MAMBO KUMI YANAYOWEZA KUWACHELEWESHA WACHUMBA KUFUNGA NDOA. Bwana YESU
KRISTO
-
Na Peter & Jemimah Mabula Watendakazi katika Shamba la MUNGU wa
Mbinguni Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.Karibu upate maarifa
ya kukusaidia kat...
Wednesday, 15 March 2017
SANDUKU LA AGANO
Sanduku la Agano ni sanduku lililokuwa ni hekalu la Bwana wakati wa Agano la Kale. Ndani ya sanduku kulikuwa na vitu mbali mbali. Mungu aliwapa amri kuwa wana wa Israel wawe wanatengeneza Hema la Kukutania, ambalo lilikuwa na sehemu kuu tatu:-
Malangoni pa Bwana
Patakatifu
Patakatifu pa patakatifu.
Sehemu ile yenye patakatifu pa patakaitifu ndipo ambapo Sanduku la Agano lilikuwa likiwekwa.
2 NYAKATI 5:7….[Makuhani wakaliingiza sanduku la agano la Bwana mahali pake katika chumba cha ndani cha nyumba, patakatifu pa patakatifu, yaani, chini ya mabawa ya makerubi.]
2 NYAKATI 6:11…[Ndimo nilimoliweka hilo sanduku, ambalo ndani yake mna agano la Bwana, alilolifanya na wana wa Israeli.]… Kumbe hili ni Agano la mtu awe na afya njema, azae watoto, awe tajiri, awe na amani, awe na ndoa njema, awe na kazi n.k.
EBRANIA 9:4 ….. [yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano;]… Mana kwa maisha yetu ya leo inawakilisha Neno la Mungu. Kila mahali Sanduku la Agano lilipokuwa, Mungu mwenyewe alikuwemo hapo. Na endapo mtu mwenye dhambi angeingia patakatifu pa patataktifu, lazima angekufa kwani mahali pale aliingia Kuhani pekee aliyekwishatakaswa dhamibi zake.
1 SAMWELI 4:5-7…. [Na sanduku la agano la Bwana lilipoingia kambini, Israeli wote wakapiga kelele kwa sauti kuu, hata nchi ikavuma. 6 Nao Wafilisti waliposikia mshindo wa zile kelele, walisema, Maana yake nini mshindo wa kelele hizi kubwa katika kambi ya Waebrania? Wakatambua ya kuwa sanduku la Bwana limefika kambini. 7 Wafilisti wakaogopa, maana walisema, Mungu ameingia kambini. Wakasema, Ole wetu! Kwani halijawa jambo kama hili tangu hapo.]….
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment