Pages

Subscribe:

Saturday, 5 September 2015

KATIKA SAA USIYODHANI, BWANA YESU YUAJA.

Na Peter M Mabula

BWANA YESU asifiwe.
Karibu tujifunze neno la MUNGU.
''kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari
kwa kuwa katika saa msiyodhani MWANA WA
ADAMU yuaja {Mathayo 24:44}
Ndugu Zangu,
Siku Ya BWANA I Karibu.
Siku Hiyo Hakutakuwa Na Mwanadamu Wa Kutoa
Udhuru, Hakutakuwa Na Wa Kujitetea "Kwa
Sababu Mambo Yasiyoonekana Na Kufahamika
Kwa Kazi Zake; Yaani, Uweza Wake Wa Milele
Na Uungu Wake; Hata Wasiwe Na Udhuru-
Warumi 1:20 .
Ndugu Utakaa Wapi Katika Maisha Yako Ya
Milele? .
Biblia Inasema
"Mwenye Busara Huyaona Mabaya Na Kujificha;
Bali Wajinga Huendelea Mbele Wakaumia-
Mithali 22:3" .
-Ndugu Yangu Je Wewe Ni Mwenye Busara Au
Mjinga?
Wajinga Wataumia Na Wenye Busara
Watajificha.
-Ndugu Zangu, Siku Ile Pa Kujificha Ni Sehemu
Moja Tu Yaani Kwa KRISTO.
-Ndugu, Nakuuliza Tena Je Wewe Ni Mwenye
Busara Au Mjinga? Hilo Unalijua Wewe Moyoni
Mwako Ila Kama Unataka Kuwa Mwenye Busara
"Mwamini BWANA YESU KRISTO, Nawe
Utaokoka-Matendo 16:31" .
Kama Unautaka Kweli Uzima Wa Milele
KUOKOKA NI LAZIMA. -Kukataa WOKOVU Wa
BWANA YESU Ni Kuukataa Uzima Wa Milele.
- Ndugu Amua Vyema Leo Na Utapata Raha
Nafsini Mwako. YESU Anakuita Leo, Itika Ndugu
Na Mpokee Awe BWANA Na Mwokozi Wa Maisha
Yako.
Dunia nzima wanaungojea ujio wa BWANA YESU,
Na katika saa usiyodhani atakuja, mtii MUNGU
na ishi kama neno la MUNGU linavyokuamuru.
Usijitenge na wokovu wa BWANA YESU maana
katika saa usiyodhani kuna kuondoka. na makazi
kama hujaokoka yatakuwa kuzimu ambapo
haitakiwi mtakatifu yeyote afike huko.
-Kama YESU Atakukwaza Kwa Jambo Lolote
Tambua Kwamba Wewe huuhitaji uzima wa
milele. Yeye anasema
'' Naye heri mtu ye yote asiyechukizwa nami.-
Luka 7:23 ''
-Ukiwa kwa MUNGU unakuwa hauko kwa
shetani.
Ukiwa nje ya MUNGU, moja kwa moja unakuwa
uko kwa shetani. Hakuna sehemu ya kati!
Na BWANA hawataki wote ambao wanasitasita.
Ufunuo 3:15 {Nayajua matendo yako ya kuwa hu
baridi wala hu moto ingekua heri kama ungekua
baridi au moto] -Tunapomchagua MUNGU
tuachane na ya shetani yote sio kwa MUNGU
50% na shetani 50%,
MUNGU BABA atuwezeshe tuchague YESU
KRISTO 100%
Ndugu, kuna kuitazamia hukumu mbaya kama
hatutautambua wakati huu kwamba ni wakati wa
kutubu na kuishi maisha matakatifu.
Kama unapanga kutubu baadae je unauhakika
hiyo baadae yako utakuwa hai?
Wengi walipanga kutubu wakiwa wazee lakini
hata uzeeni hawakufika na kujikuta wako
matesoni kuzimu.
Waebrania 10:26-27 '' Maana, kama tukifanya
dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile
kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;
bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na
ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.
''
Ndugu zangu, huu sio wakati wa kufurahia
dhambi, kama kuna dhambi ambayo unadhani
huwezi kuiacha nakuomba uende na kumweleza
mchungaji wako naye atakuombea. pia okoka na
kuomba maombi ya ushindi kupitia jina la YESU
KRISTO. Damu ya YESU ina mamlaka ya
kukuweka huru mbali na dhambi zilizokutesa
miaka mingi.
-Damu ya YESU inauwezo wa kuvunja
minyororo yote ya shetani iliyokua imekufunga
kama roho ya pombe, pepo la ngono,uongo,wizi
na chochote cha shetani ambacho ulidhani
haiwezekani wewe kukiacha kitu hicho, muhimu
ni kumpa YESU maisha yako ili uwe huru . -
mfanye BWANA YESU kuwa namba moja
maishani mwako ili uishi mbali na kuonewa na
nguvu za giza pia baada ya ulimwengu huu
upate uzima wa milele.
-Mfanye YESU kuwa rafiki yako wa karibu zaidi.
-kwa sababu YESU ndie rafiki yako wa karibu
zaidi usiache kumshirikisha chochote
kinachokusibu kwani yeye ni msaada wa karibu
sana. BWANA YESU anasema
Yohana 14:13-15 ''Nanyi mkiomba lo lote kwa
jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe
ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa
jina langu, nitalifanya. Mkinipenda, mtazishika
amri zangu. ''
-shetani asikuteke ndugu ukashindwa kwenda
kanisani bali mshinde na kumwaibisha kwa
kwenda kanisani ukiwa wa kwanza na tena tenda
mema sawasawa na neno la MUNGU.
Hakuna ambacho BWANA YESU hawezi
kukitengeneza na kikawa sawa. Sauli alikuwa
Jambazi muuaji aliyeshindikana lakini
alipokutana na BWANA YESU akageuka muhubiri
wa neno la MUNGU kwa mataifa.
-Kuna siku usiyoidhani huko mbeleni utaondoka,
je ukiondoka utaenda mbinguni? maana
mbinguni wanaingia watakatifu tu waliomtii
KRISTO enzi za uhai wao. je utakuwa mmoja
wao?
-Zishinde dhambi kwa kumwita BWANA YESU
akushindie.
-Zishinde dhambi kwa kuondoka katika baraza
za watenda dhambi.
-Zishinde dhambi kwa kukaa mbali na picha za
ngono pamoja na kuangalia filamu za nusu uchi.
1 Yohana 2:15-17 '' Msiipende dunia, wala
mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda
dunia, kumpenda BABA hakumo ndani yake.
Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya
mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima,
havitokani na BABA, bali vyatokana na dunia.
Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali
yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata
milele. ''
-Ndugu yangu, kama YESU amenibadilisha
mimi kutoka dhambi zote mbaya unazozifahamu
nina hakika anaweza kukubadirisha hata wewe
ili ufanyike mtoto wa MUNGU kupitia yeye.
changamka ndugu kwani wakati wa wokovu ni
sasa.
Yohana 3:16-21 '' Kwa maana jinsi hii MUNGU
aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe
pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali
awe na uzima wa milele. Maana MUNGU
hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu
ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika
yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini
amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu
hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na
hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja
ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko
nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.
Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia
nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake
yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli
huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane
wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU. ''
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi
tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea
ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika
jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki
upotelee motoni anataka uende uzimani aliko
KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

0 comments:

Post a Comment