skip to main |
skip to sidebar
 |
|
BWANA YESU atukuzwe ndugu.
Nakuomba usome ujumbe huu hadi mwisho.
Karibu uijue na kuitambua kweli inayoweka huru watu walio tayari kuwekwa huru.
Usiichezee wala kuijaribu Neema ya MUNGU ndugu yangu.
Usione kwamba muda unao sana hata huoni umuhimu wa kuokoka leo.
Usipoteze muda wako katika mambo ambayo hayakujengi kiroho.
Kumbuka kwamba siku ya mwisho hata kazi yako haitakuwa na maana sana hata kama ilikupotezea muda mrefu.
''Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.-Mathayo 11:12''
-Wanaoupata ufalme wa MUNGU ni wale ambao wamewekeza rohoni na sio mwilini.
-Walioupata ufalme wa MUNGU ni wale waliompokea BWANA YESU na kuishi maisha matakatifu siku zote.
Inawezekana kabisa ka dhambi kadogo tu kamekushinda kukaacha na hujui
hata kwanini huachi. Kumbe tatizo ni muda wako unautumia vibaya.
Huna hata dakika 50 kwa siku kwa ajili ya MUNGU lakini muda wa kuangalia
filamu au tamthilia unao. muda wa kuangalia mpira au kusikiliza miziki
ya kidunia unao.
Muda wa kufanya jambo lolote unao isipokuwa muda wa kwenda kanisani tu ndio huna.
Muda wa kila jambo ulitakalo unao lakini muda kwa ajili ya mambo ya MUNGU tu ndio huna.
Ndugu.
''Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama
ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya
kichwa chako mwenyewe.-Obadia 1:15''
-Neno la MUNGU lipo na halibadiliki.
Neno linasema siku ya BWANA i karibu, kila mtu atalipwa sawa na matendo yake yalivyo.
Kuna wakati natamani nimfuate kila mtu na kumwambia aokoke na kuanza kuishi maisha matakatifu.
Kuna wakati natamani MUNGU ampe kila ndugu na rafiki yangu moyo wa toba.
Watu wengi leo hawataki neno la MUNGU la uzima.
Kuna wengine husikiliza neno la MUNGU la kweli kama hili lakini halifuati wala kulitii.
Kuna wengine hutii neno la MUNGU kwa sabab tu ya magumu wanayopitia lakini akipata hitaji lake anamsahau MUNGU.
Ni hatari sana.
Ndugu yangu, uzima wa milele n wako binafsi na sio wa jumuiya.
Kama mwenzi wako wa ndoa ndie chanzo cha wewe kumwacha YESU nakupa pole
maana bado hujatambua kwamba uzima wa milele hamtashare bali kila mtu
sawasawa na matendo yake.
Kila siku MUNGU BABA ananipa ujumbe ili tu
ndugu yangu usikose uzima. MUNGU kila siku anawapa watumishi wake
mbalimbali neno lake ili tu Mwanadamu usiende jehanamu lakini binadamu
waliowengi wanaona kawaida kawaida tu.
Ndugu yangu, nakuomba uone kila kitu cha kawaida kawaida lakini sio Neno la MUNGU.
Anapofariki mtu tunalia na kuomboleza lakini ukweli ni kwamba zamu yake
yeye amemaliza na ameenda ama mbinguni ama kuzimu kutegemea na matendo
yake. lakini kifo chake ni taarifa kwetu kwamba ipo siku tena inakuja
siku hiyo ambapo hata sisi tutaondoka duniani.
Shetani alivyofunga watu unaweza ukaona mtu analia msibani lakini akiondoka hapo anaenda kufanya uzinzi na uasherati.
Mtu analia msibani lakini jioni ya siku hiyo hiyo anaenda dhambi kama kawaida.
Ndugu zangu ni wakati wa neema lakini neema hiyo ina mwisho.
Mwenye sikio la kusikia na asikie leo.
Siku moja katika maono nilimuona BWANA YESU amesimama kwa mbali kidogo
na pale nilipokuwa mimi na watu wengine wengi. akaniita nikaenda,
nilipoenda alipo akanionyesha kitabu cha uzima, nikaliona jina langu
humo na majina machache ya watu ninaowafahamu.
