Pages

Subscribe:

Friday, 7 April 2017

TUMEOKOLEWA HALELLUYAH


7. TUMEOKOLEWA KUTOKA KATIKA UMASKINI

Angalia,
utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake.

Na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka.

Na kila kitu ulichonacho kitakapoongezeka;

Basi hapo moyo wako usiinuke ukamsahau
Bwana Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa … hapo usiseme moyoni mwako, nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu, ndio ulionipatia utajiri huo;

Bali utamkumbuka Bwana Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri,
ili alifanye imara agano lake …
Kumb 8:12-18

Lakini hawatakuwepo masikini kwenu, kwakuwa Bwana atakubariki kweli, katika
nchi akupayo Bwana Mungu wako, uimiliki,
iwe urithi wako.
Kumb 15:4.

Naye Abrahamu alikuwa tajiri sana kwa mifugo,
kwa fedha na kwa dhahabu .
Mwa 13:2.

Maana mmejua Neema ya Bwana wetu, Yesu Kristo,
jinsi alivyokuwa masikini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajri. Ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
2Kor 8:9

… mkitajirishwa katika vitu vyote, mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani
kwa kazi yetu.
2Kor 9:11.

… Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
Fil 4:19)

… Maana yeye yule ni Bwana wa yote, mwenye utajiri kwa wote wamuitao; kwa kuwa,
kila atakayeliitia jina la Bwana ataokoka.
Rum 10:12.

Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula
katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi, mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni,
na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye,
wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba,
asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi
ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.
Malaki 3:10 – 12.

Thawabu ya unyenyekevu, ambao ni kumcha Bwana, ni utajiri na heshima, nayo ni uzima.
Mith 22:4.

Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya
maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya dunia;
na baraka hizo zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.

Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani, utabarikiwa na uzao wa tumbo lako,
na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo. Maongeo ya Ngombe wako,
na wadogo wa kondoo zako: utabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.

Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo Bwana atawafanya adui zako wainukao
juu yako kupigwa mbele yako watakutokea kwa njia moja;

lakini watakimbia mbele kwa njia saba. Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika
ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako;

naye atakubariki katika nchi akupayo Bwana wako Mungu wako. Bwana atakuweka
uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia;

utakapoishika maagizo ya Bwana Mungu wako na kutembea katika njia zako na
mataifa yote ya dunia watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa
na hofu kwako.

Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri,
katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako, na uzao wa nchi yako, kama Bwana alivyowaapia baba zako kwamba atakupa.

Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni Mbingu,
kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake,

na kwa kubariki kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi wala hutokopa wewe.

Bwana atakufanya uwe kichwa wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini;
utakapo yasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo
kuyaangalia na kuyafanya;

msipokengeuka katika maneno niwaamuruo leo kwa lolote, kwenda mkono
wa kuume wala wa kushoto kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia.
(Kumb 28:1-14)

Damu ya msalaba iliyoondoa dhambi, ndiyo iliyoondoa umasikini pia, Yatupasa kuuona
umasikini kama tunavyoiona dhambi. Umaskini
ni matokeo ya anguko la mwanadamu katika dhambi.

Tukiisha okolewa katika dhambi, yatupasa kuokolewa katika umasikini pia.
Utajiri ni matunda ya msalaba kama ilivyo wokovu.

Yatupasa kuchukia umasikini kama tunavyochukia dhambi.
Kifo cha Yesu, kitakuwa hakina maana kamili,

kama tutaokolewa katika dhambi, halafu tubaki maskini katika mwili pia, wakati Yesu
aliyefia dhambi, ndiye aliyefia umasikini pia.

Msalaba ulifanya vyote, yaaani uliondoa dhambi na umasikini pia.
Biblia inasema;
“Maana mmejua Neema ya Bwana wetu, Yesu Kristo,
jinsi alivyokuwa masikini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri. Ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
2Kor 8:9.

… mkitajirishwa katika vitu vyote, mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.
2Kor 9:11.

