Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu.....
Ev. Elimeleck Ndashikiwe
Nawapenda sana sana.
Fundisho hili linawahusu watu wote hususani wale wanaohudumu kanisani kwenye nafasi mbali mbali,
mfano waimbaji,
wakuu na viongozi wa idara mbali mbali,
pamoja na wale waliopo katika zile huduma tano
Waefeso 4:11.
Mpango wa Mungu sio kutoa adhabu kwa watu wake,
bali mpango wake ni kuwafanya watu kumtumikia Yeye tu kwa moyo,roho akili na nguvu zote.
Lakini panapo stahili kupata adhabu basi Mungu hasiti kuachilia adhabu sawa sawa na dhambi au kosa lillilopo.
Tukumbuke ya kwamba Mungu wetu sio dhalimu,
bali ni mwaminifu na mpole si mwepesi wa hasira naye ni mwingi wa huruma
Yoeli 2:13.
Hata hivyo tunakubaliana kwamba adhabu haiji bila kosa. Ikiwa mtu amekosa anapewa nafasi ya toba/kugeuka na kusamehewa mara moja.
Lakini anapoendelea kukosea kwa nia ya kupenda kukosea basi anastahili anyooshwe kwa adhabu,
ukizingatia kazi ya Mungu sio kazi ya kuchezea chezea wala sio kazi ya kuleta masihara.
Ikiwa umeitwa tu “mkristo” na umeokoka basi ujihesabu wewe ni mtumishi wa Mungu mahali ulipo,na uwe makini sana na njia
zako~
chunga unaongea nini!,
chunga marafiki zako ni akina nani ! Chunga unafanya nini!! N.K
“Adhabu ya kuliwa na chango madhabahuni”
Huu ni msamiati mgumu kwa sababu hata neno “chango” ni msamiati bado.
Hivyo neno “chango” ni aina fulani ya minyoo au wadudu wanaotafuna tumbo.
Sasa
kivipi minyoo ikawa ni adhabu kwa mkristo/mtumishi?
~ Kumbuka;
Bwana Mungu ana namna yake ya kuwanyoosha watu wake kwa adhabu pale inapostahili,
Yeye Mungu anaweza kufanya chochote kile kwa mtu yoyote yule.
Adhabu ya namna hii inakuja kwa mtu yule anayetwaa utukufu wa Mungu na kujilingalinisha
na Mungu mfano mzuri ni Herode yule aliyemuua Yakobo ndugu wa Yohana kwa upanga
(Matendo 12:1-4)
Biblia inatuambia;
“ Basi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifalme, akaketi katika kiti cha enzi,
akatoa hotuba mbele yao.
Watu wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu,
si sauti ya mwanadamu.
Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho.”
Matendo 12:21-23
Simulizi hii ya kifo cha Herode ni onyo kwa watu wote
wanaotwaa utukufu wa Mungu.
Herode hali akijua hotuba anayoitoa sio ya Mungu ni ya kwake lakini hakutaka kuonesha
hivyo bali alipendezwa na sauti za watu kuona yeye ni Mungu atoae hotuba.
Watu waliokuwa wakimsikiliza hawakuwa na ufahamu sahihi wa kuitambua sauti ya Mungu
bali yeye hali akijua sio sauti ya Mungu na hakutaka kumpa utukufu Mungu,Mungu akampiga kwa chango nao wakamla.
Hivyo Herode hakuuwawa na wanadamu bali Mungu mwenyewe kwa sababu hakutaka kumpa Mungu utukufu. Ikiwa kama hakutaka kumpa Mungu utukufu,basi ni
dhahiri mtu huyu alijiinua na kujifanya yeye ndio mungu mtu.
Kitu ambacho ni machukizo makubwa sana kwa Bwana ni kutwaa utukufu wake na kumpa mwingine,
kwa maana Bwana mwenyewe asema ;
“Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.”
Isaya 42:8
Leo hii nini kinaendelea madhabahuni?
Watu wengi wanapenda sifa na kujiinua ili watazamwe kuwa wao ni miungu watu.
Tena baadhi ya watu wanadiriki hata kusema
“Mungu kaniambia…”
na kumbe ndani yao wanashuhudiwa hawajaambiwa chochote kile,bali ni maneno yao wao wenyewe.
Hata kama ni kweli Bwana amekuambia,
swali la kujiuliza Je umeambiwa useme kwa wakati huo?
Haya na mengineyo mengi yanaendelea leo kwenye madhabahu ya Bwana. Hakika mimi
ninakuambia watu wa namna hii wanaojiiunua na kuchukua utukufu wa Mungu watapigwa na chango mpaka kufa kama
ilivyokuwa kwa Herode.!
Kuna adhabu ya kupigwa na chango kwa wale watakao iacha kweli wakajitwalia utukufu ambao utukufu huo ulitakiwa
uwe ni kwa Bwana tu.
Mimi nachelea kusema kila wakati neno hili “Bwana kaniambia…au Bwana kanisemesha...”
ikiwa sijaongea na Bwana kwa nini niseme uongo kwa nia ya kujiinua?
Sitaki kupigwa na adhabu ya chango!!!
~ Herode alikufa kimwili kwa kuliwa na minyoo ya gafula kama adhabu bali leo unaweza ukaliwa na magonjwa au ukaliwa kiroho
kiasi kwamba mbele za Mungu hakika ni umekufa hali kimwili upo hai. Ni hali mbaya sana hii!!!
Sio kila adhabu au majanga yote yanaletwa na shetani bali mengine ni adhabu ya Kiungu yenyewe
~ kuna wakati Mungu anaweza akaruhusu adhabu fulani mbaya kwenye maisha yako kwa sababu ya tabia ya kupenda kujiinua kwamba
unatwaa utukufu wa Mungu.
Wito wangu kwako wewe mkristo uliyeokoka ni kwamba,
epuka tabia ya kujitwalia utukufu wa Mungu.
Ikiwa Mungu amekutumia kwenye eneo lolote lile,
basi usiseme umefanya wewe kwa mikono yako bali sema Mungu ndie amefanya yote hayo,
na papo hapo kumbuka kuzikataa sauti za watu wanaokusifia bali kaza kusema ni Bwana tu ndie kayafanya yote.
Usijiinue kwa namna yoyote ile kwa maana usije ukafanana na Herode aliyepigwa na chango.
Ikiwa unaona unasumbuliwa na roho ya kujisifu fulani hivi,
au ikiwa una mtu anayekuumiza kwa tabia yake ya namna hii,
nawe hupendi awe nayo,
kwa maana hiyo roho ni ya rusifa/shetani basi
naomba usisite kunipigia simu kwa namba zangu hizi tuombe pamoja
+255715445846
+255684485460
WATU WA MATAIFA HUCHUKIA NINI HASA KATIKA INJILI YA KRISTO?
-
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.Karibuni sana tujifunze Neno
la MUNGU.Kama umewahi kushuhudia Injili mitaani utanielewa vizuri Zaidi
juu y...