Pages

Subscribe:

Friday, 25 March 2016

KAZI YA MSALABANI

Ushindi kwa Nguvu ya Msalaba”.

I KORINTHO 6:18… [Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.]…
Nguvu ni uweza wa kutenda jambo Fulani. Nguvu ya Mungu inahitajika kuifanya kazi ya Mungu. Biblia inasema hatuwezi lolote kama hatuna nguvu ya Mungu. Yesu Kristo aliwaambia wanafunzi wake wakae Jerusalemu waisubiri nguvu…..
MATENDO 1:4…. [Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu;]…..

Katika mstari wa 8 ahadi hii imezungumzwa:

“ Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”

Kwa hiyo ukiongelea Ukristo, unaongelea nguvu ya Mungu. Endapo Ukristo hauna nguvu, basi huo hautatofautiana na dini zingenezo zote duniani.

1 KORINTHO 2:4…[Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,]….

Nguvu hii ikiwepo kwako, utatofautishwa na imani nyingine zote.
2 KORINTHO 4:20…. [ Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu.]….

Mtu anaweza kushawishi wengine sana, lakini endapo maneno yake hayana nguvu ya Mungu,basi hayana maana.

1 THESALONIKE 1:5….[ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.]….

Nguvu ya Bwana Yesu inatutofautisha na watu wengine. Mtu amjuaye Yesu kristo lazima nguvu ya Mungu ikae kwake: Nguvu ya uponyaji, kutoa mapepo, kufufua wafu n.k.
WAEFESO 3:20…[Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;
21 naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.]…

LUKA 4:18…[Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,]….

Huu ni utambulisho wa Yesu Kristo na kazi aliyoijia. Baada ya kuifanya kazi hii kwa miaka 3 na nusu, alikamatwa, akateswa na kusulubishwa msalabani….

YOHANA19:28…[Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.].

MATUKIO YA MSALABA
Jua lilipoteza NURU na dunia ilikuwa giza.
LUKA 23:44-…..[Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda, 45 jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati.]….

Jua lilisalimu amri. Utukufu wa jua ni kuwaka na kuichoma nchi. Jua likinyamaza maana yake kwenye msalaba, vitu ambavyo kihistoria haviondoki kamwe, vinaweza kutiishwa na kuondoka.
Endapo tutautazama msalaba ina maana, magonjwa yatainama, vilivyopotea vitarudi kwa Jina la Yesu. Kila kilichopotea kinapatikana pale msalabani.

Je, unalo jambo umelipoteza katika maisha yako?

Msalaba ni kama mtambo ambao vitu vilivyopotea: mfano, Kazi/mke/mume/watoto/elimu n.k vilivyopotea vinarudi upya katika Jina la Yesu.

Msalaba sio mti kama ambavyo wengine wanawaza na hata kuchonga miti yenye mfano wa msalaba na na kupeleka majumbani kwao. Pazia la hekalu likapasuka toka juu hadi chini….

Leo ndugu yangu unatakiwa ubebe nguvu ya msalaba na kisha utembee nayo, ili utakapofanya mambo yafanikiwe katika Jina la Yesu.

Wakati wa Agano la Kale, Mungu aliwahi kuwaagiza wana wa Israeli kutengeneza Hema la Kukutania, lenye maeneo matatu:- ·

Nyuani mwa Bwana ·
Patakatifu ·
Patakatifu pa Patakatifu

KUTOKA 26:31-33 …. [Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi;
32 kisha litungike katika nguzo nne za mti wa mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika matako ya fedha manne.
33 Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana.]…..

Mahali pale palipowekwa Sanduku la Agano palitengwa kwa pazia, maana hapa ni Patakatifu pa Patatkatifu.

Pazia liliwakilisha kuwatenga wasiostahili kuingia mahali hapa Patakatifu pa Patakatifu.

YESU alivunja vizuizi vyote vya kumuona Mungu, ili kila mmoja aende kwa Mungu endapo ataukimbilia Msalaba.

Nguvu ya msalaba inatupa nguvu ya kumuendea Mungu moja kwa moja. Ukiona umeshindwa na dhambi, siyo wakati tena wa kusemaMtakatifu Petro uniombee/ au Mtakaatifu X uniombee”…

Msalaba wa Yesu ulipasua kizuizi hicho, na sasa tunamwendea Mungu moja kwa moja kwa njia ya Msalaba.
Kumbuka kuwa Patakatifu pa patakatifu pana Utukufu.

