Pages

Subscribe:

Wednesday, 30 May 2018

BIBLE STUDY By Ev. Elimeleck S Ndashikiwe

Bwana Yesu asifiwe mtu wa MUNGU.

KARIBU TUJIFUNZE KUHUSU BIBLIA

     Biblia ni nini?
Biblia ni sauti ya Mungu iliyohifadhiwa kwenye maandishi.

         Sauti hii i hai hata leo ikifanya kazi ya kutufundisha, kutuonya makosa yetu, kutuongoza katika njia itupasayo kuiendea na
kutuadabisha katika haki
     (2 Timotheo 3:16).

Hivyo basi BIBLIA ni makusanyo ya vitabu vitakatifu vilivyohifadhi sauti ya Mungu.
        Na kwa sababu Biblia inatupa muongozo mzuri wa namna ya kumlingana Mungu kwanza kwa kumpokea Yesu Kristo,
kupitia hilo na ndio maana wengine husema kwamba
Biblia ni Katiba ya Mbinguni.

          Biblia ina mgawanyo wa Maagano mawili ambayo ni; 
Agano la kale ( vitabu 39 ) na
Agano jipya ( Vitabu 27)

A). AGANO LA KALE  (VITABU 39)
Neno “AGANO” ni mapatano/makubaliano ya kudumu baina ya watu wa pande mbili zaidi, au baina ya Mungu na watu wake.
       Makubaliano ya namna hii hayavunjwi kiwepesi kwa maana Agano si mkataba.

         Kwa kuwa mkataba unaweza ukavunjwa, kuahirishwa au kuisha muda wake na kuandika mkataba mwingine.
        Agano hudumu kwa muda usiojulikana.

      Bwana Mungu aliingia Agano na wana wa Israeli, AGANO hili lilikuwa ni la kwanza lijulikanalo kuwa ni agano la kale.

       Akawapa sheria na maagizo 613 lakini mwishoe walilivunja kwa maana hawakuliweza.
           Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya Agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
        Si kwa mfano wa AGANO lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono ili kuwatoa katika nchi ya Misri;
          AGANO langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema BWANA.
     Yeremia 31:31-32

Sheria zilikuwa ni nyingi mno, hawakuweza kutembea katika sheria na magizo, na mausia na hukumu hizo zote.

   HIVYO BASI TUNAJIFUNZA MAMBO YAFUATAYO KUPITIA AGANO LA KALE ;
      Agano la kale ni kivuli cha agano jipya
(Wakolosai 2:17).

        Agano la kale linatazamia sadaka ya Kristo msalabani
( Mwanzo 3:15- ........
tabiri ya kwanza ya ujio wa uzao wa mwanamke atakaye ukomboa ulimwengu na dhambi zake)
Agano la kale limebeba Ahadi ya ukombozi (Ahadi juu ya umwagaji wa Roho Mtakatifu
      Yoel 2:28,

       Ahadi ya ukombozi, Ahadi ya neno la Kristo.

       Agano la kale limebeba maelezo juu ya taifa la Israeli Agano la kale ni zamani za ujinga ambapo Mungu alifanya kama hazioni,
hakukuwa na neema ya kutubu kama ilivyo agano jipya.
       Matendo 17:30.

MTAZAMO KUHUSU VITABU 39 VYA AGANO LA KALE.
           Agano la kale liliandikwa zaidi katika lugha ya Kiebrania lakini ikumbukwe kwamba katika uhamisho wa Babeli,
lugha ya Kiaramu ndio lugha iliyotawala ndio maana baadhi ya mafungu ya maneno katika kitabu cha Ezra, Yeremia na Danieli yaliandikwa kwa lugha hiyo ya Kiaramu.

       Katika vitabu hivi 39 viliandikwa kwa chanda cha Mungu akitumia watu maalumu aliowachagua na kuwavuvia uweza wake.

      Sasa vitabu hivi nimevigawa katika makundi matano, nayo ni;

01.Vitabu vya sheria; ( vitabu 5)
     Mwanzo. Kutoka. Mambo ya walawi. Hesabu Kumbu kumbu la torati.
            Vitabu hivi hujulikana kuwa ni vitabu vya torati,
au Pentateuko vyenye kueleza sheria yote alitoa Mungu kupitia Musa.

      Tena hujulikana kuwa ni vitabu vya Musa.
            Hivyo vifungu vingi katika Pentateuko (vitabu vitano) vinamtaja Musa kuwa anaiandika sheria na historia ya watu wa Israeli.
      Soma  ( Kutoka 17:14, 24:4, 34:27, Hesabu 33:1-2,
Kumb. 31:9).
Na hata waandishi wa baadae walieleza habari ya uandishi wa Musa Ezra 6:18 n.k.
       Yesu naye anazungumzia Torati kama kitabu cha Musa-  (Marko 12:26), na sheria ya Musa,
Luka 24:44.

