Pages

Subscribe:

Saturday, 5 September 2015

KWANINI NI LAZIMA KULITAFAKARI NENO LA MUNGU USIKU NA MCHANA?

Na Mtumishi Peter Mabula

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Yoshua 1:8 “kitabu hiki cha Torati kisiondoke
kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake
mchana na usiku, upate kuangalia kutenda
sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa
humo……..)
Hapa tunaona jinsi Mungu alivyomtisitiza Joshua
kwa habari ya kulitafakari neno la Mungu usiku
na mchana .
Lengo la waraka huu mfupi kwako mpendwa
msomaji ni kukueleza sababu za msingi kwa
nini ni lazima na sio ombi kwamba usome na
kulitafakari Neno la Mungu usiku na
mchana.Kabla sijakueleza sababu nikupe tafasiri
ya Neno la Mungu kwa ufupi, neno la Mungu ni
jumla ya mawazo ya Mungu juu ya mwanadamu.
Ndani ya Neno kuna maamuzi (hukumu), sheria,
maagizo na njia za Mungu za kumtoa
mwanadamu katika shida aliyonayo,
kumfanikisha katika mambo yote na kumsaidia,
kuishi kwa kulishika shauri (kusudi) la Bwana.
Sababu hizo ni ;
(a) uweze kuelewa nini mawazo ya Mungu juu
yako .
Katika kitabu cha Yeremia 29:11 Mungu
anasema nayajua mawazo ninayokuwazi si
mawazo mabaya ………, sasa ili uweze kuelewa
Mungu anakuwazia nini ni lazima usome kwa
kulitafakari neno lake ili upate anachokueleza
kuhusu maisha yako, huduma, kazi, biashara nk.
(b) upate kuifanikisha njia yako.
Yoshua 1:8b. Mungu anasema nitakufundisha na
kukuonyesha njia utakayoiendea ………….( Zaburi
32:8), kumbuka kila mmoja ana njia yake ya
kupita ili kilitumikia shauri la Bwana. Sasa ili
uweze kufanikiwa katika njia yako ni lazima
usome na kulitafakari Neno la Mungu maana ni
taa ya miguu yako. Zaburi 119:105.
(c) usimtende Mungu dhambi .
Zaburi 119:11. mwimbaji wa zaburi anasema,
moyoni mwangu nimeliweka neno lako ili
nisikutende dhambi. Neno linawekwa moyoni
kwa kulitafakari. Kadri unavyolitafakari
kimapana ndivyo linavyokusaidia na kukulinda
na dhambi. Litakuonyesha hila na mitego ya
dhambi ya shetani, na litakupa ushindi kwa kila
ushawishi wa adui.
(d)Ili uongezeke kiimani.
warumi 10:17. Ikiwa chanzo cha Imani ni
kusikia, na kusikia huja kwa neno la kristo,
maana yake kadri unavyolisoma na kulitafakari
Neno la kristo mara kwa mara, kisha
ukajitamkia mwenyewe ili ulisikie hii ina maana
lazima imani yako itaongezeka tu.
(e)Neno limebeba jibu la mahitaji yako.
Zaburi 107:20. kwa kuwa ndani ya neno kuna
mawazo na njia (mikakati) ya kukufanikisha
kimaisha, hii ina maana, unapolitafakari licha ya
kuelewa mipango ya Mungu juu yako, pia
utaelewa na njia za Mungu za kukuondoa katika
shida uliyo nayo kiroho, kimwili, kindoa ,
kibiashara nk.
(f)uweze kustawi sana .
Yoshua 1:8b, Biblia inapozungumzia kustawi ina
maana ya kutawala na kumiliki vema, kimapana
yale ambayo Mungu ameyaweka chini yako .Mtu
ambaye ndani yake amejaa Neno la Mungu kwa
wingi huyo ana uwezo mkubwa sana wa kutawala
na kuongoza watu pia.
(g)Litakupa miaka mingi duniani . Mithali 3:1.
Ukilitafakari Neno la Mungu katika maisha
yako.Neno litakupa miaka mingi ya amani
(mafanikio) hapa duniani na kila ulifanyalo
litafanikiwa.
(h)uwafundishe wengine kumjua Mungu.
kumbukumbu 6:1-10. Mungu anataka watu
wamjue yeye, kwa hiyo pindi unapotafakari
anajifunua kwako, akajifunua kwako anataka
uwaambie na wengine jinsi alivyo na ukuu wake
ili wasimsahau yeye
Naamini baada ya kuwa umejua umuhimu wa
kusoma na kutafakari Neno la Mungu usiku na
mchana, utaamua kuanza pia kulisoma na
kulitafakari usiku na mchana.
Ubarikiwe sana.

0 comments:

Post a Comment