Na Peter M Mabula |
BWANA YESU asifiwe ndugu zangu.
Karibu tujifunze.
Ndugu Zangu Huu Ni Wakati Wa Mwisho.
Wakati Kibiblia Unaweza Kumaanisha Miaka
Kadhaa Ambayo MUNGU Ndie Ajuaye. Nyakati
Moja Inaweza Hata Kuwa Na Zaidi Ya Miaka
1000.
2 Timotheo 3:1-7, Lakini ufahamu neno hili, ya
kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za
hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda
wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu,
wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi
wao, wasio na shukrani, wasio safi,
wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya
suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali,
wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye
kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda
MUNGU; wenye mfano wa utauwa, lakini
wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao
katika nyumba za watu, na kuchukua mateka
wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi,
waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;
wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa
kuufikia ujuzi wa kweli.
Siku moja kama miezi miwili iliyopita nilikuwa
kwenye gari la abiria maarufu kama costa
nikitoka Kawe kwenda Ubungo, njiani kabla ya
kufika Mwenge kuna dada mmoja alipanda gari
na kukaa siti jirani na mimi, Dada yule alikuwa
anasoma Gazeti ambalo nilipoliangalia nililiona
kama jipya kwangu lakini la kidini, gazeti lile
lilikuwa na vichwa vya habari vizuri sana na
hakika ni gazeti linalovutia, nilitamani kulinunua
gazeti hilo jipya la kikristo ambalo hakika halina
udaku bali mambo mengi ya Biblia, nilimuomba
dada yule aniambie linauzwa wapi.
Nilipomwambia tu hivyo akanipa na kusema
nichukue tu maana yeye anayo mawili ya toleo
moja, muda kidogo yule dada akashuka kabla
hata ya Mlimani city, Nilimshukuru kwa tendo
lake jema la kunipa gazeti. Sikusoma kwa muda
huo bali nilikusudia kusoma nikifika ubungo, ni
kweli baadae nilianza kusoma na ndipo
nilipojisemea kwamba ''Mwisho wa dunia
umefika''. Gazeti hilo lilikuwa na kichwa cha
habari kimojawapo kiitwacho ''KRISTO
ANATAWALA NA KANISA'', Nilipenda kichwa cha
habari hicho lakini nilipofungua ndani kuhusu
ujumbe wa kichwa hicho cha habari nilikutana na
kasheshe ambalo sijawahi kulisikia kabla. Yule
Kristo anayetajwa sio BWANA YESU
tunayemfahamu mimi na wewe bali ni
mwanadamu mmoja ambaye kwa sasa ni
marehemu na alikuwa kiongozi wa dhehebu moja
la kikristo. huyo ndio anaitwa Kristo na licha ya
kufariki bado waumini wake wanajua kwamba
bado anatawala. Ufafanuzi wa taarifa hiyo ya
kishetani gazetini ni kwamba BWANA YESU ni
KRISTO wa kwanza lakini kizazi Hiki cha sasa
eti MUNGU ameletwa kristo wa pili ambaye ni
mwafrika wa Tanzania. Niliumia sana na kuwaza
mengi sana na binafsi hadi leo naamini kwamba
viongozi wa dhehebu hilo ni mawakala wa
shetani na wapo kwa ajili ya kuhakikisha
waumini wao hawaendi mbinguni. Waumini wa
dhehebu hilo mimi siamini kama huwa
wanasoma Biblia bali huwa wanasomewa tu.
Nilichojifunza ni kwamba dhehebu hilo halina
mpango wa waumini wake kwenda mbinguni. hili
dhehebu ni hatari kama wachawi walivyo hatari,
Hakika ni siku za mwisho.
Tunajua Kwamba Hizi Ni Siku Za Mwisho Kwa
Sababu Ya Dalili Zilizoko Kwenye Biblia. Kama
Wewe Unavyoweza Kujua Dalili Za Mvua Baada
Ya Kuona Mawingu Ndivyo Hivyo Mwisho
Umekaribia baada ya kila dalili kuonekana.
( 1 Yohana 2:18-23, Watoto, ni wakati wa
mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba
mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo
wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo
twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. Walitoka
kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama
wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi.
Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote
walio wa kwetu. Nanyi mmepakwa mafuta na
Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote.
Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo
kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba
hapana uongo wo wote utokao katika hiyo kweli.
Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa
YESU ni KRISTO? Huyo ndiye mpinga Kristo,
yeye amkanaye BABA na MWANA. Kila
amkanaye MWANA, hanaye BABA; amkiriye
MWANA anaye BABA pia. ).
Dalili za siku za mwisho ni nyingi, baadhi ni
hizi:
1. Wapingakristo watatokea:hawa ni dini au
watu binafsi ambao wanakataa ukombozi kupitia
YESU KRISTO.
2. Watu kuliacha fundisho la KRISTO.
-Waongo ni wale wanaomkataa YESU na jambo
la kukumbuka ni kwamba anayemkataa YESU
huyo anamkataa MUNGU, Hakuna mtu aliye
upande wa MUNGU kama amemkataa KRISTO
katika maisha yake.
Hakika Ni Siku Za Mwisho.
3. Makristo Wa Uongo Wameshakuja( Mathayo
24:5,Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu,
wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya
wengi. ).
-Wengi hata sasa wameshakuja waongo na
kuleta dini zao na wao kusimama kama nembo
(icon) ya dini hizo, hawa hujifanya wakombozi
wa watu na kwa hali hiyo hujifanya KRISTO.
-Wengi wanahubiri kama wanamhubiri KRISTO
lakini ndani yao wana ajenda za kuzimu za
kuwapotosha watu, hawawezi kukemea dhambi
wala kufundisha toba.
4. Manabii Wa Uongo Wapo Na Hawakawii
Kukwambia Kwamba YESU Atarudi Akiwa Shehe
( Mathayo 24:24-27, Kwa maana watatokea
makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao
watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate
kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi
wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo
nyumbani, msisadiki. Kwa maana kama vile
umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata
magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja
kwake Mwana wa Adamu. )
-Ndugu zangu, kuna watu hukimbilia miujiza,
ndugu zangu sio kila wafanya miujiza ni
watumishi wa MUNGU aliye hai, hata shetani
naye ana watumishi wake ambao anawatumia.
-Mtu akileta fundisho tofauti na fundisho la
KRISTO huyo ni nabii wa uongo.
-Wanaotangaza tarehe za kuja kwa YESU hao
ndio hata hawajui walifanyalo.
Ndugu zangu mwisho umekaribia ila hakuna
ajuaye siku wala saa, sisi tulichopewa kujua ni
dalili tu na hakika dalili huonyesha kwamba
mwisho umekaribia..
1 Petro 4:7 '' Lakini mwisho wa mambo yote
umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika
sala. ''
5. Nyakati Za Mwisho Watu Watapenda Pesa
Kuliko MUNGU Tena Wasaliti ( 2 Timotheo 3:1-7)
6. Nyakati Za Mwisho Watu Watasikiliza
Mafundisho Ya Mashetani
7. Watajitenga Na Imani
8. Na Watazuia Watu Kuoa
9. Na Watakataza Watu Kula Baadhi Ya Vyakula
1 Timotheo 4:1-4 ''Basi ROHO anena waziwazi
ya kwamba nyakati za mwisho wengine
watajitenga na imani, wakisikiliza roho
zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa
unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa
moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu
wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula,
ambavyo MUNGU aliviumba vipokewe kwa
shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo
kweli. Kwa maana kila kiumbe cha MUNGU ni
kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama
kikipokewa kwa shukrani; ''.
10. Siku Za Mwisho Watu Watajaa Dhihaka 2
Petro 3:3-4 '' Mkijua kwanza neno hili ya
kwamba katika siku za mwisho watakuja na
dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao
tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi
ile ya kuja kwake(YESU)? Kwa maana, tangu
hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa
hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa. ''
11. Watu wengi watakua Hawana ROHO
MTAKATIFU( Yuda 1:18-21, ya kwamba
waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho
watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata
tamaa zao wenyewe za upotevu. Watu hao ndio
waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio
na ROHO. Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya
imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika
ROHO MTAKATIFU, jilindeni katika upendo wa
MUNGU, huku mkingojea rehema ya BWANA
wetu YESU KRISTO, hata mpate uzima wa
milele. ).
Ndugu Zangu Wanamume Kwa Wanawake YESU
KRISTO Anatuita Kwenye Ufalme Wake. Amua
Vyema Leo Kwa KUOKOKA.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi
tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea
ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika
jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki
upotelee motoni anataka uende uzimani aliko
KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
0 comments:
Post a Comment