Pages

Subscribe:

Friday, 2 July 2021

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

MH: PASTOR TARIMO
SOMO:   AINA ZA KARAMA ZA ROHO NA HUDUMA 
    

       Bwana Yesu asifiwe sana ndugu yangu mpendwa msomaji wangu, MUNGU wangu wa Mbinguni akubariki sana kwa kuendelea kuwa nami.

              1Korintho 12:1............ Basi ndugu kwa habari ya karama ...................

   Mtume Paulo anaongelea kwa habari ya KARAMA ZA ROHO ambazo Mungu ameziachilia kwa kanisa ili tu kuukamilisha utumishi kwa watu  wake katika ulimwengu wa Roho na ule wa mwili.

            Ukiendeloea kusoma hadi mstr wa 11 utakutana na namna karama hizi za Roho zinavyofanya kazi kwa masaidizano chini ya uongozi wa ROHO MTAKATIFU.

AINA ZA KARAMA ZA ROHO
         Ziko aina mbalimbali sana za Karama za Roho, lakini katika karama zote hizo zilizo kuu ni karama tisa.
       Aina hizi za karama tunakutana nazo katika kitabu hiki cha 1Kor 12:8

1. Neno la Maarifa
           Aina hii ya karama  inasimamia juu ya utambuzi katika kuwahudumia watu,  mtumishi anaweza kutambua uhitaji wa mtu juu ya kile kinachomsibu kiroho na kimwili.
         Roho wa Mungu atahakikisha anakuonesha kwa ishara kupitia mwili wako mwenyewe.

    Mfano unaweza kujisikia unaumwa kichwa wakati ukiwa ktk huduma,  kumbe Mungu anakuonesha kuwa kuna mtu pembeni anasumbuliwa na kichwa.

2. Neno la Hekima
            Aina hii ya karama inasimamia juu ya utatuzi ktk masuala malimbali ya kiroho na kimwili katika maamuzi.      Mfano wa jambo hili tunaliona kwa mtumishi wa MUNGU Mfalme Suleimani alipoletewa mtoto aliyekuwa akigombewa na wanawake wawili makahaba  
 1Wafalme 3:16-27 utakutana na habari hii.

3. Karama ya Imani
             Aina hii ya Karama inasimamia misingi ya namna Wokovu ulivyojengeka na kujengwa ndani yake.
Maana chanzo cha imani huja kwa kusikia, itategemea umesikia nini na  kwa nani.

Isipokuwa chanzo cha imani ya KRISTO huja kwa kusikia NENO la Kristo mwenyewe.
.............................. IMANI wakati mwingine ni kitu anachopewa mtu kama karama.

4. Karama ya Kinabii na Huduma ya Kinabii
                    =Karama ya kinabii huwa sio ya kudumu, Mungu huiachilia ndani ya mtu maalumu, kwa wakati maalumu na kwa kusudi maalumu.

                    =Huduma ya kinabii hii huwa ni ya kudumu na huwa ni kama ofisi maalumu kwa kazi hiyo.

5. Karama ya Kuponya
                 Aina hii ya karama huwa inasimamia juu ya uwezo katika kuponya, kuwa na juhudi na nguvu ya imani juu ya NGUVU NA UWEZA ULIO KATIKA MUNGU kupitia jina la YESU KRISTO.


6. Matendo ya Miujiza
7. Kupambanua Roho
              si kila roho inatokana na Mungu

8. Aina za Lugha na
9. Tafsiri za Lugha.

......................Karama zina tabia tofauti tofauti ambazo haziwezi kufanana ingawa zinaweza kuingiliana katika utendaji kazi maana zinaongozwa na Roho yule yule mmoja wa MUNGU.

NB;
         KATIKA UTUMISHI WA KUTUMIKIA KWA AJILI YA KRISTO, kuna mikoba mitatu ya muhimu na ya lazima sana ambayo hutakiwi kuikosa.
                .Huduma tano EFES 4;11-12
           .Karama Tisa  1KOR 12;8-10
           .Matunda Tisa  GALAT 5;22-23

TUTAENDELEA NA KIPENGELE CHA HUDUMA.......................

MUNGU WANGU WA MBINGUNI AZIDI KUKU INUA 

Karibu sana katika ibada zetu zinazoendelea hapa kanisani 

PENTECOST TABARNACLE OF PRAISE Kisanga "B" Wazo!

KIJANA NA MAISHA YA UTAKATIFU

INJILI YA AMANI


UTANGULIZI:


       Nakukaribisha msomaji katika tafakari ya somo jingine linalohusu kijana na maisha ya kikristo ni jinsi gani kijana aishi maisha Matakatifu kama inavyompendeza Mungu na si kuwafurahisha tu wanadamu katika maisha yetu tukimchukiza MUNGU. 


   Kristo ni mpakwa mafuta. Ambaye ni tofauti na watu wengine. Sasa basi Ukiwa kama kijana wa kikristo ambaye umebatizwa kwa Roho Mtakatifu ndani mwako na si tu kwa ishara ya Wanadamu ya nje tambua kuwa Mungu amekuweka kwa kusudi lake kama mpakwa mafuta umzalie matunda kwa njia ya Kristo YESU. 

    WARUMI 7:4 
       “Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda”.


     Hivyo basi ili kijana wa Kijana wa kikristo awe katika viwango vya usafi wa maisha ya kiroho lazima kufuata na kutafakari neno hili.


1THESALONIKE 4:1-8

  •        "Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana. Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.

  •        Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.

  •        Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana.

  •        Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso. Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu".


i.                    Kijana wa Kikristo lazima aweke mipaka ya ukuaji wake.


