Pages

Subscribe:

Thursday, 11 August 2016

UCHAWI UPO Acha Ubishi

MASHAMBULIZI KATIKA NDOTO  Lengo Kuu:
Kujua Jinsi gani wachawi hupambana na wanadamu kwenye ndoto

Lengo Mahususi:
Tunawezaje kuwashinda Mashambulio haya katika ndoto.
Tafiti zinaonesha kuwa,
Karibu kila aliyeuawa na nguvu ya wachawi aliota kwa namna moja au nyingine.

Ndoto hizo ni pamoja na kuota unapigwa risasi,
unagombana na mtu unayemjua au usiyemjua
anaweza akawa,
jirani,
mme,
mke,
mtoto n.k.

Ndoto nyingine ni pamoja na zile za kufukuzwa na vichaa,
kukimbizwa na wanyama wakali na hatimaye kukupa hofu sana.
Hizo ni roho ambazo wachawi huzitumia kujaribu imani yako na kupitia ndoto hizo hukushambulia sana.

Aidha,
inakupasa ujue kuwa endapo utakamatwa na vichaa hao wanaokukimbiza,
au kama ukianguka wakati unakimbizwa,
hiyo ni dalili ya kushindwa kwako.

Unapaswa kuomba Mungu sana na Kujifunika kwa damu ya YESU.
Pia,
kama unaota unaongea na watu waliokufa huku wakisema kuwa ni rafiki zako,
kutokewa na sauti za watu waliokufa hususani unapokuwa peke yako hata kama ni mchana,
jua hiyo ni mbinu ya kipepo kwa kuwa unatumiwa mizimu ili ije kukuita na kukutambulisha kuzimuni.

Ita jina la Yesu kwa kumaanisha ili ujiepushe na nguvu hizo zinazokufuatilia.

Ndoto nyingine zinazotumiwa ni sawa na zile za kuota uko porini peke yako,
kuota uko kwenye giza nene linalokupa hofu.

Pia,
kuota umeumwa na wadudu wakali kama siafu,
nge,
tandu,
nyuki,
manyigu,
nyoka na
mbwa
ni dalili mbaya hasa kwa wajawazito kwani huashiria kuchukuliwa kwa mtoto aliyeko tumboni,
hii husababisha mimba kuharibika zaidi karibu na kujifungua.

Pia ndoto zinazokuja zikikuonesha kuwa unajifungua alafu anaepokea mtoto humfaham,
au pengine unaona mikono tu ikipokea mtoto,
ni ndoto za kipepo ambazo zinachukua mtoto wako;
ndoto hizi zinaweza kupelekea mtoto kufia tumboni,
na hata wakati mwingine mama kupata kifafa cha uzazi ambacho kinaweza kusababisha kifo chake.

Jambo la msingi hapa,
ni kukemea nguvu zote za giza zilizokuzunguka,
huku ukiukabidhi ujauzito wako kwa Yesu ili aulinde wala adui asiweze kuuharibu.

Kwa kufanya maombi haya, unaweza kuzuwia kifo hiki,
unaweza kuzuwia upasuaji wakati wa kujifungua na unaweza kunusulu maisha ya mama na mtoto,
japo mara nyingi mtoto.

Kufanya hivi kunakupa usalama kutoka na ahadi ya neno la Mungu ya kuwa

“...kila atakayeliita jina la BWANA ataokoka” (Warumi 10:13).

Kuoka hapa maana yake ni Kunusurika, kuponea chupu chupu.
Unapaswa kujua kuwa jina la Yesu lina nguvu sana na lina mamlaka kamili juu ya vitu vyote duniani na mbinguni,

vinavyoonekana na visivyoonekana, hivyo kwa kufanya hivyo utakuwa umeahirisha msiba wako.

“Kwa kuwa katika yeye,
vitu vyote viliumbwa,
vilivyo mbinguni, na vilivyo juu ya nchi vinavyoonekana na visivyoonekana ikiwa ni vitu vya enzi au malaika, vyote viliumbwa kwa njia yake na kwaajili yake.” (Wakolosai 1:16,)”

...Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia jina lipitalo kila jina, ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni na vya nchi kavu....”
(Wafilipi 2:9-11)

Hatahivyo, pamoja na nguvu iliyoko kwenye jina la Yesu na mamlaka yote,
unapaswa kujua kuwa,
unapaswa kuishika haki yote ili kuweza kupata msaada huu yaani kuwa na imani na kusihi katika hali ya kumpendeza Mungu.

