Pages

Subscribe:

Friday, 7 April 2017

HONGERA KWA KUOKOKA


By Ev. Elimeleck S Ndashikiwe

UHAKIKA WA WOKOVU.

Sasa elewa vizuri kuwa,

TAYARI UMEOKOLEWA,

hapa hapa duniani, na si baada ya kufa. Kwasababu Biblia inasema,

“Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa (ni) hukumu”
(Ebr 9:27).

Mungu ametuletea wokovu hapa hapa duniani,
ili tuupokee hapa hapa duniani. Baada ya kufa, hakuna wokovu tena, bali hukumu. Mtu
anayesubiri wokovu baada ya kufa, atakuwa amechelewa!

Kumbuka habari ambayo Yesu alisema “Palikuwa
na mtu mmoja tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula siku zote kwa anasa.

Na alikuwepo masikini mmoja, jina lake Lazaro,
aliyewekwa mlangoni pa tajiri, na ana vidonda vingi.

Naye masikini alitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya
yule tajiri, hata mbwa wakalamba vidonda vyake”.

Hii ina maana kwamba, tajiri hakuwa mcha Mungu;
Kwa maana hakumjali masikini, pamoja na kwamba alikuwa na uwezo.
Masikini alikuwa na hali mbaya sana, ya njaa na ugonjwa,
hata hakuweza tena kuwafukuza mbwa waliomkaribia.

Ndio maana, Tajiri alipokufa, alikwenda motoni. “ikawa yule masikini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu”. (Hii ina maana, masikini alikuwa mcha Mungu).

“Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro kifuani mwake.

Akalia, akasema,
Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini,
auburudishe ulimi wangu;
kwasababu
ninateswa katika moto huu.

Ibrahimu akasema, mwanangu, kumbuka
ya kwamba, wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro
vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi, kumewekwa
shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu,
wasivuke kuja huku.

(Tajiri) akasema,
basi, Baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu (duniani), kwakuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie,
wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, (kule duniani) wanao Musa na Manabii; na wawasikilize wao.

(Tajiri) akasema,
La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
(Ibrahimu) akamwambia, wasipowasikia Musa na Manabii (wahubiri mbalimbali), hawatashawishiwa, hata mtu akifufuka katika wafu”.

BAADA YA KUFA NI HUKUMU! HAKUNA WOKOVU!
Mungu ametuletea wokovu hapa hapa duniani, ili tuupokee hapa hapa duniani, kabla ya kifo kutujia.

Baada ya kufa, hakuna wokovu tena, bali hukumu.
Mtu anayesubiri wokovu baada ya kufa, atakuwa amechelewa, kama yule Tajiri! Ni muhimu pia uelewe kwamba,
tajiri
hakwenda motoni kwa sababu alikuwa tajiri;

wala masikini hakusalimika au hakuokoka kwasababu alikuwamasikini.

Utajiri si dhambi,
wala umasikini si utakatifu. Uhusiano wako na Mungu ndicho kitu kitakachoamua utakwenda kuishi wapi milele.

Wala si fedha yako, wala elimu yako, wal dini yako!
Kitu pelee kitakachoamua wapi utaishi milele, ni uhusiano wako na Mungu.
“Basi
tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote
NA HUO UTAKATIFU (ucha Mungu) ambao hapana mtu atakayemwona Mungu,
asipokuwa nao” .
Ebr 12:14.

Unaweza ukaupata ulimwengu wote, ukawa na kila kitu duniani; utajiri, elimu nzuri,
dini nzuri, kazi nzuri, nyumba nzuri, mshahara
mzuri, magari mazuri, viwanda hata migodi ya thamani.

Lakini kama huna wokovu,
yaani uhusiano mzuri na Mungu, hutaweza
kuingia mbinguni.

“Kwani itamsaidia nini mtu, akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake?”
Math 16:26.

