Pages

Subscribe:

Thursday, 25 August 2022

NGUVU YA AGANO


Alhamisi 25 August 2022

NGUVU YA AGANO 

Na Mwalimu ELIMELECK NDASHIKIWE

        Hakika ni jambo la kushangaza kwani siku chache zilizopita nilikuaidi kukuandikia kitabu hiki cha Nguvu ya Agano kama Mungu atanipa kibali na siku ile alinipa, leo amenitaka kuanza kukumegea baadhi ya vitu vilivyomo kwenye hicho kitabu na nilikuaidia kuwa katika kitabu hiki nitazungumzia kiundani aina yote ya maagano ikiwemo yale ya Mungu na yakipepo.

          Atukuzuzwe Mungu juu mbinguni na duniani ilipo sehemu ya kuweka miguu yake, leo nitakujuza kiundani kuhusu maagano ama Nguvu iliyopo kwenye maagano ambayo tunaingia na Mungu. Pia jambo hili likupe kiu yakuingi agano ama maagano binafsi na Mungu ili kuwa katika uwakika mkubwa wakutembea na Mungu, kwani kama kuna kitu Mungu hukiheshimu ni Agano.


        Agano ni mapatano baina ya pande kuu mbili au zaidi dhidi ya jambo fulani. 

       Katika maagano ama Agano kuna mambo kadha wa kadha kama nilivyokujuza huku nyuma, ikiwemo, Ishara, Mapatano, ama makubaliano, Kiapo cha uamainifu na kadhalika. Huko mbeleni katika kitabu hiki nitakujuza kwa undani zaidi kuhusu mambo hayo.

      Nataka tuione hiyo Nguvu iliyopo katika maagano ya kimungu ikiwa ni baada ya kuiona iliyopo kwenye maagano ya kipepo siku kadhaa zilizopita kwenye makala ya Msaada kwa wanaoota ndoto wakiwa wanakula vyakula.Pamoja na zile za Namna ya kujinasua kwenye vifungo vya pepo mahaba.

         Kumbuka pia Bibilia ni Agano au ni mkusanyiko wa maagano makuu mawili, yaani lile la Kale na Jipya, ndio maana hutaacha kumuona Mungu kama utasoma Bbilia kwa Sura ya Kiagano, na ufahamu ni kati ya Mwanadamu na Mungu. Na Agano ni mapatano. Ukisoma kwa mtazamo huo wa kuona kilichopo ndani yake kuwa ni mapatano baina yako na Mungu hutatoka kama ulivyo mara baada ya kusoma maandiko na hutakubali kusoma kwa sura ya kawaida ama mazoea.



1. AGANO LA IBRAHIMU:
         Kuna Agano Mungu alifunga na Ibrahimu aliye baba yetu wa imani na Agano hili limekuwa na Nguvu kubwa sana  na Nguvu moja wapo ni hii. Tulione hilo Agano, Agano hili limetiwa nguvu katika sura kadha wa kadha za kitabu hiki cha Mwanzo kwa hiyo tutatazama kila kipengele kilichopo miongoni mwa Agano hili kulingana na uhitaji wa hoja nitakayo ijenga katika mada ama pwenti husika,ila nataka kukudokezea kipengele kimoja kabla ya kusonga mbele zaidi.

           Ni Mwanzo 15: 18 
Siku ile Bwana akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
19 Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni,
20 na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai,
21 na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, na Myebusi.

    Umeliona hilo jambo hapo? Tutalichambua huko mbeleni.
(a) Lili husika katika kumbariki Kiuzao Ibrahimu, Kikawaida Ibrahimu umri wake wa kupata mtoto ulikuwa umepita, ila kwa sababu ya Agano hili la Mungu kumpa uzao na ambao utakuwa kama Mchanga wa Bahari na kuwa tajiri Mungu alilazimika kutimiza jambo hilo bila kuangalia kikwazo cha Umri wake ama ule wa mkewe.

       Tuone hiyo ahadi ya uzao kiagano, 
Mwanzo 17: 
      Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.

     8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.

     9 Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako.

     10 Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa.

Katika hilo hakuna namna Mungu angeweza kuacha kumpa Isaka, maana tayari ameshajifunga na kiapo, na makubaliano yaliyopo kwenye Agano hilo.

      Kumbuka Lengo kuu la kitabu ama mafundisho haya ni kukupa mwanga wa kuyatumia maagano haya yaliyopo kweye bibilia ili kujinasua mahali ulipo ama kunufaika na Baraka zilizomo ndani ya Bibilia maana bibilia ni mkusanyiko wa maagano makuu mawili yaani lile la Kale na Jipya ambalo maandiko huliita kuwa ni bora zaidi.