Pepo wanamjua Yesu,
na wanamwogopa,
ila hawashituliwi na anayetumia jina hilo kama hajashika haki kamili ya jina la Yesu.(Matendo 19:13-16)

“baadhi ya wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga mapepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na mapepo....
yule pepo mchafu akawajibu,
akawambia,

Yesu tunamjua na Paulo tunamfahamu, lakini ninyi ni nani?
Na yule mtu mwenye pepo mchafu akawarukia wawili,
akawaweza, akawashinda hata wakatoka mbio ili hali wa uchi na kujeruhiwa.”

Ninachotaka kukwambia hapa ni kuwa, unapaswa utambulike katika ulimwengu wa roho kwanza na hapo ndipo Jina la Yesu litakupa ushindi,
na ukisomeka kwa kuwa na jina la Yesu,

kila utakacho kiamuru kitakutii,
kutokana na mamlaka unayotumia ambalo ni jina la Yesu ambalo kila kilichoumbwa kinatii na kutetemeka mbele yake.

Unapaswa kujua kuwa,
kulitaja jina la Yesu bila kutambulika katika ulimwengu wa roho ni sawa na kuwa na simu isiyo na chaji japo kweli salio linatosha,
ila huwezi kupiga simu wala kutuma ujumbe wowote,
kwasababu hauko hewani;

hivyo basi unapaswa kuwa kwenye mtandao na malaika wa mbinguni ili kuambatana na jina la Yesu Kristo.

Na hii ndiyo maana Yesu mwenyewe anasema
“ninyi mkikaa ndani yangu,
na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote,
nanyi mtapewa” (Yohana 15:7).

Ndugu yangu,
naomba ni kwambie kuwa maombi yako daima,
yapeleke mbele za Yesu mwenyewe,
hapo ndipo utakapojibiwa,

naomba nikwambie kitu kimoja,
epuka mafundisho ya uongo ambayo maombi
yanapitia watu waliokufa eti kwa kuwa ni watatifu,

mitume au manabii wa zamani,
bibilia inasema
hayo ni machukizo mbele za Mungu, wala Mungu hawezi kuyajibu,
kwa kuwa anasema hayuko radhi na wapumbavu,
ebu omba kupitia Jina la Yesu kwa kuwa ndiyo anuani tuliyopewa.

Kuomba kupitia wafu au watu wengine kama
Paulo,
Isaya,
Bikra Maria
na Watakatifu wengine,
siyo njia sahihi,

ni sawa na mtu unampigia simu halafu, unakosea namba,
kimsingi hutampata,
nawaomba mbadilike,

liangalie neno la Mungu linavyosema, yapuuze mafundisho ya upotovu. Hayatakusaidia lolote.

Kwa upande mwingine,
unapoota unaumwa na mbwa au nyoka, au
kukimbizwa na wanyama hata wakakuangusha,
humaanisha kuwa uko dhaifu kiroho.

Pia,
unaweza kuota majitu yenye sura zisizo tambulika sahihi na pengine kuona vivuli vinakukaribia
au vinyago,
hii ni hatari sana kwani ni ishara ya kuwa adui yuko karibu yako,
anaweza akawa rafiki au hata ndugu na amekushinda kumtambua,
hivyo amekudhoofisha kiimani na karibu atakuangamiza.

Ndoto hizo pamoja na zile zakuota unaliwa na wanyama mwitu kama vile simba,
chui na
mbwa mwitu,
au kuota unachukuliwa hewani,
huweza kusababisha mtu kuvurugika akili na hata kuehuka.

Hii ni hatari sana,
kwani zinatumika sana kuangamiza watu kupitia njia hii.

Pia,
mara nyingi huweza kuota umetoka huko unatembea na watu ambao huwajui, aghalabu huongea vitu/lugha ambavyo huijui,
na wakati mwingine hujisikia unagandamizwa chini,

ukijaribu kupiga kelele au kuamka unashindwa,

zote hizi ni dalili za kulegea kiroho na huweza kukupelekea mashambulizi makubwa ambayo hukuotesha ndoto chafu huku ukiwa unalishwa vitu mara nyingi nyama,

ukifanya tendo la ndoa na watu usiowajua.

