1. TARATIBU ZA UTOAJI WA FUNGU LA KUMI
Ni mpango wa Mungu wa Kuwabariki watu waliookoka.
MITHALI 15:8…...
[Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.]
…Dhambi ni kikwazo cha kupata majibu kutoka kwa Bwana.
EFESO 2:8-9…
[Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa
njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu
, ni kipawa cha Mungu;
9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.]…
Mtu hapaswi kujisifu kwamba ameshabarikiwa, kwa sababu ni kwa neema tu.
Ndiyo maana baadhi ya watu shida haziishi miongoni mwa waliookoka.
YOHANA 3:16…
[Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,
hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.]…
Hata uzimawa milele tulio nao unatokana na utoaji wa Mungu kwa ajili yetu.
Ibrahimu alitoa fungu la Kumi
MWANZO 14:17….
[Abramu aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye,
mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme.
18 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.
19 Akambariki,
akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi.
20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.]….
Mungu ana uwezo wa kuvaa mwili wa kibinadamu.
Melkisededki ni mfano wa aina yake katika Biblia.
Tafsiri ya jina la huyu mfalme ndiyo inayotupa uhakika wa kuwa Mungu alijifunua
kwa namna ya kipekee.
EBRANIA 7:1-3....
[Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu,
kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu
alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;
2. Ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote;
(tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki,
tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho
wa uhai wake,
bali amefananishwa na Mwana wa Mungu);
huyo adumu kuhani milele.]….
Kawaida,
tafsiri ya jina la mtu huwa moja, na hayupo mtu wa kawaida awezaye kuwa na jina lenye maana nyingi zaidi ya moja.
Hata katika Agano Jipya, watu walitoa fungu la kumi.
MATHAYO 23:23…
[Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa
na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani;
hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.]…
Ni mpango wa Mungu kwa watu kutoa fungu la kumi.
2. KAZI YA FUNGU LA KUMI
Ni kuhakikisha kuwa nyumbani mwa Mungu pana chakula.
MALAKI 3:8-9…..
[Je!
Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi.
Lakini ninyi mwasema,
Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia
zaka na dhabihu.
9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia
mimi, naam, taifa hili lote.
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula
katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo,
asema Bwana wa majeshi;
mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni,
na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Kwa hiyo mojawapo ya kazi ya fungu la kumi
ni kuona kuwa kipo chakula katika nyumba ya Bwana.
Chakula kwenye nyumba ya Bwana kina maana gani?
YOHANA 4:34….
[Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi.
33 Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula?
34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka,
nikaimalize kazi yake.]…
Chakula katika nyumba ya Bwana ni kufanya
kanisani pasiwe ukiwa, bali Injili ya Mungu iweze kusonga mbele.
3. FAIDA YA KUTOA FUNGU LA KUMI
Mungu atakaufunulia madirisha ya mbinguni.
MALAKI 3:10….
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu
kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi;
mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Mungu atamkemea ibilisi alaye biashara zetu, afya zetu, ndoa yak n.k.
MALAKI 3:11…
Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye,
wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.]
Ibilisi anakula.
Kanuni inasema kuwa,
Kama humtolei Bwana fungu la kumi, basi unamtolea Yule alaye. Ndiyo maana,
unamkuta mtu Mataifa yatakuita heri.
MALAKI 3:12…
Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema
Bwana wa majeshi.… .....
Siyo kwamba kwa kutoa fungu la kumi,Mungu atakupa fedha, bali atakaupa vitu
vya rohoni,
mfano akili nzuri, karama, ujuzi n.k ambavyo vitawafanya watu/mataifa kukuita heri.
Your beloved friend
Ev. Elimeleck Ndashikiwe.
+255767445846
0 comments:
Post a Comment