Pages

Subscribe:

Sunday, 23 October 2016

IBADA HALISI INAANZIA ROHONI Yohana 4;23-24 IBADA ni ushirika kati yako na Mungu sawasawa na nafasi zenu. MAANA YAKE; Mungu ni baba yako na wewe ni mwana wake. Hivyo, unanyenyekea na kusikiliza anachokuagiza baada ya hapo unampa mahitaji yako. >Yeye anakupa maagizo na kusikiliza unachohitaji.( You MUST appreciate not only what God has done,but also what he IS ABLE to do. Katika Ibada halisi kuna:- >Kuabudu halisi >Imani halisi >Ushuhuda halisi >Maono halisi na, >MIUJIZA halisi. Bila kuzama rohoni mambo yako yanakuwa ni ya kuigiza. Warumi 8;5-6 · Unalia machozi ya samaki baharini (yasiyokumbukwa) · Unapigana na upepo adui yupo upande mwingine *Wahubiri wengi huhubiri kwa hekima za kibinadamu siyo kwa Roho mtakatifu na kwa NGUVU kwa kuwa Ibada zao si za rohoni. 1korintho 2;4-5 *Huwezi ukajua uliyokirimiwa na Mungu (KARAMA ZA MUNGU KWAKO) kama hauabudu katika Roho na kweli. 1korintho 2;9-12 *Huwezi ukaabudu katika Roho na kweli bila kuwa na Roho wa Mungu ndani yako. Galatia 5;25, Efeso 5;18 *Huwezi ukawa na Roho wa Mungu ndani yako kama haujapewa uwezo wa kufanyika MWANA WA MUNGU(haujaokoka) .Yohana 1;14 Maombi na Neno ndio kiunganishi cha wewe na Mungu kwa Ibada ya Rohoni. >Maombi ni mawasiliano ya rohoni kati yaw ewe na Mungu.MAANA YAKE:-Unaweza ukaingia kanisanin na kutoka bila maombi ya Rohoni haujafanya Ibada halisi. >>NDIO MAANA wengi huja kanisani wakiwa wamebeba dhambi, matatizo, magonjwa n.k. na kurudi nayo hivyohivyo. >>Hata katika makanisa mengi wanafuga mapepo, wachawi, majini, magonjwa na matatizo bila kujijua kwani ni vitu vya rohoni na kuvitambua lazima kuwepo watu wa rohoni (wanaofanya Ibada halisi) Lazima ifike mahali kila mtu awe ni mwombaji na si watumishi tu peke yao. Ndio maana watu wanahama hama makanisa kwavsababu hakuna nguvu za rohoni zaidi ni porojo tu.Mungu atusaidie sana. Nguvu za Mungu hazipatikani isipokuwa tu kwa kuomba ,kufunga na kusoma Neno la Mungu. Mfano; KATIKA MAHUSIANO, Kwa sababu ya kutokuwa na Ibada halisi, watu wameingia KUTAMANI badala ya KUPENDA. Mhubiri 6;9, “Heri kuona kwa macho(ya rohoni) kuliko kutangatanga kwa tamaa(macho ya mwilini)……..”. KUTAMANI – Macho ya nyama, sifa za nje k.m urefu, weupe, wembamba n.k KUPENDA – Macho ya rohoni, sifa za ndani k.m utu wema, amani na watu wote, uvumilivu n.k. Galatia 5;22-23 Ukiambiwa nakupenda uliza kwa nini? Akikutajia sifa za nje(MWILINI) ujue kuwa Hiyo ni TAMAA na wala si UPENDO. ‘’Bali utamkumbuka BWANA Mungu wako……”. Kumbukumbu 8;18-20 >>Unaweza ukaomba mpaka ukakonda lakini bila kujifunza IBADA HALISI utabaki maskini. Hagai 1;5-7. Usifanye biashara ndani ya nyumba ya Mungu(HEKALU) mahali pa Ibada yaani mwili wako.Warumi 12;1.utoe mwili wako…….ndiyo ibada yako yenye maana. Unapokaa na Mungu shetani hapati kibali cha kukutesa. Isaya 35;8,10. Isaya 33;24. >>Ndio maana hakuna utendaji kazi wa NENO katika maisha ya watu. >>Maisha yao ni tofauti kabisa na kile wanachojifunza au kukisema makanisani.Hilo linaitwa (JINA LA KUWA HAI LAKINI NDANI MFU).Ufunuo 3;1 --Unatakiwa uabudu mpaka uone NGUVU ZA MUNGU zinashuka kiuhalisi kutoka juu. 2nyakati 5;13-14. --Shetani kukuweza ni mpaka wewe uache kuenenda kiroho badala yake uenende kimwili. 2korintho 10;3-5. NAMWOMBA MUNGU AKUUMBIE MOYO SAFI WA IBADA NA UWEZE KUMWABUDU YEYE KWA ROHO NA KWELI IBADA HALISI ITAKAYO KUBALIWA NA BWANA KATIKA JINA LA YESU.

