Pages

Subscribe:

Sunday, 22 November 2020

NGUVU ILIYOKUWAMO NDANI YA UPENDO KUTUOKOA

MUNGU KWETU SISI NI KIMBILIO NA NGUVU
MSAADA UTAKAOONEKANA TELE NYAKATI ZOTE


Bwana Yesu Kristo asifiwe sana mtumishi wa Mungu,

Hakika ninapokaa na kuutafakari upendo mkuu ambao Mungu ameudhihirisha kwetu, macho yangu ya rohoni yanaona vitu vingi ndani ya huo upendo.

        Ndipo nilipogundua ya kwamba kumbe UPENDO ni kama kifurushi kilochotumika kubebea mahitaji ya wanadamu, au zawadi za watoto wa Mungu zitokazo kwa Mungu mwenyewe!


Ev. Elimeleck S Ndashikiwe



      Ndipo nikagundua ya kuwa ndani ya huo upendo kuna vitu vingi sana, nikaona moyo wa Mungu kwa kanisa, wokovu kwa kanisa, mavazi yatupasayo watoto wake vikiwa ndani ya huo upendo!


YOHANA 3:16

Kwa maana jindi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanae wa pekee ili tumuamini yaani tumpokee,

Tupate uzima wa milele uliokuwa umefichwa ndani ya Upendo!


        Msukumo wa kiMungu kutuhitaji wanadamu ili turudi kwenye njia yake, shabaha yake ilikuwa kwanza atuandalie vijizawadi ambavyo vitatushawishi na kuwa chambo kitupeleka kwenye wokovu!

       Pasipo upendo yawezekana angetumia njia nyingine, lkn aliona kuutumia upendo kama package au kifurushi inafaa! Akatununua kwa damu yake ya thamani ili tumuamini.


   KWA NINI TUMUAMINI?

Ni kwa sababu ulimwengu mzima ulikuwa umeigeukia miungu mingine na kuiamini,

        Mungu akaona kabisa haipendezi, ili atuondoe kwenye mikono ya imani nyingine ni lazima atuletee vizawadi vitakavyotushawishi kuvikimbilia kwake, tukishavikimbilia kwake tupate kumsikiliza,

Na tukishamsikiliza tu Imani yake mpya inaingia ndani yetu kwa upya tena, ndiposa tumuamini kwa kuwa chanzo cha imani ni kusikia, tena kulisikia Neno la Kristo.




      Mwamini leo Yesu Kristo kupotia Neno lake, nawe utapokea wokovu mkuu tuliodhihirishiwa bure kabisa!

Tusonge hapa;

              Zaburi 91

1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

2 Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.

3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.

4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.

5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,

6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,

7 Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.

8 Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki.

9 Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.

10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.

11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.

12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.


     Nawapenda sana tena sana, Mungu wa mbinguni akubariki sana wewe uliyejaaliwa kuusoma ujumbe huu!


    Na kama una maoni au swali lolote niulize kwa namba

+255 689 240 840


Inapatikana pia kwa njia ya WhatsApp.