Pages

Subscribe:

Thursday, 15 September 2016

Hatareeeeeee kwa Vijana

Uzinzi Mungu ametuonya tusi zini. Katika
Kutoka 20:14 imeandikwa,
"usizini".

Kumwacha mke wako au mume wako na kuoa mtu mwingine yaweza kuwa halali kwetu lakini kwa Mungu ni dhambi.

Luka 16:18 inasema
"Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini;
naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini." Kutamani mtu asiye mume au mke wako nikuzini katika

Mathayo 5:27 -28 "Mmesikia kwamba imenenwa, usizini; lakini mimi nawaambia, kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini moyoni mwake."
Yesu alimchukulia vipi mwanamke aliyeshikwa akizini?

Yohana 8:10-11 Inasema,
" Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia mwanamke, wako wapi wale washitaki wako?
je! hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? akamwambia, hakuna Bwana.

Yesu akamwambia wala mimi sikuhukumu. Endazako;
wala usitende dhambi tena." Nimapenzi ya Mungu tusizini. Imeandikwa katika

1Wathesa 4:3 "Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, muepukane na usherati."

Yes, dunia inahitaji kizazi bora ili iendane na mfumo sahihi wa maadili

Tuesday, 6 September 2016

Ishara Mawinguni Yesu akaendelea hivi: Lakini mara baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika, ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu (Mathayo 24:29-31). Mifano au picha katika sehemu hii ya mafundisho ya Yesu pale Mlima wa Mizeituni bila shaka ingekuwa inafahamika na Wayahudi wa siku Zake, maana inatoka katika Isaya na Yoeli, na inazungumzia hukumu ya mwisho ya Mungu, mwisho wa dunia. Mara nyingi huitwa “siku ya Bwana”, wakati jua na mwzi vitatiwa giza (ona Isaya 13:10, 11; Yoeli 2:31). Ndipo wakazi wote wa dunia watakapomwona Yesu akirudi mawinguni katika utukufu Wake, nao wataomboleza. Kisha malaika wa Yesu “watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu,” kuonyesha kwamba waamini watanyakuliwa na kukusanywa ili kumlaki Yesu mawinguni, na hayo yote yatatokea baada ya mlio wa “baragumu”. Hapa tena, kama ungemwuliza Petro, Yakobo au Yohana ikiwa Yesu angewarudia kabla au baada ya wakati wa mpingakristo na dhiki kuu, bila shaka wangesema, “Baada.” Kurudi Kwake, Na Unyakuo Hii sehemu ya Mafundisho ya pale Mlima wa Mizeituni inaeleweka sana, kulingana na tukio ambalo Paulo aliandika juu yake, ambalo bila shaka ni Unyakuo wa kanisa, ingawa waandishi wengi wa vitabu vya kufafanua Biblia wanasema linatokea kabla ya kipindi cha Dhiki kuanza. Hebu tazama andiko lifuatalo, tulilotazama mwanzoni mwa sura hii. Lakini ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko,na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tuli hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo. Lakini ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. Wakati wasemapo, Kuna amani n salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa (1Wathes. 