Tuesday, 18 October 2016

NIFANYE NINI NIPATE KUOKOKA? NENO LA MSINGI: MATENDO YA MITUME 16:30, 32 “Kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, YANIPASA NIFANYE NINI NIPATE KUOKOKA? Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake” Watu waliookoka katika Kanisa la Kwanza lililokuwa linaongozwa na Mitume, walijua sana jinsi ya kumweleza mtu maana ya wokovu hata yeye naye akaokolewa. Katika Neno hili la msingi, tunaona mtu mmoja akiuliza afanye nini apate kuokoka, na hapohapo anaambiwa neno la Bwana na kuelewa analopaswa kulifanya. Watu wote tuliookoka, ni wajibu wetu kuwaambia watu wote neno la Bwana linalohusu wokovu ili yamkini wote wapate kuokolewa. Jambo la huzuni ni kwamba watu wengi waliookoka, hawawezi kumweleza mtu mwingine neno la BWANA hata akaelewa, na yeye akaokolewa. Kanisa la Mungu halipaswi kuwa hivi na kuwaacha wengi wakiangamia! Basi, ni makusudi ya somo la leo la Kanisa la Nyumbani, kujifunza hatua kwa hatua yanayotupasa kufahamu katika kumwambia mtu neno la BWANA hata na yeye aokolewe. Ikiwa wewe uliyehudhuria leo katika Kanisa la Nyumbani hujaokolewa basi unapokuwa unajifunza somo hili hujaokolewa basi ni siku yako pia kuokolewa baada ya kufahamu yote yanayokupasa kufahamu na kuyafanya. A: NINI MAANA YA NENO “KUOKOKA” AU “KUOKOLEWA?“ Kuokoka au kuokolewa, ni kunusurishwa, kuopolewa, kusalimishwa au kuponywa kutoka katika maafa makubwa yaliyo dhahiri kabisa kukupata. Inaweza ikawa kuponywa kutoka katika hatari ya kifo adhabu kali au madhara yoyote makubwa yaliyo dhahiri. Katika hali ya kukosa matumaini ya kukwepa maafa hayo yaliyo dhahiri, inapotokea ghafla njia ya kusalimika hapo inasemekana umeokoka. ANGALIA MIFANO KATIKA BIBLIA: Baada ya Yusufu kuuzwa na ndugu zake na kupelekwa kuwa mtumwa huko Misri, ilitokea njaa kubwa sana katika ulimwengu wote wa wakati huo. Watu wengi mno walikufa kwa kukosa chakula, na kulikuwa hakuna matumaini. Ndugu zake Yusufu nao walikuwa katika hatari ya kifo. Kabla ya njaa, huko Misri Yusufu kwa uwezo wa ajabu wa Mungu, aliaminiwa na kuwa Waziri Mkuu wa nchi ya Misri na akatumiwa na Mungu kuhifadhi chakula kingi ambacho hatimaye, kilitumika kuwaokoa ndugu zake katika maafa ya kufa kwa njaa. MWANZO 45: 5 – 7: “Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu. Maana miaka hii miwili njaa imekuwa katika nchi, na iko tena miaka mitano isiyo na kulima wala kuvuna. Mungu alinipeleka mbele yenu kuwahifadhia masazo katika nchi,NA KUWAOKOA NINYI KWA WOKOVU MKUU“. Daudi akiwa katika hali ya hatari anaelezea juu ya hali ya mtu anayehitajika kuokolewa mtu ambaye yuko katika hatari ya kufa baada ya kuzama katika matope mengi na maji yakiwa yamefika nafsini mwake. ZABURI 69:1 – 2: “Ee Mungu, UNIOKOE, maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu. Ninazama katika matope mengi, pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, mkondo wa maji unanigharikisha.” Wakati wa Nuhu, Mungu akiwa amechukizwa na dhambi za watu wa wakati ule, aliwaonya watu juu ya maafa yatakayokuja, kuwaangamiza wote wasiomtii Mungu. Watu wote wakapuuza ujumbe huo, isipokuwa Nuhu aliyetii na kuunda Safina iliyotumika kumwokoa yeye na watu wa nyumba yake kutoka katika maafa ya kufa kwa gharika kuu. Watu wote walikufa kutokana na gharika hiyo isipokuwa Nuhu na wenzake saba waliookolewa katika maafa hayo. WAEBRANIA 11:7: “Kwa Imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu aliunda safina, APATE KUOKOA NYUMBA YAKE”. B: MAISHA YA BAADAYE YA MTU MWENYE DHAMBI: Mtu yeyote mwenye dhambi lazima atapata adhabu ya milele. Adhabu yake inaitwa MAUTI YA PILI auMAUTI YA MILELE ambayo ni kutupwa motoni na kuteswa milele. Hakuna mwenye dhambi atakayekwepa adhabu. Kila mmoja atapata mshahara huu wa dhambi, mauti ya milele au kutupwa Jehanum ya moto. MITHALI 11:19 – 21: “——- Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe—— Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu——-“. EZEKIELI 18:4, 20: “—-Roho itendayo dhambi itakufa————-“. WARUMI 6:25: “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.” UFUNUO 21:8: “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao, ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo MAUTI YA PILI.” Hakuna mtu yeyote mwenye dhambi yaani asiyekuwa na haki mbele za Mungu atakayeokoka katika maangamizo hayo. Kwa sasa mtu mwenye dhambi anaona kwamba yuko salama na kwamba amani iko kwake, lakini ghafla uharibifu wake utamwijia. 1 WATHESALONIKE 5:3: “Wakati wasemapo, kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba wala hakika hawataokolewa.” ZABURI 119:155: “Wokovu u mbali na wasio haki kwa maana hawajifunzi amri zako (na kuzitenda)”. C. NI NANI MWENYE DHAMBI? Jibu ni kwamba kila mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke, kutokana na asili ya Adamu, yuko miongoni mwa wenye dhambi. Wote wamefanya dhambi. Kwa mtu mmoja Adamu, dhambi iliingia ulimwenguni; na WATU WOTE wakahesabiwa kuwa wenye dhambi. Kutokana na kila mtu kuzaliwa akiwa na asili ya dhambi, kila mtu anatenda dhambi pia. Hivyo watu wote pamoja, na wewe, wanazaliwa katika dhambi na pia wote wanatenda dhambi. MHUBIRI 7:20: “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.” ZABURI 53:3: “Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja, hakuna atendaye mema, La! hata mmoja.” ISAYA 53:6: “Sisi sote kama kondoo tumepotea, kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe———“. WARUMI 3:23: “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” WARUMI 5:12: “Kwa hiyo kama kwa mtu mmoja (Adamu) dhambi iliingia ulimwenguni na kwa dhambi hiyo mauti na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi”. 