Hii huufanya mwili kuwa najisi na kuibomoa madhabahu ya roho mtakatifu anayekaa ndani yako,
hivyo mapepo kupata nafasi.

La msingi,
chukua hatua ya kufanya maombi ya muda mrefu usiku huo,
na anza maombi makavu yaani kufunga bila kula wala kunywa walau masaa kumi na mawili.

Fanya hivyo mara nyingi zaidi,
na tenga muda wa kusoma neno la Mungu,
huku ukilitafakari kwa kina.

Aidha,
jenga mazoea ya kuamka usiku na kuomba na kukemea nguvu zote za giza, huku ukiita ulinzi wa malaika wa Mungu. Kumbuka,

“....kushinda kwetu sisi si juu ya damu na nyama;
bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza hili,
juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” Efeso 6:12.

Pia,
Yesu mwenyewe anasema,
“Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge,
na nguvu zote za adui wala hakuna kitu cha kuwadhuru” Luka 10:19.

Mungu awabariki na kuwapa Ulinzi daima.
Akupeni uwezo wa kuzishinda njia zote za adui,
na mipango yote ya kipepo iwe chini ya nyayo zako.

Ameeeeeeen

Ni mimi ndugu yako
Ev. Elimeleck S. Ndashikiwe

UTANGULIZI HALI YA KANISA LA KWANZA Ahadi ya Yesu kwa Mitume Kitabu cha Matendo ya Mitume moja kwa moja kinaanza kutambulisha kusudi la kufufuka na kupaa kwa Bwana Yesu Kristo. Tukio linalosimuliwa ni namna ya kuzaliwa kwa kanisa (Mdo. 1.8). Kwamba kuzaliwa kwa kanisa na utume ni kazi ya Mungu kupitia Roho Mtakatifu ambaye anakuja kuendeleza kazi aliyoianzisha Yesu. Tukio la kupaa na ahadi ya Yesu kwa wanafunzi wake, inafuatiwa na tukio muhimu sana kwa Kanisa (Mdo. 2:1-10). Wanafunzi wanavuviwa na Roho Mtakatifu na kupata nguvu kama ahadi ya Yesu ilivyosema. Kuanza kwa Kanisa la Kwanza Kwa tukio hili, kasi ya kuineza injili kwa ujasiri mkubwa wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Kwa njia ya Roho Mtakatifu, Mitume walitambua na kuelewa hasa maana ya huduma ya Yesu Kristo kwa ulimwengu na kuanza kuihubiri injili kwa watu wote. Kituo kikuu cha umisheni kilikuwa Yerusalem kama walivyoagizwa na Yesu. Lakini kutokana na upinzani mkubwa ulioongozwa na makundi ya dini ya kiyahudi ilipelekea Injili kwenda nje ya Yerusalem na kupokelewa zaidi. Kanisa matesoni Kasi ya kukuwa kwa kanisa, kama nilivyokwisha sema hapo juu, inaletea kanisa kukutana na uadui na kusababisha kuuwawa kwa baadhi ya mitume. Kifo cha Stephano ni mfano mkuu dhidi ya vifo vingi ambavyo vilitokea wakati huo. Ikumbukwe kuwa wakati huu utawala wa dola ya kirumi ulichangia pia kudhoofu nguvu ya ukuaji wa neno la Mungu kupitia mitume (Mdo. 4-7). HISTORI YA MAISHA YA PAULO Sauli kama Falsayo Historia ya Paulo, inatambulishwa mara ya kwanza kama kijana mtesaji wa kanisa, wakati wa kifo cha Stefano alikuwepo. Lakini kimsingi Paulo alikuwa mmoja wapo katika kundi la mafarisayo. Kundi ambalo lilikuwa kinyume na mafundisho yake Yesu Kristo na Mitume ambao walitumika kuendeleza kazi au utume huo. Paulo ambaye ni Sauli aliamini kwamba Mungu ni mmoja, na muumbaji wa vitu vyote. Imani aliyoikiri kama myahudi, mwebrania na falisayo. Kwamba Mungu katika kuhusiana: watu na ulimwengu alijitenga mbali zaidi, ili aweze kutawala kila kitu na kwa kupita