Pages

Subscribe:

Monday, 3 April 2017

UTII UNA NGUVU KULIKO


Kumtii Mungu ni jambo la msingi sana katika maisha yetu,

akisema hata kama jambo ni gumu sana wewe tii tu kwa kuwa kamwe hafanyi jambo
hili kumkomoa mwanadamu, ila yeye ufanya yote kwa utukufu wake na hili kumfanya mwanadamu afurahie wema wake.

Kwa Ibrahimu ukiendelea kusoma utaona kuwa Mungu anamuambia kwa kuwa hakumzuilia mwanae pekee ni lazima ambariki.

Sauti ya Mungu wakati mwingine inakuja kinyume na
wewe ulivyo na waweza jiuliza mbona mimi nina vichache sana kwa nini amechagua mimi nitoe na si wale wenye navyo,

ila jawabu ni kuwa Mungu amekuheshimu na amechagua kukubariki ndiyo maana amekuchagua wewe kati ya wengi.

        Mathayo 19:21-22
“Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini,

Nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.

22 Yule kijana aliposikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa
na mali nyingi.”

Kutoa na kuacha unavyomiliki kwa ajili ya Mungu ni suala la kujikana,

kwa yule kijana alipoambiwa atoe alivyonavyo awape maskini aliondoka kwa kuhuzunika na akaona kuwa Mungu hamtakii
mema kwa kumuagiza kutoa vitu vyake,

ila laiti angejua siri iliyomkuta Ibrahimu na mjane
wa Sarepta basi angetoa naye kwa kuwa angepata maradufu ya vile alivyokuwa navyo.

       1 Wafalme 17:13-16
“Eliya akamwambia,
Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema;
lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao.

14 Kwa kuwa BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi,
Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha,

hata siku ile BWANA atakapoleta mvua juu ya nchi.

15 Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya;
na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi.

16 Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa
na neno la BWANA alilonena kwa kinywa cha Eliya.”

Kutoa si kuwa navyo vitu vingi sana ila hata vile vidogo ulivyonavyo Mungu anataka umtumikie navyo,
mjane wa Sarepta alidhani kuwa kutoa kwa ajili ya mtumishi wa Mungu ni mpaka
awe na vitu vingi sana ila sivyo Mungu anavyotaka kwa watu wake.

Kutoa ni moy na wala si wingi wa vitu ulivyo navyo. Kutoa ni muhimu sana kwa kuwa
ni kujiwekea hazina mbinguni ambapo nondo na kutu hawali,

kama isemavyo katika
Mathayo 6:19-21
“Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;
20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu,
wala wevi hawavunji wala hawaibi;

21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.”

Kutoa mbele za Mungu unajiwekea hazina mbinguni mahali ambapo utakuwa
ukiishi milele,

mfano mmoja aliutoa
Mzee Moses Kulola kwa kusema

“unakuta mtu anajisifu kuwa ana milioni kumi (10)
benki ana mali nyingi sana ila hana hazina yoyote mbinguni na ni bahiri katika kutoa,

ukimuuliza mtu huyu anaenda mbinguni, akifika bila shaka hata mahali pake kama
atapata bahati hiyo hakutakuwa na hazina halizojiwekea.”

Ukifahamu kuwa wewe duniani unapita kuelekea mbinguni weka juhudi katika siri hii pia.
Kutoa katika hali ya kawaida ni kama kupoteza ila ni njia ya kujazwa vingi zaidi,

ndiyo maana biblia usema kuwa “amfadhiliye/amsaidiaye maskini amkopesha BWANA”

Mungu anataka watu wake kujitoa kwa ajili ya kuifanya kazi ya injili na ana thamini sana wote wanaojitoa kwa ajili ya injili.

        Hagai 1,
Na BWANA uumizwa sana na watu wanaothamini
mambo ya nyumba zao na kusahau kazi ya nyumba ya BWANA.

Alisema nami mama yangu kuwa imenipasa
kujisikia vibaya na kuona aibu sana pale napopendeza na kuonekana nipo vizuri sana
huku wakitazama familia yangu na wazazi wangu hata kwa sehemu ndogo sana hatufananii,

yaani nimewaacha mbali sana na hata aibu kutambulisha kuwa ni wazazi wangu.

Lengo la nasaha hii kwangu mimi Ev. Elimeleck Ndashikiwe

ni kunihimiza
kuwa
"Nina wajibu wa kuwafanya wazazi wangu wang’ae na kupendeza hata watu wakitazama waone namna ninavyowajali na kuwahudumia".

Jitahidi uwe kielelezo na mtu wa kuigwa

2Tim 2:15......!

I love you my dears

By your friend
         Ev. Elimeleck S Ndashikiwe

0 comments:

Post a Comment