Leo omba ukiamuru baraka zako zikufuate.
Jambo muhimu kabla ya yote hakikisha uhusiano wako na Bwana YESU ni mzuri ndipo uombe.
Wakati mwingine baraka fulani haijaja kwako kwa sababu hujaiamuru ije kwako kwa njia ya maombi au maombi ya kufunga.
Kumb 28:8
'' BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia
mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako. ''
MUNGU huiamuru baraka ije kwako kwa kukufungulia mlango wa baraka hiyo kupita na kuja kwako.
Ona Mfano hapa ambapo MUNGU aliamuru baraka ya chakula cha mbinguni ishuke kwa wana wa Israeli.
Biblia inasema
Zaburi 78:23-25
'' Lakini aliyaamuru mawingu juu; Akaifungua milango ya mbinguni; Akawanyeshea mana ili wale; Akawapa nafaka ya mbinguni.
Mwanadamu akala chakula cha mashujaa;
Aliwapelekea chakula cha kuwashibisha.''
Lakini ni muhimu kujua kwamba kama uhusiano wako na MUNGU uko vibaya hakika
MUNGU hataiamuru baraka yako ije kwako kupitia maombi yako.
Biblia inasema
'' Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka,
hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu,
na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona ubaya.
Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.
-Isaya 59"1-4''
Mkono wa MUNGU wa baraka haukupungua hata usiweze kukubariki ila maovu yako ndio yamekufarakanisha wewe
na Muumba wako hata hukupokea baraka zako..
Ni muhimu sana kutengeneza na MUNGU ndipo uzihitaji baraka zake.
Bwana YESU alitupa kanuni ya kupokea kutoka ulimwengu wa roho.
Mathayo 7:7-8
'' Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona;
bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona;
naye abishaye atafunguliwa.''
Kwa maana nyingine unaweza kusema hivi ombeni nanyi mtapokea ila msipoomba hamtapokea
maana hamukuomba.
Baraka zako ni zipi hata usipokee?
Nakupenda msomaji wangu, endelea kubarikiwa na blog yangu hii.
By Ev. Elimeleck Ndashikiwe
Ndugu leo omba ukiziamuru baraka zako zikufuate na utazipokea kwa jina la YESU KRISTO.
MAMBO KUMI YANAYOWEZA KUWACHELEWESHA WACHUMBA KUFUNGA NDOA. Bwana YESU
KRISTO
-
Na Peter & Jemimah Mabula Watendakazi katika Shamba la MUNGU wa
Mbinguni Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.Karibu upate maarifa
ya kukusaidia kat...
0 comments:
Post a Comment