4:13 – 5:3. Maneno mepesi kukazia). Paulo aliandika juu ya Yesu kuja kutoka mbinguni kwa parapanda ya Mungu na kwamba waamini watanyakuliwa “mawinguni ili kumlaki Bwana hewani.” Ni sawa kabisa na yale Yesu aliyokuwa akieleza katika Mathayo 24:30, 31 – yanayotokea baada ya kutokea kwa mpingakristo na dhiki. Tena, Paulo alipoendelea kuandika kuhusu kurudi kwa Kristo, anataja kwamba ingetokea lini – “majira na nyakati” – na kuwakumbusha wasomaji wake kwamba walikuwa wanafahamu vizuri sana kwmaba “siku ya Bwana ingekuja kama mwivi anavyokuja usiku.” Paulo aliamini kwamba kurudi kwa Kristo na Unyakuo wa waaminio ungetokea “siku ya Bwana,” siku ambapo hasira kali na maangamizi vingewapata wale waliokuwa wanatazamia “amani na salama.” Kristo anaporudi kulinyakua kanisa Lake, hasira Yake itashuka juu ya dunia. Hili linakubaliana vizuri sana na kile ambacho Paulo aliandika katika barua kwa Wathesalonike baadaye, kuhusu kurudi kwa Kristo na hasira Yake. Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi; na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu,na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; watakaoadhibiwa kwa maagamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake; yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakaifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu). (2Wathes. 1:6-10. Maneno mepesi kukazia) Paulo alisema kwamba wakati ambao Yesu angerudi kuwapa nafuu Wathesalonike waliokuwa wanateswa (ona 1Wathes. 1:4, 5), angetokea “pamoja na malaika wake katika mwali wa moto” ili kuwaadhibu wale waliokuwa wanawatesa wao, kutoa hukumu ya haki, inayostahili. Hii haifanani na kile kinachosemwa na wengi, kwamba Unyakuo utatokea kabla ya dhiki, na kanisa kunyakuliwa na Kristo kabla ya kile kipindi cha dhiki cha miaka saba kuanza. Hii pia huitwa kuja kwa siri kwa Yesu ili kunyakua kanisa Lake. Hapana kabisa! Maelezo haya yanafanana na kile ambacho Yesu alieleza katika Mathayo 24:30, 31 – kurudi Kwake karibu au mwishoni mwa kipindi cha dhiki kuu – anapowanyakua waaminio na kumimina hasira Yake juu ya wasoiamini. Siku Ya Bwana Baadaye, katika barua hiyo hiyo, Paulo aliandika hivi: Basi ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo (2Wathes. 2:1, 2). Kwanza: Ona kwamba mada ya Paulo ni kurudi kwa Kristo na Unyakuo. Aliandika kuhusu “kukusanyika kwetu mbele zake,” akitumia maneno yale yale ambayo Yesu alitumia katika Mathayo 24:31, alipozungumza juu ya malaika ambao “wangekusanya” wateule Wake “kutoka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho ule.” Pili: Ona kwamba Paulo anayaita matukio hayo kuwa ni “siku ya Bwana,” sawa na alivyofanya katika 1Wathesalonike 4:13 hadi 5:2. Hilo liko wazi kabisa. Kisha anaendelea hivi: Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu (2Wathes. 2:3, 4. Maneno mepesi kukazia). Wakristo Wathesalonike walikuwa wanadanganywa kwa namna fulani kwamba siku ya bwana – ambayo kulingana na Paulo lazima ianze kwa Unyakuo na kurudi kwa Kristo – ilikuwa imekwisha fika. Akatamka wazi wazi kwamba haiji mpaka baada ya ule ukengeufu (labda ndiyo kule kurudi nyuma ambako Yesu alizungumzia katika Mathayo 24:10) na baada ya mpingakristo kujitangaza kwamba ni Mungu kutoka hekalu la Yerusalemu. Basi, Paulo anawaambia waamini Wathesalonike wazi wazi kwamba wasitazamie kurudi kwa Kristo – au Unyakuo – wala siku ya Bwana, mpaka baada ya tamko la mpingakristo kwamba ni Mungu.[6] Kisha, Paulo anaelezea kuhusu kurudi kwa Kristo na jinsi anavyomwangamiza kabisa mpingakristo. Je, hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo? Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake. Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake; yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa (2Wathes. 