       Wakati tunasonga mbele  nataka kukupa uwakika wa kwamba Baraka hizi ni matokeo ya Agano hilo, ndiposa Ibrahimu akampata huyo mwana bila kuangalia umri wake ama kigezo chochote kile cha kibaolojia ili na wewe kama mwana wa Agano hili uwe na ujasiri wakumuomba Mungu bila kuangalia kizuizi chochote kile kilichopo mbele yako.


     Tudhibitishe jambo hili kutoka kwenye kinywa cha Mungu mwenyewe, 
Ni Mwanzo 17: 21 
        Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao.
22 Mungu akaacha kusema naye, akapanda kutoka kwa Ibrahimu.

Hapo Ni Mungu anayanena hayo wala Sio Jirani yake na Mungu.

(b) Lilimpa Baraka za Mali, Kumbuka Agano hufanywa Imara kwa sadaka, maombi na kadhalika, ndio maana wale wanaofanya maagano na mapepo hupaswa kutoa kafara za damu za wanyama, ndege, hata watu. Na kanuni hiyo Shetani ameiiga kwa Mungu.
Mara baada ya Ibrahimu kukubali kumtoa Mwanaye Mungu alinena naye kuhusu kumbariki kiuchumi ikiwa ni sehemu ya kiagano.

      Mwanzo 22: 15 
Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni

16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,

17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;

18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.

Hapo panatajwa kumiliki malango ya Adui, maana yake ni kuwa na uwezo wa ulimwengu wa roho wakuteka na kutaifisha mali ama utajiri wa adui zako kisha kuugeuza kuwa wako, kwa kifupi ni kuwafanya mateka wa uchumi. Tulihakiki jambo hilo kwenye kitabu hiki hapa:
Isaya 60: 11 Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.

Pia sentesi inayofunga mazungumzo hayo ipo katika mstari wa 18, hapo kwenye kitabu cha Mwanzo, ambayo inadhiirisha dhairi kuwa Agano hili ndilo lililopenyeza Baraka kwa kila taifa duniani, ndio maana mataifa yakitaka kubarikiwa ni vyema kujiunganisha ama kujiambatanisha kiroho na Taifa la Iziraeli. Nataka kukuonyesha sentensi hiyo; “na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia
Najua unatamani kuendelea nami ila kwa kweli muda sio rafiki yangu, ila kabla sijakutaka tuonane kesho, ambapo nitaendelea na Agano hili kabla ya kuchambua lile la Nuhu, na mengineyo, ninataka kukupa uwakika kwamba wewe ni sehemu ya Agano hili la Ibrahimu ili kukujengea Imani dhabiti itakayokusaidia kupata uwalali wa kuingia kwenye maombi leo ili kudai Baraka zako za kiagano kama mwana wa Mungu.

Kabla ya andiko hilo kumbuka Yesu alikuwa akiwaponya watu wengi ila alitia mkaza sana kwa watu wa Uzao wa Ibrahimu, ndio maana alipomuona yule mama mgonjwa alimuhurumia na kusema kuwa imekuaje hivi kwa mtu wa uzao wa Ibrahmu, alikadhalika kwa mama mkaninayo yule aliyebembeleza na kusema kuwa hata mbwa hula makombo ya bwana zao na kisha kutendewa mujuza. Pale unamuona Yesu akisema kuwa alitumwa kwa ajili ya watu wa Uzao wa Ibrahimu, ukiona Uzao wa Ibrahmu kama wewe uliyepita darasa hili langu picha unayoipata pale ni kwamba hii ilikuwa ni kauli ya KIAGANO.

Maana yake ni kwamba Yesu alipaswa kutilia mkazo kwa watu hawa kwa sababu ya Nguvu ya kiagano. Kwa mantiki hiyo Mungu hapendezwi na mateso ama taabu kwa mtu wa Uzao wa Ibrahimu. Yaani wewe uliyeokoka na mimi pia. Maana wapo wa uzao huo kibaolojia ambao ni Wayahudi na wapo wa Uzao huo ambao ni wale wa Imani yaani waliokoka. Na jambo hili limetiwa muhuri na Mungu mwenyewe kimaandiko.

Kwa ujasiri fungua nami maandiko haya hapa: Ni WAGALATIA 3.29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Neno ahadi hapo linawakilisha AGANO, Maana kama umekuwa mwanafunzi wangu Mwaminifu na Makini utakumbuka vipengele vyote tulivyo visoma vimesheheni ahadi za Ibrahimu kubarikiwa.
Tukutane kesho, ila kama huja Okoka fahamu kuwa hutaweza kuridhi Baraka hizi na maombi utakayoomba hayatakuwa na Nguvu ya kiagano. Na kwa aliyeokoka hivi sasa ninamtaka kuingia kwenye hayo maombi ya kiagano ili kufungua milango iliyofungwa nakudai baraka zako za Watoto, Utajiri na kadhalika.

