Pages

Subscribe:

Monday, 3 October 2016

SOMO;
MACHUKIZO NDANI YA NYUMBA YA MUNGU

(YEREMIA 32:33-34)
“Tena wamenigeuzia visogo vyao, wala si nyuso zao;
ingawa naliwafundisha, nikiondoka mapema na kuwafundisha, lakini hawakusikiliza ili wapate mafundisho.
Bali waliweka machukizo yao ndani ya nyumba iliyoitwa kwa jina langu, ili kuinajisi.

Machukizo ya aina yoyote hayaruhusiwi ndani ya nyumba ya Mungu na ndani ya nyumba zetu.

( KUMBUKUMBU LA TORATI 7:26 )
“na machukizo usitie ndani ya nyumba yako, usije wewe kuwa kitu cha haramu mfano wake; ukichukie kabisa, na kukikataa kabisa; kwa kuwa ni kitu kilichoharamishwa”.

Machukizo yanatajwa kuwa ni kitu kilichoharimishwa.
Neno machukizo linatokana na neno la lugha ya kiebrania linaloitwa” toebah.

Neno “TOEBAH” lina maana ya kitu au mtu ambaye ni wa tofauti katika hali. Mtu ambaye ni hatari ukilinganisha na watu wengine.
Yatakuwa ni mambo au tabia ambazo ziko kinyume na asili yake. Machukizo sasa ni vitu vya kipagani ambavyo vimeingia ndani ya nyumba ya Mungu. Yapo mambo ambayo ni machukizo ndani ya nyumba ya Mungu. Mambo ambayo ni haramu kuingizwa ndani ya nyumba ya Mungu.

( i ). Mwanamke kuvaa mavazi ya wanume na mwanamume kuvaa mavazi ya wanawake.
( KUMBUKUMBU LA TORATI 22:5 ). ‘ Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA,
Mungu wako”.
Mungu anasema maumbile yetu ndiyo yatufundisheni vazi lipi linafaa kuvaliwa na wanaume na ni nlipi linafaa kuvaliwa na wanawake ( 1 WAKORINTHO 11:14 ). Mitindo ya ushonaji nguo iadizainiwa kutokana

na maumbile yetu. Ndiyo maana wanawake wana mavazi yao na wanaume wana mavazi yao na Mungu ameliweke hilo mwenyewe. Kwa hiyo vazi kama suruali siyo la mwanamke, limedizainiwa kwa ajili ya mwanamume na si vinginevyo.

Katika biblia ni wanaume pekee wanaotajwa wakiwa wamevaa suruali, hatuoni sehemu yoyote ikimtaja mwanamke akiwa amevaa suruali. Ingia katika blog yangu ujifunze somo la “MAVAZI YA KIKAHABA” utajifunza mengi kuhusiana na mavazi.

Suruali kwa wanawake ni vazi la kikahaba kabisa
( MITHALI 7:10 ) ( ii ). Sadaka ya kahaba na Mbwa ni machukizo mbele za Mungu ( KUMBUKUMBU LA TORATI 23:18 ) “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani

haya ni machukizo kwaBWANA, Mungu wako yote mawili”. Mbwa ni mtu anayerawiti au mtu anayerawitiwa. Mshahara wa kahaba na watu wote wanaoshiriki katika uchafu wa kurawiti na kurawitiwa ni machukizo kwa BWANA, Mungu wetu. Hatutakiwi kupokea sadaka zao kwa ajili ya BWANA, ni machukizo kwake. ( iii ). Miungu na chochote kinachohusiana na miungu ni machukizo mbele za Mungu. ( EZEKIELI 8:1-18 ) Namna yoyote ya sanamu tunapoihusisha katika ibada tayari inakuwa ni ibada ya miungu. Mapambo ya aina yoyote ni chukizo mbele za Mungu wetu kwa sababu kuna uhusiano kati ya mapambo na miungu. Ni muhimu kufahamu kuwa mapambo hayakuvaliwa na Waisraeli. ( WAAMUZI 8:24 ) “ Kisha Gideoni akawaambia, Mimi nina haja yangu kwenu, ni yakila mtu kunipa hizo pete za masikio ya mateka yake. ( Kwa maana walikuwa na pete za masikio za dhahabu, kwa sababu walikuwa ni Waishmaeli )”. Waishmaeli walikuwa ni wapagani ( mataifa ) vilele waliitwa Wamidiani. ( MWANZO 35:1-4 ). “……………Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu,………..Nao wakampa Yakobo, miungu migeni yote iliyokuwa masikioni mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao…………….”. Mwanamke Yezebeli alikuwa mataifa tena mwabudu miungu. Mwanamke huyo alikuwa staid sana kwa kujipamba na aliingia katika Taifa la Israeli baada ya kuolewa na mfalmeAhabu. Kwa hiyo mapambo yalikuwa yakivaliwa na Waisraeli kwa kuiga tabia za mataifa

( 2 WAFALME 9:30-37;
UFUNUO 2:20 ) Makanisa mengi leo yanahudu mafundisho ya Yezebeli ya kuruhusu mapambo kwa watu wa Mungu. Mungu aliwatumia
mitume kwa ishara na miujiza mikubwa kutokana na injili yao kuwa kinyume na machukizo. Kanisa la kwanza walifundishwa kuwa mbali na mapambo ya kila namna ( 1 TIMOTHEO 2:9-10; 1PETRO 3:3-5 ). Kinyume na asili ya Mungu ndiyo maana ya machukizo ( un contrallel to his nature ). Machukizo kwa asili yalikuwa ni ya mataifa na hayakuwa ya Waisraeli.