MAOMBI:
Pazia lolote lililozuia maisha yako leo nalipasua kwa Jina la Yesu.
Ee pazia la kunizuia nisikutane na Baraka zangu,kwa nguvu ya msalaba pasuka…………
Kwa Jina la Yesu.

Lipo pazia ambalo ndugu yangu haulioni. Ndiyo maana watu wengine mnaota ndoto za kukutana na wazuiao maishani mwenu. Unaweza kuwa umeomba kwa muda mrefu kumpata mume/mewnza wa maisha yako, lakini zuio linatokea kwa mmoja wa wazazi wako akisema
“Huwezi kuolewa na mtu wa kabila hilo”.

Dunia ikatetemeka, dunia ikatikisika:.. MATHAYO 27:51… [51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;]…

Ukiibeba nguvu ya msalaba, mtaa/kata/ukoo/nchi/mkoan.k. vinaweza kutikisika.
Uwezo wa msalaba ni zaidi ya matikisiko haya ya kidunia kama vile tsunami, kwani haya yote hutokea eneo mojatu la dunia lakini upande mwingine halitoke.lakini msalaba wa Yesu ulikitisika maeneo yote,ndiyo maan Biblia inasema nchi ikatisika.

MAOMBI:
Natikisa magonjwa, taabu, dhiki, kuharibu mimba, kukosa kazi…..Tikisika, kwa Jina la Yesu. Miamba ikapasuka:

Ule mtikiso ulizaa tukio hili la nne la msalaba. Miamba ni vitu vigumu sana. kuna miamba ya maisha yako ambayo unaona ngumu sana kuondoka maishani mwako. Yesu ni mwamba.imeandikwa Yesu ni jiwe la pembeni.

MAOMBI:
Miamba ya maisha yako, tunaipelekea nguvu ya msalaba ukaisagesage na kupasuka pasuka yote kwa Jinala Yesu.

Makaburi yakafunuka: Msalaba unayo nguvu ya kupasua na kufunua. Kibinadamu, kaburi likeshafunikwa inakuwa ni mwisho wa maisha ya binadamu, na hakuna awezaye kufanya lolote (siyo mbunge, rais au ndugu yeyote yule awezaye).

Makaburi yana tabia ya kuficha ilivyovishikilia.

MAOMBI:
Leo naileta nguvu ya msalaba kwenye kata/wilaya/ukoo/ popote ambapo wachawi wameniweka kwenye makaburi yao, name nayapasua yote kwa Jina la Yesu.

Miili mingi ya waliolala ikainuka….. Hapa inamaanisha ni wale watu wailiokuwa wamekufa siku nyingi.
MATHAYO 27:52…. [52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;]….
Kwenye msalaba ipo nguvu ya kufufua vitu vilivyokufa. Nguvu ya msalaba inao uwezo huo wa kuleta hai tena kwa Jina la Yesu.
Miradi iliyokufa inafufuliwa, ndoa iliyokufa na kuzikwa inafufuliwa n.k kwa Jina la Yesu.

MAOMBI:
Naagiza nguvu ya msalaba kwa damu ya mwanakondoo, kazi iliyokufa ifufuke, mitaji iliyokufa ifufuke, ndoa zilizokufa zifufuke kwa Jina la Yesu. Aliyekuzika ukiwa hai, majeneza yapasuke na kukuachia kwa Jina la Yesu.

Akida wa kikosi cha kumsulubisha Yesu akasema mwenyewe “Hakika huyu ni Mwana wa Mungu”….
MATHAYO 27:54…[ Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.]….

Kwenye msalaba pana nguvu ya kujua /kugundua vitu ambavyo ulikuwa hujui )it is the centre for discovery).
Yamkini yapo mambo ambayo familia, ofisi, au mamlaka Fulani yameshindwa kujua uwezo ulio ulioko ndani yako wewe.

Hii ni kwa sababbu umefichwa. Iponguvu katika malaba wa Yesu ukiuendea, na baada ya hapo watu wataanza kuuona uwezo huo.

