Kama ambavyo tumekuwa tukijifunza Nguvu Ya Nidhamu binafsi Katika nafasi Ya Mafanikio
Sasa lazima tutambue Kuwa tunaishi Kwenye ulimwengu,Dunia hii
Kama tunaishi Kwenye ulimwengu huu Lazima tutakutana na Changamoto za hapa na Pale, lazima tutakutana na Vita , lazima tutakutana na Upinzani Kwenye Mambo mbalimbali, lazima tutakutana na vipindi vigumu Kwenye Maisha
Maadam tunaishi Kwenye Dunia hii lazima tutakutana na hayo mambo hatuwezi Kuyakwepa Kamwe Wala Kuyakimbia
Sasa Moja Kati Ya SILAHA KUBWA itakayokusaidia Kuishi Maisha Ya Ushindi katika Dunia hii Katikati Ya Vita Zote, Katikati Ya Mazingira yoyote, Katikati Ya Changamoto Zozote, Katikati Ya Magumu Yoyote
SILAHA HIYO NI KUISHI MAISHA YA NIDHAMU BINAFSI KATIKA MAMBO YA MUNGU KWA MWENDELEZO
Ukifanikiwa Kuishi Maisha Ya Nidhamu Binafsi Kwenye Mambo Ya MUNGU Kwa Mwendelezo utafanikiwa Kuishi Maisha Ya Ushindi Katika Dunia hii
Hiyo ndiyo Siri iliyosababisha Watu Wengi sana Kuishi Maisha Ya Ushindi katika Dunia hii,hii ndiyo Siri inayotufanya Watu Wengi sana tuishi Maisha Ya Ushindi katika Dunia hii
Pamoja na Changamoto Zote tunazokutana nazo lakini tunashinda,Pamoja na Vita Zote tunazokutana nazo lakini tunashinda, Pamoja na Magumu Yote tunayokutana nayo lakini tunashinda, Pamoja na Upinzani tunaokutana nao kwenye huduma, kwenye Ndoa , kwenye uchumi lakini tunashinda na zaidi Ya Kushinda
MAISHA YA NIDHAMU BINAFSI KWA MWENDELEZO KATIKA MAOMBI KUHAKIKISHA KILA SIKU UNAOMBA, USOMAJI WA NENO, UTOAJI BILA KUJIHURUMIA HURUMIA, MAISHA YA MIFUNGO, MAISHA YA IBADA, NIDHAMU BINAFSI KWENYE KUISHI MAISHA MATAKATIFU NDIYO SIRI YA KUKUWEZESHA KUISHI MAISHA YA USHINDI KATIKA DUNIA HII
NINAO Ushahidi wa hili ninalokuambia
Kwa SABABU UNAPOISHI MAISHA YA NIDHAMU BINAFSI KWA MWENDELEZO KATIKA MAMBO HAYO YANASABABISHA UWEPO WA MUNGU UNAKUWA NAWE, YANASABABISHA MKONO WA MUNGU KUTENDA KAZI KWAKO, YANASABABISHA KUWA KARIBU NA BWANA ALIYE NGUZO ,ALIYE NGAO ,ALIYE MSAADA WA KWELI NA HIVYO KABLA LOLOTE HALIJATOKEA BWANA ANAKUPA TAARIFA
Tunajifunza hili Kupitia mfano huu Wa Daniel
👇👇👇👇
Baada Ya Daniel Kuwekwa Juu Ya Viongozi wengine kwenye nchi Ya Babeli Na Wale viongozi walio chini Yake Wakapanga njama za kusababisha Daniel anaondolewa kwenye ile nafasi
Danieli 6:2
[2]na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.
Na ikawekwa Sheria Mtu yeyote asiombe Kwa mungu awaye yeyote Kwa muda Wa Siku 30 na endapo Mtu yeyote atafanya kinyume angetupwa kwenye tundu la SIMBA
Danieli 6:7
[7]Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba.
Na tunaona Daniel akitupwa kwenye tundu la SIMBA baada Ya kukaidi agizo hilo
Danieli 6:16
[16]Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.
Tundu hilo la SIMBA ambapo Daniel alitupwa lilikuwa ni mahali ambapo Mtu akitupwa humo hawezi kutoka tena Maisha Yake ndiyo Yalikuwa Yamefikia Mwisho ni lazima tu ataliwa na kugeuzwa kuwa chakula Cha SIMBA
Lakini Safari hii ikawa ni tofauti Kwa Daniel historia mpya ikaandikwa
Lakini Nini Siri Ya Ushindi Wa Daniel
👇👇👇
Danieli 6:10
[10]Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
👆👆👆 Hii ndiyo Siri Ya Ushindi Wa Daniel alikuwa akiishi MAISHA YA NIDHAMU BINAFSI KATIKA MAMBO YA MUNGU KWA MWENDELEZO
Alikuwa Kila Siku lazima ahakikishe anaomba mara 3 Kwa Siku bila Kuacha Wala kukatisha Katisha, licha Ya majukumu aliyokuwa nayo lakini alikuwa lazima ahakikishe anaomba mara 3 Kwa Siku
Maisha Ya hayo Ya Nidhamu Binafsi Yalisababisha Uwepo Wa MUNGU Kuwa naye , Yalisababisha BWANA Kuwa karibu naye , Yalisababisha Mkono Wa MUNGU kutenda kazi kwake
Hata alivyotupwa kwenye tundu la SIMBA hawakuweza kumfanya chochote
Unataka Kuishi Maisha Ya Ushindi katika Dunia hii Jifunze Siri hii kubwa
Ishi Maisha Ya Nidhamu Binafsi Kwenye Mambo Ya MUNGU Kwa Mwendelezo
Hakikisha Unakuwa na ratiba zinazoeleweka za Maombi,ratiba zinazoeleweka za Usomaji Wa Neno, ratiba zinazoeleweka za Mifungo, ishi Maisha Ya Utoaji Kwenye Kile ambacho BWANA anapitisha kwenye mikono Yako, ishi Maisha Matakatifu
Ninao Uhakika UTAUONA MKONO WA BWANA Katikati Ya Magumu utakayopitia, UTAUONA MKONO WA BWANA Katikati Ya Vita utakazokutana nazo, UTAUONA MKONO WA BWANA Katikati Ya Upinzani utakaokutana nao kwenye eneo lolote la maisha Yako
BARIKIWA