1 YOHANA 1:8, 10: “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.” Unaona basi! Kila mtu anakuwa mwenye dhambi kutokana na uzao wa Adamu. Kila mtu anazaliwa akiwa ana asili ya dhambi. Kama Adamu alivyofanya dhambi, wote tunazaliwa na dhambi ya asili. ANGALIA MAANDIKO: AYUBU 15:14: “Je mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi? Huyo aliyezaliwa na mwanamke hata awe na haki?” AYUBU 25:4: “Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu? au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke? ZABURI 51:5: “Tazama, MIMI NALIUMBWA KATIKA HALI YA UOVU; MAMA YANGU ALINICHUKUA MIMBA HATIANI.” AYUBU 14:4 “Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu (Adamu)? Hapana awezaye.” MAOMBOLEZO 5:7: “Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; na sisi tumeyachukua maovu yao.” ZABURI 58:3: “Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao; TANGU TUMBONI WAMEPOTEA, wakisema uongo.” Unaelewa sasa! Tatizo la mwanadamu liko tangu akiwa tumboni mwa mamaye! Ana dhambi! Ndiyo maana mtoto mdogo utamuona anakuwa na hasira, wivu, chuki, ukaidi na ujeuri. Mtoto mdogo atampiga kofi mamaye kwa kumchelewesha kumpa titi anyonye. Mtoto mdogo atagombana na mwenzie. Mtoto mdogo, mapema sana huweza kusema neno “SITAKI” kabla ya maneno ya utii; kuonyesha asili ya uasi na ukaidi iliyomo ndani ya mwanadamu. Mtoto mdogo atatumwa kununua mafuta dukani, na kuzitumia fedha hizo kununua maandazi akirudi kwa mama atasema uongo kwamba fedha zimepotea. Mtoto mdogo anavutwa kutenda dhambi kuliko kufanya haki. Hali ya asili ya dhambi kwa mwanadamu, inamfanya pia kutenda dhambi. Maisha ya dhambi ndiyo yanayoonekana kuwa ya kawaida kwa mwanadamu. Kunywa pombe, kuvuta sigara, kufanya uasherati na uzinzi, wizi, rushwa, uongo, usengenyaji, kiburi na majivuno, chuki, ugomvi, hasira, wivu n.k.; ndiyo sehemu ya maisha ya watu. Sasa basi, kama tulivyoona, kila mwanadamu ni mwenye dhambi kwa kuzaliwa na kwa kutenda. Kwa sababu hiyo, kila mwanadamu anastahili hukumu. Anastahili adhabu. Anastahili mauti ya milele. Huu ndiyo mshahara halisi wa kila mwanadamu. Mungu hawezi kumwacha mwenye dhambi bila kumpa mshahara wake [SOMA AYUBU 10:14]. D: MWANADAMU AFANYE NINI BASI ILI AKWEPE MAUTI YA MILELE? Jibu ni kwamba, ili mwanadamu aokolewe kutoka katika hukumu, ni lazima atoke katika hali ya kuwa “hana haki” na kuwa “mwenye haki” mbele za Mungu. MITHALI 11:21b: “Bali wazao wa wenye haki wataokoka”. Sasa hapa ndipo penye mtego mkubwa wa shetani. Wanadamu katika njia zao, wamefanya matendo fulani kwa kudhani yatawafanya wahesabiwe haki kinyume na mpango wa Mungu wa kuwahesabia haki. Sasa basi, ebu tuangalie mipango hii miwili tofauti. (a) MPANGO WA WANADAMU WA KUHESABIWA HAKI AMBAO SIYO SAHIHI Wanadamu katika dini zao wamepanga kwamba mtu afanye tendo hili na lile ili ahesabiwe haki. Wengine wamedhania watahesabiwa haki kwa kufanya sakramenti zote, wengine wamedhania watahesabiwa haki kwa kushika nguzo fulani za dini; kutoa sadaka sana kwa maskini, kufunga, kusali mara tano au saba kwa siku, kushika sabato, kwenda Jumapili Kanisani, kuimba kwaya, kuacha sigara na pombe, kujenga mahali pa kuabudia iwe ni Kanisa au msikiti n.k. Zote hizi ni njia za mwanadamu – kutenda jambo fulani ili kutafuta kuhesabiwa haki. Hii siyo njia sahihi inayokubalika mbele za Mungu. WAGALATIA 2:16: “——– Wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.” Maana yoyote ya mwanadamu ya kujiosha na kujisafisha moyo wake kwa matendo yoyote ya sheria,sakramenti au kuacha hili na lile; YOTE HAYA NI KUTAABIKA BURE! Bado tu mbele za Mungu utahukumiwa kuwa ni mkosa na Mungu atakutupa shimoni yaani kuzimu na Jehanum ya moto. ANGALIA MAANDIKO: AYUBU 9:29 – 31: “Nitahukumiwa kuwa ni mkosa; ya nini basi nitaabike bure? Ingawaje najiosha kwa maji ya theluji, na kuitakasa mikono yangu kwa sabuni; lakini utanitupa shimoni, nami hata nguo zangu zitanichukia.” Tatizo la mwanadamu linaanzia mbali kama tulivyoona. Kufikiria kwamba ujitahidi kuacha dhambi hii na hii ni kazi bure. Kwanza huwezi, na pili, matendo yako ya haki bado mbele za Mungu yanahesabiwa kama nguo iliyotiwa unajisi, kwa sababu sisi sote ni wachafu kutokana na asili ya Adamu ya dhambi ambayo pekee inatosha kukupeleka Jehanum bila kuongezea lolote. ISAYA 64:6: “Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi, sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.” Yesu Kristo akielezea jambo hili, alisema kwamba, kufanya matendo ya haki fulani fulani, ni kusafisha nje ya kikombe na huku ndani kikombe ni kichafu. Ni kufanana pia na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. Akatoa ushauri kwamba inatupasa kusafisha ndani kwanza [SOMA MATHAYO 23:25-28] . Matendo mema yanakuja baada ya mtu kuokolewa. [SOMA WAEFESO 2:10]. (b) MPANGO WA MUNGU WA KUHESABIWA HAKI Tunahesabiwa haki kwa imani tu! Angalia maandiko: WARUMI 5:1: “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.” WARUMI 3:28: “Basi twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.” Kwa imani, tunazaliwa mara ya pili na kuwa na haki ya kuuona ufalme wa Mungu au kuingia mbinguni. Bila ya kuzaliwa mara ya pili, mtu hawezi kuingia mbinguni: YOHANA 3:3: “Yesu akajibu, akamwambia, Amini, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” E. Nikodemo hakuelewa maana ya kuzaliwa mara ya pili kama jinsi ambavyo wengi hawafahamu leo. Nikodemo aliuliza: YOHANA 3:4: “Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee! Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?” Jibu ni hapana! Kuzaliwa mara ya pili siyo kurudi tumboni mwa mama yako. Kuzaliwa mara ya pili ni hivi: Yesu Kristo anaitwa Adamu wa pili au mtu wa pili aliyetoka mbinguni. Adamu wa kwanza alitoka katika udongo na alipojaribiwa na shetani, alifanya dhambi. Adamu wa pili au Adamu wa mwisho, Yesu Kristo, alipojaribiwa na shetani, hakufanya dhambi kamwe. Kama atulivyoichukua sura ya Adamu wa kwanza na tukawa watenda dhambi, basi kwa imani katika Kristo, Yesu, tunazaliwa mara ya pili na kuchukua sura ya Adamu wa mwisho, Yesu Kristo; mwenye uwezo wa kushinda dhambi. [SOMA 1 WAKORINTHO 15: 45, 47-49; WAEBRANIA 4:15]. Tunakuwa tumezaliwa kwa Roho yenye kuhuisha. Hapo mwanzo tumboni mwa mama zetu tulizaliwa katika mwili, tukachukua sura ya yule wa mwili Adamu, sasa tunazaliwa kwa Roho na kuchukua sura ya yule wa Roho; Yesu Kristo. [YOHANA 3:6]. Kwa sababu hiyo, kama jinsi Yesu Kristo alivyokuwa na uwezo wa kushinda dhambi, sisi nasi tunakuwa na uwezo huo pia. Matokeo haya yanatufanya tuishinde dhambi na kuhesabiwa haki ya kuingia mbinguni. HATUA SITA (6) ZA KUFUATA ILI KUZALIWA MARA YA PILI, KUHESABIWA HAKI, NA KUOKOLEWA KUTOKA KATIKA GHADHABU YA MUNGU 1. UKUBALI KWAMBA WEWE NI MWENYE DHAMBI, UMEMWASI MUNGU, NA UNASTAHILI HUKUMU Umekwisha fahamu kwamba wewe ni mwenye dhambi kwa kuzaliwa na kwa kutenda. Ndivyo ulivyo. Huwezi kukataa. Maisha yako yanakushuhudia mwenyewe kwamba uko mbali na mapenzi ya Mungu. Ukiri wazi jambo hili kama walivyofanya watu hawa katika Biblia: 2 SAMWELI 12:13: “Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia BWANA dhambi ……….” 1 SAMWELI 15:24: “Ndipo Sauli akamwambia Samweli, nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya BWANA…” YOSHUA 7:20: “Akani akamjibu Yoshua akasema kweli nimefanya dhambi juu ya BWANA Mungu wa Israeli nami nimefanya mambo haya na haya.” ZABURI 32:5: “Nalikujulisha dhambi yangu, wala sikuuficha upotevu wangu. Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA ………….” 2. USIKITIKE KABISA KWA DHAMBI ZAKO, UZIUNGAME NA KUWA TAYARI KUZIACHA KUANZIA SASA NA UWE TAYARI KUOMBA MSAMAHA ZABURI 38:18: “Kwa maana nitaungama uovu wangu, na kusikitika kwa dhambi zangu.” MITHALI 28:13: “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.” LUKA 18:13: “Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.” 1 SAMWELI 15:25: “Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu …………….” 2 SAMWELI 24:10: “Ndipo moyo wake Daudi ukamchoma ……. Naye Daudi akamwambia BWANA, nimekosa sana kwa haya niliyofanya; lakini sasa, Ee BWANA, Nakusihi uuondolee mbali uovu wa mtumishi wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa.” EZRA 10:1: “Basi hapo Ezra alipokuwa akiomba kuungama, akilia, na kujiangusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Mungu wakamkusanyikia katika Israeli wote kusanyiko kubwa sana la wanaume na wanawake na watoto maana watu hao walikuwa wakilia sana.” EZEKIELI 18:30 – 31: “…..Rudini, mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote …… Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa; jifanyieni moyo mpya na roho mpya …….” 1. UKIRI KWAMBA HUWEZI KUACHA DHAMBI KWA NGUVU NA UWEZO WAKO NA UOMBE MSAADA WA YESU KRISTO MWENYE NGUVU. Huwezi kuacha dhambi kwa nguvu zako au uwezo wako! Dhambi ina nguvu na uwezo juu ya mwanadamu. Kwa nguvu zako, utajaribu kuacha sigara na kutafuna pipi au peremende lakini siku mbili tatu unajikuta unarudia tena kuvuta sigara. Kiu ya sigara huwezi kuishinda kwa uwezo wako. Kwa nguvu zako utajaribu kuacha uasherati na uzinzi kwa kuogopa magonjwa ya hatari kama UKIMWI, kisonono au kaswende; lakini utajikuta baada ya muda mfupi tamaa iko palepale. Utajitahidi kuacha pombe na kuanza kunywa kahawa lakini muda mfupi unashindwa kabisa kuishi bila kunywa pombe. Ni lazima ukiri kwamba huwezi. Dini haiwezi kumfanya mtu aishinde dhambi. Tangu uwe na dini, hujaweza kushinda dhambi. Watu wenye dini ndiyo ambao wamejaa magerezani wakiwa ni wahalifu wakubwa. Unachotakiwa kufanya ni kusalimu amri na kuanguka miguuni pa Yesu Kristo aliyeshinda dhambi, yeye atakupa msaada na uwezo wa kuishinda dhambi. AYUBU 26:2: “Jinsi ulivyomsaidia huyo asiye na uwezo! Jinsi ulivyouokoa mkono usio na nguvu!” 