Pages

Subscribe:

Wednesday, 23 September 2015

NGAO YA IMANI KWA MWAMINI

16 zaidi ya yote mkiitwaa NGAO YA IMANI, amabayo kwa hiyo Mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu” (efe. 6:16) Bwana Yesu asifiwe! Ujumbe huu umekufikia kwa kusudi kabisa na ninaamini Mungu atakusaidia na utatoka hatua moja kwenda nyingine. Hebu chukua nafasi twende tujifunze pamoja na ni maombi yangu kwamba Mungu akufunulie akili zako ili uelewe kile ambacho anakwenda kutufundisha! Kabla ya yote ni muhimu ufahamu kwanza juu ya imani maana tunachojifunza hapa ni jinsi ya kuitumia imani kama ngao wakati shetani atakapokutupia mishale yake yenye moto. Biblia inasema,”1 Basi imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo, Ni bayana ya mambo yasiyoonekana” (ebr.11:1) Sikiliza tafsiri nyingine kutoka katika Kiswahili cha kisasa biblia inasema hivi,“kuwa na imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayoyatumainia Kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona” Kwa hiyo kuwa na IMANI ni kuwa na HAKIKA ya mambo uanayoyatarajia au unayoyatumainia. Kwa maana hiyo imani ni sasa hata kama kitu unachotarajia hakipo imani inabaki kuwa sasa, imani inaleta mambo unayoyatarajia kuwa halisi hata kama hujakiona kile kitu! Kitu kingine unachopaswa kujua ni chanzo cha imani na unisikilize hapa nikwambie kitu, kila imani chanzo chake ni kusikia haijalishi ni imani ya kimungu au la zote chanzo chake ni kusikia! Angalia Biblia yako katika kitabu cha warumi 10:17, “17 Basi imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia Huja kwa neno la Kristo” Kwa nini nataka uelewe chanzo cha imani? Ni kwa sababu watu wengi sana wamekuwa wakiomba kwa Mungu ili waweze kuwa na imani na wengine wamejaribu hata kufunga wakiomba imani, sikiliza ndugu yangu! Imani chanzo chake ni kusikia na si kusikia tu bali kusikia kunakotokana na neno la Kristo, kwa hiyo kama imani chanzo chake ni kusikia kunakotokana na neno la Kristo basi huwezi kuwa na imani kama huna neno la Kristo! Nimesema hivi huwezi kuwa na imani kama hauna neno la kristo! Ndiyo, ni lazima uwe na neno la Kristo ambalo kwa hilo utaamini kile unachoamini! Imani lazima iwe na kitu cha kushikilia huwezi ukaamini kitu from no where lazima uwe na kitu kinachokufanya ushikilie hicho unachoamini na hicho kitu kinaitwa neno la kristo au neno la Mungu (haleluya!) Ngoja twende kwa mifano utanielewa tu,angalia rumi 4:17-21 inasema hivi, “17 Kama ilivyoandikwa,nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi;mbele zake yeye aliyemwamini, Yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu,ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako. 18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa,ili apate kuwa baba wa mataifa mengi,kama ilivyonenwa,ndivyo utakavyokuwa uzao wako.19 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani,alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwishakufa,(akiwa amekwishakupata umri wa miaka mia),na hali ya kufaya tumbo lake sara. 20 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwaimani,akimtukuza Mungu;21 huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi”. Nitafafanua vizuri hii habari huko mbele lakini nachotaka uone hapo ni hiki chanzo cha imani ni kusikia neno na kama ni hivyo chanzo cha imani ni neno la Mungu na utaona kwenye habari hiyo hapo juu ibrahimu alikuwa na miaka mia na mpaka anafikisha miaka mia hakuwa na mtoto lakini kama ni msomaji mzuri wa biblia utakumbuka kuna maneno aliyatamka Mungu kwa ibrahimu huko nyuma kuhusu mtoto na biblia inasema Ibrahimu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kuwa ni haki kwake. Ilipita miaka mingi na ibrahimu hakuwa na mtoto kwa hiyo kama mwanadamu alianza kufikiri hali ya mwili wake(uzee alionao maana alishafikisha miaka mia) akafikiria na hali ya kufa kwa tumbo la mkewe sara maana kibinadamu sara hakuwa na uwezo wa kubeba mimba tena, lakini akiiona AHADI ya MUNGU, hakusita kwa kutokuamini bali ALITIWA NGUVU kwa imani……….. sikiliza! hapo anaposema akiiona ahadi ya Mungu umeshawahi kujiuliza ni ahadi gani hiyo? Na anaposema alitiwa nguvu umeshajiuliza alitiwa nguvu na kitu gani? Sikia ahadi aliyokuwa akiiona Ibrahim ilikuwa ni NENO ambalo Mungu alimuahidi huko nyuma na kwa neno hilo imani ya Ibrahim ilijengwa hapo,(kumbuka nataka uelewe chanzo cha imani ili uache kufunga na kuomba imani)! Na kwasababu neno hilo ambalo imani ya Ibrahim ilijengwa hapo ndilo lilikuwa likimpa Ibrahim nguvu ya kuendelea kuamini japokuwa uzee ulikuwa umemlemea na hali ya kufa kwa tumbo la mkewe Sara ilikuwa inamzonga lakini akiiona ahadi ya Mungu (neno) hakusita kwa kutokuamini bali alitiwa nguvu! (haleluya!) Biblia inasema imani huja kwa kusikia wala haijasema imani huja kwa kufunga na kuomba na hata ukiomba upewe imani Mungu atakupeleka kwenye neno lake tu ambalo ndiyo chanzo cha imani. Angalia mfano huu labda tutamalizia hapa kwa habari ya chanzo cha imani, luka 17:5,6 inasema hivi, “5 mitume wakamwambia Bwana, tuongezee imani. 