Baada ya kuliona jina
langu BWANA akanituma niende nikawaambie wanadamu kwamba wampokee yeye
na kuanza kuishi maisha matakatifu.
Lilikuwa jambo la ajabu sana
lakini kwenye maono nilijiona nikienda na kuwaeleza wanadamu, kuna ambao
nilikuwa mpaka nawaambia na kuwalazimisha waokoke, niliifanya kazi hiyo
kwa muda mrefu. kuna waliookoka na wengine hawakuokoka, baadae BWANA
YESU akasema inatosha akaniiita niende alipokuwa amesimama yeye,
nikaenda.
Ndugu nakushauri kumpokea YESU na kuanza kuishi maisha matakatifu kuanzia leo.
Hatuna injili nyingine zaidi ya Wokovu wa BWANA wetu YESU KRISTO aliye pekee na uzima wetu wa milele.
Wakolosai 3:5-10 '' Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi,
uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada
ya sanamu;kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya MUNGU.Katika hayo
ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo.Lakini sasa yawekeni
mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na
matusi vinywani mwenu. Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa
kale, pamoja na matendo yake; mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate
ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba. ''
Ndugu yangu,
tunapohubiri injili ya KRISTO inayookoka hatuhubiri jambo ambalo ni
labda tu kuwepo, bali tunahubiri jambo ambalo ni ndio katika ndio tena
ni kweli katika kweli zote.
Kama kweli wewe binafsi unautaka uzima
wa milele nakushauri kimbilia kanisa la kiroho na ukaokoke kisha kuanzia
leo anza kuishi maisha matakatifu.
Wokovu ni wako binafsi na sio wa ukoo wala familia yako.
Ukisema kwamba unafuata mila au taratibu za ukoo wako haitakusaidia.
Kama unasubiri hadi baba na mama yako waokoke ndio na wewe utampokea YESU hiyo haitakusaidia.
Neema ipo leo na neema hiyo nakuomba sana uitumie vizuri.
Heri kuokoka kuliko kujifurahisha kwenye dhambi kisha ukifa unaenda kulia milele jehanamu.
BWANA YESU anaokoka na ukimpokea leo hakika unaokoka.
Saa yako moja inaweza kuamua ni wapi utaenda baada ya kufa.
Muda wako wa leo ni muhimu sana kuliko muda wa kesho.
Itumie leo vizuri ndipo utakapoiona kesho yako ikiwa vizuri zaidi.
BWANA YESU amenituma kwa ndugu zangu wote na marafiki.
Mwenye sikio LA kusikia na asikie Leo na kuchukua hatua.
Jehanamu inawangoja watenda dhambi lakini ashukuriwe MUNGU maana mbingu inawasubiri watakatifu wa MUNGU.
Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi
tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea
ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika
jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
ROHO aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee
motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO
BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
0714252292
MUNGU akubariki sana uliyesoma
 |
|
Ndugu nakukaribisha katika somo hili muhimu
kwa maisha ya waenda mbinguni.Na kumbuka
kuwa HUWEZI KUWA MKRISTO KAMA HUNA
KRISTO MOYONI MWAKO. Hivyo hakikisha
kwanza unakuwa na KRISTO maishani mwako
ndipo utakuwa MKRISTO sahihi na sio mkristo
jina.
Je mtu anaweza kuwa baharia bila kwenda
baharini?
Mkristo maana yake ni mfuasi wa
YESU KRISTO. Tunasoma katika Biblia kuwa
YESU alikuwa na desturi ya kwenda hekaluni na
angali anapatikana mahali pa ibada hata leo.
Wakristo ni watu wanaompenda MUNGU, na kwa
hivyo wanawapenda watu wa MUNGU na nyumba
ya MUNGU. Biblia haiwapendekezi Wakristo
pekee, Hata ile hali ya kuwa Mkristo
asiyekwenda kanisani haimfai mtu yeyote. Ni
kama mtu anayeishi kwa kula tu mkate na maji
hali anaweza kupata chakula kizuri kwa afya
yake. Kama alivyosema mwana mpotevu.