JE UMEOKOKA?
UMEOKOLEWA KATIKA HUKUMU IJAYO?

Yesu alikuja kutafuta na kuokoa sisi tuliopotea.
Ndio maana alileta wokovu. Kuokoka si dini Fulani au dhehebu Fulani. Kuokoka uzima wa milele ndani ya mtu. “Amini , amini,

nawambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka, yuna (ana) uzima wa milele; wala haingii hukumuni,
bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani”.

Ina maana AMEOKOKA kutoka mautini (jehanum).

Jehanum ndio mauti ya pili.

(Ufu 20:14-15)
Watu wengi wnadhani kutokunywa pombe, kutovuta sigara, kutofanya zinaa, kutoiba,
n.k

ndio kuokoka na hukumu ya Mungu. Wengi wanadhani, kwenda kanisani, kuimba kwaya,
kuhubiri, kuwa mzee wa kanisa au kiongozi wa kikundi, n.k ndio kuokoka na hukumu ya Mungu.

Si kweli. Kuna wokovu halisi na matendo au maisha ya wokovu.

Watu wengi wanaishi maisha ya wokovu, lakini kwa uhalisi,
hawajaokoka bado, hawajampa Yesu mioyo yao na maisha yao. Kushika sheria
za dini na kuishi maisha ya wokovu, siko kunakompendeza Mungu, kama huyo mtu hajampokea
Yesu na kumwamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.

Yesu alisema hivi kwa Mungu Baba, “ Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe,
Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma”
Yoh 17:3.

Hatuokoki na hukumu ya Mungu kwa kushika sheria, bali kwa kuipokea neema ya wokovu kwa kumwamini Yesu Kristo.

“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa
njia ya imani, ambayo hiyo haitokani na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu (zawadi).
Wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu
Efe 2;8-9.

Kushika sheria za dini na kuishi maisha ya wokovu, siko kunakompendeza Mungu,
kama huyo mtu hajampokea Yes una kumwamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.

“hali tukijua ya kuwa,
mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu;

Sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala
si kwa matendo ya sheria. Maana kwa matendo ya sheria, hakuna mwenye mwili
atakayehesabiwa haki”
Gal 2:16; Gal 3:7-14.

Kuna wokovu halisi na matendo au maisha ya wokovu.
Watu wengi wanaishi maisha ya wokovu, lakini kwa uhalisi,

hawajaokoka bado, hawajampa Yesu mioyo yao na maisha yao.

Kuna habari ya mtu wa namna hiyo katika Biblia; aliye shika sheria, aliyedumu katika sala, aliyefunga na kuomba,
aliyetoa sadaka nyingi kwa watu maskini, n.k

lakini alikuwa hajafanya hatua muhimu kuliko zote ya kumwamini na kumpokea Yesu Kristo,
ilia pate uzima wa milele na kuokolewa. Aliitwa Kornelio.

Isome katika
Matendo ya Mitume 10:1-8, 23-48.

Mungu akamhurumia kuwa, japo amekuwa mwaminifu kushika sheria na kuishi
maisha ya kumcha Mungu, lakini kwasababu hajamjua Yesu bado, asingeokoka na hukumu ya milele, kwa maana
hana uzima wa milele.

Mungu akamtuma malaika kumwambia Kornelio,
amfuate Petro, naye atamweleza cha kufanya. Ndipo Petro akaja na akamweleza habari za Yesu, Kornelio na familia yake, wote wakamwamini na kumpokea Yesu.

Wakapata wokovu halisi (uzima wa milele).
Baada ya hapo, maisha ya wokovu ndipo yanakuwa na maana. Kushika sheria za dini na kuishi maisha ya wokovu, siko kunakompendeza
Mungu,
kama huyo mtu hajampokea Yesu na kumwamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.

Inawezekana nawe umekuwa mcha Mungu kama Kornelio,
lakini hujampokea Yesu moyoni na kumkiri.

Mpokee sasa!

Barikiwa sana hadi ushangae.

By Ev. Elimeleck S Nadashikiwe.

0 comments:

Post a Comment