Pages

Subscribe:

Friday, 2 July 2021

KIJANA NA MAISHA YA UTAKATIFU

INJILI YA AMANI


UTANGULIZI:


       Nakukaribisha msomaji katika tafakari ya somo jingine linalohusu kijana na maisha ya kikristo ni jinsi gani kijana aishi maisha Matakatifu kama inavyompendeza Mungu na si kuwafurahisha tu wanadamu katika maisha yetu tukimchukiza MUNGU. 


   Kristo ni mpakwa mafuta. Ambaye ni tofauti na watu wengine. Sasa basi Ukiwa kama kijana wa kikristo ambaye umebatizwa kwa Roho Mtakatifu ndani mwako na si tu kwa ishara ya Wanadamu ya nje tambua kuwa Mungu amekuweka kwa kusudi lake kama mpakwa mafuta umzalie matunda kwa njia ya Kristo YESU. 

    WARUMI 7:4 
       “Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda”.


     Hivyo basi ili kijana wa Kijana wa kikristo awe katika viwango vya usafi wa maisha ya kiroho lazima kufuata na kutafakari neno hili.


1THESALONIKE 4:1-8

  •        "Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana. Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.

  •        Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.

  •        Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana.

  •        Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso. Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu".


i.                    Kijana wa Kikristo lazima aweke mipaka ya ukuaji wake.


      Ukisoma katika mstari wa kwanza unaonesha kuwa Mkristo ni lazima aenende katika Bwana Yesu maana yake lazima kuwe na mpaka/utofauti kati ya kijana wa Kikristo na kijana asiye wa Kikristo.

      Si kwamba kama kijana asiyemwamini Yesu Kristo anakuwa Mlevi, Mzinzi, Mwasherati, Mwizi, Mwongo n.k. lakini na wewe kijana wa kikristo ukaonekana unayafanya haya bado utaonekana ndani mwako hakuna kweli ya Kristo.


ii.                  Kusudi la Mungu kijana wa Kikristo atakaswe.


     1THESALONIKE 4:3

  “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;”


Uasherati ni kufanya tendo la ngono kwa mtu au kijana ambaye hajaoa au kuolewa ambayo ni tofauti pia na uzinzi ambao mtu anafanya tendo la ngono akiwa ameolewa au kuoa na mtu ambaye siye mke au mme wake.

       My dear vijana wengi shetani ametushikilia kwenye suala hili la uasherati maana miili yetu inawaka kwa kuukimbilia uasherati hata tukashindwa kuweka usafi wa mwili na ROHO zetu na kumkosea MUNGU wetu.


       iii.         Kijana wa Kikristo ni lazima ajue kuutunza mwili wake.


     1THESALONIKE 4:4

      “kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;”


  Vijana wa Kikristo ni wale wanaoweza kuimudu miili yao ambapo inakuwa inawaka tamaa ya uasherati hivyo ndivyo Biblia inavyosema kwamba kuuweza mwili yaani kuhakikisha unaweza kuongoza mwili na sio mwili kukuongoza. Lakini hili pia haliwezekani kama kijana wa kikristo hajatambua thamani ya mwili wake. Jiulize kama kijana wa kikristo mwili wako una thamani gani? Maana kuna vijana wamethaminisha miili yao na chipsi, soda, nguo, pombe n.k. lakini jua ya kwamba hakuna kitu cha thamani kuufikia mwili wako zaidi ya damu ya Yesu Kristo.


      iv.          Mungu anataka Vijana wa Kikristo tusiharibiwe katika suala la mahusiano.


     1THESALONIKE 4:7-8

    “Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso. Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu".


       Mungu anamtaka kijana wa Kikristo kuishi maisha ya kuendelea kuwa mtakatifu na kuto kumkosea Mungu ndio maana katika kitabu cha warumi anasema

     Tumeitwa ili tumzalioe Mungu matunda na ukisoma katika aya hii ya saba inasema hatujaitiwa uchafu bali tuishi katika hali ya utakatifu yaani utakaso.

       Mungu alijua kabisa kwamba mwanadamu peke yake hawezi kuishi katika hali hiyo ya utakaso ndio maana akaweka amri kumi. Lengo la amri zake Mungu ni kutulinda na kutupa mahitaji tunayoyahitaji kwa wakati sahihi.