MAOMBI:
Bwana Yesu kwa nguvu ya msalaba, vile vitu vyote ndani yangu ambavyo wengine hawajavigundua, kwa nguvu ya msalaba wako wavigundue mapema kwa Jina la Yesu. Isiwepo kuchelewa kama Akida kwa Jina la Yesu.

Akida alichelewa sana kugundua nguvu ya msalaba (late discovery). Unaweza kuwa Mkristo kabisa na matumaini yako yakiendelea. Pindi utakapofikia miaka 80 pengine ndiyo watu wengine wataanza kushtukia uwezo wako.

MAOMBI:
Nakataa kutoonekana, kutotambulika kwa Jina la Yesu. Naagiza kuanzia sasa, watu wote ambao wanapaswa kuniona,wagundue leo mapema kwa Jina la Yesu. Uwezo wangu uonekane kwa nguvu ya msalaba. Nakataa kufunikwa na kutoonekana kwa Jina la Yesu. Nami binafsi weze kugundua mapema vitu vile vinavyonihusu kuvifanya kwa Jina la Yesu.

Ipo nguvu katika msalaba ya kugeuza mioyo ya watu. Wale waliokuwazia vibaya, wanapaswa kugeuza mioyo yao kwa nguvu ya msalaba. Waliokupinga siku zote,watafika wakati wa kubadili mawazo yao juu yako kwa nguvu ya msalaba kama yule Akida.

Waliokuwa wamekukataa kabisa wataanza kukupigia debe. Mkristo mwenye msalaba anayo nguvu hii ya msalaba.

MAOMBI:
Nageuza mioyo ya waliokukataa ikugeukie kwa Jina la Yesu.

Mungu wangu wa Mbinguni akubariki.
No Mimi ndugu yako
EV. Elimeleck S Ndashikiwe

Tel. +255767445846
        +255715445846

Wednesday, 23 March 2016

Nguvu ya Mungu Kwetu

Ngao ya Imani Ngao Ngao hukinga, Mungu wetu ni ngao hutukinga na mashambulizi, alimwambia Abramu, “…Usiogope, Abramu mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.” (Mwanzo 15:1). Imani katika Mungu hutukinga na maadui zetu, tunapomwamini kwa kuutumaini uaminifu na upendo wake, yeye huwa ngao kwetu. Kumwamini kunaendana na yeye kufanyika ngao, “Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na makimbilio yangu;” (2 Samweli 22:3). Tukiweka imani yetu kwa Mungu, tukimkiri na kumtegemea anakuwa kinga yetu pande zote, “Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.” (Zaburi 3:3). Unataka Mungu awe kinga yako pande zote? Mtegemee na kumsema hivyo, naye atakuwa hivyo kwako. Tumwaminipo Mungu, nguvu yake huwa ngao kwetu na kutukinga na mashambulizi. Ngao ya imani ni nguvu ya Mungu ambayo hutuzingira dhidi ya mashambulizi ya adui, tunapoziweka imani zetu kwa Mungu. Biblia inaonyesha kwa kusema, “Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.” (1 Petro 1:5). Maana mojawapo ya neno “mnalindwa” katika andiko hili ni “mnakingwa” kwa mfano wa kukingwa na ngao. Imani zetu zikiwa thabiti kwa Mungu humpinga Shetani, huachilia nguvu ya Mungu ambayo huwa ngao ya kumpinga Shetani, “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.” (Yakobo 4:7), “Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani,…” (1 Petro 5:9). Katika Waefeso 6:16 maandiko yanasema, “zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu,” Hapa imani imetajwa kama silaha ikifananishwa na ngao. Ngao hii imeonekana kuwa na uwezo wa kuzuia mishale ya moto ya Shetani. Mishale hii bila shaka ni hila zote ambazo Shetani huzitumia katika fikra au mawazo ili kumtoa mtu katika hali ya kuamini kwa kumtumaini Mungu katika kudhihirisha alichosema. Wakati fulani nilikuwa katika jaribu, wazo likanijia lisemalo “Mungu hakupendi angekuwa anakupenda yasingekupata haya” Wazo hili lilikuwa kama mshale, moto wake ulikuwa hali ya mashaka na wasiwasi kuhusu upendo wa Mungu kwangu. Niliweza kupinga wazo hilo kwa imani katika pendo la Mungu kama maandiko yanavyoonyesha, alinipenda na kumtoa Yesu kwaajili yangu ili nipate uzima (1Yohana 4:9). Hatutikisiki katika imani zetu kwa Mungu kwa kuwa tunalijua pendo lake kwetu na kuliamini, imani ya namna hii ni ngao kwetu kwa kuwa humfanya Mungu awe ngao yetu pande zote kwa nguvu zake. Wazo lolote lililo na hofu ndani yake ni mfano wa mshale wenye moto, lazima imani katika uaminifu wa Mungu kwa yale aliyosema ilizuie, kwa kuachilia nguvu ya Mungu. Mshale ni mfano wa wazo la kishetani, moto ni mfano wa woga au hofu inayokuja na wazo hilo. Ngao ya imani hufanya kazi kwa njia ya kuamini uaminifu na upendo wa Mungu, Biblia inasema, “…uaminifu wake ni ngao na kigao” (Zaburi 91:4). Pia Biblia inasema, “Nasi tumelifahamu pendo alilonalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini…” (1Yohana 4:16). Shetani aletapo wazo kama mshale lisemalo, “ugonjwa huu utakuua” , imani zetu hulipinga kama ngao kwa kuwa tunajua Mungu aliyesema kwa kupigwa kwa Yesu tumepona ni mwaminifu na anatupenda kiasi cha kudhihirisha uponyaji wake kwetu, Wakati huo huo Mungu anakuwa ngao kwetu na kutukinga kwa imani zetu kwake.

