Pages

Subscribe:

Sunday, 19 March 2017

BARAKA ZAKO

Chochote ukitakacho kutoka kwa MUNGU kiamuru leo kikufuate.

Wewe mteule wa MUNGU unayo mamlaka ya kuomba katika jina la YESU KRISTO na baraka ikakufuata.

Kumbuka baraka ya MUNGU ni muhimu sana kwako na baraka hiyo ni tofauti na baraka za kipepo.


Mithali 10:22
'' Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo.''


Iamuru leo baraka ya MUNGU ikufuate.
Hakikisha tu una uhusiano mzuri na MUNGU.
Hakikika unaishi maisha matakatafu na hakikisha wewe ni mtii kwa MUNGU katika utoaji
wa fungu la kumi na sadaka.

Kama ni hivyo basi iamuru baraka yako uitakayo kutoka kwa MUNGU ikufuate.
Inawezekana
Maombi yako ya leo ni muhimu sana.


Isaya 45:23
'' Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba,
na kukata-kata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya
kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, MUNGU wa Israeli.''

MUNGU naweza kukupa hazina za gizani ambazo wabaya wako walificha ili usipate.

Leo amuru baraka zako zikufuate.

Kupitia maombi yako hakika baraka yako itakufuata kwa jina la YESU KRISTO.
Amuru uponyaji wa mwili wako ukufuate.
Amuru kuwa mzima.


Zaburi 103:3-6
'' Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi,
Akutia taji ya fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai;

BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki, Na hukumu kwa wote wanaoonewa.''


Leo hakikisha unaziandika baraka zako kisha
tubu kwa Bwana YESU na anza kuiamuru baraka moja
baada ya nyingine ikufuate.

Hakika baraka yako ni yako tu.

Mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi,

HAIKANUSHIKI hiyo.


Ni mimi ndugu yako Ev. Elimeleck Ndashikiwe



0 comments:

Post a Comment