SANDUKU LA AGANO NYAKATI ZA AGANO JIPYA
Bwana Mungu ameamuru kwa sasa yawepo masanduku mbali mbali ya Agano
kwa kazi yake hapa duniani, lisiwepo moja tu,
kama wakati wa Agano la Kale.
Kumbe kwa sasa, RP, AP,MP, Shepherds,
Shepherd on Training, Potential Shepherds,
na watumishi wengine wa Bwana wamefanyika kuwa Sanduku la Agano pale walipo.
Mungu aliona hatari iliyopo kwa kuwepo Sanduku la Agano moja tu katika Nyakati kama hizi.
Ndiyo maana kila mmoja wetu anageuzwa kuwa Sanduku la Agano kwa Jina la Yesu….
1 KORINTHO 3:16…
[Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?]…
Uwezo wa Sanduku hili kukaa kwa mtu ni yeye
mwenyewe kuruhusu uwezo huu kwa kulibebea Sanduku la Agano.
Enzi ya
Agano la Kale, waisraeli walilibeba Sanduku la Agano.
Kwa sasa hekalu la Mungu ambalo ni takatifu
lipo ndani mwako na hayupo mtu wa kuligusa katika Jina la Yesu. Endapo atakuwepo mtu wa kuligusa, Bwana atamharibu.
1KORINTHO 3:17…...
[Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo.
Kwa maana
hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.]…
Barikiwa mtu wa Mungu.
Ni mimi Ndugu yako
Ev. Elimeleck Ndashikiwe
0 comments:
Post a Comment