4. MWAMINI BWANA YESU MATENDO 16:31: “….. akamwambia, mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.” INAKUPASA KUYAAMINI YAFUATAYO (a) YAAMINI MANENO YOTE YA BWANA YESU Kumwamini mtu maana yake ni kuyaamini maneno yake. Kuyaamini maneno ya mtu, kunathibitishwa pale tu unapochukua hatua ya kuyatenda. Mtu akikuelekeza kwamba njia hii ndiyo inayokwenda Nairobi, ishara ya kuyaamini maneno yake ni kuanza kuifuata njia hiyo. Kumwamini Bwana Yesu ni kuyaamini maneno yote ya Bwana Yesu yaani Biblia na kuwa tayari kulitii na kulitenda kila neno ambalo anatuagiza tulifanye bila uasi wa namna yoyote. Tunaokolewa kutoka katika uasi. ZABURI 119:6: “Ndipo mimi sitaaibika, nikiyaangalia maaagizo yako YOTE”. (b) UAMINI KWAMBA YESU ALIKUFA MSALABANI KWA AJILI YA DHAMBI ZETU NA KUCHUKUA HUKUMU YETU Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. Baraba ambaye alikuwa ahukumiwe kifo, aliachwa huru na Yesu akachukua nafasi yake. Aliposulibishwa, tulisulibishwa pamoja naye na kuisulibisha asili ya Adamu inayotufanya tutende dhambi. Tulizikwa pamoja naye na kufufuka naye na kupata upya wa uzima. WARUMI 5:8: “………. Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” ISAYA 53:5: “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu.” WARUMI 6:5-6: “Kwa maana kama tulivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; tukijua neno hili, ya kuwa utuwetu wa kale, (utu wa Adamu) ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena.” (c) UAMINI KWAMBA DAMU YA YESU ILIYOMWAGIKA MSALABANI INA UWEZO WA KUSAFISHA DHAMBI ZOTE. UAMINI KUWA HAKUNA WOKOVU NJE YA DAMU YA YESU. Mpango wa Mungu, tangu mwanzo kabisa ni damu. Mungu anapoiangalia damu, ndipo ukombozi unapotokea. Habili alihesabiwa haki kwa sababu Mungu aliiangalia damu iliyotokana na dhabihu yake[WAEBRANIA 11:3; MWANZO 4:4] ili mwana wa Israeli aweze kuwa salama wakati wana wa Misri walipokuwa wanapata pigo la kufiwa na kila mzaliwa wa kwanza, sharti lililokuwapo ili kuokoka; ni kwamba BWANA alitaka kuona damu katika kizingiti cha juu na miimo miwili ya mlango. Bila damu, hakukuwa na wokovu. [KUTOKA 12:5-7, 12-13, 22-23]. Katika Torati pia karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu, hakuna ondoleo la dhambi [WAEBRANIA 9:22]. Sasa, kwa jinsi hiyo hiyo, hakuna kusamehewa dhambi na kupata wokovu nje ya damu ya Yesu. MATHAYO 26:28: “Kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.”Amini sasa kwamba damu ya Yesu ikinyunyiziwa kwako leo, dhambi zote zitaondolewa na utawekwa huru mbali na dhambi. Utakuwa na uwezo wa kuishinda dhambi. 5. MKIRI YESU KUWA BWANA WAKO: WARUMI 10:9: “Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa Kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.” WARUMI 10:13: “Kwa kuwa, kila atakayeliitia jina la Bwana ataokoka.” Neno “BWANA” maana ya “MTAWALA”. Kumkiri Yesu kuwa ni Bwana wako au kuliitia jina la BWANA wako; maana yake kukubali Yesu akutawale katika mambo yote. Mtu mwenye dhambi anakuwa ni mtawala wa maisha yake. Anafanya analolitaka. Huu ni uasi. Kulielezea jambo hili vizuri, ni kwamba mtu mwenye dhambi, amekalia kiti katika moyo wake na kuushika usukani wa moyo. Yeye mwenyewe ndiye dereva. Anakwenda popote anapotaka mwenyewe. Iwe ni dansini, kwenye sinema, katika baa ya pombe n.k. Sasa, kumkubali Yesu kuwa Bwana wako, ni kuwa tayari kuondoka katika kukikalia kiti cha moyo wako na kumpisha Yesu akikalie. Yeye awe dereva wako. Akupeleke anakotaka na wewe umfuate bila ubishi wowote. Ukubali kwenda sawasawa na neno la Mungu. Linakokupeleka, na wewe ulifuate mara moja. Ukubali kuwa mtumwa na ukubali kuwa huna haki yoyote ya kujitawala. Je uko tayari kumfanya Yesu awe BWANA wako? Tazama, yuko katika mlango wa moyo wako leo anabisha. Anataka kuingia akikalie kiti cha moyo wako. Je uko tayari kumpokea na kumfungulia mlango wa moyo wako aingie? Ukimfungulia, utakula pamoja naye katika Ufalme wa Mungu. UFUNUO 3:20: “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.” 6. CHUKUA MANENO PAMOJA NAWE, MWENDEE HAKIMU: Hii ndiyo hatua ya mwisho: Yesu Kristo ndiye Hakimu atakayeuhukumu ulimwengu [SOMA YOHANA 5:22; MATENDO 17:31]. Hata kabla ya hukumu ya mwisho, mtu yeyote asiyemwamini Yesu katika hatua hizi ulizozifahamu, amekwisha hukumiwa tayari. Ghadhabu ya Mungu inamkalia, na hata akifa sasa kabla ya kutubu, anakwenda Jehanum moja kwa moja. YOHANA 3:18, 36: “Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.” Kwa hiyo ili ukwepe hukumu au uokolewe, njia ni rahisi tu! Ukiwa umeyaamini na kuyakubali haya yote, chukua maneno yote haya kwa ufupi na mwendee Hakimu ukamwambie akuondolee maovu yako yote. Unafanya hivi kwa kutoa sadaka ya mdomo wako au kinywa chako. Kwa kinywa chako unakiri kwamba ni mwenye dhambi na kuhitaji kusamehewa na kumpokea Yesu awe BWANA wako. Maneno haya tunayoyatamka katika sala kwa Hakimu, ndiyo yanayojulikana kwa jina “SALA YA TOBA”. Ni muhtasari wa haya yote tuliyojifunza. Siyo lazima yawe sawasawa kwa kila tunayemwabia ayatamke, maana yake ni kwamba hakuna sala maalum ya kukariri ambayo lazima itumike kwa kila mmoja. Ila ni kwamba misingi ya sala hiyo inabidi iwe ni hatua hizi sita tulizojifunza. HOSEA 14:2: “Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie BWANA, mkamwambie Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo tutakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng’ombe.” Ungeweza kuomba mwenyewe ingekuwa pia ni sawa, lakini kwa sababu hujui kuomba, fuatisha maneno haya na kuyatamka. (Huu ni mfano wa sala ya toba inavyopasa kuwa).