2:5-10). Paulo alitamka kwamba mpingakristo atakomeshwa “kwa ufunuo wa kuja Kwake” Kristo. Kama “ufunuo” Wake ni sawa na ule unaotajwa wakati wa Unyakuo – kiasi cha mistari tisa nyuma (ktk 2:1), basi mpingakristo atauawa wakati huo huo ambapo Kanisa litakusanywa ili kumlaki Bwana hewani. Hii inalingana na taarifa itolewayo katika Ufunuo sura ya 19 na 20. Hapo tunasoma juu ya kurudi kwa Kristo (ona Ufunuo 19:11-16), kuangamizwa kwa mpingakristo na majeshi yake (ona 19:17-21), kufungwa kwa Shetani (ona 20:1-3) na “ufufuo wa kwanza” (ona 20:4-6), ambapo waamini waliouawa katika kipindi cha Dhiki yamiaka saba watafufuliwa. Kama huu ndiyo ufufuo wa kwanza kweli kweli kwa maana ya jumla kwamba ni kwa ajili ya wenye haki, basi hakuna mashaka kwamba Unyakuo na kurudi kwa Kristo katika hasira Yake kunatokea wakati huo huo ambapo mpingakristo anaharibiwa, maana, Maandiko yanatuambia wazi kabisa kwamba wote waliokufa katika Kristo watafufuliwa wakati wa Unyakuo (ona 1Wathes. 4:15-17).[7] Kuwa Tayari Hebu turudi tena kwenye Mafundisho pale Mlima wa Mizeituni. Basi kwa mtini jifunzeni mfano. Tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu. Nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni. Amin nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.[8] Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe (Mathayo 24:32-35). Yesu hakutaka wanafunzi Wake wanaswe bila kufahamu – na hilo ndilo jambo la msingi katika Mafundisho ya pale Mlima wa Mizeituni. Wangejua kwamba “yuko malangoni” baada ya kuona “mambo hayo yote” – dhiki duniani kote, kurudi nyuma kwa watu, kutokea kwa manabii na makristo wa uongo, tangazo la mpingakristo kwamba ni Mungu, na kutiwa giza jua na mwezi pamoja na kuanguka kwa nyota, wakati karibu na kurudi Kwake. Ila, baada tu ya kuwaambia kuhusu ishara zitakazotangulia kuja Kwake kwa miaka michache, au miezi au siku, aliwaambia sasa wakati hasa wa kurudi Kwake ungebakia kuwa siri. Walakini kwa habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake (Mathayo 24:36). Mara nyingi andiko hili linatajwa kinyume cha mantiki yake! Kwa kawaida linatajwa ili kuunga mkono dhana kwamba hatuna habari Yesu atarudi lini, kwa sababu anaweza kurudi wakati wowote na kunyakua kanisa. Lakini katika mantiki yake, Yesu hakumaanisha hicho. Alikuwa ndiyo kamaliza kuhakikisha kwamba wanafunzi Wake wangekuwa tayari kwa ajili ya kurudi Kwake kwa kuwaambia ishara nyingi ambazo zingetokea muda mfupi tu kabla ya kurudi Kwake. Sasa anachowaambia ni kwamba, siku hasa na saa havitafunuliwa kwao. Tena, Yesu hasemi juu ya kuja Kwake mara ya kwanza kabla ya kipindi cha Dhiki ya miaka saba kuanza, wakati ambapo kanisa lingenyakuliwa, bali kuhusu kurudi Kwake wakati wa mwisho au karibia mwisho wa Dhiki. Hilo halina matatizo ukitazama mantiki vizuri. Je, Kurudi Kwake Hakujulikani Kabisa? Hoja ambayo mara nyingi hutumika dhidi ya Unyakuo kutokea karibu au wakati wa mwisho wa Dhiki ni kwamba kurudi kwa namna hiyo kusingekuwa kitu kisichojulikana kama Yesu alivyodaiwa kusema, kwa sababu kurudi kwa namna hiyo kungetazamiwa kwa matukio ya Dhiki. Lazima kuwe na Unyakuo kabla ya dhiki, la sivyo waamini wasingehitaji kuwa tayari na kukaa macho kama Maandiko yasemavyo wanapaswa kuwa, maana watajua ni miaka saba au zaidi kabla