Shalom shalom
Mtu wa Mungu, nikusalimie kupitia jina pekee la Yesu
Kristo aliye hai;
Ninalo neno moja juu yako Leo hii,
Moyo wangu umeugua sana kiasi kwamba siwezi kuachilia tu na kuendelea kuziona ahadi zetu zikishindwa kutimia ktk maisha yetu.
Ni kweli tunaomba sana,
Ibada tunahudhuria sana,
Mikesha nayo bila kukosa
Lakini tatizo tumeshindwa kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo.
Pengine naweza nisieleweke, lkn ukweli ni kwamba
Hatujifunzi. Mwanafunzi mzuri Sikh zote ni yule anayepokea vitu vipya kila siku kutoka kwa mkufunzi wake.
Mfano, swali dogo tu::::::.......
Ibada iliyopita unakumbuka kanisani ulijifunza kuhusu nini?
Unaweza ukakubaliana na Mimi kuwa Siku hizi tunaingia tu katika nyumba zetu za ibada kuimba nyimbo, kucheza na hatimaye kurudi majumbani kwetu.
EV. Elimeleck mwana wa Ndashikiwe
naugua sana na tukio kama hili.
Maandiko yanasema kuwa chanzo cha imani in kusikia, na huko kusikia huja kwa Neno la
Kristo.
Hivyo hakuna Imani nje ya Neno la Kristo,
Kinyume na hapo, hutaishi kwa imani Bali
Kwa
Matumaini tu.
Ebr 11:1-2 Imani ni bayana ya mambo au kile kinachotarajiwa kuwa kipo au kitakuwepo bila ya wewe kukiona kwa macho ya nyama.
Ukiendelea kuisoma hii sura ya kumi na moja ya kitabu cha Waebrania
Utakutana na habari za watu waliokuwa na
Imani isiyo
ya kawaida.
Hawa walimshawishi Mungu hata yeye kuwaita marafiki zake.
Hawa watumishi tunawaita
Mashujaa wa
Imani.
Mungu wangu wa Mbinguni akubariki na kukulinda mpendwa wangu.
Shalom shalom
Ni Mimi
Ndugu yako
EV. Elimeleck S. Ndashikiwe
+255767445846
+255715445846
0 comments:
Post a Comment