Bwana Yesu asifiwe mpendwa wangu,
Kwa kila anayeamini ya kuwa Bwana Yesu Bwana na Mwokozi wa maisha yake,
anafanyika KIPAWA CHA BWANA,
anapewa karama kama zawadi YOH3:16
Ktk EFES 2:8-9 kuokolewa kwetu
hakukuwa jinsi tulivyoonekana au kumfanyia BWANA
bali
ni kwa matokeo ya neema au upendeleo wa kipawa
kutoka kwa Mungu mwenyewe.
MUNGU hugawa karama nyingi tofautitofauti
kama viungo vya mwili ktk kuujenga mwili wa Kristo ambao ni kanisa 1PET 5:5
KANUNI TANO (5) ZA KUFAHAMU KTK KARAMA.
1.Karama ni kwa ajili ya kanisa ktk kuujenga mwili wa Kristo 1KOR 12:12,17 na mtu.
viungo hutegemeana 1KOR 12:24-26
Mfano Petro alipofungwa gerezani,
kanisa liliomba kwa ajili yake na akawa huru.
2. Karama ni kwa manufaa ya kundi zima
wala si kwa faia yako mwenyewe 1PETR 4:10,11
karama mzitumie kwa kuhudumiana
maana tumejaaliwa na Mungu na atukuzwe ktk karama zetu.
3.Vipawa ni vya ki Mungu!
1KOR 14:23-25
Paulo alijaribu kueleza na kulifundisha kanisa
akawauliza,
kuwa na maongozo ya ki Mungu na unyenyekevu
kuweza kumsaidia mpumbavu.
Jinsi gani anaweza kuishi na mtu ambaye hajaokoka.
4.Karama na vipawa hutawaliwa na upendo
Ukikosa upendo au kupendwa, karama zako hupotea sawa na
GAL 6:7.
5.Karama hutawaliwa na mafundisho ya NENO LA MUNGU
RUM 12:3-16.
Huwezi kuendeleakuitunza karama/kipawa kama zawadi kutoka kwa Mungu
kwa kutokupenda neno la Mungu.
Nashukuru mpendwa wangu kwa kulisikiliza somo hili
ambalo limekufikia maalumu kukuvusha hatua moja mbele.
NI MIMI MPENDWA WAKO
MWALIMU NA MWINJILISTI
Elimeleck S Ndashikiwe.
+255767445846
+255715445846.
BARIKIWA NA BWANA.
0 comments:
Post a Comment