NB. MOYO SAFI KWA MWANZO MPYA.

v  Pamoja na kufanya Dhambi au maovu mengi lakini MUNGU anaweza kukusamehe na kukufanya mpya


NOTE. MAISHA MAPYA YA KIKRISTO.

v  Maisha mapya ya mahusiano ya kikristo ni kumpenda Kristo kwanza. DANIELI 1:8.



NGUVU ILIYOPO KATIKA NENO LA MUNGU    Karibu ndugu  www.elimelecksimon.blogspot.com

       Kwa ajili ya kujifunza machache haya ambayo Mungu amenipa kibali kuyaachilia kwako kupitia kichwa cha somo kinachosema
   “ NGUVU ILIYOPO KATIKA NENO LA MUNGU ”.  

      Tuanze na kutafakari maana Kamili ya neno kibiblia.     Neno ni ujumbe wa Mungu ambao unaotumika na mwanadamu kwaajili ya kumfundisha na kumwongoza mwanadamu kuishi maisha matakatifu ya kumtafuta Mungu.

       Sambamba na kwamba neno la Mungu limehifadhiwa na mwanadamu kwa njia ya mandishi lakini kutokana na kukua kwa teknolojia hadi kwa njia ya sauti hili neno limehifadhiwa pia.     S asa basi neno hili ndilo ambalo Mungu ametupa kama sehemu ya msingi au njia ya mwanadamu kutatua matatizo yake kwa kulitumia hilo neno. Na hili neno pia baada y

READ MORE

TUMIA MAOMBI KAMA SILAHA.

October 09, 2017

TUMIA MAOMBI KAMA SILAHA:         BWANA Yesu asifiwe!!!!!!!!    Nawakaribisha katika somo hili la “ KUTUMIA MAOMBI KAMA SILAHA ” kama ilivyonenwa katika   WAEFESO 6:12 “ Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama;bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya pepo wabaya katika ulimwengu wa Roho ”    Maana yake vita tuliyonayo sisi Wakristo si katika mwili bali ni katika Roho maana yake kama vita vyetu vingekuwa ni vya mwili tungeandaa mapanga, visu, mashoka, bunduki, mishale na kila aina ya silaha za mwili. Lakini kwa sababu vita tulivyonavyo ni vya Roho ni lazima tutumie silaha za Rohoni ili kushinda vita hiyo maana silaha za mwili hazitatufaa kitu.    

     Sasa kwa maana hiyo lazima tujue kuwa kama wapiganao vita vya mwili hutumia silaha tofauti tofauti na zenye uwezo tofauti kama SMG… hata sisi tulio na vita vya rohoni tunatakiwa kuwa na SMG… za Rohoni ili kuvipiga vita vilivyo vizuri.  
     Ukisoma WAEFESO 6:11-13, 18.  “

Sunday, 22 November 2020

NGUVU ILIYOKUWAMO NDANI YA UPENDO KUTUOKOA

MUNGU KWETU SISI NI KIMBILIO NA NGUVU
MSAADA UTAKAOONEKANA TELE NYAKATI ZOTE


Bwana Yesu Kristo asifiwe sana mtumishi wa Mungu,

Hakika ninapokaa na kuutafakari upendo mkuu ambao Mungu ameudhihirisha kwetu, macho yangu ya rohoni yanaona vitu vingi ndani ya huo upendo.

        Ndipo nilipogundua ya kwamba kumbe UPENDO ni kama kifurushi kilochotumika kubebea mahitaji ya wanadamu, au zawadi za watoto wa Mungu zitokazo kwa Mungu mwenyewe!


Ev. Elimeleck S Ndashikiwe



      Ndipo nikagundua ya kuwa ndani ya huo upendo kuna vitu vingi sana, nikaona moyo wa Mungu kwa kanisa, wokovu kwa kanisa, mavazi yatupasayo watoto wake vikiwa ndani ya huo upendo!


YOHANA 3:16

Kwa maana jindi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanae wa pekee ili tumuamini yaani tumpokee,

Tupate uzima wa milele uliokuwa umefichwa ndani ya Upendo!


        Msukumo wa kiMungu kutuhitaji wanadamu ili turudi kwenye njia yake, shabaha yake ilikuwa kwanza atuandalie vijizawadi ambavyo vitatushawishi na kuwa chambo kitupeleka kwenye wokovu!

       Pasipo upendo yawezekana angetumia njia nyingine, lkn aliona kuutumia upendo kama package au kifurushi inafaa! Akatununua kwa damu yake ya thamani ili tumuamini.


