Huyu ndiye mama yetu Mzazi aliyetumiwa na Mungu kutufikisha hapa tulipo. Mungu amzidishie ktk kila alichonacho na afya njema. |
Bwana Yesu Kristo asifiwe sana ndugu yangu Mpendwa, SIKU zote maisha ni hatua,
Aliyeniona Jana anaweza kuniona wa tofauti akibahatika tena kuniona Leo au hata Kesho na Kesho Kutwa yake.
Kadri siku zinavyozidi kubadilika Leo na Kesho, maisha nayo yanabadilika, umri nao unabadilika, afya nayo kimaumbile inabadilika pia,
Lakini yote haya tunayatambua kuwa ni nyakati na majira ya Bwana aliyoyaweka kwa ajili yangu na hata kwa mtu mwingine yeyote.
KILA KIUMBE CHENYE UHAI KINAKUA, KINAONGEZEKA NA CHAWEZA KUPUNGUA PIA,
Lakini kinaposhindwa kukua wala kubadilika, basi hicho kitakuwa kimedumaa au kimekufa kabisa.
Binafsi namshukuru MUNGU wangu wa Mbinguni ananilinda na kunihuisha kila iitwapo Leo na kesho, nafurahia tu tena saaaaaana........
HISTORIA YANGU KWA UFUPI
Majina yangu kamili naitwa ELIMELECK SIMON NDASHIKIWE
Ni mtoto wa pekee mzaliwa wa kwanza kati ya watoto sita (6) wa baba yetu
Mzee SIMON L NDASHIKIWE ambaye ktk ujana wake wote amemtumikia Mungu akiwa ni MCHUNGAJI WA KANISA LA KRISTO,
Akiwa pamoja na mama yetu mzazi aitwaye ELINA KABABA SINDUHIJE,
Wazazi wetu wote hawa wamezaliwa Mkoani KIGOMA, wilaya ya KASULU katika kijiji cha KWAGA.
........nasi yangu tukiwa watoto wadogo tumekulia Kule na kupata Elimu ya msingi katika
SHULE YA MSINGI KWAGA,
,......na elimu ya Sekondari nimeipata katika SHULE YA SEKONDARI UJIJI - KIGOMA.
Wazazi wetu hawa wametumika sehemu kadha wa kadha chini ya Dhehebu la
EVANGELISTIC ASSEMBLIES OF GOD (T) hadi Leo hii.
(Nisiwazungumzie sana wazazi...).
Mimi kama mzaliwa wa kwanza ktk familia ya Pastor SIMON NDASHIKIWE, nimepata Neema ya kuwa lango nikiwa na wadogo zangu watano (5),
Wawili wa kike ambao ni
. PRICILLA S NDASHIKIWE
. ESTHER S NDASHIKIWE
Watatu wa kiume ambao ni
. ISACK S NDASHIKIWE
. PAULO S NDASHIKIWE na
. AMOS S NDASHIKIWE
NB:
Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu wetu wa Mbinguni kutupatia kibali hiki cha kuzaliwa ktk familia ya MLAWI,
Nasi pia kama watoto, ni shauku yetu kumtumikia Mungu na kumpenda kwa mioyo yetu yote.
Yako mengi ambayo ametutendea
na hata sasa bado anatenda.
Asante sana Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo kwa kutufanya kuwa WATOTO WA MUNGU.
Ni MAOMBI yetu ya dhati kabisa
uzidi kuwalinda wazazi wetu na kuwapa afya NJEMA na uwatie nguvu katika kazi yako ya Utumishi (UCHUNGAJI).
SIFA, HESHIMA NA UTUKUFU
VIKURUDIE WEWE UWEZAYE KUTENDA MAMBO MAKUBWA NA YA AJABU ZAIDI YA YALE YOTE
TUYAWAZAYO NA KUYAOMBA.........!
EFES 3:20.........
AMEEEN.