''Nyumbani mwa Baba yangu kuna chakula kingi,
wanakula mpaka wanakiacha''(Luka 15:17).
Katika kanisa utapokea mkate wa uzima ambao
ni neno la MUNGU. Kumbuka ya kuwa vitabu
fulani katika Biblia viliandikwa kama barua kwa
makanisa na faida yake kamili inaweza tu
kupatikana unaposhirikiana na wengine..
Ni
afadhali kupata kilicho bora zaidi.
Kumbuka
mwanajeshi hufanya kazi kwenye jeshi .
kaa
la moto likitengwa na mengine litazima.
Hakuna ndoa ya mtu mmoja tu peke yake, Ndoa
ni uhusiano na upendo. Ndoa inakuhusisha na
jamaa wa pande zote mbili.
Hakuna mtu
anayeweza kuwa mkristo wa peke yake tu.
mtu
hawezi kuzaliwa tu peke yake bila ya kuwa na
wazazi na jamaa wa karibu..
Unapozaliwa mara
ya pili yaani unapobatizwa ubatizo wa maji
mengi na pia unapobatizwa ubatizo wa ROHO
MTAKATIFU unafanyika sehemu ya jamii ya
waaminio, Biblia katika Marko 16:16 inasema
''Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini
atahukumiwa'' hivyo kubatizwa pia ni muhimu ili
kuitimiza haki yote ya MUNGU. Jambo hili la
kuamini na kubatizwa lina manufaa makubwa
kwako, huu ni urithi wako na kama mtume Paulo
anavyosema , MKRISTO NI WA AINA MOJA TU-
MSHRIKA WA MWILI WA KRISTO.
Sisi ni washirika wa mwili wake katika
ulimwengu huu. Kanisa liko duniani kwa sababu
sisi sio roho tu bali pia ni watu wenye mwili na
damu. BWANA aliliunda Kanisa hapa duniani
kwa manufaa yetu na ametukirimia vipawa
kutoka mbinguni ili tuweze kupata nguvu kutoka
kwa wenzetu na kufurahia ushirika wa KIKRISTO
na upendo. Maandiko yamejaa habari za ushirika
na kutushauri kwamba tusiache kutumia nafasi
nzuri za ushirikiano na kushauriana na kwamba
tusiache kukusanyikana pamoja kumwabudu
MUNGU wetu.
JINSI YA KUWA KRISTO MWENYE AFYA .
1: Kula chakula kizuri yaani NENO LA MUNGU.
2: Kunywa maji mengi yaani ROHO MTAKATIFU.
3: Fanya mazoezi yaani MTUMIKIE MUNGU NA
KUTENDA KAZI KWA AJILI YAKE.
4: Pata hewa safi yaani HUSIKA KATIKA IBADA
NA SIFA.
J5: iburudishe yaani KWENYE USHIRIKIANO NA
WAKRISTO WENGINE.
MUNGU awabariki sana na kama hujamba
BWANA YESU maisha yako wakati wa kufanya
hivyo ni sasa maana hakuna uzima wa milele
bila YESU KRISTO (Yohana 14:6) hivyo kwa
sababu ndugu unataka uzima wa milele mpe
YESU maisha yako na utakuwa huru mbali na
uonevu wa shetani.
MUNGU akubariki tena
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.
 |
| Na Peter M Mabula |
BWANA YESU asifiwe ndugu zangu.
Karibu tujifunze.
Ndugu Zangu Huu Ni Wakati Wa Mwisho.
Wakati Kibiblia Unaweza Kumaanisha Miaka
Kadhaa Ambayo MUNGU Ndie Ajuaye. Nyakati
Moja Inaweza Hata Kuwa Na Zaidi Ya Miaka
1000.
2 Timotheo 3:1-7, Lakini ufahamu neno hili, ya
kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za
hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda
wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu,
wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi
wao, wasio na shukrani, wasio safi,
wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya
suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali,
wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye
kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda
MUNGU; wenye mfano wa utauwa, lakini
wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao
katika nyumba za watu, na kuchukua mateka
wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi,
waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;
wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa
kuufikia ujuzi wa kweli.
