TOBA Toba ni tendo la kiimani la kuungama dhambi na maovu yote yaliyokwisha kufanyika kwa nia ya kujenga upya mahusiano na Mungu aliye hai sawasawa na Neno lake. Maana dhambi ni uasi hivyo atendaye dhambi hujitenga na rehema za Mungu. “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.” Mithali 28:13 Yako malango na milango iliyofungwa kwa watu wa Mungu kwa sababu ya dhambi. Maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Palipo dhambi na makosa panahitaji toba si vinginevyo.
Watu wengi wameruka ufunguo huu matokeo yake wamefunga na kuomba hawakupata majibu kwa kuwa Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu ndicho atakacho vuna. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” Warumi 6:23
Tunajifunza kwa mtumishi wa Mungu Danieli baada ya kuvisoma vitabu vyenye maneno ya Mungu alipata ufahamu utokanao na Neno, akaamini sawasawa na Neno la Mungu jambo la tatu akachukua hatua ya kutubia maovu na dhambi zake na za Taifa lake. Ili kwa njia ya toba BWANA awafungulie milango na malango yaliyokuwa yamefungwa kwa nguvu za miungu ya Babeli. “Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo; katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii, yaani, miaka sabini. Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu. Nikamwomba BWANA, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake; tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako; wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi. Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa. Ee Bwana, kwetu sisi kuna haya ya uso, kwa wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, kwa sababu tumekutenda dhambi. Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi, wala hatukuitii sauti ya BWANA, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii. Naam, Israeli wote wameihalifu sheria yako, kwa kugeuka upande, wasiisikilize sauti yako; basi kwa hiyo laana imemwagwa juu yetu, na uapo ule ulioandikwa katika sheria ya Musa, mtumishi wa Mungu; kwa sababu tumemtenda dhambi. Na ye ameyathibitisha maneno yake, aliyoyanena juu yetu, na juu ya waamuziwetu waliotuamua, kwa kumletea mambo maovu makuu; maana chini ya mbingu zote halikutendeka jambo kama hili, lilivyotendeka juu ya Yerusalemu. Kama ilivyoandikwa katika sheria ya Musa, mabaya haya yote yametupata lakini hata hivyo hatukumwomba BWANA, Mungu wetu, atupe fadhili zake, ili tugeuke na kuyaacha maovu yetu, na kuitambua kweli yake. Basi BWANA ameyavizia mabaya hayo, akatuletea; maana BWANA, Mungu wetu ni mwenye haki katika kazi zake zote azitendazo; na sisi hatukuitii sauti yake. Na sasa, Ee Bwana Mungu wetu, uliyewatoa watu wako hawa katika nchi ya Misri kwa mkono hodari, ukajipatia sifa, kamailivyo leo; tumefanya dhambi, tumetenda maovu. Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi, hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe na kuuacha mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu; maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamepata kulaumiwa na watu wote wanaotuzunguka. Basi sasa, Ee Mungu wetu, yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya Bwana. Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi. Ee Bwana, usikilize, ukatende, usikawie; kwa ajili yako wewe, Ee Mungu wangu; kwa sababu ya mji wako na watu wako wanaitwa kwa jina lako. Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za BWANA, Mungu wangu, kwa ajili yam lima mtakatifu wa Mungu wangu; naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni. Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu. Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya. Muda wa majuma sabini umuamuriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na akuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu. Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba, na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu. Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika , na hata mmwisho ule vita vitakuwepo; ukiwa umekwisha kukusudiwa. Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.” Danieli 9:1-27 Danieli anaanza kwa Kuungama ili apate kufungua Malango na Milango iliyofungwa. Unapotubu dhambi na kuziacha ni Mlango wa kuinuliwa, Hata kama umetupwa chini, Maandiko yanasema wazi Mtu mwaminifu atakuwa na Baraka tele na Malango yake yatafunguliwa daima. “Haya njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theruji, zijapokuwa nyekundu kama bendera zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi, bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga maana kinywa cha BWANA kimenena haya.” Isaya 1:18-19 Angalia pia watu wa Ninawi, walivyofungua Malango yao kwa nguvu ya TOBA, maana Walilisikia Neno, Wakaliamini na Kutubu, Naye Yehova akawafungua. Walibatilisha lango la mauti kwa njia ya toba. Hivyo toba ina nguvu katika Mungu hata kuangusha ngome za mauti na kuzimu. Mfalme wa Ninawi aligeuza hasira ya Mungu juu yake na watu wake pale alipoomba rehema za Mungu kwa njia ya toba. Nasi tukiomba rehema kwa ajili yetu na watoto wetu hakika BWANA ni mwingi wa rehema si mwepesi wa hasira, yeye husamehe wote wanao jinyenyekeza kwake. “Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu akatangaza habari katika mji wa Ninawi kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng’ombe, wala makundi ya kondoo, wasile wala wasinywe maji bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi na kuiacha hasira yake kali ili msiangamizwe? Mungu akaona matendo yao ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akaghairi neno lile baya ambalo alisema atawatenda, asilitende.” Yona 3:6-10 TOBA ilirejesha upya uhai kwa watu wa Ninawi. Nasi Kanisa hatuwezi kufunguliwa Malango na Milango pasipo kufanya TOBA ya kweli. “Tazama mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.” Isaya 59:1-2 Lazima uiondoe dhambi katikati yako kwa Kutubu na Kuungama mbele za Mungu. Ufunguo huo wa TOBA ndio unaotupa Uwezo na Ujasiri wa kupaingia Patakatifu pake Mungu aliye hai kwa jinsi ya Imani. Ni lazima MKRISTO UZAE MATUNDA YAPASAYO TOBA. “Basi zaeni matunda yapasayo toba.” Mathayo 3:8” Wokovu maana yake ni Kutengwa mbali na dhambi. Hatuwezi kufunguliwa Milango ya Baraka na Ustawi kama hatutajitenga na maovu. “Ndipo Yona akamwomba BWANA Mungu wake, katika tumbo la yule samaki, akasema, Nalimlilia BWANA kwa sababu ya shida yangu, naye akaniitikia; katika tumbo la kuzimu naliomba. Nawe ukaisikia sauti yangu. Maana ulinitupa vilindini, ndani ya moyo wa bahari, gharika ya maji ikanizunguka pande zote, Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu. Nami nikasema nimetupwa mbali na macho yako, lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu. Maji yalinizunguka hata nafsini mwangu, Vilindi vilinizunguka, mwani ulikizinga kichwa changu, Nalishuka hata pande za chini za milima, Huyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele. Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee BWANA, Mungu wangu, Roho yangu ilipozimia ndani yangu, nalimkumbuka BWANA; maombi yangu yakakuwasilia katika hekalu lako takatifu. Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo, Hujitenga na rehema zao wenyewe; lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukurani, nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa BWANA. BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.” Yona 2:1-10 Nabii Yona alipo Omba toba na Rehema akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, BWANA akamwinua tena, akamfungulia Milango na Malango ya Utumishi. Angalia pia Samsoni pamoja na kumkosea Mungu kwa kiwango kikubwa kwa uzinzi mpaka akatobolewa macho, Lakini alipo Omba TOBA, Jehova Elshadai, Mungu anayetenda zaidi ya tarajio akamwinua tena. “Samsoni akaenda Gaza, akaona huko mwanamke kahaba, akaingia kwake. Watu wa Gaza wakaambiwa yakwamba, huyo Samsoni amekuja huku, wakamzingira wakamvizia usiku kucha penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, na tungoje mpaka mapambazuko, ndipo tutamwua. Basi Samsoni akalala hata usiku wa manane, akaondoka katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la mji na miimo yake miwili, akaing’oa pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hata kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni. Ikawa baada ya hayo akampenda mwanamke mmoja katika bonde la Soreki, jina lake akiitwa Delila. Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja. Delila akamwambia Samsoni, Tafadhali uniambie asili ya nguvy zako nyingi, na jinsi uwezavyo kufungwa, ili uteswe. Samsoni akamwambia, wakinifunga kwa kamba mbichi saba ambazo hazija kauka bado, hapo ndipo nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamletea kamba mbichi saba zisizokauka, naye akamfunga nazo. Na yule mwanamke alikuwa na watu katika chumba cha ndani, wakimwotea. Basi akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakuja. Ndipo akazikata zile kamba kama vile uzi wa pamba ukatwavyo ukiguswa na moto. Basi hiyo asili ya nguvu zake haikujulikana. Delila akamwambia Samsoni, Tazama, umenidhihaki na kuniambia uongo; sasa tafadhali, niambie, wawezwa kufungwa kwa kitu gani? Akamwambia wakinifunga tu kwa kamba mpya ambazo mtu hakufanya kazi nazo, hapo ndipo nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. Basi Delila akatwaa kamba mpya akamfunga nazo, akamwambia, Wafilisti wanakuji, Samsoni, na wale wenye kuotea walikuwa katika chumba cha ndani. Naye akazikata, akazitupa kutoka mikononi mwake kama uzi. Delila akamwambia Samsoni, hata sasa umenidhihaki, umeniambia maneno ya uongo; niambie sasa, waweza kufungwa kwa kitu gani? Akamwambia, ukivifuma hivi vishungi saba vya nywele za kichwa changu katika mtande wa nguo. Basi akazifunga kwa msumari, akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Naye akaamka usingizini, akaung’oa ule msumari, na ule mtande. Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi. Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa. Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, wembe haukupita juu ya kichwa change kamwe; maana mimi nimekuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku nmara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao. Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka. Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA amemwacha. Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza. Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake. Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu. Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu. Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili. Samsoni akamwambia yule kijana aliyemshika mkono, niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate kuzitegemea. Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza. Samsoni akamwita BWANA, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili. Kisha Samsoni akazishika nguzo mbili za katikati ambazo nyumba ile ilikaa juu yake, akazitegemea, moja kwa mkono wake wa kuume na moja kwa mkono wake wa kushoto. Samsoni akasema; na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. Basi wale watu waliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko wale waliowaua wakati wa uhai wake. Ndipo ndugu zake, na watu wote wa nyumba ya baba yake wakatelemka, wakamtwaa wakamchukua, wakamzika kati ya Sora na Eshtaoli, katika kiwanja cha kuzikia cha Manoa baba yake. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka ishirini.” Waamuzi 16:1-31 TOBA ilimfanya Samsoni ahesabiwe kuwa miongoni mwa Mashujaa wa Imani maana wokovu aliouleta siku ya kufa kwake ulikomesha ufalme wa Wafilisti kwa kuwa aliwaangamiza kuanzia mdogo mpaka mfalme wao. “Nami niseme nini tena? Maana wakati usingetosha kuleta habari za Gidioni na Baraka na Samsoni na Yefta na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya samba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga, walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.” Waebrania 11:32-34 Israeli wakafanya dhambi kwa kukosa uaminifu katika kitu kilichowekwa wakfu. Walipokwisha kuangusha mji wa Yeriko na kuta zake na wakauingia mji wa Ai. Akani mwana wa Zabdi mwana wa Zera wa kabila la Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu, hasira ya BWANA ikawaka juu ya wana wa Israeli kutokana na kutokuwa waaminifu katika maagizo ya Mungu aliye hai. “Lakini wana wa Israeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya BWANA ikawaka juu ya wana wa Israeli. Kisha Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko mpaka mji wa Ai, ulio karibu na Bethaveni, upande wa mashariki wa Betheli, akawaambia, akisema, pandeni juu mkaipeleleze nchi, basi wakapanda juu wakaupeleleza Ai. Wakarejea kwa Yoshua wakamwambia, wasiende watu wote, ila waende watu kama elfu mbili, tatu, wakupige Ai; usiwataabishe watu wote kwa kuwaendesha huko; maana watu hao ni wachache tu. Basi watu wakaenda huko wapata elfu tatu tu; nao wakakimbia mbele ya watu Ai. Watu wa ai wakawapiga watu kama thelathini na sita; wakawafuatia kutoka mbele ya mlango mpaka Shebarimu, wakawapiga huko kwenye matelemko; mioyo ya watu ikayeyuka, ikawa kama maji. Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA hata jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao. Yoshua akasema, Ee Bwana MUNGU, kwa nini umewavusha watu hawa mto wa Yordani, ili kututia katika mikono ya Waamori, na kutuangamiza? Laiti tungelikuwa radhi kukaa ng’ambo ya Yordani Ee Bwana, niseme nini baada ya Israeli kuwapa visogo adui zao? Maana Wanaani na wenyeji wote wan chi hii watasikia habari hii, naowatatuzingira, na kulifuta jina letu katika nchi. Nawe utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu? BWANA akamwambia Yoshua, Haya! Inuka, mbona umeanguka kifudifudi hivi? Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu, tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe. Ndiposa wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele ya adui zao; wakawapa visogo adui zao, kwa sababu wamelaaniwa; mimi sitakuwa pamoja nanyi tena, msipokiharibu kitu kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu. Haya! Inuka, uwatakase watu, ukaseme, Jitakaseni, mwe tayari kesho; maana BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi; kitu kilichowekwa wakfu kiko katikati yako, Ee, Israeli; huwezi kusimama mbele ya adui zako, hata mtakapokiondoa kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu. Basi asubuhi mtaletwa karibu nami kabila kwa kabila; kisha itakuwa ya kwamba kabila ile atakayoitwaa BWANA itakaribia jamaa kwa jamaa; na jamaa ile atakayoitwaa BWANA itakaribia nyumba kwa nyumba; na nyumba ile atakayoitwaa BWANA itakaribia mtu kwa mtu. tena itakuwa ya kwamba yeye atakayetwaliwa, naye anacho kitu kile kilichowekwa wakfu, akateketezwa kwa moto, yeye na vitu vyote alivyo navyo; kwa sababu amelivunja agano la BWANA, na kwa sababu ametenda upumbavu katika Israeli. Basi Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, akawasogeza Israeli kabila kwa kabila; kabila ya Yuda ikatwaliwa. Akazisogeza jamaa za Yuda, akitwaa jamaa ya Wazera; akaisogeza jamaa ya Wazera mtu kwa mtu; Zabdi akatwaliwa. Akawasogeza watu wa nyumba yake mmoja mmoja; na Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda akatwaliwa. Yoshua akamwambia Akani, mwanangu, nakusihi, umtukuze BWANA, Mungu wa Israeli, ukaungame kwake; uniambie sasa ulilolitenda; usinifiche. Akani akamjibu Yoshua, akasema, kweli nimefanya dhambi juu ya BWANA, Mungu wa Israeli, nami nimefanya mambo haya na haya. Nilipoona nyara katika joho nzuri ya Babeli, na shekel mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu, uzani wake shekel hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa; tazama vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake. Basi Yoshua akatuma wajumbe wakapiga mbio mpaka hemani; na tazama, vile vitu vilikuwa vimefichwa hemani mwake, na ile fedha chini yake. Wakavitoa kutoka hapo katikati ya hema, wakavileta kwa Yoshua, na kwa wana wa Israeli wote, nao wakaviweka chini mbele za BWANA. Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori. Yoshua akasema, mbona umetufadhaisha hivi? BWANA atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe. Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa yam awe hata leo; naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori hata hivi leo.” Yoshua 7:1-26 Kitu kilichowekwa wakfu maana yake ni cha Mungu. Mfano: ZAKA ni sehemu ya kumi ya mali, mazao, mifugo, fedha n.k BWANA ametoa maagizo na sheria maalumu katika vitu vitakatifu, nayatupasa kupambanua kati ya vitu vitakatifu (wakfu) na vya siku zote. Maandiko matakatifu yanasema; “Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.” Kumbukumbu 14:22 Inasisitizwa kuwa makini na kuvitenga vitu vitakatifu kwa Mungu visiwe au kuliwa katika malango ya nyumba zetu maana kufanya kinyume na maagizo ya neno la Mungu ni kukaribisha laana na ukaufu katika kazi zetu za mikono. Maandiko matakatifu yanasema; “Usile ndani ya malango yako zaka ya nafaka zako, wala divai yako, wala mafuta yako, wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng’ombe wala ya kondoo, wala nadhiri zako uwekazo zo zote, wala sadaka zako za hiari, wala sadaka ya kuinuliwa ya mkono wako;” Kumbukumbu 12:17 Jilinde nafsi yako usile zaka siku zote za maisha yako; maana ukila zaka umekula kitu kilichowekwa wakfu ni dhambi. “Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo. Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, name nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani? Je! Mwanadamu atamwambia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa nanmna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, nakuwamwagieni Baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi. Na mataifa yote watawiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.” Malaki 3:6-12 Kutokutoa zaka ni kwenda kinyume na maagizo ya Mungu hivyo mtu uliyeokoka ukila zaka utapigwa mbele ya adui zako; · Biashara yako itapigwa. · Ndoa yako itapigwa. · Elimu ya watoto wako itapigwa. · Ustawi wako utapigwa. “Je mwanadamu utamwibia Mungu? Lakini ninyi; mnaniibia mimi lakini ninyi mwasema tumekuibia kwa namna gani” Kutokutoa zaka ni kumpora Mungu haki yake katika kazi zako za mikono (sehemu ya kumi ya mapato yako) ni sehemu takatifu kwa Mungu. BWANA anasema; “Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, NI YA BWANA; NA KAMA MTU AKITAKA kukomboa cho chote cha zaka yake, ATAONGEZA SEHEMU YAKE YA TANO juu yake.” Mambo ya Walawi 27:30-31 Sehemu ya kumi ni takatifu kwa Mungu. Hivyo kutoa zaka sio swala la hiari bali ni lazima kama kulivyo kuokoka ni lazima, nje ya hapo utatupwa Jehanamu. Kumwacha Mungu siyo lazima unywe pombe au ufanye uzinzi lakini kwa tendo la kukosa uaminifu ni dhambi na Kristo anasema TUBUNI NA MREJEE, tafuteni ufalme wa Mungu na haki yake na mengine yote mtazidishiwa. BWANA Yesu Kristo akasema; “Ole wenu waandishi na mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo IMEWAPASA KUYAFANYA, WALA YALE mengine msiyaache.” Mathayo 23:23 Yesu Kristo aliunga mkono utoaji wa fungu la kumi alipowakemea Mafalisayo waliotilia mkazo fungu la kumi tu huku wakiwa wamesahau mambo ya adili na sheria. Wengine hudhani alipinga utoaji wa fungu la kumi, lakini sivyo, yeye alikuwa anaweka uwiano. Wako wanaodhani kuwa fungu la kumi sio lazima wakidai ni kwaajili ya waumini wa agano la kale. Wao hudhani fungu la kumi ni agizo la torati. Lakini sivyo. Fungu la kumi liliamriwa kabla ya torati unaweza kusoma “Abramu aliporudi kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni bonde la mfalme. Na Melkizedek mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu sana… Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.” Mwanzo 14:17-20 Kwa kuwa Imani tu pasipo matendo ya haki ya kiimani, ufalme wa Mungu hauwezi kuwa kwako. Ili malango na milango ifunguke sharti kuwa mwaminifu. Maana BWANA ameahidi kwa ajili yetu atamkemea yeye alaye: · Asile tena Kazi zetu. · Asile tena Ndoa zetu. · Asile tena Familia zetu. Maana Kristo Yesu “Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.” Luka 16:10 Ukishindwa kutoa zaka ya hicho kidogo unachopata, huwezi kupewa kikubwa. BWANA anasema angamiza vyote lakini wewe kwa tamaa unaficha, matokeo yake unaleta mauti katika familia yako badala ya Baraka na ustawi. BWANA Yesu Kristo anasema “Akawaambia, Ninyi ndinyi mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini Mungu awajua mioyo yenu; kwa kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu. Luka 16:15 Maana vyote vitapita lakini Neno la Mungu halitapita kamwe katika maisha yetu. Ufalme wa Mungu umo ndani yetu pale tunaposhika Neno lake kwa uaminifu. AKANI kwa tamaa ya joho tu na shekeli mia mbili za fedha (Akani anasema NALITAMANI MKAVITWAA katika hema yangu na ile fedha. Akani na familia yake waliangamizwa “Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori. Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? BWANA atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe. Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa yam awe hata leo; naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde ka Akori, hata hivi leo.” Yoshua 7:24-26 Baada ya TOBA ya wana wa Israeli BWANA akasema “…Inukeni mwende Ai; angalia mimi nimeutia Ai na watu wake; mji wake na nchi yake mikononi mwenu na hawatasimama tena mbele yenu.” Ushindi wetu wa ki-Mungu hutoka kwa Mungu hivyo afichaye dhambi zake HATAFANIKIWA bali yeye aziungamaye atapata rehema mbele za Mungu. Ufunguo huu ni wa muhimu sana katika maisha yetu “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema” Mithali 28:13 Kukosa uaminifu huleta kupigwa. Lazima tuchunguze mwenendo wetu na tuyatubie matendo yetu mafu. “[Ikiwa siku zile Wafilisti walikusanyika ili kupigana na Israeli], nao Waisraeli wakatoka juu ya Wafilisti kwenda vitani; wakatua karibu na Ebenezeri, nao Wafilisti wakajipanga juu ya Israeli wakapigwa mbele ya Wafilisti; wakauawa watu wa jeshi lao lililokuwa uwandani wapata watu elfu nne. Hata watu walipofika kambini, wazee wa Israeli wakasema, mbona BWANA ametupiga leo mbele ya Wafilisti? Twende tukalilete sanduku la agano la BWANA toka Shilo hata huku, lije kati yetu, na kutuokoa katika mikono ya adui zetu. Basi wakatuma watu kwenda Shilo, nao wakalileta toka huko sanduku la agano la BWANA wa majeshi, akaaye juu ya makerubi; na Hofni na Finehasi, wana wawili wa Eli, walikuwako huko pamoja na sanduku la agano la Mungu. Na sanduku la agano la BWANA lilipoingia Kambini, Israeli wote wakapiga kelele kwa sauti kuu, hata nchi ikavuma. Nao Wafilisti waliposikia mshindo wa zile kelele, walisema, Maana yake nini mshindo wa kelele hizi kubwa katika kambi ya Waebrania? Wakatambua ya kuwa sanduku la BWANA limefika kambini. Wafilisti wakaogopa, maana walisema, Mungu ameingia kambini. Wakasema, Ole wetu! Kwani halijawa jambo kama hili tangu hapo. Ole wetu! Ni nani atakayetuokoa na mkono wa miungu hawa walio hodari? Hawa ndio miungu waliowapiga Wamisri kwa mapigo ya kila namna jangwani. Iweni hodari, na kufanya kiume enyi Wafilisti, msije mkawa watumwa wa Waebrania, kama wao walivyokuwa watumwa wenu; fanyeni kiume, mkapigane nao. Wafilisti wakapigana nao, Israeli wakapigwa, wakakimbia kila mtu hemani kwake; wakauawa watu wengi sana; maana katika Israeli walianguka watu thelathini elfu wenye kwenda vitani kwa miguu. Hilo sanduku la Mungu likatwaliwa; na Hofni na Finehasi, wale wana wawili wa Eli, wakauawa. Basi, mtu mmoja wa Benyamini akapiga mbio kutoka mle jeshini akafika Shilo siku ile ile, hali nguo zake zimeraruliwa, na mavumbi kichwani mwake. Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia, akingojea; maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule mtu alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia. Naye Eli aliposikia kelele za kile kilio, akasema, maana yake nini kelele za kishindo hiki? Yule mtu akafanya haraka, akaenda, akamwambia Eli. Basi Eli umri wake umepata miaka tisini na minane; na macho yake yamepofuka hata asiweze kuona. Yule mtu akamwambia Eli, Mimi ndimi niliyetoka jeshini, nami leo hivi nimekimbia toka jeshini. Naye akasema, Yalikwendaje, mwanangu? Yeye aliyeleta habari akajibu, akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi sana wameuawa, hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na sanduku la Mungu limetwaliwa. Ikawa walipotaja sanduku la Mungu, Eli akaanguka kitini pake kwa nyuma, kando ya mlango, shingo yake ikavunjika, akafa; maana alikuwa mzee, tena mzito. Naye alikuwa amewaamua Israeli miaka arobaini. Tena mkwewe, mke wa huyo Finehasi, alikuwa mja-mzito, karibu na kuzaa; basi, aliposikia habari ya kutwaliwa sanduku la Mungu, nay a kwamba mkwewe na mumewe wamekufa, akijiinamisha, akazaa; maana utungu wake ulimfikilia. Hata alipokuwa katika kufa, wale wanawake waliohudhuria karibu naye wakamwambia, Usiogope; kwa maana umezaa