Pages

Subscribe:

Friday, 1 December 2017

THE HEAVENLY KINGDOM "GOD".

By
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe

         Ufalme waMbinguni una wakili mkuu ambaye ni Yesu Kristo.

           1 Yohana 2:1
       Watoto wangu wapendwa, nawaandikieni haya ili msitende dhambi. Lakini kama mtu ye yote akitenda dhambi,
tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo Mwenye haki.

        Ufalme wa Mbinguni una hakimu Mkuu (Mungu).
          Na mbingu zitatangaza haki yake,
kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu
(Zaburi 50:6).

UBARIKIWE SANA TENA SANA.

Ufalme wa Mbinguni ni urithi wetu watoto wa MUNGU tupendwao sana.

UFALME WA MBINGUNI Sehemu II..

Tunaendelea na Sehemu hii ya Pili.

BWANA YESU ASIFIWE SANA MTU WA MUNGU, Karibu sana,

UFALME WA MBINGUNI UNA KATIBA NA SHERIA.
            Katiba inatoa kanuni na taratibu ambazo raia wanazitumia ili waweze kuishi na kutawaliwa.

         Katika ufalme wa Mungu katiba inaitwa Biblia.

  Pia hujulikana kama neno la Mungu au sheria ya Mungu.
Mathayo 5:18
“18 Kwa maana, amin, nawaambia, mpaka Mbingu na Dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yo yote kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe kimetimia.”

  UFALME WA MBINGUNI UNA LUGHA YA TAIFA.
      Kunena kwa lugha ndiyo lugha ya taifa katika ufalme wa Mungu,
     Matendo 2:1-4
Ilipowadia siku ya Pentekoste, walikuwa wote mahali pamoja.
       2 Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo uliotoka mbinguni, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi.
      3. Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao.
       4 Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia”.

Ufalme wa Mbinguni una utamaduni (Tunda la Roho pamoja na kusifu na kuabudu).
     Kusifu na kuabudu ni utamaduni katika ufalme wa Mbinguni
      Ufunuo 4:8
“Kila mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na macho pande zote, hadi chini ya mabawa.
         Usiku na mchana hawakuacha kusema‘‘Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
        ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.’’

Tunda la Roho pia ni utamaduni wa Mbinguni ambao ni upendo,
furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
upole, kiasi.
          Wagalatia 5:22-23

 
UFALME WA MBINGUNI UNA SERIKALI.
         Kanisa siyo chombo cha kidini,
bali kanisa ni muundo wa serikali iliyopewa mamlaka ambayo Mfalme (Yesu Kristo) hutumia ili kuutawala ufalme wake.
           Mathayo 16: 18-19
‘‘Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya kuzimu hayataweza kulishinda.
        19 Nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni na lo lote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, lo lote
utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.’’

UFALME WA MBINGUNI PIA UNA JESHI.
      Jeshi la Mbinguni ni malaika,
raia walioko katika ufalme wa Mungu wanalindwa na malaika.
     Zaburi 34:7
“Malaika wa BWANA hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa.”

         Ufalme wa Mbinguni una ulipaji wa kodi
(Fungu la Kumi).
Sisi kama raia wa ufalme wa Mungu, tunatakiwa kulipa kodi (zaka/ fungu la kumi).
      Malaki 3:8-10 “8
‘‘Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Hata hivyo mnaniibia.
‘‘Lakini mnauliza, ‘Tunakuibia kwa namna gani?’ ‘‘Mnaniibia zaka(mnaniibia kodi) na dhabihu.
         9.Mko chini ya laana, ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi. 10Leteni zaka kamili
(leteni kodi kamili) ghalani , ili kiwemo chakula katika nyumba yangu.

Nijaribuni katika hili,’’
asema BWANA Mwenye Nguvu,
‘‘nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni
baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha au la.”

        Ufalme wa Mbinguni una Mabalozi.
       Tumechaguliwa na Mungu na kuteuliwa kama mabalozi ili kuwakilisha matakwa na mawazo ya ufalme wa Mungu.
           Mkakati wa Mungu wa kueneza habari njema ya ufalme ulikuwa ni kutumia mabalozi.
           2 Korintho 5:20
“Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo, kana kwamba Mungu anawasihi kwa kupitia vinywa vyetu,
nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu.”

Ufalme wa Mbinguni una Mwanasheria mkuu ambaye ni Roho mtakatifu.
           Roho mtakatifu ni mwanasheria mkuu wa Mbinguni, yeye ndiye aliyehusika katika uandikaji wa katiba (Biblia)
          2:Petro 1:20-21.
     Roho mtakatifu kama mwana sheria mkuu katika ufalme wa Mungu, yeye ndiye anayehusika katika kuwaongoza na
kuwafundisha raia wa ufalme wa Mungu jinsi ya kusema wanapopelekwa mbele ya mabalaza na mahakama au masinagogi,

      Unaposoma kitabu cha
   Luka 12:11-12
Neno la Mungu linasema hivi:-
       ‘‘Watakapowapeleka katika masinagogi mbele ya watawala na wenye mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu namna mtakavyojitetea au mtakavyosema:
          12 Kwa maana Roho Mtakatifu atawafundisha wakati uo huo mnachopaswa kusema.”

Ufalme wa Mbinguni una fedha (currency) ambayo ni IMANI.
             Ufalme wa Mungu ni nchi ambayo fedha yake ni Imani.
        Huwezi ukafanya biashara yoyote katatika ufalme wa Mungu bila ya kuwa na Imani.

          Kama vile ambavyo huwezi kuishi katika nchi yoyote duniani bila fedha, vilevile huwezi kuishi katika
Ufalme wa Mungu bila ya kuwa na Imani
(Warumi 1:17, Marko 5:34).

BARIKIWA SANA MTUMISHI KWA KUENDELEA KUFUATANA NAMI.

            Ni Mimi ndugu yako
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe.