Pages

Subscribe:

Tuesday, 4 April 2017

MACHUKIZO NDANI YA NYUMBA YA MUNGU

(YEREMIA 32:33-34) “Tena wamenigeuzia visogo vyao, wala si nyuso zao; ingawa naliwafundisha, nikiondoka mapema na kuwafundisha, lakini hawakusikiliza ili wapate mafundisho. Bali waliweka machukizo yao ndani ya nyumba iliyoitwa kwa jina langu, ili kuinajisi”. Machukizo ya aina yoyote hayaruhusiwi ndani ya nyumba ya Mungu na ndani ya nyumba zetu. ( KUMBUKUMBU LA TORATI 7:26 ) “na machukizo usitie ndani ya nyumba yako, usije wewe kuwa kitu cha haramu mfano wake; ukichukie kabisa, na kukikataa kabisa; kwa kuwa ni kitu kilichoharamishwa”. Machukizo yanatajwa kuwa ni kitu kilichoharimishwa. Neno machukizo linatokana na neno la lugha ya kiebrania linaloitwa” toebah”. Neno “TOEBAH” lina maana ya kitu au mtu ambaye ni wa tofauti katika hali. Mtu ambaye ni hatari ukilinganisha na watu wengine. Yatakuwa ni mambo au tabia ambazo ziko kinyume na asili yake. Machukizo sasa ni vitu vya kipagani ambavyo vimeingia ndani ya nyumba ya Mungu. Yapo mambo ambayo ni machukizo ndani ya nyumba ya Mungu. Mambo ambayo ni haramu kuingizwa ndani ya nyumba ya Mungu. ( i ). Mwanamke kuvaa mavazi ya wanume na mwanamume kuvaa mavazi ya wanawake. ( KUMBUKUMBU LA TORATI 22:5 ). ‘ Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako”. Mungu anasema maumbile yetu ndiyo yatufundisheni vazi lipi linafaa kuvaliwa na wanaume na ni nlipi linafaa kuvaliwa na wanawake ( 1 WAKORINTHO 11:14 ). Mitindo ya ushonaji nguo iadizainiwa kutokana na maumbile yetu. Ndiyo maana wanawake wana mavazi yao na wanaume wana mavazi yao na Mungu ameliweke hilo mwenyewe. Kwa hiyo vazi kama suruali siyo la mwanamke, limedizainiwa kwa ajili ya mwanamume na si vinginevyo. Katika biblia ni wanaume pekee wanaotajwa wakiwa wamevaa suruali, hatuoni sehemu yoyote ikimtaja mwanamke akiwa amevaa suruali. Ingia katika blog yangu ujifunze somo la “MAVAZI YA KIKAHABA” utajifunza mengi kuhusiana na mavazi. WWW.davidcarol719.wordpress.com Suruali kwa wanawake ni vazi la kikahaba kabisa ( MITHALI 7:10 ) ( ii ). Sadaka ya kahaba na Mbwa ni machukizo mbele za Mungu ( KUMBUKUMBU LA TORATI 23:18 ) “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwaBWANA, Mungu wako yote mawili”. Mbwa ni mtu anayerawiti au mtu anayerawitiwa. Mshahara wa kahaba na watu wote wanaoshiriki katika uchafu wa kurawiti na kurawitiwa ni machukizo kwa BWANA, Mungu wetu. Hatutakiwi kupokea sadaka zao kwa ajili ya BWANA, ni machukizo kwake. ( iii ). Miungu na chochote kinachohusiana na miungu ni machukizo mbele za Mungu. ( EZEKIELI 8:1-18 ) Namna yoyote ya sanamu tunapoihusisha katika ibada tayari inakuwa ni ibada ya miungu. Mapambo ya aina yoyote ni chukizo mbele za Mungu wetu kwa sababu kuna uhusiano kati ya mapambo na miungu. Ni muhimu kufahamu kuwa mapambo hayakuvaliwa na Waisraeli. ( WAAMUZI 8:24 ) “ Kisha Gideoni akawaambia, Mimi nina haja yangu kwenu, ni yakila mtu kunipa hizo pete za masikio ya mateka yake. ( Kwa maana walikuwa na pete za masikio za dhahabu, kwa sababu walikuwa ni Waishmaeli )”. Waishmaeli walikuwa ni wapagani ( mataifa ) vilele waliitwa Wamidiani. ( MWANZO 35:1-4 ). “……………Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu,………..Nao wakampa Yakobo, miungu migeni yote iliyokuwa masikioni mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao…………….”. Mwanamke Yezebeli alikuwa mataifa tena mwabudu miungu. Mwanamke huyo alikuwa staid sana kwa kujipamba na aliingia katika Taifa la Israeli baada ya kuolewa na mfalmeAhabu. Kwa hiyo mapambo yalikuwa yakivaliwa na Waisraeli kwa kuiga tabia za mataifa ( 2 WAFALME 9:30-37; UFUNUO 2:20 ) Makanisa mengi leo yanahudu mafundisho ya Yezebeli ya kuruhusu mapambo kwa watu wa Mungu. Mungu aliwatumia mitume kwa ishara na miujiza mikubwa kutokana na injili yao kuwa kinyume na machukizo. Kanisa la kwanza walifundishwa kuwa mbali na mapambo ya kila namna ( 1 TIMOTHEO 2:9-10; 1PETRO 3:3-5 ). Kinyume na asili ya Mungu ndiyo maana ya machukizo ( un contrallel to his nature ). Machukizo kwa asili yalikuwa ni ya mataifa na hayakuwa ya Waisraeli. ( YEREMIA 4:1 ) “Kama ukitaka kurudi, Ee Israeli, asema BWANA, utanirudia mimi; na kama ukitaka kuyaondoa machukizo yako, yasiwe mbele ya macho yangu, ndipo hutaondolewa”. Kuna uwezekano mkubwa hata wakuu wa makuhani ( maaskofu ) kuruhusu machukizo kuingia nyumbani mwa Mungu. Machukizo yakiingia madhara yake ni makubwa kwa watu wa Mungu. Tunaona katika andiko hilo chini kuwa hata uwezo au mkono wa Mungu wa kuponya unaondoka kwa w ( 2 NYAKATI 36:14-16 ). “Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya BWANA aliyoitakasa katika Yerusalemu.

0 comments:

Post a Comment