Pages

Subscribe:

Thursday, 11 August 2016

UTANGULIZI HALI YA KANISA LA KWANZA Ahadi ya Yesu kwa Mitume Kitabu cha Matendo ya Mitume moja kwa moja kinaanza kutambulisha kusudi la kufufuka na kupaa kwa Bwana Yesu Kristo. Tukio linalosimuliwa ni namna ya kuzaliwa kwa kanisa (Mdo. 1.8). Kwamba kuzaliwa kwa kanisa na utume ni kazi ya Mungu kupitia Roho Mtakatifu ambaye anakuja kuendeleza kazi aliyoianzisha Yesu. Tukio la kupaa na ahadi ya Yesu kwa wanafunzi wake, inafuatiwa na tukio muhimu sana kwa Kanisa (Mdo. 2:1-10). Wanafunzi wanavuviwa na Roho Mtakatifu na kupata nguvu kama ahadi ya Yesu ilivyosema. Kuanza kwa Kanisa la Kwanza Kwa tukio hili, kasi ya kuineza injili kwa ujasiri mkubwa wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Kwa njia ya Roho Mtakatifu, Mitume walitambua na kuelewa hasa maana ya huduma ya Yesu Kristo kwa ulimwengu na kuanza kuihubiri injili kwa watu wote. Kituo kikuu cha umisheni kilikuwa Yerusalem kama walivyoagizwa na Yesu. Lakini kutokana na upinzani mkubwa ulioongozwa na makundi ya dini ya kiyahudi ilipelekea Injili kwenda nje ya Yerusalem na kupokelewa zaidi. Kanisa matesoni Kasi ya kukuwa kwa kanisa, kama nilivyokwisha sema hapo juu, inaletea kanisa kukutana na uadui na kusababisha kuuwawa kwa baadhi ya mitume. Kifo cha Stephano ni mfano mkuu dhidi ya vifo vingi ambavyo vilitokea wakati huo. Ikumbukwe kuwa wakati huu utawala wa dola ya kirumi ulichangia pia kudhoofu nguvu ya ukuaji wa neno la Mungu kupitia mitume (Mdo. 4-7). HISTORI YA MAISHA YA PAULO Sauli kama Falsayo Historia ya Paulo, inatambulishwa mara ya kwanza kama kijana mtesaji wa kanisa, wakati wa kifo cha Stefano alikuwepo. Lakini kimsingi Paulo alikuwa mmoja wapo katika kundi la mafarisayo. Kundi ambalo lilikuwa kinyume na mafundisho yake Yesu Kristo na Mitume ambao walitumika kuendeleza kazi au utume huo. Paulo ambaye ni Sauli aliamini kwamba Mungu ni mmoja, na muumbaji wa vitu vyote. Imani aliyoikiri kama myahudi, mwebrania na falisayo. Kwamba Mungu katika kuhusiana: watu na ulimwengu alijitenga mbali zaidi, ili aweze kutawala kila kitu na kwa kupita malaika wake. Na baadhi ya malaika wake hawakuwa waaminifu hata kutenda dhambi ‘uasi’ (Kol. 2.15). Na uovu uliingia kwa mwanadamu wa kwanza Adam (Rum. 5.12). Mambo mengine kama sabato, torati, familia, na mifumo mbalimbali ya maisha katika jamii ya kiyahudi alijifunza na kuyashika sawa sawa. Sauli kama Mtesi wa Kanisa Kwa kutekeleza sera ya dini yake, Sauli aliongoza makundi ya kuwakamata, kuwafunga, kuwatesa na kuwauwa mitume kwa lengo la kuteketeza utume uliasisiwa na Yesu (8.1-3). Kutokana na adha hiyo, wanafunzi walikimbia Yerusalem na kwenda mbali huko na huko walifuatwa na kukamatwa na hata kuuwawa. Mateso hayo yalisaidia sana kukuwa kwa kanisa, kwani