KUOKOKA

Watu wengi wamekua wakijiuliza kuhusu kuokoka ni nini,
jamii nyingine wamekua wakipinga jambo la kuokoka hapa duniani kana kwamba wataweza kutenda jambo wakiwa marehemu ambalo litawafanya waokoke.

Lakini kuokoka wanadamu tunaokoka hapa hapa duniani maana hatuwezi kufanya chochote tukiwa wafu hivyo kwa maamuzi ya leo unaweza kuokoka, kwa matendo yako ya sasa unaweza kuokoka na sio baadae baada ya kufa.

*Kuokoka ni kumwamini YESU KRISTO.
Yohana 1:12 -13
‘’Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake;
waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.

‘’ Kumwamini YESU ni kumkubali YESU na pia kumtegemea kwa kila kitu, na yeye alisema kwamba sisi bila yeye hatuwezi kufanya lolote hata lile lililo dogo kabisa.

Matendo 16:30-31
Biblia inasema
‘’ kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?
Wakamwambia,
Mwamini BWANA YESU, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. ‘’

*Tukimwamini BWANA YESU tunakuwa na ROHO MTAKATIFU ambaye hutufanya kuchukia dhambi kwani bila ROHO MTAKATIFU hakuna awezaye kuacha dhambi.

BIBLIA katika
Yohana 3:3
‘’YESU akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa MUNGU. ‘’

*Kuzaliwa mara ya pili ni
1: Kumwamini YESU.
2: Kubatizwa .
3: Kuwa na ROHO MTAKATIFU.

Yohana 3:17-18’’
Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU.

‘’ Tunaokoka hapa hapa duniani kwa sababu ‘’
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama!
Yamekuwa mapya. ‘’
- 2 Korintho 5:17.

*Ndugu ukiamua kuokoka usirudi nyuma maana unaweza ukapoteza wokovu wako.
Luka 9:61-62'' Mtu mwingine pia akamwambia, BWANA, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu.
YESU akamwambia,
Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa MUNGU.''

*Watu wengine huogopa kuacha dhambi eti kwa sababu shetani atawatesa kwa sababu wamewahi kuingia maagano naye ya kishetani huo ni uongo.

Maana YESU akikuokoa anakuhamisha kutoka katika kila agano lako na shetani na kuanzia muda hu unakua mtoto wa MUNGU ambaye huwezi kurogwa tena maana mamlaka ya BABA yako wa mbinguni uliyeamua kumpa maisha yako ni kuu sana na hakuna anayeweza kukudhuru tena

na BWANA YESU atakuwa ndiye anayekuchunga 
Zaburi 23:1’
’ BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. ‘’ .

*Ndugu duniani hapa tunapita tu maana hata kama ukiishi miaka 98 hapa duniani lakini ni bure kabisa kama utapotelea motoni baada ya kufa kwa hiyo bora kumpa YESU maisha yako na utakuwa huru kabisa pia utapata uzima sasa na baadae uzima tele.