      Ukiwa msomaji mzuri utaona Yesu anasema ya kwamba Musa aliandika habari zake (za Yesu) soma
Yoh 5:46-47

        Vitabu hivi vitano vinatoa taswira halisi ya mwanzo wa kila kitu kama vile uanzapo kusoma kitabu cha mwanzo.

     ukweli usiopingika kwamba kama unataka kujifunza neno la Mungu basi huna budi kuvisoma vitabu hivi.

Ni Mimi ndugu yako

      Ev. Elimeleck S Ndashikiwe.

Tuesday, 8 May 2018

UCHAMBUZI WA BIBLIA kitabu cha MWANZO.

👉 Maelezo ya Kitabu cha Mwanzo Cha Biblia👇✔

Utangulizi
Neno  Mwanzo”  linatokana na neno la Kiyunani “genesis”
       ambalo maana yake ni “asili,” “chimbuko” au “chanzo,”
         ambalo ndilo jina lililopewa kitabu hiki na watafsiri wa Agano la Kale la Kiyunani lijulikanalo kama Septuagint.

       Katika karne ya tatu kabla ya Kristo.

Ingawa kitabu hiki cha Mwanzo kinaanza kuelezea uumbaji wa vitu vyote,
mtazamo mkubwa ni uumbaji wa mwanadamu.

           Kitabu hiki kinaeleza mwanzo wa ulimwengu,
mwanzo wa mwanadamu yaani, mwanamke na mwanamume,
       mwanzo wa dhambi ya mwanadamu,
mwanzo wa ahadi na mipango ya Mungu ya wokovu na
      uhusiano wa kipekee kati ya Abrahamu na Mungu.

Kitabu kinaelezea juu ya watu mahsusi wa Mungu na mipango Yake katika maisha yao.
  Baadhi ya watu hawa ni Adamu na Eva, wanadamu wa kwanza kabisa kuumbwa,
Nuhu, Abrahamu, Isaka, Yakobo, Yusufu na ndugu zake na wengine wengi.

             Mwanzo ni kitabu cha kwanza miongoni mwa vile vitabu vinavyoitwa,
‘‘Vitabu Vitano vya Musa,’’ 
      vilivyoko mwanzoni mwa Biblia.

Vitabu hivi vinaitwa pia vitabu vya sheria kwa sababu ndipo palipoandikwa maagizo na sheria za Mungu kwa watu wa Israeli.
                   Kitabu hiki cha Mwanzo kama kitabu cha utangulizi katika habari za Mungu kuendelea kujifunua mwenyewe katika jamaaa ya wanadamu,

     jambo hili ni la muhimu sana.

Katika kitabu hiki ndiko tunapopata ahadi ya kwanza kabisa ya ukombozi wa mwanadamu aliyeanguka, “….uzao wa mwanamke utakaoponda kichwa…”(3:15).

Mwanzo kinaelezea jinsi ilivyotokea hadi Israeli wakafanyika watu maalum wa Mungu.

      Wazo Kuu Kueleza uumbaji, anguko, Ukombozi wa uzao wa mwanadamu kwa njia ya Yesu Kristo.

        Katika maeneo haya ndipo ulipo ufunuo wote wa ki-Mungu na kweli yote katika Maandiko.

           Kitabu hiki ni kama kitalu cha mbegu cha Biblia nzima,
         hivyo ni muhimu sana kuwa na uelewa sahihi wa kila sehemu.

         Mwanzo ndio msingi ambako ufunuo wote wa ki-Mungu ulipo na ambako umejengwa.

         Kila msingi mkuu wa imani katika Maandiko, mizizi yake iko katika Mwanzo kama asili, kitu kamili au mfano,au ufunuo wa halisi.

Mwandishi Musa

Kuna uwezekano mkubwa kwamba Mwanzo ambacho ni mojawapo ya vile vitabu vitano vilivyoandikwa na Musa, isipokuwa sura ya mwisho ya kitabu cha Kumbukumbu la Torati  inayoelezeajuu ya kifo cha Musa.

Mahali Sehemu ambayo kwa sasa inaitwa Mashariki ya Kati.
Wahusika Wakuu ni Adamu, Eva, Kaini, Abeli, Enoki, Nuhu, Abrahamu, Sara, Loti, Isaka, Rebeka, Yakobo, Yusufu na ndugu zake.

Tarehe Kitabu hiki kiliandikwa 1688 K.K.

Mgawanyo
• Kuumbwa kwa ulimwengu, dunia, mwanadamu. (1:1-2:25)

• Anguko la mwanadamu na matokeo ya dhambi. (3:1-5:32)

• Habari za Noa. (6:1-9:29)

• Kutawanywa kwa mataifa. (10:1-11:32)

• Maisha ya Abrahamu. (12:1-25:18)

• Isaki na familia yake. (25:19-26:35)

• Yakobo na wanawe. (27:1-37:1)

• Maisha ya Yosefu. (37:2-50:26)

Barikiwa sana mtumishi wa MUNGU,

Ni Mimi ndugu yako
Ev. Elimeleck Ndashikiwe.