mtoto mwanamume. Walakini hakujibu, wala hakumtazama. Akamwita mtoto, Ikabodi, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la Mungulilikuwa liketwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe.” 1Samweli 4:1-21 Israeli walipopigwa hawakuangalia kwa makini sababu ya kupigwa kwao matokeo yake badala ya kufanya toba wakaanza kusaka vitu vya upako viwasaidie katika vita vyao, matokeo yake wakapigwa navyo, wakafa watu wengi sana na sanduku la BWANA Mungu wa majeshi likatekwa. Ndivyo walivyo wakristo wengi siku za leo, milango na malango yao yanapofungwa badala yakutengeneza njia zao mbele za Mungu, matokeo yake wanasaka vitu vya upako, kama vile maji, mafuta chumvi, vipande vya sabuni matokeo yake wamefarakana na Mungu kwa kufuata ibada ziliotungwa kwa namna ya wanadamu. Maana Mungu ni Roho na wale wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli, kwa mantiki hiyo mtu wa Mungu zingatia kweli ya Mungu ndani ya Neno lake si vinginevyo, mahali pa toba fanya toba. BWANA anasema; “Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu. Basi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni bali sasa amewaagiza watu wote wa kila mahali watubu.” Matendo17:29-30 Nasi yatupasa tutengeneze mienendo yetu maana pasipo kuwa na matendo ya haki tukakimbilia kulitaja jina la Kristo Yesu tu, malango na milango havitafunguka. “Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, Na kuliweka agano langu kinywani mwako? Maana wewe umechukia maonyo, na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye, ukashirikiana na wazinzi. Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, na ulimi wako watunga hila. Umekaa na kumsengenya ndugu yako, na mwana wa mama yako umemsingizia. Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza; ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe. Walakini nitakukemea; nitayapanga hayo mbele ya macho yako.” Zaburi 50:16-21 Dhabihu ya Mungu ni Roho iliyopondeka na kutubu. “Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.” Zaburi 51:17 Anania na mkewe Safira walikufa kwa sababu ya kutokuwa waaminifu katika kitu kilichowekwa wakfu mbele za Mungu. “Lakini mtu mmoja jina lake Anania pamoja na Safira mkewe, aliuza mali, akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. Petro akasema, Anania, kwanini shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa.ofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya. Vijana wakamchukua nje, wakamzika. Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia naye hana habari ya hayo yaliyotokea. Petro akamjibu, niambie mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. Petro akamwambia imekuaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia miguu yao ya waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe. Mara akaanguka miguuni pake akafa. Wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mume wake.” Matendo 5:1-10 Usituppe neno la Mungu nyuma yako, maana mshahara wa Dhambi ni Mauti. “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawata urithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi wala watukanaji, wala wanyang’anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii lakini MLIOSHWA, LAKINI MLITAKASWA, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.” 1 Wakorintho 6:9-11 Lazima kuoshwa kwa Damu ya Yesu Kristo kwa njia ya TOBA, hapo ndipo Malango na Milango yako itakapofunguliwa mbele yako. Lazima Kristo amiliki na kutawala maisha yako, hivyo hatulegei bali tunapiga mbio katika Maombi; ijapokuwa Utu wetu wa nje unachakaa lakini Utu wetu wa ndani sharti ufanywe upya siku kwa siku. Lazima tuyavue matendo yote maovu na Tumvae Kristo. “Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.” 1Petro 1:17 Kwa hiyo tujifunge viuno vya nia zetu tukitumainia kwa utimilifu ile neema inayoletwa katika ufunuo wake Yesu Kristo. Kama watoto wa kutii tusijifananishe na tamaa zetu za kwanza za ujinga wetu, bali kama yeye aliyetuita alivyo mtakatifu, sisi nasi yatupasa tuwe watakatifu katika mienendo yetu wote. Kwa maana imeandikwa mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
0 comments:
Post a Comment