Pages

Subscribe:

Monday, 5 October 2015

KARAMA AU VIPAWA KAMA ZAWADI KUTOKA KWA MUNGU

Bwana Yesu asifiwe mpendwa wangu,
Kwa kila anayeamini ya kuwa Bwana Yesu Bwana na Mwokozi wa maisha yake,
anafanyika KIPAWA CHA BWANA,
anapewa karama kama zawadi YOH3:16

Ktk EFES 2:8-9 kuokolewa kwetu
hakukuwa jinsi tulivyoonekana au kumfanyia BWANA
bali
ni kwa matokeo ya neema au upendeleo wa kipawa
kutoka kwa Mungu mwenyewe.

MUNGU hugawa karama nyingi tofautitofauti
kama viungo vya mwili ktk kuujenga mwili wa Kristo ambao ni kanisa 1PET 5:5

KANUNI TANO (5) ZA KUFAHAMU KTK KARAMA.
1.Karama ni kwa ajili ya kanisa ktk kuujenga mwili wa Kristo 1KOR 12:12,17 na mtu.

viungo hutegemeana 1KOR 12:24-26
Mfano Petro alipofungwa gerezani,
kanisa liliomba kwa ajili yake na akawa huru.

2. Karama ni kwa manufaa ya kundi zima
wala si kwa faia yako mwenyewe 1PETR 4:10,11
karama mzitumie kwa kuhudumiana
maana tumejaaliwa na Mungu na atukuzwe ktk karama zetu.

3.Vipawa ni vya ki Mungu!
1KOR 14:23-25
Paulo alijaribu kueleza na kulifundisha kanisa
akawauliza,
kuwa na maongozo ya ki Mungu na unyenyekevu
kuweza kumsaidia mpumbavu.

Jinsi gani anaweza kuishi na mtu ambaye hajaokoka.

4.Karama na vipawa hutawaliwa na upendo
Ukikosa upendo au kupendwa, karama zako hupotea sawa na
GAL 6:7.

5.Karama hutawaliwa na mafundisho ya NENO LA MUNGU
RUM 12:3-16.
Huwezi kuendeleakuitunza karama/kipawa kama zawadi kutoka kwa Mungu
kwa kutokupenda neno la Mungu.

Nashukuru mpendwa wangu kwa kulisikiliza somo hili
ambalo limekufikia maalumu kukuvusha hatua moja mbele.

NI MIMI MPENDWA WAKO
MWALIMU NA MWINJILISTI
Elimeleck S Ndashikiwe.

+255767445846
+255715445846.

BARIKIWA NA BWANA.

UKUU WA MUNGU KATIKA MAISHA YANGU

Kila kunapokucha nazidi kuushangaa ukuu wa Mungu ktk maisha yangu,

ashukuriwe yeye awezaye kutenda mambo makuu zaidi ya yote niyawazayo EFES 3:20b

Jana ktk ibada niliuona uweza wake
baada ya mimi kukutana na yeye ktk hitaji langu binafsi.

Huwezi amini
kama Bwana aishivyo
niliuona mkono wake ukinivusha
toka hatua moja hata nyingine zaidi.

Nashindwa hata kuelezea.

NIKUFANANISHE NA NANI MUNGU WANGU?
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiwaza
ni lini BWANA ataniinua.....!

Kwa uaminifu wake amenutoa chini na kuniketisha na wakuu.

Ameniongezea mipaka ya utumishi
na sasa
naendelea vema kwa msaada wake (EBEN EZER) maishani mwangu.

Nampenda sana kwa kuwa yeye ndiye aliyenipenda kwanza
YOH 3:16.

MUNGU AKUBARIKI MPENDWA WANGU
pamoja nami
Ev. Elimeleck S Ndashikiwe
      +255767445846
      +255715435846.

AMEEEEEEEEEEEN……………!

Sunday, 4 October 2015

REST IN PEACE PASTOR J MTIKILA

MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI DUNIA  Mwili wa Mchungaji Mtikila mara baada ya ajali    Gari alilokuwa Mchungaji Mtikila, dereva na mlinzi wake Mwenyekiti  wa  Chama  cha DP,Mchungaji Christopher Mtikila amepata ajali mbaya ya gari maeneo ya Chalinze na kufariki Dunia papo hapo. Mtikila alikuwa na mlinzi na dereva na yeye Mtikila amefia pale pale na wengineo hali zao ni mbaya na kuwahishwa katika hospitali ya Tumbi. RPC wa Pwani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo eneo la Msolwa. Mwili wa Mchungaji Mtikila umehifadhiwa hospitali ya Tumbi. Mwenyezi Mungu ampe mwanga wa milele. Amen!!