YESU anasema katika
Yohana 10:10b’’
mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. ‘’.

ndugu dunia hii tuliikuta na tutaiacha hivyo ni heri kwa sasa kuishi maisha ya kumcha MUNGU.

Neno la MUNGU linakushauri kwamba ‘’

Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia.
Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele. ‘
’-1 Yohana 2:15-17

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho,

amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU
ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.

MUNGU akubariki sana.

Ni Mimi ndugu yako

Ev. Elimeleck Ndashikiwe

+255767445846
+255715445846

Monday, 3 October 2016

SOMO;
MACHUKIZO NDANI YA NYUMBA YA MUNGU

(YEREMIA 32:33-34)
“Tena wamenigeuzia visogo vyao, wala si nyuso zao;
ingawa naliwafundisha, nikiondoka mapema na kuwafundisha, lakini hawakusikiliza ili wapate mafundisho.
Bali waliweka machukizo yao ndani ya nyumba iliyoitwa kwa jina langu, ili kuinajisi.

Machukizo ya aina yoyote hayaruhusiwi ndani ya nyumba ya Mungu na ndani ya nyumba zetu.

( KUMBUKUMBU LA TORATI 7:26 )
“na machukizo usitie ndani ya nyumba yako, usije wewe kuwa kitu cha haramu mfano wake; ukichukie kabisa, na kukikataa kabisa; kwa kuwa ni kitu kilichoharamishwa”.

Machukizo yanatajwa kuwa ni kitu kilichoharimishwa.
Neno machukizo linatokana na neno la lugha ya kiebrania linaloitwa” toebah.

Neno “TOEBAH” lina maana ya kitu au mtu ambaye ni wa tofauti katika hali. Mtu ambaye ni hatari ukilinganisha na watu wengine.
Yatakuwa ni mambo au tabia ambazo ziko kinyume na asili yake. Machukizo sasa ni vitu vya kipagani ambavyo vimeingia ndani ya nyumba ya Mungu. Yapo mambo ambayo ni machukizo ndani ya nyumba ya Mungu. Mambo ambayo ni haramu kuingizwa ndani ya nyumba ya Mungu.

( i ). Mwanamke kuvaa mavazi ya wanume na mwanamume kuvaa mavazi ya wanawake.
( KUMBUKUMBU LA TORATI 22:5 ). ‘ Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA,
Mungu wako”.
Mungu anasema maumbile yetu ndiyo yatufundisheni vazi lipi linafaa kuvaliwa na wanaume na ni nlipi linafaa kuvaliwa na wanawake ( 1 WAKORINTHO 11:14 ). Mitindo ya ushonaji nguo iadizainiwa kutokana

na maumbile yetu. Ndiyo maana wanawake wana mavazi yao na wanaume wana mavazi yao na Mungu ameliweke hilo mwenyewe. Kwa hiyo vazi kama suruali siyo la mwanamke, limedizainiwa kwa ajili ya mwanamume na si vinginevyo.

Katika biblia ni wanaume pekee wanaotajwa wakiwa wamevaa suruali, hatuoni sehemu yoyote ikimtaja mwanamke akiwa amevaa suruali. Ingia katika blog yangu ujifunze somo la “MAVAZI YA KIKAHABA” utajifunza mengi kuhusiana na mavazi.

Suruali kwa wanawake ni vazi la kikahaba kabisa
( MITHALI 7:10 ) ( ii ). Sadaka ya kahaba na Mbwa ni machukizo mbele za Mungu ( KUMBUKUMBU LA TORATI 23:18 ) “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani

haya ni machukizo kwaBWANA, Mungu wako yote mawili”. Mbwa ni mtu anayerawiti au mtu anayerawitiwa. Mshahara wa kahaba na watu wote wanaoshiriki katika uchafu wa kurawiti na kurawitiwa ni machukizo kwa BWANA, Mungu wetu. Hatutakiwi kupokea sadaka zao kwa ajili ya BWANA, ni machukizo kwake. ( iii ). Miungu na chochote kinachohusiana na miungu ni machukizo mbele za Mungu. ( EZEKIELI 8:1-18 ) Namna yoyote ya sanamu tunapoihusisha katika ibada tayari inakuwa ni ibada ya miungu. Mapambo ya aina yoyote ni chukizo mbele za Mungu wetu kwa sababu kuna uhusiano kati ya mapambo na miungu. Ni muhimu kufahamu kuwa mapambo hayakuvaliwa na Waisraeli. ( WAAMUZI 8:24 ) “ Kisha Gideoni akawaambia, Mimi nina haja yangu kwenu, ni yakila mtu kunipa hizo pete za masikio ya mateka yake. ( Kwa maana walikuwa na pete za masikio za dhahabu, kwa sababu walikuwa ni Waishmaeli )”. Waishmaeli walikuwa ni wapagani ( mataifa ) vilele waliitwa Wamidiani. ( MWANZO 35:1-4 ). “……………Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu,………..Nao wakampa Yakobo, miungu migeni yote iliyokuwa masikioni mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao…………….”. Mwanamke Yezebeli alikuwa mataifa tena mwabudu miungu. Mwanamke huyo alikuwa staid sana kwa kujipamba na aliingia katika Taifa la Israeli baada ya kuolewa na mfalmeAhabu. Kwa hiyo mapambo yalikuwa yakivaliwa na Waisraeli kwa kuiga tabia za mataifa

( 2 WAFALME 9:30-37;
UFUNUO 2:20 ) Makanisa mengi leo yanahudu mafundisho ya Yezebeli ya kuruhusu mapambo kwa watu wa Mungu. Mungu aliwatumia
mitume kwa ishara na miujiza mikubwa kutokana na injili yao kuwa kinyume na machukizo. Kanisa la kwanza walifundishwa kuwa mbali na mapambo ya kila namna ( 1 TIMOTHEO 2:9-10; 1PETRO 3:3-5 ). Kinyume na asili ya Mungu ndiyo maana ya machukizo ( un contrallel to his nature ). Machukizo kwa asili yalikuwa ni ya mataifa na hayakuwa ya Waisraeli.

