Pages

Subscribe:

Thursday, 8 October 2015

DANIELI 9:25-27

IFUATAYO NI TAFSIRI POTOFU YA ANDIKO LA DANIELI 9:25-27. Tukirudi kwa upande wa William Miller: Yeye William Miller alitafsiri kule kujengwa upya kwa Yerusalemu ni pale palipoelezwa kwenye kitabu cha EZRA 7:11-26 (unaweza kusoma andiko hilo kwenye Biblia Takatifu kwa muda wako), ambao ulikuwa mwaka wa 457 k.K. William Miller naye pia akatafsiri katika unabii siku moja ni sawa na mwaka mmoja; kwa hiyo majuma 70 ni sawa na miaka 490 kwa mujibu wa hesabu za kinabii. Alichukua mwaka 457 k.K akajumlisha miaka 490 akapata mwaka 33 b.K ambao ndiyo mwaka aliosulibiwa Yesu na kufa msalabani (lakini kinabii hesabu yake hiyo inagoma, kwani ukichukua mwaka 457 k.K ukajumlisha 490 utapata mwaka 34 b.K kwa sababu hakuna mwaka 0 b.K). William Miller akatafsiri unabii huo kwa namna hiyo. Kisha baada ya hapo; William Miller akasoma DANIELI 8:13-14, akaona hapo kuna watakatifu wawili wakijadiliana: "...mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi? Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa." - (Dan 8:13-14) Andiko hilo linaongelea juu ya kutakaswa kwa patakatifu kwa kipindi cha "...nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu..." Kwa hiyo William Miller akatafsiri maana ya patakatifu kutakaswa ni dunia hii iliyochafuliwa na dhambi, na utakaso huo utakuwa ndiyo hukumu (Kiyama). Hivyo basi, kwa kutumia kanuni ile ile ya unabii ambayo siku moja ni sawa na mwaka mmoja; William Miller alichukua hizo asubuhi na jioni 2300 akazihesabu ni sawa na miaka 2300. Pia Akachukua mwaka 457 k.K akajumlisha miaka 2300 akapata mwaka wa 1843 b.K (lakini kinabii nayo hii hesabu yake inagoma, kwani ukichukua mwaka 457 k.K ukajumlisha 2300 utapata mwaka 1844 b.K kwa sababu hakuna mwaka 0 b.K). Na kwa upotofu wake yeye William Miller akaamini mwaka huo wa 1843 ndiyo ambao Yesu Kristo angerudi na ungekuwa mwisho wa dunia (Kiyama). Ingawa mwanzoni William Miller hakutaja tarehe rasmi ya kurudi kwa Yesu, lakini baadaye alipata ujasiri wa kutangaza hadharani kwamba Yesu angerudi tarehe 21 Machi 1843. Lakini tarehe na mwaka huo ulivyopita, William Miller akabadiri tena unabii wake na akasema itakuwa tarehe 21 Machi 1844 (hapo inaonyesha alikiri kukosea hesabu yake ya awali ya kinabii.) Kinyume na jinsi vile alivyotarajia, siku hiyo nayo ilifika na kupita pasipo unabii wake kutimia. Kisha ndipo mfuasi wa karibu wa William Miller aitwaye Samweli Snow alipata ujasiri zaidi na kutangaza Yesu angerudi tarehe 22 Oktoba mwaka 1844 saa sita usiku (yeye mwenyewe anajua alipoyatoa hayo mafunuo.) Samweli Snow akasema katika siku hiyo parapanda ingepigwa, mbingu zingekunjwa kama ukaratasi, na Yesu angekuja katika utukufu mwingi. Waadventista wengi walibadili tabia zao kwa hofu ya Mungu zaidi ya zamani, baadhi ya wafanya biashara na wakulima waliuza mali na mashamba yao na kuwapa masikini pesa zao. Lakini; siku hiyo nayo ilifika, kisha ikapita pasipo unabii ule kutimia. Siku hiyo kwa Waadventista ikawa ni "THE DAY OF GREAT DISAPPOINTMENT" au kwa lugha ya Kiswahili "SIKU YA KUVUNJIKA MOYO". Zingatia neno hili, Bwana Yesu anasema kwamba: "But of that day and hour knoweth no man, no, not the angels of heaven, but My Father only." - (Matthew 24:36 - KJV) Tafsiri yake kwa Kiswahili ni hii: "Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna mtu aijuaye, hata malaika walio mbinguni, ila Baba Yangu pekee."  Mungu anasema: "Watu Wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, Mimi nami natakukataa wewe..." - (Hosea 4:6) Maarifa hayo ni neno la Mungu. Bwana Yesu amesema kwa uwazi kabisa kwamba: "Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna mtu aijuaye, hata malaika walio mbinguni, ila Baba Yangu pekee." Vile vile Biblia Takatifu inatuambia kuwa neno la Mungu la kinabii halitafsiriwi kama apendavyo mtu binafsi. Endapo kama unayo nia ya dhati kuifahamu kweli, basi zingatia kwamba: "Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapoikubali kweli." Hivyo basi William Miller alikiri kukosea kwake, lakini akawasihi wafuasi wake wajue tu kwamba Yesu Kristo atarudi upesi. Ifahamike kwamba; hadi kufa kwake alikuwa ni Mbaptisti ambao wao wanasali siku ya kwanza ya juma (yaani Jumapili au Sunday ya kisasa) Alizaliwa mwaka 1782 b.K na kufariki mwaka 1849 b.K. Huko mbeleni tutaona jinsi mafundisho hayo ya Williamu Miller ambayo baadae yakatumiwa na Samweli Snow, na tena huko mbeleni tutaona jinsi yanavyotumika sasa kwa Waadventista Wasabato wa leo. Mtu mwingine aliyehusika katika uanzilishi wa imani ya Waadventista Wasabato ni huyu: ii/: Hiram Edson Mtu huyu alikuwa mmoja kati ya wafuasi wa William Miller. Baada ya SIKU YA KUVUNJIKA MOYO, Hiram Edson pamoja na baadhi Waadventista walibaki kumwomba Mungu usiku kucha. Walimwomba Mungu awape ishara kwa nini Yesu akurudi kama walivyo tegemea. Asubuhi yake waliondoka kwenda kuwafariji wenzao kutokana na huzuni iliyowapata. Wakiwa njiani, Hiram Edson alidai alipata ufunuo wa yaliyofanyika siku hiyo ya tarehe 22 Oktoba 1844. Aliwaambia kwamba; alioneshwa hekalu la mbinguni ambalo lina mfano wa hekalu la duniani. Hekalu hilo lina sehemu mbili ambazo ni ; i/: PATAKATIFU, na ii/: PATAKATIFU PA PATAKATIFU.

0 comments:

Post a Comment