6 Bwana akasema,kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali,mngeuambia mkuyu huu,ng’oka ukapandwe baharini nao ungewatii”. Unaona kitu ambacho mitume walikuwa wanaomba! Walikuwa wanaomba waongezewe imani lakini kumbe hata hiyo imani yenyewe amabayo wao walitaka waongezewe hawakuwa nayo hata kidogo! Ndo maana unaona Bwana anawaambia kama wangekuwa hata na hiyo imani ya kiasi cha chembe ya haradali wangeuambia mkuyu ng’oka ukapandwe baharini nao ungewatii, mi sijui kama unaelewa alichokuwa anamaanisha Bwana lakini kama unaisoma Biblia kwa kuitafakari mistari yake utagundua alichomaanisha Bwana ni kwamba imani ina chanzo chake ni kama mwanzo wa mti ambapo kwanza huanza mbegu ndogo sana lakini unapoipanda inakua na kuwa mti mkubwa sana. Kitu ni kilekile ukirudi kwenye somo tunalojifunza ni kwamba kama unataka kuwa na imani ni lazima uwe na mbegu ambayo ukiipanda itaota na kukua nakukufaya uwe na imani kubwa sana na hiyo mbegu ni neno la Mungu! Angalia kitabu cha luka 8:11 inasema, “11 Na huo mfano,maana yake ni hii MBEGU ni NENO la MUNGU” Hapo Yesu alikuwa akifafanua mfano wa mpanzi ambapo anafananisha moyo wa mtu na shamba (udongo) na mbegu anazifananisha na neno lake, kwa hiyo neno la mungu ni mbegu ambayo kama ukiipanda ndani ya moyo wako itakua na kuzaa matunda sawasawa na ulivyolipanda, ukipanda mahindi utavuna mahindi ukipanda neno la imani utavuna imani sawasawa na ulivyoamini! Ni matumaini yangu wewe uliyekuwa ukifunga na kuomba upewe imani utakuwa umepata kitu cha kukusaidia. Hebu sasa nikumbushe maneno ya Mungu yanayoongoza somo hili ambayo tunayapata katika efeso 6:16 inasema , “16 Zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani,ambayo kwa hiyo Mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu”. Hapa mtume Paul alikuwa anazungumzia silaha za Mungu ambazo wsomaji wengi wa biblia tumekuwa tukizisoma na tumekuwa tukifundishwa na watumishi wa Mungu lakini sijui kama umeshawahi kukaa ukatafari hizi silaha mojamoja! Sasa katika silaha alizotaja mtume paul mojawapo ni hii ngao ya imani na kumbuka kila silaha zilizotajwa kila moja ina kazi yake na wakati wake wa kuitumia na ndo maana paul mtume anasema mkiitwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo yaani hiyo ngao ya imani mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu (shetani). Kwa hiyo kama mristo unapaswa kuwa na silaha hii muhimu kabisa ili kujikinga na mishale inayorushwa na adui, hii siyo imani ya kusema namwamini Yesu kristo kama Bwana na mwokozi hii ni imani inayotumika kama silaha. Ok! wengi tunafahamu ngao ni nini? Ngao ni kifaa kinachotengenezwa maalum kwa ajili ya kumkinga mtu anayeitumia dhidi ya silaha zinazotoka kwa adui anaye au anaopigana nao na hii ni silaha ya zamani sana ambayo ilitengenezwa kwa kutumia miti au ngozi ngumu au shaba laikini vilevile hata sasa inatumika na baadhi ya makabila machache pamoja na askari wakati wanapozuia fujo za waandamanaji wanaorusha mawe chupa n.k. mtume paul ametumia mfano huu wa ngao ili kuwaelewesha watu waweze kumuelewa au kelewa kazi ya imani inapotumika kama silaha. Sasa unisikilize! Ninapozungumzia ngao ya imani ninazungumzia NENO LA IMANI. Usichanganyikiwe!!! Ndo maana hapo nyuma nimeanza kukufundisha kwanza imani na chanzo chake ili uweze kuelewa huku tunakokwenda. Sikia! hakuna NENO hakuna IMANI -hakuna MATENDO hakuna MATOKEO. Ili uweze kushindana na mwovu unahitaji kuvaa silaha za Mungu,ili uweze kuizima mishale yenye moto ya yule mwovu unahitaji kuwa na silaha inayoitwa ngao ya imani na labda utajiuliza hii mishale ya mwovu ni ipi au inakujaje na nitatumia vipi ngao ya imani? Swali zuri, sasa fungua biblia yako nikupe mifano ambayo itakutoa hatua moja kwenda hatua nyingine na ninaamini hautakuwa kama ulivyo bali utatoka imani hata imani, amen? Lakini kabla sijakupa mifano sikiliza maneno haya, “12 Piga vita vile vizuri vya imani,shika uzima ule wa Milele ulioitiwa,ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi” (1Timotheo 6:12) Ili uweze kupigana vita hivi vya kiimani ni lazima uwe na neno au maneno ya imani yatakayokuwa kwako kama ngao wakati adui atakapourushia mishale yake yenye moto! Angalia tena 1timotheo 1:18 inasema, “ 18 Mwanangu Timotheo nakukabidhi agizo hilo liwe akiba,kwa ajili ya MANENO ya unabii yakiyotangulia juu yako, ili KATIKA HAYO uvipige vile vita vizuri”. Sikiliza tafsiri nyingine ambayo inatupa ufunuo zaidi, inasema hivi, “ 18 Mwanangu timotheo, nakukabidhi amri hii kufuatana na maneno ya unabii Yaliyosemwa zamani juu yako. Yatumie MANENO HAYO yawe silaha yako katika

0 comments:

Post a Comment