Siku moja kama miezi miwili iliyopita nilikuwa
kwenye gari la abiria maarufu kama costa
nikitoka Kawe kwenda Ubungo, njiani kabla ya
kufika Mwenge kuna dada mmoja alipanda gari
na kukaa siti jirani na mimi, Dada yule alikuwa
anasoma Gazeti ambalo nilipoliangalia nililiona
kama jipya kwangu lakini la kidini, gazeti lile
lilikuwa na vichwa vya habari vizuri sana na
hakika ni gazeti linalovutia, nilitamani kulinunua
gazeti hilo jipya la kikristo ambalo hakika halina
udaku bali mambo mengi ya Biblia, nilimuomba
dada yule aniambie linauzwa wapi.
Nilipomwambia tu hivyo akanipa na kusema
nichukue tu maana yeye anayo mawili ya toleo
moja, muda kidogo yule dada akashuka kabla
hata ya Mlimani city, Nilimshukuru kwa tendo
lake jema la kunipa gazeti. Sikusoma kwa muda
huo bali nilikusudia kusoma nikifika ubungo, ni
kweli baadae nilianza kusoma na ndipo
nilipojisemea kwamba ''Mwisho wa dunia
umefika''. Gazeti hilo lilikuwa na kichwa cha
habari kimojawapo kiitwacho ''KRISTO
ANATAWALA NA KANISA'', Nilipenda kichwa cha
habari hicho lakini nilipofungua ndani kuhusu
ujumbe wa kichwa hicho cha habari nilikutana na
kasheshe ambalo sijawahi kulisikia kabla. Yule
Kristo anayetajwa sio BWANA YESU
tunayemfahamu mimi na wewe bali ni
mwanadamu mmoja ambaye kwa sasa ni
marehemu na alikuwa kiongozi wa dhehebu moja
la kikristo. huyo ndio anaitwa Kristo na licha ya
kufariki bado waumini wake wanajua kwamba
bado anatawala. Ufafanuzi wa taarifa hiyo ya
kishetani gazetini ni kwamba BWANA YESU ni
KRISTO wa kwanza lakini kizazi Hiki cha sasa
eti MUNGU ameletwa kristo wa pili ambaye ni
mwafrika wa Tanzania. Niliumia sana na kuwaza
mengi sana na binafsi hadi leo naamini kwamba
viongozi wa dhehebu hilo ni mawakala wa
shetani na wapo kwa ajili ya kuhakikisha
waumini wao hawaendi mbinguni. Waumini wa
dhehebu hilo mimi siamini kama huwa
wanasoma Biblia bali huwa wanasomewa tu.
Nilichojifunza ni kwamba dhehebu hilo halina
mpango wa waumini wake kwenda mbinguni. hili
dhehebu ni hatari kama wachawi walivyo hatari,
Hakika ni siku za mwisho.
Tunajua Kwamba Hizi Ni Siku Za Mwisho Kwa
Sababu Ya Dalili Zilizoko Kwenye Biblia. Kama
Wewe Unavyoweza Kujua Dalili Za Mvua Baada
Ya Kuona Mawingu Ndivyo Hivyo Mwisho
Umekaribia baada ya kila dalili kuonekana.
( 1 Yohana 2:18-23, Watoto, ni wakati wa
mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba
mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo
wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo
twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. Walitoka
kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama
wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi.
Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote
walio wa kwetu. Nanyi mmepakwa mafuta na
Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote.
Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo
kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba
hapana uongo wo wote utokao katika hiyo kweli.
Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa
YESU ni KRISTO? Huyo ndiye mpinga Kristo,
yeye amkanaye BABA na MWANA. Kila
amkanaye MWANA, hanaye BABA; amkiriye
MWANA anaye BABA pia. ).
Dalili za siku za mwisho ni nyingi, baadhi ni
hizi:
1. Wapingakristo watatokea:hawa ni dini au
watu binafsi ambao wanakataa ukombozi kupitia
YESU KRISTO.