Hakuna faida!
Utajiri halisi ni ule wa ndani (wokovu) ukiunganishwa na wanje (mali na pesa). Ndio maana

Yesu anasema
“Nayajua matendo yako, yakuwa hu baridi wala hu moto;
ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

Basi kwasababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto,
nitakutapika utoke katika kinywa changu.
Kwakuwa wasema, mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe ni mnyonge, na
mwenye mashaka, na masikini, na kipofu, na uchi.”
Ufu 3:15-17.

Kumbe unaweza ukavaa na kupendeza mbele za watu, na kumbe mbele za Mungu
uko uchi kabisa!
Unaweza ukawa mbabe na mjanja mbele
za watu, na kumbe mbele za Mungu ukawa mnyonge na si kitu kabisa!

Unaweza kudhani unaona kwa macho, na kumbe umefichwa vitu vingi halisi, huvioni!

Unaweza ukawa tajiri wa mali za ulimwengu, na kumbe mbele za Mungu ukawa masikini kabisa, kwasababu huna ule
utajiri halisi,yaani wokovu. Yesu anamalizia kwa kusema

“Nakupa ushauri, ununue kwangu
dhahabu
iliyosafishwa kwa moto
(yaani WOKOVU),
UPATE KUWA TAJIRI,
na mavazi upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane,
na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.”

Dhahabu inayotajwa hapo ni
WOKOVU,

kama ilivyoandikwa katika Mathayo 13:44-46;
“Tena Ufalme wa mbinguni umefanana na HAZINA iliyositirika katika shamba, ambayo mtu aliopoiona, aliificha; na kwa furaha yake,
akaenda akauza vyote alivyo navyo, akalinunua lile shamba. Tena Ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara,

mwenye kutafuta LULU NZURI; naye alipoona
LULU MOJA YA THAMANI KUBWA,
alikwenda akauza vyote alivyo navyo, akainunua”.

Hapa, tunaambiwa habari za wokovu kuwa ni KITO cha thamani! Wokovu ni LULU! Wokovu ni DHAHABU Ya thamani nyingi!

Wokovu ni HAZINA njema! Maadam umempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako,
Mungu anakwambia “unao uzima wa milele”
sasa hivi ukiwa hapa hapa duniani.

“Amini amini nawaambia, yeye alisikiaye neno langu na
kumwamini yeye aliyenipeleka,

YUNA (ANAO) UZIMA WA MILELE;
WALA HAINGII HUKUMUNI,
BALI
AMEPITA KUTOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANi”
Yoh 5:24.

Mungu anakwambia “unao uzima wa milele”
sasa hivi ukiwa hapa hapa duniani. Sio kwamba “utakuwa nao” bali ansema “unao” yaani sasa!

Na tena anasema, kwa kuwa unao uzima moyoni mwako, hutaingia hukumuni, bali “umepita”
kutoka mautini kuingia uzimani!

Sio “utapita”,
bali Mungu anasema, “tayari umepita” kutoka mautini, kuingia uzimani.

Pia imeandikwa hivyo katika

1Yoh 3:14
. Na tena 2Wakorintho 6:2 inasema; “… Tazama,
wakati uliokubalika ndio sasa;

TAZAMA, SIKU YA WOKOVU NDIO SASA.

Baada ya kufa, hakuna wokovu tena, bali hukumu.
Mtu anayesubiri wokovu baada ya kufa,
atakuwa amechelewa!

UWE NA UHAKIKA WA WOKOVU WAKO. JUA KWAMBA,
KWA NEEMA YA MUNGU,
UMEOKOKA!

Kwa maana imeandikwa

“MMEOKOLEWA KWA NEEMA, KWA NJIA YA IMANI;
HIYO HAIKUTOKANA NA NAFSI ZENU, NI KIPAWA CHA MUNGU”.
(Efe 2:8)

Mungu akubariki tena na tena mtu wa Mungu .

Ni mimi ndugu yako mpenzi

            Ev. Elimeleck S Ndashikiwe.

0 comments:

Post a Comment