Pages

Subscribe:

Wednesday, 25 October 2017

UNAWEZAJE KUWA ROHONI?

           KUWA ROHONI?

        Kuwa Rohoni ni kuwa na Daiolojia na Mungu.

Daiolojia ni mazungumzo baina ya pande mbili,
nikimaanisha Mungu na Mwanadamu.

Tuangalie daiolojia Agano la Kale na Agano Jipya.

   A. AGANO LA KALE
Agano la Kale Mungu alizungumza na Wanadamu kwa njia mbalimbali,

Mgawanyo wangu wa daiolojia na Mungu nimeugawanya kwa kuzingatia idadi ya wahusika.

       1. Moja kwa moja na mtu binafsi (wachache)
a. NdotoDanieli 2:19
b. MaonoEzekieli 1:1
c.Ana kwa ana – Kutoka 33:11, Hesabu 12:7-8

      2. Kupitia Mtu mwingine(wengi)
a. Kuhani (Urim, Thumimu na Naivera) – Kutoka 28:30-31, 1 Samweli 28:6
b. UnabiiKumbu Torati 18:18

      3. Kupitia Kitu(Kiumbe) kingine
a. PundaHesabu 22:28
b. Samaki – Yona 2:10
c.KiganjaDanieli 5:5-6
d. MalaikaKutoka 33:2a

     B. AGANO JIPYA
Agano Jipya Mungu ameboresha Daiolojia,
ni kinyume cha Agano la Kale.
Lakini bahati mbaya wahusika wa Agano Jipya hawapo makini ukilinganisha na wale wa Agano la Kale.

1. Moja kwa moja na Mtu binafsi (wengi)
a. YesuEbrania 1:1-2
b. Roho MtakatifuUfunuo 2:7, Matendo 13:2
c. Kuwa RohoniUfunuo 1:10

2. Kupitia Mtu mwingine(wachache)
     a. Nabii – Matendo 11:27-28
      b. Malaika – Matendo 10:3-4

C. KIZAZI KIPYA --
         Zaburi 24:6
Pamoja na njia zote nilizozitaja hapo juu, bado Mungu anaweza akazungumza na Mwanadamu kwa njia yoyoyte na kaktumia chochote.

          Mungu hana mipaka,
vitu vyote ni watumishi wake.
    Njia zote za Mwanadamu kuongea na Mungu au Mungu kuongea na Mwanadamu ni nzuri
           lakini iliyo bora kuliko zote ni kuongea kwa kupitia
Yesu Kristo Ebr 1:1,

kwa njia ya Roho Mtakatifu,

       wewe utatakiwa kuwa rohoni ili uwe na Daiolojia itakayokuwezesha kuwasiliana na MUNGU.

     Mungu wangu wa Mbinguni akubariki sana kwa ujumbe huu mfupi sana.

NI MIMI RAFIKI YAKO NA NDUGU YAKO
Ev. Elimeleck Ndashikiwe

NAKUPENDA SANA TENA SANA TU.

BARIKIWA ZAIDI KUPITIA Blog yangu HII.

0 comments:

Post a Comment