ya Yesu kurudi. Ila, hoja hii inapingwa na ukweli kwamba lengo kuu la Mafundisho ya Yesu pale Mlima wa Mizeituni lilikuwa ni kuhakikisha kwamba wanafunzi Wake wawe tayari kwa ajili ya kurudi Kwake wakati au karibu na mwisho wa Dhiki, naye aliwafunulia ishara nyingi tu ambazo zingetangulia kuja Kwake. Mbona Mafundisho ya Mlimani yamejaa mashauri mengi sana kwamba watu wawe tayari na kuwa macho, ingawa Yesu alijua kwamba kurudi Kwake kuko mbele miaka mingi sana baada ya kusema maneno hayo? Bila shaka ni kwa sababu Yesu aliamini kwamba Wakristo wanahitaji kuwa tayari na kuwa macho hata ingawa kurudi Kwake bado kuko miaka mingi mbele. Mitume ambao katika barua zao waliwashauri waamini kuwa macho na kuwa tayari kwa ajili ya kurudi kwa Yesu walikuwa wanamwiga Yesu Mwenyewe. Tena, wale wanaoamini kwamba Unyakuo kabla ya dhiki ndiyo wenye kuhalalisha mashauri yoyote ya kuwa tayari, wana tatizo lingine. Kulingana na mawazo yao, kurudi kwa Yesu mara ya kwanza hutangulia dhiki kwa miaka saba. Kwa hiyo, kurudi kwa Yesu mara ya kwanza kulingana na hoja zao hakuwezi kutokea wakati wowote – lazima itakuwa ni miaka saba kabla ya Dhiki kuanza. Basi, hakuna haja ya kutazamia kwamba Yesu atarudi mpaka matukio duniani yakamilike na kuwa tayari kuanza miaka saba ya Dhiki. Matukio hayo yanaweza kutazamiwa na kuhakikishwa kabisa. Wengi wenye kuamini Unyakuo kabla ya dhiki – kama ni wakweli – watasema kwamba wanajua Yesu hatarudi leo wala kesho kwa sababu ya hali ya kisiasa duniani. Bado yapo matukio yaliyotabiriwa ambayo hayana budi kutimizwa kabla ya ile miaka saba ya Dhiki kuanza. Kwa mfano: Kama tutakavyoona katika kitabu cha Danieli, mpingakristo atafanya agano na Israeli kwa miaka saba, na huo utakuwa ndiyo mwanzo wa kipindi cha Dhiki. Hivyo basi, kama Unyakuo unatokea miaka saba kabla ya dhiki kuanza, lazima utokee wakati mpingakristo atakapofanya agano lake la miaka saba na Israeli. Basi, hakuna haja ya wale wanaoshikilia kwamba Unyakuo utafanyika kabla ya Dhiki kutazamia Yesu atarudi kabla ya kuona kitu katika siasa kinachofanya hayo yawezekane. Zaidi ya hayo – kwa wale wanaoamini kwamba Unyakuo utatokea kabla ya dhiki, na kuamini kwamba Yesu atarudi mwishoni mwa Dhiki pia, maana yake ni kwamba siku kamili ya kurudi kwa Yesu mara ya pili inaweza kujulikana kimahesabu. Mara tu Unyakuo utokeapo, mtu yeyote angeweza kukadiria na kujua kile ambacho Yesu alisema ni Baba tu akijuacho. Unachofanya ni kuhesabu mbele miaka saba tu. Tuseme tena hivi – Kutokana na yale ambayo Yesu alisema, Yeye hakutaka kurudi Kwake kuwe kitu cha kuwashtua watu. Ukweli ni kwamba alitaka kurudi Kwake kutazamiwe, na hivyo akataja matukio kadhaa ya Dhiki. Yesu hakutaka wanafunzi Wake wakutwe hawako tayari, kama ambavyo dunia itakutwa. Basi anaendelea kusema hivi katika Mafundisho Yake pale Mlima wa Mizeituni: Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile ziliozkuwa kabla ya gharika watu walivyokuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. Wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.