( YEREMIA 4:1 ) “Kama ukitaka kurudi, Ee Israeli, asema BWANA, utanirudia mimi; na kama ukitaka kuyaondoa machukizo yako, yasiwe mbele ya macho yangu, ndipo hutaondolewa”.

Kuna uwezekano mkubwa hata wakuu wa makuhani ( maaskofu ) kuruhusu machukizo kuingia nyumbani mwa Mungu. Machukizo yakiingia madhara yake ni makubwa kwa watu wa Mungu. Tunaona katika andiko hilo chini kuwa hata uwezo au mkono wa Mungu wa kuponya unaondoka

( 2 NYAKATI 36:14-16 ).
“Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya BWANA aliyoitakasa katika Yerusalemu. Naye BWANA, Mungu wa baba zao akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake;

Lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya”. Miujiza ya Mungu ya uponyaji kama wakati wa Yesu na wakati wa mitume haiwezi kuonekana dhahiri kwa watu wanaoruhusu machukizo kwa watu wa Mungu na ndani maskan i(nyumbani) yake Mungu, Utakuta watu wanashughulika na mapepo tu kila siku lakini miujiza ya vipofu kuona, viziwi kusikia, viwete kutembea, mabubu kuongea, wenye kigugumizi kuongea sawasawa, wenye makengeza kuponywa na kila namna ya miujiza mingine kama nyakati za mitume havionekani. Mamlaka waliyokuwa nayo mitue ya kumwambia kuwete ‘ Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende ( MATENDO 3;6 )’. Mamlaka haiko leo kwa watumishi wengi sababu ni kwamba wameruhusu machukizo nab ado tu wanaendelea kuyatetea kwa bidii nyingi.

( YOHANA 2:13-17 ) Yesu Kristo alipokuta watu wamegeuza hekalu soko alichukizwa mno na kitendo kile ndipo akaamua kupundua meza zao, na kuwaondoa wote hekaluni kwa kutumia kikoto.

Aliuliza, Yesu hakuyavumilia machukizo nyumbani mwa baba yake. Watumishi wa Mungu leo wanatakiwa kufuata msingi aliouweka
BWANA YESU na si kuyaacha machukizo eti kwa visingizio vya kulinda kundilisipungue, hatuwasaidii washirika wetu. Tunapaswa kumwondoa mwovu miongoni mwetu ili wengine wajifunze kukaa katika viwango vyote vya neno la Mungu.

( iv ). Wanawake wanapaswa kufunika kichwa wakiwa katika ibada. Wanapaswa kufunika wakiwa kanisani, wanapofanya huduma yoyote ya kiroho mfano, kuomba, kuhutubu au kuhubiri.

( 1 WAKORITHO 11:4-5,7,10,13
‘ Sheria inayomkataza mwanamume kumwomba Mungu akiwa amevaa kofia pia inayomkataza kuvaa kofia kanisani hiyo hiyo ndiyo inayomtaka mwanamke afunike kichwa

kwa ajili ya Malaika. Wanaosema ilikuwa desturi za Wakorintho hawayaelewi maandiko vizuri. Biblia inasema ‘ Imempasa mwamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani kwa ajili ya Malaika”. Angalia vizuri neno ‘ imempasa=lazima”. Hakuna Biblia ya Wakorintho pekee yao, tukichambua Biblia hivyo sisi Watanzania hatutabaki na kitabu chichote.Yote yaliyoandikwa, yaliandikwa kwa ajili yetu wote ( WARUMI 2;16 ), Mungu atayahukumu mataifa yote kwa injili hiyohiyo Tukitaka kuziona nguvu za Mungu waziwazi lazima tuwe mbali na machukizo ya aina yoyote. Mafuta ya Mungu yanakuwa juu ya mtu anayechukia machukizo

( WAEBRANIA 1:9 ). Mtu ambaye anatetea machukizo yaliyomo ndani ya maskani ya Mungu lakini akifanya miujiza au maajabu lazima tujiulize ni nguvu ipi inatenda kazi hapo?. Mungu mwenyewe anasema kuwa mahali penye machukizo, ukono wake wa kuponya hauwezi kuwepo ( 2 NYAKATI 36:14-16 ), Pia hawezi kupakwa mafutaNA Mungu ( WAEBRANIA 1:9 ). Nyakati hizi tulizonazo watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli, wanapenda kudanganywa. Paulo mtume alitabiri juu ya nyakati hizi jinsi watu watakavyotafuta waliu wa kuwafundisha uongo na kuikataa kweli ya neno la Mungu ( 2 timotheo 4:3-4). Hata wakati wa nabii Isaya walikuwepo watu waliotafuta walimu wengine wa mbali na Isaya aliyehubiri kweli yote. Walisema kuwa wanataka mafundisho laini yadanganyayo ( ISAYA 30;9-10 ).Kama tunataka kuishi na Mungu milele hatuna budi kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha na kuwa tayari kuyafuata maagizo yote ya Neno la Mungu ( ZABIRI 119:6 ). Tunasafisha njia zetu kwa kutii neno la Mungu na siyo walimu wetu wanaotufariji tuendelee kufanya machukizo mbele za Mungu ( ZABURI 119;9 ). Walimu wanaowatia moyo watu ili waendelee kuvaa mapambo na suruali kwa wanawake wote ni wafariji wa kutaabisha ( AYUBU 16:2 ). Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!

0 comments:

Post a Comment