kutokana na hofu, mitume walitawanyika sehemu mbalimbali bila kuacha kuitangaza injili (8.1). Kwa ujumla Sauli alizaliwa Tarso, mji ulikuwa nje ya Palestina chini ya utawala wa Kirumi, Lugha iliyotumika ni kiyunani na kirumi (Greceo Romana). Lakini kwa asili alikuwa myahudi wa kabila la Benjamini (Fil. 3.3-5). Kuongolewa kwa Sauli Katika mpango wake wa kwenda Dameska kuwaangamiza mitume, njiani alikutana na muujiza ulio badili maisha yake. Sauli anakutana na ufahamu tofauti juu ya Yesu Kristo ambaye alitambua kuwa alikufa na hakufufuka (9.1-19; 22.1-22 na 26.9-23). Uzoefu huu unafanya mapinduzi makubwa katika maisha yake. Anaongolewa katika imani ya Kikristo, anabatizwa, na kupokelewa katika kanisa la Dameska (9.10-31). Yesu alimtuma kuifanyakazi ya injili kama chombo kwa mataifa (9.15). Kumbuka kuwa Sauli alizaliwa na kukulia Tarso ambako wenyeji wake ni wayunani na kwa uchache sana wayahudi waishio Tarso. Majina yote hayo mawili yana maana sawa kwa ujumla wa utofauti wa matumizi kwa makabila haya. Sauli ni jina la Kiyahuidi lenye maana ‘kijana nadhifu wa akili’ kwa kiyunani ‘saulos’ lilikuwa tusi – ujinga. Paulo ni jina la asili ya Kiyunani lenye maana sawa na Sauli kwa kiebrania ‘mjuvi wa mambo’. Hivyo Sauli aliamua kutumia jina la kiyunani ili isiwe kwazo kwao na bado ikawa sawa kwa kabila lake mwenyewe. HUDUMA NA UTUMISHI WA PAULO Mwanzo wa huduma ya Paulo Paulo alikutana na upinzani mkubwa kutoka kwa mitume, kwani hawakuamini kabisa juu ya kuongolewa kwake, ilimpelekea Paulo kuondoka Yerusalem si tu kwa kuwaepuka wanafunzi wa Yesu ila pia kuwatoroka mafarisayo wenzake. Aliondoka na kurudi nyumbani kabla ya kuanza huduma kamili. Pamoja na kuwa katika hali ya upinzani wa ndani, Paulo hakuacha kumshuhudia Kristo. Baada ya kuokolewa 32 BK, Paulo aliishi na kuhubiri Damaska kwa muda wa miaka mitatu 32 – 35 BK (Gal. 1.15-19 na Mdo. 9.20-25). Paulo alifanya ziara ndogo kwenda Yerusalem 35 BK, na ilifuata baraza la mitume, na kurudi tena mjini alikozaliwa (Mdo. 9.26-31). Paulo alibakia Tarso kwa muda wa miaka nane 35-44 BK. Hakuna shaka kuwa alifanyakazi ya Injili kwa wayahudi wa uhamishoni na wayunani pia. Kwa kipindi hiki, idadi ya wakristo na makanisa iliongezeka mara dufu. Hata Mitume kule Yerusalem walimtuma Barnaba kwenda Antiokia kukutana na Paulo kwa ajili ya kazi ya injili kati ya mwaka 45 na 46 (Mdo. 11.19-30). Waliondoka Antiokia na kuelekea mbali zaidi kuihubiri injili katika maeneo yote ya utawala wa kirumi hasa waliozungumza kirumi na kiyunani (Mdo. 13.1-3). Siku za Paulo kama mchungaji zilikamilika. Paulo alikuwa akihudumu kama msafiri mmisionari katika ulimwengu wa wakati wake. Safari za Paulo za Kimitume Paulo kama mtume wa mataifa alifanya safari kubwa tatu; safari ya kwanza ilifanyika mwaka 47 – 49 BK, alipeleka ujumbe wa neno la Mungu pande za Syria na Asia ndogo (Mdo. 13-14). Safari ya Pili na ya tatu zilifanyika 49 -52 BK na 52-57 BK. Ambako alisafiri kuelekea maeneo ya Asia ndogo, Makedonia na uyunani yote (Mdo. 15.38-18.21 na 18.22 – 21.16. Kama matokeo ya juhudi za Paulo katika kuhubiri na kufundisha; wayunani wengi walimgeukia Kristo na kuanzishwa kwa makanisa mengi madogo madogo. Kutumika kwa Paulo kama mtume kwa mataifa, kulileta sintofahamu kati ya wayahudi juu ya kuwatambua wayunani kama wamoja katika imani yake Kristo. Wakristo ambao walikuwa bado katika kifungo cha kanuni za kiyahudi, ndio walioleta shida katika kuwajumuisha wayunani kushiriki Baraka za neema ya Mungu ya wokovu. Paulo alishambuliwa hata kuuwawa na kundi hilo (Mdo. 21-22). Masingizio mengi yalimkabili Paulo ili mradi akatishwe tamaa ya kuupeleka ujumbe wa Mungu kwa mataifa. Alikamatwa na kuwekwa gerezani huko Yerusalem na kisha akahamishiwa Kaisaria kwa miaka miwili 59-59 BK (Mdo. 23-24). Paulo alitumia nafasi ya uraia wake na sifa ya kuzaliwa kwake kujitetea panapotokea utatanishi wa uamuzi wa mashitaka yake (Mdo. 25.1-12). Paulo alifungwa Rumi kwa miaka miwili 59-61 BK. (Mdo. 28.17). hadi mashitaka dhidi yake yalipofutwa na kuachwa huru. Mara akatoka kifungoni, Paulo aliendelea kuihubiri injili pembezoni mwa viuga vya Spaini na mji wa Rumi. Lakini mwaka 54-68, Mfalme Nero wa Rumi alikuwa na mpango wa mauji na mateso makali kwa wakristo na kufanikiwa kumuuwa Paulo mnamo mwaka 68 BK. Nyaraka za Paulo Kimsingi, Paulo aliwezeshwa sana kuandika Nyaraka mbali mbali si kwa lengo la vitabu, bali kufundisha, kukumea na kusahihisha makosa ya uelewa wa mafundisho yake kwa njia ya barua. Nyaraka alizoziandika hazikuwa zenye mtazamo ya kitheologia kama hivi leo, bali ulikuwa ni ujumbe wa moja kwa moja kwa makundi husika na eneo husika ikiambatana na ujumbe tarajiwa. Paulo aliweza kuandika nyaraka nyingi zaidi ya nyaraka tuzisomazo katika Biblia. Nyaraka hizo zilipitishwa na kanuni za maandiko ili zitumike kama sehemu ya nyaraka zilizobeba ujumbe wa wokovu wetu. Vyaraka zipatazo 13 ziliandikwa na Paulo mwenyewe, ya mkini waraka kwa Waebrania, Paulo aliuandika pia. Wapo wanazuoni wanasisitiza kuwa si Paulo aliyeandika ila chanzo kikuu ni makuhani kwa vile kina mazingira ya kikuhani zaidi. Lakini watheoligia wa sasa wanapendekeza uandishi wa waraka huo ni kazi ya Paulo iliyokusanywa na kuhaririwa na ama Luka, Apollo, au Barnaba, kwa lengo la kuwaabarisha wayahudi wa uhamishoni juu ya msingi wa imani yao juu ya Wazee wa imani, Kristo Yesu, Hekalu ufalme wa Mungu na kanisa Nyaraka zilizoandikwa kwenye makundi maalum ya wakristo; Warumi, 1 na 2 Wakorinto, Wagalatia, Wafilipi, Wakolosai, 1 na 2 Wathesalonike.

0 comments:

Post a Comment