[9] Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja (Mathayo 24:37-44). Hapa tena, kitu ambacho Yesu anajali ni kwamba wanafunzi Wake wawe tayari kwa ajili ya kurudi Kwake. Hicho ndicho kilisababisha yote aliyosema kabla ya hapa na baada ya hapa, katika mafundisho Yake. Maonyo Yake mwengi kwamba wawe tayari na wakeshe si kwamba ni kwa kuwa kurudi Kwake kutakuwa kwa kushtukiza, bali ni ishara ya jinsi ambavyo itakuwa vigumu kwa sababu ya upinzani wa wakati wenyewe, kuendelea kuwa macho na kuwa tayari. Basi, wale wanaotarajia Unyakuo kabla ya Dhiki, wakati wowote, wanaodhani kwamba wako tayari kuliko Wakristo wengine, wanaweza wasiwe tayari kwa uhalisi kabisa, kwa kile kinachokuja. Kama hawatazamii dhiki yoyote na wajikute katikati ya mateso ya dunia nzima, wakati wa utawala wa mpingakristo, jaribu la kuanguka linaweza kuwazidi nguvu. Afadhali kuwa tayari kwa kile kinachofundishwa na Maandiko kwamba kitatokea. Halafu tena – kama ungemwuliza Petro, Yakobo au Yohana kwamba walitazamia kumwona lini Yesu akirudi, wangekwambia kuhusu ishara hizo zote ambzo Yesu aliwaambia zingetokea, kabla ya kurudi Kwake. Wasingetazamia kumwona kabla ya kipindi cha dhiki, au kutokea kwa mpingakristo.
Agano la Kale kuna makatazo ya vyakula, kuwa usile hiki, usile kile, kuwa hiki ni najisi, na kile ni najisi hivyo usile. Andiko,lililo maarufu na inalotumika sana na wakristo wanaovuta juu ya vyakula ni lile la Walawi 11, ambalo naamini hata wanafunzi wale wa Yesu Kristo wa asili ya kiyahudi walikuwa wanalitumia sana ili kuwabananisha wanafunzi wengine wa asili ya mataifa. Kama ilivyo leo, watu wanatumia andiko hilo kwa habari ile ile. Ila ashukuriwe Mungu kwakuwa tunayo maandiko katika Agano Jipya yanayotuweka huru kabisa na habari hii ya vyakula. Tena unajua mimi namshangaa hata huyu mtume Petro, siku ile Bwana Yesu aliposema yale maneno katika Mathayo 15:10-17, yeye Petro alikuwa anawaza nini sijui hata akaendelea na ule msimamo juu ya unajisi wa vyakula, ila ashukuriwe Mungu aliyemfungua na ngome ile. Ngome zingine huwa zinahitaji hekima na maarifa ya Mungu kuziangusha, na hekima na maarifa hayo ndiyo yanahitajika leo na ninakuhakikishia kuwa yaja yapo njiani, na ngome zinakwenda kubomolewa kwa kiwango cha kustaajabisha na wengi waliofungwa na maagizo na mafundisho ya wanadamu yenye hila wanaenda kufunguliwa. Maandiko yako wazi nayo yanasema hivi: Mathayo 15:11, 17 "Sikilizeni sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi bali kitokacho ndicho kimtiacho mtu unajisi....Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni kikatupwa chooni?" Marko 7:15,18,19 "Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu...hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu kikimwingia hakiwezi kumtia unajisi kwasababu hakimwingii moyoni ila tumboni tu, kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote." Matendo ya Mitume 10:11-15 "Akaona mbingu zimefunuka na chombo kikishuka kama nguo kubwa inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi, ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne na hao watambaao na ndege wa angani. Kisha sauti ikamjia kusema ondoka Petro uchinje ule, lakini Petro akasema, hasha Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi. Sauti ikamjia mara ya pili ikimwambia, vilivyotakaswa na Mungu usiviite wewe najisi." Warumi 14:1-14 "Yeye ALIYE DHAIFU WA IMANI, mkaribisheni, WALAKINI MSIMHUKUMU MAWAZO YAKE. MTU MMOJA ANAYO IMANI, ANAKULA VYOTE, LAKINI YEYE DHAIFU HULA MBOGA. Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye, kwa maana Mungu amemkubali.....KILA MTU NA ATHIBITIKE KATIKA AKILI ZAKE MWENYEWE....Basi ni hivyo kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu....NAJUA TENA NIMEHAKIKISHIWA SANA KATIKA BWANA YESU, YA KUWA HAKUNA KITU KILICHO NAJISI KWA ASILI YAKE, LAKINI KWAKE YEYE AKIONAYE KITU KUWA NAJISI, KWAKE HUYO KITU KILE NI NAJISI." Wakolosai 2:16,17 "Basi mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji.....mambo hayo ni kivuli cha yajayo bali mwili ni wa Kristo. BASI IKIWA MLIKUFA PAMOJA NA KRISTO MKAYAACHA YALE MAFUNDISHO YA AWALI YA ULIMWENGU, KWANINI KUJITIA CHINI YA AMRI, KAMA WENYE KUISHI DUNIANI. MSISHIKE, MSIONJE, MSIGUSE (mambo yote hayo huharibika wakati wa kutumiwa), hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea na KUUTAWALA MWILI KWA UKALI, lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili." 1 Timotheo 4:1-4 "Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani.....wakiwazuia watu wasioe na kuwaamuru wajiepushe na vyakula ambavyo Mungu aliviumba VIPOKEWE KWA SHUKRANI NA WALIO NA IMANI WENYE KUIJUA HIYO KWELI. Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa kama kikipokewa kwa shukrani, kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba." Sasa hayo ni maandiko kutoka katika Agano Jipya lililowekwa kwa damu ya Yesu Kristo. Maandiko haya yanaweka msimamo juu ya vyakula mbali na Walawi 11. Agano la Kale ni kivuli cha Agano Jipya, yote yaliyosemwa ama kufanywa katika Agano la kale yalikuja kutimilizwa katika Agano Jipya. Yalitimilizwa na kugongomelewa msalabani, yalitimilizwa kabla na katika kazi ya Yesu Kristo pale msalabani. Hakuna habari ya siku, hakuna habari ya mwandamo wa mwezi, hakuna habari ya sabbaths, tena hakuna habari ya vyakula wala habari ya vinywaji kwakuwa Bwana Yesu alitupa kula mwili wake na kuinywa damu yake katika jioni ile ya Pasaka alipoketi chakulani na wenzetu wale na kula nao na kunywa nao. Akamega mkate pamoja nao, na kula nao na kuinywa divai pamoja nao, huku akiacha agizo kufanya vile kwa pamoja kwa ukumbusho wake. Hadithi zote zinazotajwa katika Wakolosai 2:16 zilikomea msalabani nazo zilikuwa ni kivuli tu. Sasa hatuko chini ya amri wala hatujitii chini ya amri kwa habari ya vyakula au vinywaji au siku au mwandamo wa mwezi au sabbaths Lakini ikiwa mtu anaamua kujitia chini ya amri kama mwenye kuishi duniani, sasa hapa hekima ya Mungu na itambulikane, maana yake watoto wa Mungu ni tofauti na watoto wa Ibilisi walio watoto wa ulimwengu huu, watoto wa Mungu ni wapitaji, ni wasafiri, ndiyo maana Paulo akauliza "kwa nini kujitia chini ya amri kama wenye kuishi duniani?". Watoto wa Mungu imewapasa kuenenda kwa Roho tangia siku ile Bwana Yesu alipoitimiliza Torati na Manabii pale msalabani, sasa ni nini kujitia chini ya maagizo ambayo yalikuwa ni kivuli cha mambo yajayo? Ikiwa umejiondoa katika kuzishika sabbaths, kwa nini hujiondoi katika kushika vyakula? Kwa nini kunakuwa na double standard katika mambo ya Mungu? Je Mungu anajipinga mwenyewe ama ni sisi wanadamu ndo tunaopotoshana kwa kusikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani kama alivyonena mtume Paulo katika 1 Timotheo 4:1,2 Yeye aliye na hekima na apambanue, na athibitike katika akili zake mwenyewe. Bwana Yesu Kristo ni Kichwa cha Kanisa, viungo vyote imewapasa kukishika Kichwa - Wakolosai 2:18,19 MUNGU akubariki sana.