( YEREMIA 4:1 ) “Kama ukitaka kurudi, Ee Israeli, asema BWANA, utanirudia mimi; na kama ukitaka kuyaondoa machukizo yako, yasiwe mbele ya macho yangu, ndipo hutaondolewa”.

Kuna uwezekano mkubwa hata wakuu wa makuhani ( maaskofu ) kuruhusu machukizo kuingia nyumbani mwa Mungu. Machukizo yakiingia madhara yake ni makubwa kwa watu wa Mungu. Tunaona katika andiko hilo chini kuwa hata uwezo au mkono wa Mungu wa kuponya unaondoka

( 2 NYAKATI 36:14-16 ).
“Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya BWANA aliyoitakasa katika Yerusalemu. Naye BWANA, Mungu wa baba zao akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake;

Lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya”. Miujiza ya Mungu ya uponyaji kama wakati wa Yesu na wakati wa mitume haiwezi kuonekana dhahiri kwa watu wanaoruhusu machukizo kwa watu wa Mungu na ndani maskan i(nyumbani) yake Mungu, Utakuta watu wanashughulika na mapepo tu kila siku lakini miujiza ya vipofu kuona, viziwi kusikia, viwete kutembea, mabubu kuongea, wenye kigugumizi kuongea sawasawa, wenye makengeza kuponywa na kila namna ya miujiza mingine kama nyakati za mitume havionekani. Mamlaka waliyokuwa nayo mitue ya kumwambia kuwete ‘ Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende ( MATENDO 3;6 )’. Mamlaka haiko leo kwa watumishi wengi sababu ni kwamba wameruhusu machukizo nab ado tu wanaendelea kuyatetea kwa bidii nyingi.

( YOHANA 2:13-17 ) Yesu Kristo alipokuta watu wamegeuza hekalu soko alichukizwa mno na kitendo kile ndipo akaamua kupundua meza zao, na kuwaondoa wote hekaluni kwa kutumia kikoto.

Aliuliza, Yesu hakuyavumilia machukizo nyumbani mwa baba yake. Watumishi wa Mungu leo wanatakiwa kufuata msingi aliouweka
BWANA YESU na si kuyaacha machukizo eti kwa visingizio vya kulinda kundilisipungue, hatuwasaidii washirika wetu. Tunapaswa kumwondoa mwovu miongoni mwetu ili wengine wajifunze kukaa katika viwango vyote vya neno la Mungu.

( iv ). Wanawake wanapaswa kufunika kichwa wakiwa katika ibada. Wanapaswa kufunika wakiwa kanisani, wanapofanya huduma yoyote ya kiroho mfano, kuomba, kuhutubu au kuhubiri.

( 1 WAKORITHO 11:4-5,7,10,13
‘ Sheria inayomkataza mwanamume kumwomba Mungu akiwa amevaa kofia pia inayomkataza kuvaa kofia kanisani hiyo hiyo ndiyo inayomtaka mwanamke afunike kichwa

kwa ajili ya Malaika. Wanaosema ilikuwa desturi za Wakorintho hawayaelewi maandiko vizuri. Biblia inasema ‘ Imempasa mwamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani kwa ajili ya Malaika”. Angalia vizuri neno ‘ imempasa=lazima”. Hakuna Biblia ya Wakorintho pekee yao, tukichambua Biblia hivyo sisi Watanzania hatutabaki na kitabu chichote.Yote yaliyoandikwa, yaliandikwa kwa ajili yetu wote ( WARUMI 2;16 ), Mungu atayahukumu mataifa yote kwa injili hiyohiyo Tukitaka kuziona nguvu za Mungu waziwazi lazima tuwe mbali na machukizo ya aina yoyote. Mafuta ya Mungu yanakuwa juu ya mtu anayechukia machukizo

( WAEBRANIA 1:9 ). Mtu ambaye anatetea machukizo yaliyomo ndani ya maskani ya Mungu lakini akifanya miujiza au maajabu lazima tujiulize ni nguvu ipi inatenda kazi hapo?. Mungu mwenyewe anasema kuwa mahali penye machukizo, ukono wake wa kuponya hauwezi kuwepo ( 2 NYAKATI 36:14-16 ), Pia hawezi kupakwa mafutaNA Mungu ( WAEBRANIA 1:9 ). Nyakati hizi tulizonazo watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli, wanapenda kudanganywa. Paulo mtume alitabiri juu ya nyakati hizi jinsi watu watakavyotafuta waliu wa kuwafundisha uongo na kuikataa kweli ya neno la Mungu ( 2 timotheo 4:3-4). Hata wakati wa nabii Isaya walikuwepo watu waliotafuta walimu wengine wa mbali na Isaya aliyehubiri kweli yote. Walisema kuwa wanataka mafundisho laini yadanganyayo ( ISAYA 30;9-10 ).Kama tunataka kuishi na Mungu milele hatuna budi kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha na kuwa tayari kuyafuata maagizo yote ya Neno la Mungu ( ZABIRI 119:6 ). Tunasafisha njia zetu kwa kutii neno la Mungu na siyo walimu wetu wanaotufariji tuendelee kufanya machukizo mbele za Mungu ( ZABURI 119;9 ). Walimu wanaowatia moyo watu ili waendelee kuvaa mapambo na suruali kwa wanawake wote ni wafariji wa kutaabisha ( AYUBU 16:2 ). Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!