malaika wake. Na baadhi ya malaika wake hawakuwa waaminifu hata kutenda dhambi ‘uasi’ (Kol. 2.15). Na uovu uliingia kwa mwanadamu wa kwanza Adam (Rum. 5.12). Mambo mengine kama sabato, torati, familia, na mifumo mbalimbali ya maisha katika jamii ya kiyahudi alijifunza na kuyashika sawa sawa. Sauli kama Mtesi wa Kanisa Kwa kutekeleza sera ya dini yake, Sauli aliongoza makundi ya kuwakamata, kuwafunga, kuwatesa na kuwauwa mitume kwa lengo la kuteketeza utume uliasisiwa na Yesu (8.1-3). Kutokana na adha hiyo, wanafunzi walikimbia Yerusalem na kwenda mbali huko na huko walifuatwa na kukamatwa na hata kuuwawa. Mateso hayo yalisaidia sana kukuwa kwa kanisa, kwani kutokana na hofu, mitume walitawanyika sehemu mbalimbali bila kuacha kuitangaza injili (8.1). Kwa ujumla Sauli alizaliwa Tarso, mji ulikuwa nje ya Palestina chini ya utawala wa Kirumi, Lugha iliyotumika ni kiyunani na kirumi (Greceo Romana). Lakini kwa asili alikuwa myahudi wa kabila la Benjamini (Fil. 3.3-5). Kuongolewa kwa Sauli Katika mpango wake wa kwenda Dameska kuwaangamiza mitume, njiani alikutana na muujiza ulio badili maisha yake. Sauli anakutana na ufahamu tofauti juu ya Yesu Kristo ambaye alitambua kuwa alikufa na hakufufuka (9.1-19; 22.1-22 na 26.9-23). Uzoefu huu unafanya mapinduzi makubwa katika maisha yake. Anaongolewa katika imani ya Kikristo, anabatizwa, na kupokelewa katika kanisa la Dameska (9.10-31). Yesu alimtuma kuifanyakazi ya injili kama chombo kwa mataifa (9.15). Kumbuka kuwa Sauli alizaliwa na kukulia Tarso ambako wenyeji wake ni wayunani na kwa uchache sana wayahudi waishio Tarso. Majina yote hayo mawili yana maana sawa kwa ujumla wa utofauti wa matumizi kwa makabila haya. Sauli ni jina la Kiyahuidi lenye maana ‘kijana nadhifu wa akili’ kwa kiyunani ‘saulos’ lilikuwa tusi – ujinga. Paulo ni jina la asili ya Kiyunani lenye maana sawa na Sauli kwa kiebrania ‘mjuvi wa mambo’. Hivyo Sauli aliamua kutumia jina la kiyunani ili isiwe kwazo kwao na bado ikawa sawa kwa kabila lake mwenyewe. HUDUMA NA UTUMISHI WA PAULO Mwanzo wa huduma ya Paulo Paulo alikutana na upinzani mkubwa kutoka kwa mitume, kwani hawakuamini kabisa juu ya kuongolewa kwake, ilimpelekea Paulo kuondoka Yerusalem si tu kwa kuwaepuka wanafunzi wa Yesu ila pia kuwatoroka mafarisayo wenzake. Aliondoka na kurudi nyumbani kabla ya kuanza huduma kamili. Pamoja na kuwa katika hali ya upinzani wa ndani, Paulo hakuacha kumshuhudia Kristo. Baada ya kuokolewa 32 BK, Paulo aliishi na kuhubiri Damaska kwa muda wa miaka mitatu 32 – 35 BK (Gal. 1.15-19 na Mdo. 9.20-25). Paulo alifanya ziara ndogo kwenda Yerusalem 35 BK, na ilifuata baraza la mitume, na kurudi tena mjini alikozaliwa (Mdo. 9.26-31). Paulo alibakia Tarso kwa muda wa miaka nane 35-44 BK. Hakuna shaka kuwa alifanyakazi ya Injili kwa wayahudi wa uhamishoni na wayunani pia. Kwa kipindi hiki, idadi ya wakristo na makanisa iliongezeka mara dufu. Hata Mitume kule Yerusalem walimtuma Barnaba kwenda Antiokia kukutana na Paulo kwa ajili ya kazi ya injili kati ya mwaka 45 na 46 (Mdo. 11.19-30). Waliondoka Antiokia na kuelekea mbali zaidi kuihubiri