelee
kuvaa mapambo na suruali kwa wanawake wote ni wafariji wa kutaabisha
AYUBU 16:2.
Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?
Ni utakatifu
WAEBRANIA 12:14.
Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge
UFUNUO 21:27.
Kinyonge ni kipi?
Ni yule anayetenda dhambi.
Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!
Je, wewe ni mtakatifu?
Jibu ni la!
Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini;
hivyo wewe pia ni mnyonge,
hufai kuingia mbinguni.
Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo,
ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni
MITHALI 28:13;
YOHANA 14:6.
Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?
Najua uko tayari.
Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;
“Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.
Sistahili kuingia mbinguni.
Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.
Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.
Bwana Yesu niwezeshe.
Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.
Amen”.
Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.
Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii,
hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu lililo jirani na wewe mahali ulipo.
MUNGU AKUBARIKI !!! . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
Ni mimi rafiki yako
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe
+255715445846 &
+255684485460
0 comments:
Post a Comment