   KWA NINI TUMUAMINI?

Ni kwa sababu ulimwengu mzima ulikuwa umeigeukia miungu mingine na kuiamini,

        Mungu akaona kabisa haipendezi, ili atuondoe kwenye mikono ya imani nyingine ni lazima atuletee vizawadi vitakavyotushawishi kuvikimbilia kwake, tukishavikimbilia kwake tupate kumsikiliza,

Na tukishamsikiliza tu Imani yake mpya inaingia ndani yetu kwa upya tena, ndiposa tumuamini kwa kuwa chanzo cha imani ni kusikia, tena kulisikia Neno la Kristo.




      Mwamini leo Yesu Kristo kupotia Neno lake, nawe utapokea wokovu mkuu tuliodhihirishiwa bure kabisa!

Tusonge hapa;

              Zaburi 91

1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

2 Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.

3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.

4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.

5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,

6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,

7 Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.

8 Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki.

9 Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.

10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.

11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.

12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.


     Nawapenda sana tena sana, Mungu wa mbinguni akubariki sana wewe uliyejaaliwa kuusoma ujumbe huu!


    Na kama una maoni au swali lolote niulize kwa namba

+255 689 240 840


Inapatikana pia kwa njia ya WhatsApp.

Friday, 6 September 2019

KANUNI ZA KIROHO By Ev. Elimeleck Ndashikiwe

    Kila jambo maishani lina kanuni zake.
Kadhalika maisha ya kiroho yana kanuni zake za jinsi ya kushirikiana na Mungu.

     1. MWENYEZI MUNGU ANAKUPENDA, NAYE ANATAKA KUKUPANGIA MPANGO WA AJABU KWA MAISHA YAKO.

       UPENDO WA MUNGU
  Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
       Yohana 3:16

MPANGO WA MUNGU KWAKO
      Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
Yohana 10:10

      Je, kwa nini watu wengi hawana uzima huo? Ni kwa sababu . . .

      2. MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI.
       Dhambi zake zimemtenga na Mungu.Kwa hiyo hajui upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yake.

      MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI
Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
        Warumi 3:23

    Mungu alimwumba mwanadamu kwa kusudi la kushirikiana naye, lakini mwanadamu alikwenda kinyume cha mpango wa Mungu.
     Alichagua kumwasi Mungu badala ya kumtii.
  Kumwasi Mungu ni kufanya dhambi.

       Mtu anapoishi kinyume cha mapenzi ya Mungu anaendelea kuishi maisha ya dhambi.

      MWANADAMU AMETENGANA NA MUNGU
    Lakini maovu yenu yamewatenga ninyi na Mungu wenu.
        Isaya 59:2

       Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi.
       Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi.
    Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa nija nyingi:
   dini, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi.

     Mwanadamu bado ni mwenye dhambi. Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu . .

      3. YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI.
     Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu.
        ALIKUFA ILI ATULETE KWA MUNGU
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu.
        1 Petro 3:18

      YESU YU HAI
Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alitufuka siku ya tatu,
     kama yanenavyojil maandiko.
      1 Wakorintho 15:3,4

YESU NDIYE NJIA YA PEKEE
       Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
           Yohana 14:6

      Mwanadamu peke yake hawezi kushirikiana na Mungu. Mungu alimtuma Yesu afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na tena awe daraja kati yetu na Mungu ili atulete kwa Mungu.

      Sasa kanuni ya nne itakuambia jinsi uwezavyo kumjua maishani mwako . . .

    4. INAKUPASA KUMPOKEA YESU AWE MWOKOZI NA MTAWALA WAKO.
         Ndipo utajua upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yako.

   UNAMPOKEA KRISTO KWA IMANI
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.
        Yohana 1:12

   Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
Waefeso 2:8,9

     INAKUPASA KUMKARIBISHA YESU, MAISHANI MWAKO
     Ndashikiwe
nasimama milangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake . . .

    Kumpokea Yesu Kristo ni:
Kujua wewe ni mwenye dhambi na kugeuka nafsi yako kwa Mungu na kutubu.
      Kumtegemea Mungu kwa kukusamehe kabisa.

   MUNGU WANGU WA MBINGUNI AWABARIKI SANA TENA SANA

   By Ev. Elimeleck Ndashikiwe

    Tel: +255762 680 380