injili katika maeneo yote ya utawala wa kirumi hasa waliozungumza kirumi na kiyunani (Mdo. 13.1-3). Siku za Paulo kama mchungaji zilikamilika. Paulo alikuwa akihudumu kama msafiri mmisionari katika ulimwengu wa wakati wake. Safari za Paulo za Kimitume Paulo kama mtume wa mataifa alifanya safari kubwa tatu; safari ya kwanza ilifanyika mwaka 47 – 49 BK, alipeleka ujumbe wa neno la Mungu pande za Syria na Asia ndogo (Mdo. 13-14). Safari ya Pili na ya tatu zilifanyika 49 -52 BK na 52-57 BK. Ambako alisafiri kuelekea maeneo ya Asia ndogo, Makedonia na uyunani yote (Mdo. 15.38-18.21 na 18.22 – 21.16. Kama matokeo ya juhudi za Paulo katika kuhubiri na kufundisha; wayunani wengi walimgeukia Kristo na kuanzishwa kwa makanisa mengi madogo madogo. Kutumika kwa Paulo kama mtume kwa mataifa, kulileta sintofahamu kati ya wayahudi juu ya kuwatambua wayunani kama wamoja katika imani yake Kristo. Wakristo ambao walikuwa bado katika kifungo cha kanuni za kiyahudi, ndio walioleta shida katika kuwajumuisha wayunani kushiriki Baraka za neema ya Mungu ya wokovu. Paulo alishambuliwa hata kuuwawa na kundi hilo (Mdo. 21-22). Masingizio mengi yalimkabili Paulo ili mradi akatishwe tamaa ya kuupeleka ujumbe wa Mungu kwa mataifa. Alikamatwa na kuwekwa gerezani huko Yerusalem na kisha akahamishiwa Kaisaria kwa miaka miwili 59-59 BK (Mdo. 23-24). Paulo alitumia nafasi ya uraia wake na sifa ya kuzaliwa kwake kujitetea panapotokea utatanishi wa uamuzi wa mashitaka yake (Mdo. 25.1-12). Paulo alifungwa Rumi kwa miaka miwili 59-61 BK. (Mdo. 28.17). hadi mashitaka dhidi yake yalipofutwa na kuachwa huru. Mara akatoka kifungoni, Paulo aliendelea kuihubiri injili pembezoni mwa viuga vya Spaini na mji wa Rumi. Lakini mwaka 54-68, Mfalme Nero wa Rumi alikuwa na mpango wa mauji na mateso makali kwa wakristo na kufanikiwa kumuuwa Paulo mnamo mwaka 68 BK. Nyaraka za Paulo Kimsingi, Paulo aliwezeshwa sana kuandika Nyaraka mbali mbali si kwa lengo la vitabu, bali kufundisha, kukumea na kusahihisha makosa ya uelewa wa mafundisho yake kwa njia ya barua. Nyaraka alizoziandika hazikuwa zenye mtazamo ya kitheologia kama hivi leo, bali ulikuwa ni ujumbe wa moja kwa moja kwa makundi husika na eneo husika ikiambatana na ujumbe tarajiwa. Paulo aliweza kuandika nyaraka nyingi zaidi ya nyaraka tuzisomazo katika Biblia. Nyaraka hizo zilipitishwa na kanuni za maandiko ili zitumike kama sehemu ya nyaraka zilizobeba ujumbe wa wokovu wetu. Vyaraka zipatazo 13 ziliandikwa na Paulo mwenyewe, ya mkini waraka kwa Waebrania, Paulo aliuandika pia. Wapo wanazuoni wanasisitiza kuwa si Paulo aliyeandika ila chanzo kikuu ni makuhani kwa vile kina mazingira ya kikuhani zaidi. Lakini watheoligia wa sasa wanapendekeza uandishi wa waraka huo ni kazi ya Paulo iliyokusanywa na kuhaririwa na ama Luka, Apollo, au Barnaba, kwa lengo la kuwaabarisha wayahudi wa uhamishoni juu ya msingi wa imani yao juu ya Wazee wa imani, Kristo Yesu, Hekalu ufalme wa Mungu na kanisa Nyaraka zilizoandikwa kwenye makundi maalum ya wakristo; Warumi, 1 na 2 Wakorinto, Wagalatia, Wafilipi, Wakolosai, 1 na 2 Wathesalonike.