      Ukisoma katika mstari wa kwanza unaonesha kuwa Mkristo ni lazima aenende katika Bwana Yesu maana yake lazima kuwe na mpaka/utofauti kati ya kijana wa Kikristo na kijana asiye wa Kikristo.

      Si kwamba kama kijana asiyemwamini Yesu Kristo anakuwa Mlevi, Mzinzi, Mwasherati, Mwizi, Mwongo n.k. lakini na wewe kijana wa kikristo ukaonekana unayafanya haya bado utaonekana ndani mwako hakuna kweli ya Kristo.


ii.                  Kusudi la Mungu kijana wa Kikristo atakaswe.


     1THESALONIKE 4:3

  “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;”


Uasherati ni kufanya tendo la ngono kwa mtu au kijana ambaye hajaoa au kuolewa ambayo ni tofauti pia na uzinzi ambao mtu anafanya tendo la ngono akiwa ameolewa au kuoa na mtu ambaye siye mke au mme wake.

       My dear vijana wengi shetani ametushikilia kwenye suala hili la uasherati maana miili yetu inawaka kwa kuukimbilia uasherati hata tukashindwa kuweka usafi wa mwili na ROHO zetu na kumkosea MUNGU wetu.


       iii.         Kijana wa Kikristo ni lazima ajue kuutunza mwili wake.


     1THESALONIKE 4:4

      “kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;”


  Vijana wa Kikristo ni wale wanaoweza kuimudu miili yao ambapo inakuwa inawaka tamaa ya uasherati hivyo ndivyo Biblia inavyosema kwamba kuuweza mwili yaani kuhakikisha unaweza kuongoza mwili na sio mwili kukuongoza. Lakini hili pia haliwezekani kama kijana wa kikristo hajatambua thamani ya mwili wake. Jiulize kama kijana wa kikristo mwili wako una thamani gani? Maana kuna vijana wamethaminisha miili yao na chipsi, soda, nguo, pombe n.k. lakini jua ya kwamba hakuna kitu cha thamani kuufikia mwili wako zaidi ya damu ya Yesu Kristo.


      iv.          Mungu anataka Vijana wa Kikristo tusiharibiwe katika suala la mahusiano.


     1THESALONIKE 4:7-8

    “Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso. Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu".


       Mungu anamtaka kijana wa Kikristo kuishi maisha ya kuendelea kuwa mtakatifu na kuto kumkosea Mungu ndio maana katika kitabu cha warumi anasema

     Tumeitwa ili tumzalioe Mungu matunda na ukisoma katika aya hii ya saba inasema hatujaitiwa uchafu bali tuishi katika hali ya utakatifu yaani utakaso.

       Mungu alijua kabisa kwamba mwanadamu peke yake hawezi kuishi katika hali hiyo ya utakaso ndio maana akaweka amri kumi. Lengo la amri zake Mungu ni kutulinda na kutupa mahitaji tunayoyahitaji kwa wakati sahihi.


NB. MOYO SAFI KWA MWANZO MPYA.

v  Pamoja na kufanya Dhambi au maovu mengi lakini MUNGU anaweza kukusamehe na kukufanya mpya


NOTE. MAISHA MAPYA YA KIKRISTO.

v  Maisha mapya ya mahusiano ya kikristo ni kumpenda Kristo kwanza. DANIELI 1:8.



NGUVU ILIYOPO KATIKA NENO LA MUNGU    Karibu ndugu  www.elimelecksimon.blogspot.com

       Kwa ajili ya kujifunza machache haya ambayo Mungu amenipa kibali kuyaachilia kwako kupitia kichwa cha somo kinachosema
   “ NGUVU ILIYOPO KATIKA NENO LA MUNGU ”.  

      Tuanze na kutafakari maana Kamili ya neno kibiblia.     Neno ni ujumbe wa Mungu ambao unaotumika na mwanadamu kwaajili ya kumfundisha na kumwongoza mwanadamu kuishi maisha matakatifu ya kumtafuta Mungu.

       Sambamba na kwamba neno la Mungu limehifadhiwa na mwanadamu kwa njia ya mandishi lakini kutokana na kukua kwa teknolojia hadi kwa njia ya sauti hili neno limehifadhiwa pia.     S asa basi neno hili ndilo ambalo Mungu ametupa kama sehemu ya msingi au njia ya mwanadamu kutatua matatizo yake kwa kulitumia hilo neno. Na hili neno pia baada y

READ MORE

TUMIA MAOMBI KAMA SILAHA.

October 09, 2017

TUMIA MAOMBI KAMA SILAHA:         BWANA Yesu asifiwe!!!!!!!!    Nawakaribisha katika somo hili la “ KUTUMIA MAOMBI KAMA SILAHA ” kama ilivyonenwa katika   WAEFESO 6:12 “ Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama;bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya pepo wabaya katika ulimwengu wa Roho ”    Maana yake vita tuliyonayo sisi Wakristo si katika mwili bali ni katika Roho maana yake kama vita vyetu vingekuwa ni vya mwili tungeandaa mapanga, visu, mashoka, bunduki, mishale na kila aina ya silaha za mwili. Lakini kwa sababu vita tulivyonavyo ni vya Roho ni lazima tutumie silaha za Rohoni ili kushinda vita hiyo maana silaha za mwili hazitatufaa kitu.    

     Sasa kwa maana hiyo lazima tujue kuwa kama wapiganao vita vya mwili hutumia silaha tofauti tofauti na zenye uwezo tofauti kama SMG… hata sisi tulio na vita vya rohoni tunatakiwa kuwa na SMG… za Rohoni ili kuvipiga vita vilivyo vizuri.  
     Ukisoma WAEFESO 6:11-13, 18.  “