2. Watu kuliacha fundisho la KRISTO.
-Waongo ni wale wanaomkataa YESU na jambo
la kukumbuka ni kwamba anayemkataa YESU
huyo anamkataa MUNGU, Hakuna mtu aliye
upande wa MUNGU kama amemkataa KRISTO
katika maisha yake.
Hakika Ni Siku Za Mwisho.
3. Makristo Wa Uongo Wameshakuja( Mathayo
24:5,Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu,
wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya
wengi. ).
-Wengi hata sasa wameshakuja waongo na
kuleta dini zao na wao kusimama kama nembo
(icon) ya dini hizo, hawa hujifanya wakombozi
wa watu na kwa hali hiyo hujifanya KRISTO.
-Wengi wanahubiri kama wanamhubiri KRISTO
lakini ndani yao wana ajenda za kuzimu za
kuwapotosha watu, hawawezi kukemea dhambi
wala kufundisha toba.
4. Manabii Wa Uongo Wapo Na Hawakawii
Kukwambia Kwamba YESU Atarudi Akiwa Shehe
( Mathayo 24:24-27, Kwa maana watatokea
makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao
watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate
kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi
wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo
nyumbani, msisadiki. Kwa maana kama vile
umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata
magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja
kwake Mwana wa Adamu. )
-Ndugu zangu, kuna watu hukimbilia miujiza,
ndugu zangu sio kila wafanya miujiza ni
watumishi wa MUNGU aliye hai, hata shetani
naye ana watumishi wake ambao anawatumia.
-Mtu akileta fundisho tofauti na fundisho la
KRISTO huyo ni nabii wa uongo.
-Wanaotangaza tarehe za kuja kwa YESU hao
ndio hata hawajui walifanyalo.
Ndugu zangu mwisho umekaribia ila hakuna
ajuaye siku wala saa, sisi tulichopewa kujua ni
dalili tu na hakika dalili huonyesha kwamba
mwisho umekaribia..
1 Petro 4:7 '' Lakini mwisho wa mambo yote
umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika
sala. ''
5. Nyakati Za Mwisho Watu Watapenda Pesa
Kuliko MUNGU Tena Wasaliti ( 2 Timotheo 3:1-7)
6. Nyakati Za Mwisho Watu Watasikiliza
Mafundisho Ya Mashetani
7. Watajitenga Na Imani
8. Na Watazuia Watu Kuoa
9. Na Watakataza Watu Kula Baadhi Ya Vyakula
1 Timotheo 4:1-4 ''Basi ROHO anena waziwazi
ya kwamba nyakati za mwisho wengine
watajitenga na imani, wakisikiliza roho
zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa
unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa
moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu
wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula,
ambavyo MUNGU aliviumba vipokewe kwa
shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo
kweli. Kwa maana kila kiumbe cha MUNGU ni
kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama
kikipokewa kwa shukrani; ''.
10. Siku Za Mwisho Watu Watajaa Dhihaka 2
Petro 3:3-4 '' Mkijua kwanza neno hili ya
kwamba katika siku za mwisho watakuja na
dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao
tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi
ile ya kuja kwake(YESU)? Kwa maana, tangu
hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa
hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa. ''
11. Watu wengi watakua Hawana ROHO
MTAKATIFU( Yuda 1:18-21, ya kwamba
waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho
watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata
tamaa zao wenyewe za upotevu. Watu hao ndio
waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio
na ROHO. Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya
imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika
ROHO MTAKATIFU, jilindeni katika upendo wa
MUNGU, huku mkingojea rehema ya BWANA
wetu YESU KRISTO, hata mpate uzima wa
milele. ).
Ndugu Zangu Wanamume Kwa Wanawake YESU
KRISTO Anatuita Kwenye Ufalme Wake. Amua
Vyema Leo Kwa KUOKOKA.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi
tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea
ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika
jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki
upotelee motoni anataka uende uzimani aliko
KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.