Saturday, 12 March 2016

AMRI NA TORATI

MARA NYINGI WATU WANASHINDWA KUTOFAUTISAHA KATI YA AMRI ZA MUNGU NA SHERIA ZA MUSA ZIFUATAZO NI TOFAUTI 1. ZA MUNGU Ziliandikwa na Mungu mwenyewe Kwa kidole chake [Torati 31:18] ZA MUSA Ziliandikwa na Musa mwenyewe kwa k wa kidole 2.Ziliandikwa kwenye mbao mbili za mawe yaliyochongwa, Torati 10:1-4 ZA MUSA Ziliandikwa kwenye chuo(kitabu cha dini), Torati 31:24 3., ZA MUNGU Ziliwekwa ndani ya Sanduku la Agano Torati 10:1-4 ZA MUSA Baada ya kuandikwa, ziliwekwa nje pembeni ya Sanduku la Agano, Torati 31:24-27 4 . Waliozivunja, walionekana kutenda dhambi 1Yoh. 3:4, na iliwapasa kufa. Torati 17:2-5 ZA MUSA Waliozivunja, hawakuonekana na dhambi wala haikuwapasa kufa kwani zilikuwa ni kivuli cha Kristo Wakolosai 2:14-17 5. Yesu alikuja kuzitimiliza wala si ku zitangua. Watu wote wanapaswa kuzifundisha…Mathayo 5:17-19 - ZA MUSA Yesu aliziondoa pale msalabani maana zilikuwa ni sheria za maa gizo tu yaliyosimama kama kivuli cha mema yajayo. Kolosai 2:15 6. Sheria(torati) ya Bwana ni takatifu njema na ya haki, nayo yadumu mi lele na milele, Warumi 7:12- ZA MUSA Zilikuwa ni kivuli cha kazi ya Yesu aliyoifanya msalabani, nazo zilikomea hapo. Ebran. 10:1-12 7. Sheria za Bwana ni kamilifu, za adili, kweli na za milele Zaburi 111:7-8 ZA MUSA Ziliishia pale Kristo alipokufa Msalabani. Waebran. 9:10-12, Luka 22:37 A. Mfano wa sheria ya Musa 1. Kuchinja kondoo kama mbadala wa mdhambi. Kutoka 29…, Walawi, Torati, Nyakati nk 2. Kifo yeyote aliyevunja mojawapo au Amri zote 10 za Mungu Kutoka 31:14… Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake. B. Sheria za Mungu, Kutoka 20 :1-17 Hivyo basi Yesu alipokufa Msalabani sheria za kuchinja kondoo tena ziliisha maana mwanakondoo wa Mungu (Yesu) aichukuaye dhambi ya ulimwengu alikuwa ameshachinjwa tayari. Yohana 1:29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!