                                         

Hakuna maoni:

UTUKUFU NA HESHIMA NI VYAKO MUNGU

Mungu ndiye astahiliye kutukuzwa daima,

Anatuwazia yaliyo mema kila wakati

Friday, 2 July 2021

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

MH: PASTOR TARIMO
SOMO:   AINA ZA KARAMA ZA ROHO NA HUDUMA 
    

       Bwana Yesu asifiwe sana ndugu yangu mpendwa msomaji wangu, MUNGU wangu wa Mbinguni akubariki sana kwa kuendelea kuwa nami.

              1Korintho 12:1............ Basi ndugu kwa habari ya karama ...................

   Mtume Paulo anaongelea kwa habari ya KARAMA ZA ROHO ambazo Mungu ameziachilia kwa kanisa ili tu kuukamilisha utumishi kwa watu  wake katika ulimwengu wa Roho na ule wa mwili.

            Ukiendeloea kusoma hadi mstr wa 11 utakutana na namna karama hizi za Roho zinavyofanya kazi kwa masaidizano chini ya uongozi wa ROHO MTAKATIFU.

AINA ZA KARAMA ZA ROHO
         Ziko aina mbalimbali sana za Karama za Roho, lakini katika karama zote hizo zilizo kuu ni karama tisa.
       Aina hizi za karama tunakutana nazo katika kitabu hiki cha 1Kor 12:8

1. Neno la Maarifa
           Aina hii ya karama  inasimamia juu ya utambuzi katika kuwahudumia watu,  mtumishi anaweza kutambua uhitaji wa mtu juu ya kile kinachomsibu kiroho na kimwili.
         Roho wa Mungu atahakikisha anakuonesha kwa ishara kupitia mwili wako mwenyewe.

    Mfano unaweza kujisikia unaumwa kichwa wakati ukiwa ktk huduma,  kumbe Mungu anakuonesha kuwa kuna mtu pembeni anasumbuliwa na kichwa.

2. Neno la Hekima
            Aina hii ya karama inasimamia juu ya utatuzi ktk masuala malimbali ya kiroho na kimwili katika maamuzi.      Mfano wa jambo hili tunaliona kwa mtumishi wa MUNGU Mfalme Suleimani alipoletewa mtoto aliyekuwa akigombewa na wanawake wawili makahaba  
 1Wafalme 3:16-27 utakutana na habari hii.

3. Karama ya Imani
             Aina hii ya Karama inasimamia misingi ya namna Wokovu ulivyojengeka na kujengwa ndani yake.
Maana chanzo cha imani huja kwa kusikia, itategemea umesikia nini na  kwa nani.

Isipokuwa chanzo cha imani ya KRISTO huja kwa kusikia NENO la Kristo mwenyewe.
.............................. IMANI wakati mwingine ni kitu anachopewa mtu kama karama.

4. Karama ya Kinabii na Huduma ya Kinabii
                    =Karama ya kinabii huwa sio ya kudumu, Mungu huiachilia ndani ya mtu maalumu, kwa wakati maalumu na kwa kusudi maalumu.

                    =Huduma ya kinabii hii huwa ni ya kudumu na huwa ni kama ofisi maalumu kwa kazi hiyo.

5. Karama ya Kuponya
                 Aina hii ya karama huwa inasimamia juu ya uwezo katika kuponya, kuwa na juhudi na nguvu ya imani juu ya NGUVU NA UWEZA ULIO KATIKA MUNGU kupitia jina la YESU KRISTO.


6. Matendo ya Miujiza
7. Kupambanua Roho
              si kila roho inatokana na Mungu

8. Aina za Lugha na
9. Tafsiri za Lugha.

......................Karama zina tabia tofauti tofauti ambazo haziwezi kufanana ingawa zinaweza kuingiliana katika utendaji kazi maana zinaongozwa na Roho yule yule mmoja wa MUNGU.

NB;
         KATIKA UTUMISHI WA KUTUMIKIA KWA AJILI YA KRISTO, kuna mikoba mitatu ya muhimu na ya lazima sana ambayo hutakiwi kuikosa.
                .Huduma tano EFES 4;11-12
           .Karama Tisa  1KOR 12;8-10
           .Matunda Tisa  GALAT 5;22-23

TUTAENDELEA NA KIPENGELE CHA HUDUMA.......................

MUNGU WANGU WA MBINGUNI AZIDI KUKU INUA 

Karibu sana katika ibada zetu zinazoendelea hapa kanisani 

PENTECOST TABARNACLE OF PRAISE Kisanga "B" Wazo!